MAGUFULI ALIVYOTIKISA MJINI TABORA LEO
Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli,akiwahutubia Wananchi wa Tabora jioni ya leo kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Ali Hassan Mwinyi.Dkt Magufuli alisema kuwa Serikali yake kwa sehemu kubwa itakuwa upande wa wananchi wanyonge ili hatimaye wawe na maisha yenye neema na kwenye hilo ana uhakika atafanya kazi nzuri maana kwake yeye ni kazi tu na hakuomba kuwa Rais ili awe mwanasiasa bali anaomba nafasi hiyo kwa kujua anajua namna ambavyo amejipanga kufanya kazi kwa ajili ya maendeleo ya Watanzania wote. PICHA NA MICHUZI JR-TABORA Sehemu ya umati wa watu waliokuwa katika uwanja wa Ali Hassan Mwinyi jioni ya leo walipokuwa wakimsikiliza Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli. Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa tabora mjini na kuwaambia kuwa Dk. Magufuli ni kiongozi sahihi anayehitajika Tanzania kwa sasa na kuwataka wananchi kumpigia kura zote ifikapo Oktoba 25 mwaka huu. Mgombea wa Urai