Posts

BREAKING NEWS : BOT

Image

BREAKING NEWZZ.....RAIS MAGUFULI AWASIMAMISHA KAZI VIGOGO 4 WALIO SAFIRI KWENDA NJE YA NCHI

Image
Rais Magufuli ameagiza kusimamishwa kazi mara moja kwa watumishi waandamizi wanne wa Takururu ambao walisafiri nje ya nchi licha ya Rais Magufuli kupiga marufuku safari za nje kwa watumishi wa umma. Watumishi hao ni Mary Mosha, Ekwabi Mujungu, Doreen Kapwani na Rukia Nikitas ambao walisafiri nje ya nchi licha ya kunyimwa kibali cha safari kutoka kwa Rais ama Katibu Mkuu Kiongozi. Bw Sefue amesema atakayekiuka agizo la rais "atachukuliwa hatua kali”. Hii si mara ya kwanza kwa Dkt Magufuli kuwachukulia hatua maafisa wa Serikali tangu achukue madaraka mwezi uliopita. Siku chache baada ya kuingia afisini, a libadilisha usimamizi wa hospitali ya taifa ya Muhimbili baada ya kufanya ziara ya kushtukiza huko na kutoridhishwa na utoaji huduma

Lowassa kufanya ziara nchi nzima kuanzia kesho

Image
Edward Lowassa. Aliyekuwa mgombea urais wa Chadema akiungwa mkono na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Edward Lowassa ataanza ziara ya kuzunguka nchi nzima kuwashukuru Watanzania kwa kumpigia kura katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25 na kesho atakuwa Tanga. Katika ziara hiyo, Lowassa ataambatana na viongozi waandamizi wa Chadema na Ukawa kuwashukuru wananchi kwa namna walivyounga mkono upinzani na ajenda nzima ya mabadiliko katika Uchaguzi Mkuu uliopita. Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Chadema, Tumaini Makene imesema kiongozi huyo atatoa shukrani zake kwa wananchi kwa jinsi wanavyoendelea kuweka matumaini yao kwa upinzani. Taarifa hiyo ilieleza kwamba wananchi bado wanaamini kwamba upinzani ndiyo nguzo imara wanayoitegemea katika kuwaletea mabadiliko ya kweli kwa ajili ya maendeleo yao na ustawi wa Taifa kwa ujumla. “Wananchi wanastahili shukrani kwa imani hiyo kubwa ambayo ni ishara

RAIS DR. MAGUFULI AMFUTA KAZI MKURUGENZI MKUU WA TAKUKURU DR. HOSEA

Image

EXCLUSIVE;RASMI MBOWE ASIFU KASI NA UTENDAJI WA MAGUFULI

Image
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amezungumzia kasi aliyoanza nayo rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli pamoja na baraza lake la mawaziri. Akizungumza jana na mwandishi wa habari wa Azam TV, Mbowe alisema kuwa rais Magufuli ameanza vizuri kiutendaji na kwamba ameanza kuzifanyia kazi hoja zilizokuwa zikihubiriwa na Chadema ndani na nje ya Bunge. “Hoja ya kubana matumizi ya serikali, hoja ya kupunguza sherehe za kitaifa, hoja ya kupunguza safari za nchi za nje kwa viongozi wetu, hoja ya kupunguza watumishi wa umma ambao hawana umuhimu, hoja ya kuwa na serikali ndogo. Haya mambo tulizungumza siku zote na hawa hawa wa Chama cha Mapinduzi ndio waliokuwa wanayapinga haya,” alisema Mbowe. Mbowe alieleza kuwa dhana ya upinzani sio kupinga kila kitu kinachofanywa na serikali hivyo chama chake hakitakuwa tayari kupinga mambo mema yanayofanywa na serikali ya awamu ya tano kama baadhi ya watu wanavyotarajia, bali kitajikita katika kujad

Breaking news:..TAZAMA UOKOAJI WA ABILIA KATIKA MELI YA ROYAL INAYO UNGUA MOTO IKITOKEA PEMBA KWENDA UNGUJA

Image
  Meli ya royal ilikuwa ikitokea unguja kuelekea Pemba hivi sasa inaungua, kwa Bahati Serengeti ilikuwa inatokea Pemba kwenda unguja nimeikuta njiani hivyo shughuli za uzimaji moto na uokozi Wa abiria na Mali zao inafanyika kama invyoonekana kwenye picha

Mwigulu atoa saa 48 kwa kampuni ya Sparkway ltd kulipa wakulima

Image
Waziri wa Kilimo Uvuvi na Mifugo Mh.Mwigulu Lameck Nchemba akiongea jambo. Waziri wa Kilimo Uvuvi na Mifugo Mh.Mwigulu Lameck Nchemba atoa saa 48 kwa kampuni ya Sparkway ltd kulipa BIllion 3.4 kwa wakulima wa korosho Mkoa wa pwani. Kufuatia agizo hio,Wakulima waliouza korosho hiyo wataanza kulipwa jumatatu ya tar.21.12.2015.

