Posts

BARAZA KUU LA WAISLAMU MKOA WA MWANZA LAMUONYA ASKOFU GWAJIMA.

Image
Jana Ijumaa ya Octoba 16,2015 Baraza Kuu la Waislamu Mkoa wa Mwanza liliungana na Waislamu wengine kuadhimisha mwaka mpya wa Kiislamu ambao ni 1437. Kwa kalenda ya Kiislamu sherehe hizo zilifanyika jana tarehe mbili, mwezi Muharamu mwaka wa 1437 (02.01.1437) ikiwa maadhimisho yanayoambatana na kumbukumbu ya Kuhama kwa Mtume Muhammad kutoka Mji wa Macca kwenda Madina. Na: George Binagi-GB Pazzo Katika kuadhimisha sherehe hizo, Baraza hilo kupitia kwa Katibu wake Mkoani  Mwanza Sheikh Mohamed Balla (Kulia Pichani) alitoa tamko kwa niaba ya Waislamu wote Mkoani Mwanza kutokana na kauli inayoelezwa kutolewa na Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima Josephat Gwajima kwamba ana ndoto ya Misikiti yote nchini kugezwa kuwa Sunday School na Masheikh watakwenda kuangukia katika misalaba. Alisema kauli za namna hiyo si njema kwa mstakabali wa Taifa ambapo alisema kuwa Waislamu wote Mkoani Mwanza wanalaani na kukemea kauli hiyo na nyingine zote za aina hiyo na wale wanaozitoa. Aliwataka Watanzania

RATIBA YA KUAGA MWILI WA MAREHEMU MH DEO NFILIKUNJOMBE LEO

Image

PICHA ZA AJALI YA CHOPA YA DEO FILIKUNJOMBE

Image
PICHA KWA HISANI YA FRANCIS GODWIN Julius Kambarage Nyerere (13 April 1922 – 14 October 1999)

Mgombea Ubunge ‘Aliyetekwa’ Mtwara Apatikana.......Ndugu Wasimulia Tukio Zima, Polisi Wasema Wanachunguza Kama Ni Kweli Au Lilipangwa

Image
Mgombea  ubunge  jimbo  la  Mtwara  Mjini  kupitia  CHADEMA,  Joel Nanauka alipotea  katika  mazingira  ya  kutatanisha  tangu  juzi  na  kukutwa  ametupwa  nje  ya  mlangoni wa jengo la Kliniki/kituo cha afya  hapo  Mtwara. Ndugu  wa  mbunge  huyo  wameusimulia  mkasa  huo  kama  ifuatavyo: "Ndugu yetu Joel Nanauka ambaye anagombea Ubunge Jimbo la Mtwara Mjini kupitia CHADEMA, alipotea katika mazingira ya kutatanisha siku ya Jumatatu Tarehe 5/10/2015. Siku hiyo alitoka kwenye shughuli za kampeni akiwa na wenzake na walirudi nyumbani akiwa amechoka. "Majira ya saa kumi na mbili na nusu, alimtumia mwenzake ujumbe mfupi wa mkononi (SMS) akimjulisha kwamba kuna mtu amekua akimtafuta tangu wiki iliyopita waonena na mchana wa siku hiyo alimfuata ofisi ya CHADEMA lakini hakumkuta, hivyo anakwenda kuonana naye mara moja eneo linaloitwa Mnarani hapa mjini Mtwara. Eneo hilo sio mbali na nyumbani kwao. "Muda mrefu ulipita bila kurudi nyumbani huku giza likiwa lim

RAIS JAKAYA KIKWETE AZINDUA NYUMBA ZA MAKAZI ZA NHC MINDU UPANGA DAR ES SALAAM

Image
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe uzinduzi wa jengo la nyumba za makazi za NHC Mindu, Upanga Jijini Dar es Salaam Oktoba 7, 2015 zilizojengwa na NHC na kuuzwa kwa wamiliki . Wanaoshuhudia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa, Mama Zakhia Meghji na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Vangimembe Lukuvi . Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka jiwe la ufunguzi la jengo la nyumba za makazi za NHC Mindu, Upanga Dar es Salaam zilizojengwa na NHC na kuuzwa kwa wamiliki. Wanaoshuhudia nia Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Vangimembe Lukuvi, Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angela Kairuki na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa, Mama Zakhia Meghji  Jengo la nyumba za makazi za NHC Mindu, Upanga Dar es Salaam zilizojengwa na NHC na kuuzwa kwa wamiliki linavyoonekana. Baad