Fahamu aina za upungufu wa damu mwilini
Leo tuangalie tatizo la upungufu wa damu mwilini. Anaemia ni jina la jumla linalotumiwa kubainisha aina mbalimbali za upungufu wa damu mwilini. Kiwango cha kawaida cha chembe nyekundu za damu (Haemoglobin-Hb) katika mwili wa binadamu ni kati ya gramu 12 mpaka 14 kwa kila mililita ya damu na zikiwa pungufu ya hapo mtu huyo anakuwa na tatizo la upungufu wa damu. Upungufu wa damu mwilini hutokea iwapo mkusanyiko wa pamoja wa chembe nyekundu za damu zinapopungua kupita kiwango cha kawaida kinachotakiwa kwenye mwili wa binadamu. Tatizo hili linaweza kumpata mtu yeyote ingawa visababishi vinaweza kutofautiana. Licha ya utofauti huo mara nyingi tatizo hili husababishwa na mambo makuu matatu ambayo ni kupoteza damu mfano wakati wa hedhi kwa wanawake hasa wanaotokwa na damu nyingi au kuvuja damu kunakosababishwa na vidonda vya tumbo. Sababu nyingine ni uzalishwaji duni wa chembe nyekundu za damu unaosababishwa na upungufu wa vitamini au lishe duni pamoja na magonjwa sugu. Pia magon