BREAKING NEWZZ....ZITTO KABWE ATOA KAULI NZITO KUHUSU PRO.MUHONGO...HAKIKA ZITTO KAKOMAA KISIASA HASWA

Image
  Prof. Sospeter Muhongo alikuwa Waziri wa Nishati na Madini wakati wa sakata la ‪#‎TegetaEscrow‬. Kamati ya Bunge ilipendekeza na Bunge kuazimia kuwa Muhongo avuliwe madaraka yake ya Uwaziri. Prof. Muhongo alijiuzulu. Akafanyiwa uchunguzi na Kamishna wa Maadili kutamka kuwa hakukutwa na kosa la kimaadili. Unajengaje hoja kuwa hana haki ya kuteuliwa kuwa Waziri? Keshaadhibiwa kwa kosa la awali, kwa kujiuzulu. Sheria ipi inasema hana haki ya kuteuliwa tena? Niliongoza Kamati ya PAC. Nina uhakika Waziri muhongo kwenye sakata lile alishauriwa vibaya na kujikuta anatetea ubadhirifu. Lile nifunzo kubwa kwake na ninavyomuona sasa hatarudia tena makosa yale. Kuna mambo ya msingi lazima afanye sasa 1) Azuie kuanzia sasa malipo ya 'capacity charges' kwa kampuni ya kitapeli ya IPTL na atumie sheria kutwaa mitambo ya IPTL na kumilikisha TANESCO 2) Amtake Waziri wa Mambo ya Ndani na Jeshi la Polisi kumkamata mara moja anayejiita mmiliki wa IPTL na afunguliwe mashtaka ya utap

Kajala ajiachia na dada’ke diamond!

Image
Mwigizaji Kajala Masanja akiwa na Queen Darleen wakiponda raha. Na Musa Mateja HUKU kukiwa na madai kwamba mwigizaji Kajala Masanja ana uhusiano wa ‘kikubwa’ na Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, mwigizaji huyo amezidi kuyachochea moto madai hayo kwa kutokana na kujiachia mara kwa mara na dada wa Diamond, Queen Darleen, Risasi Mchanganyiko linakujuza. Kwa mujibu wa chanzo makini, Kajala na Queen Darleen wamekuwa ‘beneti’ kila kona ambapo pia kuna fununu kuwa hata familia ya Diamond imebariki uhusiano wake na Mbongo Fleva huyo na wanampa ushirikiano wa kutosha Kajala. “Fuatilieni tu, Kajala ameshakubalika kwa kina Diamond, ndiyo maana leo utaona Kajala na dada yake Diamond, Queen Darleen wanapiga misele pamoja, hata katika viwanja vingi vya starehe wanakwenda wote,” kilisema chanzo hicho. …..Wakifurahia jambo. Mwishoni mwa wiki hii, paparazi wetu aliwanasa laivu Kajala na Queen Darleen katika fukwe za White Sands, Mbezi Beach jijini Dar es Salaam walipokuwa

Kajala ajiachia na dada’ke diamond!

Image
Mwigizaji Kajala Masanja akiwa na Queen Darleen wakiponda raha. Na Musa Mateja HUKU kukiwa na madai kwamba mwigizaji Kajala Masanja ana uhusiano wa ‘kikubwa’ na Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, mwigizaji huyo amezidi kuyachochea moto madai hayo kwa kutokana na kujiachia mara kwa mara na dada wa Diamond, Queen Darleen, Risasi Mchanganyiko linakujuza. Kwa mujibu wa chanzo makini, Kajala na Queen Darleen wamekuwa ‘beneti’ kila kona ambapo pia kuna fununu kuwa hata familia ya Diamond imebariki uhusiano wake na Mbongo Fleva huyo na wanampa ushirikiano wa kutosha Kajala. “Fuatilieni tu, Kajala ameshakubalika kwa kina Diamond, ndiyo maana leo utaona Kajala na dada yake Diamond, Queen Darleen wanapiga misele pamoja, hata katika viwanja vingi vya starehe wanakwenda wote,” kilisema chanzo hicho. …..Wakifurahia jambo. Mwishoni mwa wiki hii, paparazi wetu aliwanasa laivu Kajala na Queen Darleen katika fukwe za White Sands, Mbezi Beach jijini Dar es Salaam walipokuwa

Kajala ajiachia na dada’ke diamond!

Image
Mwigizaji Kajala Masanja akiwa na Queen Darleen wakiponda raha. Na Musa Mateja HUKU kukiwa na madai kwamba mwigizaji Kajala Masanja ana uhusiano wa ‘kikubwa’ na Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, mwigizaji huyo amezidi kuyachochea moto madai hayo kwa kutokana na kujiachia mara kwa mara na dada wa Diamond, Queen Darleen, Risasi Mchanganyiko linakujuza. Kwa mujibu wa chanzo makini, Kajala na Queen Darleen wamekuwa ‘beneti’ kila kona ambapo pia kuna fununu kuwa hata familia ya Diamond imebariki uhusiano wake na Mbongo Fleva huyo na wanampa ushirikiano wa kutosha Kajala. “Fuatilieni tu, Kajala ameshakubalika kwa kina Diamond, ndiyo maana leo utaona Kajala na dada yake Diamond, Queen Darleen wanapiga misele pamoja, hata katika viwanja vingi vya starehe wanakwenda wote,” kilisema chanzo hicho. …..Wakifurahia jambo. Mwishoni mwa wiki hii, paparazi wetu aliwanasa laivu Kajala na Queen Darleen katika fukwe za White Sands, Mbezi Beach jijini Dar es Salaam walipokuwa

Fahamu aina za upungufu wa damu mwilini

Image
Leo tuangalie tatizo la upungufu wa damu mwilini. Anaemia ni jina la jumla linalotumiwa kubainisha aina mbalimbali za upungufu wa damu mwilini. Kiwango cha kawaida cha chembe nyekundu za damu (Haemoglobin-Hb) katika mwili wa binadamu ni kati ya gramu 12 mpaka 14 kwa kila mililita ya damu na zikiwa pungufu ya hapo mtu huyo anakuwa na tatizo la upungufu wa damu. Upungufu wa damu mwilini hutokea iwapo mkusanyiko wa pamoja wa chembe nyekundu za damu zinapopungua kupita kiwango cha kawaida kinachotakiwa kwenye mwili wa binadamu. Tatizo hili linaweza kumpata mtu yeyote ingawa visababishi vinaweza kutofautiana. Licha ya utofauti huo mara nyingi tatizo hili husababishwa na mambo makuu matatu ambayo ni kupoteza damu mfano wakati wa hedhi kwa wanawake hasa wanaotokwa na damu nyingi au kuvuja damu kunakosababishwa na vidonda vya tumbo. Sababu nyingine ni uzalishwaji duni wa chembe nyekundu za damu unaosababishwa na upungufu wa vitamini au lishe duni pamoja na magonjwa sugu. Pia magon

CHADEMA Wacharuka Baada ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda Kumweka Ndani Mbunge wao Saidi Kubenea..Watoa Tamko

Image
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI Kama ambavyo imeripotiwa kwenye vyombo vya habari na njia zingine za upashanaji habari tangu jana kuwa Mbunge wa Jimbo la Ubungo kwa tiketi ya CHADEMA, Ndugu Saed Kubenea aliwekwa chini ya ulinzi na kuamriwa kwenda kituo cha polisi kwa amri ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda ambaye inadaiwa hakutaka mbunge huyo azungumze na wananchi ambao ni Wafanyakazi wa Kiwanda cha Tanzania Took Garment, waliokuwa wamemuita mbunge huyo kwa ajili ya kumweleza matatizo wanayokumbana nayo kazini hapo, ikiwa ni pamoja na ujira kidogo na mazingira magumu ya kazi. Aidha akitambua kuwa alichofanya matumizi mabaya ya dhamana ya uongozi, hivyo akakusudia kuficha umma usijue uovu huo, katika tukio hilo Makonda aliwaagiza polisi wakamate kamera za waandishi wa habari waliokuwa katika eneo hilo wakitimiza wajibu wao wa kikazi na kitaaluma kwa jamii. Katika hatua ya sasa, tunaomba kusema ifuatavyo; 1.  Tukitambua kuwa mamlaka ya DC kuamuru watu kukamatwa yamef

Mwanasheria Albeto Msando Afunguka Kuhusu Dr Mwaka....Adai Walikuwa Wapi Siku Zote?

Image
Kuna watu watasema ni wivu! Kuna wengine watasema Mwaka ni tapeli! Kuna ambao watakuwa upande wa Kigwangwala na kuna ambao watakuwa kwa Mwaka. Ila je kwa nini mpaka leo hii tiba inahojiwa? Siku zote mamlaka husika zilikuwa wapi? Hao waliotibiwa wakapona wako wapi?  Ambao hawajapona ni kina nani? Mkurugenzi wa Baraza la Tiba Asili mpaka anafika hapo kwenye 'kliniki' alikuwa hajui kama Mwaka ana vyeti au la? Hakuwa na taarifa zozote za ziada? Je Babu wa loliondo ilikuwaje? Wanaotibu mapenzi na kupata kazi vipi? Wale madaktari wa kusafisha nyota? Au hao kuku weusi wanaokula sio dhuluma? Nadhani Naibu Waziri ameanza kushtukiza ila AENDE NA KWENYE VITUO VYA AFYA NA ZAHANATI PIA. Kuna hao madaktari waliosomea na wao ni bure kabisa huko!! Hili la Mwaka kilichomponza ni kupitiliza!! Wote huwa inatukuta tukinogewa!! Sasa ndio atajua kama bado WATAMPENDA By Alberto Msando-Instagram

WABUNGE WANNE WAKATAA UWAZIRI KWA MAGUFULI

Image
WABUNGE wanne wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wametajwa kukataa uteuzi wa nafasi ya uwaziri ili kujaza nafasi za wizara nne zilizokuwa wazi. Hatua hiyo imetokana na kile kilichoelezwa kuwa ni hofu ya wabunge hao kushindwa kwenda na kasi ya Rais Dk. John Magufuli, ambaye aliwaapisha mawaziri wapya Desemba 12, mwaka huu. Kwa mujibu wa gazeti la Mtanzania, wabunge wamedai kuwa kasi ya Rais Magufuli inawatia hofu. “Kasi ya Rais Dk. John Magufuli ni nzito na kwangu ni ngumu na nilifikiri niko mimi peke yangu kumbe baada ya taarifa hizi nasikia na wenzangu wawili nao walikataa uteuzi. “Niliarifiwa juu ya uteuzi lakini baada ya kupima nikaona hapana siwezi kazi ya uwaziri, bora ni baki na ubunge wangu,” alisema mbunge huyo ambaye hakutaka jina lake litajwe. Wizara 4 zilizokosa Mawaziri Wakati akitangaza Baraza la Mawaziri, Desemba 10, mwaka huu, Rais Magufuli alisema kuna baadhi ya wizara hazina mawaziri kutokana na sababu mbalimbali ikiwamo unyeti wa wizara hizo na kwamba a

Kubenea apandishwa Mahakamani leo

Image
Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea. Baada ya taflani iliyotokea jana Jumatatu kati ya mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea wa Chadema na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda eneo la viwanda (EPZA) Mabibo jijini Dar hali iliyopelekea DC Makonda kuwaamuru polisi wamuweke chini ya ulinzi Saed Kubenea na kumpeleka Kituo cha Polisi. Leo Saed Kubenea amepandishwa kizimbani kwenye mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam na kusomewa shtaka la kutoa lugha chafu dhidi ya Mkuu wa wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda. Hata hivyo, Kubenea amekana kufanya kitendo hicho na kesi yake kuahirishwa hadi Desema 29, mwaka huu huku uchunguzi ukiendelea.

Mwanamke wa unga jela miaka 20

Image
Anna Gemanist Mboya. Na Makongoro Oging’ Mrembo wa madawa ya kulevya ‘unga’, Anna Gemanist Mboya mkazi wa Kijitonyama, Kinondoni jijini Dar amefungwa jela miaka 20 na kupigwa faini ya shilingi milioni 148, fedha anazotakiwa kuzilipa mara atakapomaliza kifungo. Mrembo huyo ambaye ni mfanyabiashara, amefungwa Desemba, Mosi, mwaka huu mbele ya Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Wilfrida Koroso kwa kosa la kusafirisha madawa ya kulevya. Kamanda wa Kikosi cha Kupambana na Kudhibiti Madawa ya Kulevya nchini, SACP Godfrey Nzowa (pichani) amethibitisha kuhukumiwa kwa mrembo huyo na ameipongeza mahakama kwa kasi ya kuendesha kesi nyingi za madawa ya kulevya na kuzitolea hukumu. Kwa mujibu wa Kamanda Nzowa, Anna alikamatwa Januari 2, mwaka 2011 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere na kikosi kazi (task force) kilichopo katika kiwanja hicho. “Nawaomba wananchi waendelee kuwafichua wahusika wa madawa ya kulevya ili waweze kukamatwa na kufikishwa katika vyombo vya she