Posts

MSAFARA WA MAGUFULI WANUSURIKA TENA KUPATA AJALI

Image
MSAFARA wa mgombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli, umenusurika kupata ajali, baada ya lori la mizigo kuuvamia na kugonga magari matatu likiwamo lililokuwa limembeba mpiga debe wa chama hicho, Amon Mpanju. Ajali hiyo ilitokea jana asubuhi katika eneo la Njia Panda jirani kilomita chache kabla ya kuingia Maswa mjini.Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu, Gemin Mushi jana alikiri kutokea kwa tukio hilo. Alisema wakati msafara huo ukitoka wilayani Meatu, askari polisi waliokuwa wakiuongoza msafara huo walimuaru dereva wa lori hilo lenye namba za usajili T 217 DDY kuegesha pembeni gari lake, lakini alikaidi.“Msafara wa mgombea urais ulikuwa jirani kuingia Maswa, dereva wa lori aliamuriwa kuliweka pembeni akakaidi, tena kibaya akaongeza mwendo hali iliyosababisha ajali. “Lori hili ni mali ya Kampuni ya Dilchadri Mill Ltd ya jijini Mwanza, liligonga magari matatu likiwamo gari lenye namba za usajili T 217 CYM aina ya Toyota Land Cruser a

Rais Kikwete Ateua Wakuu wa Mikoa Wawili,Mganga Mkuu wa Serikali, Naibu Mwanasheria Mkuu

Image
 TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amewateua wakuu wawili wapya wa mikoa kujaza nafasi zilizoachwa wazi na wakuu wa Mikoa ambao wanawania ubunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.  Taarifa iliyotolewa Jumatatu, Septemba 14, 2015 na Katibu Mkuu Kiongozi (KMK), Balozi Ombeni Sefue inasema kuwa katika uteuzi wake, Rais Kikwete amemteua Ndugu Amos Makalla kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro na Ndugu Jordan Rugimbana kuwa Mkuu wa Mkoa wa Lindi.  Aidha, Rais Kikwete amewahamisha wakuu wawili wa mikoa – Ndugu Mwantumu Bakari Mahiza aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Lindi kwenda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga na Ndugu Saidi Magalula ambaye anakuwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa akitokea Mkoa wa Tanga.  Ndugu Magalula anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Ndugu Stella Manyanya anayewania ubunge mkoani Ruvuma pia.  Ndugu Makalla ambaye alipata kuwa Mbunge wa Jimbo la Mvomero, Morogoro na Naibu Waziri wa Maji anach

MAMA SAMIA, NAPE NA MAMA SALMA KIKWETE WAITIKISA LINDI MKUTANO WA KAMPENI

Image
 Mgombea Mwwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akiwa na Mama Salma Kikwete na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Lindi Mzee Mtopa, baada ya kuwasili kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika leo eneo la Mnazi Mmoja mkoani Lindi  Mgombea Mwwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akijadiliana jambo na Mama Salma Kikwete na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Lindi Mzee Mtopa, baada ya kuwasili kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika leo eneo la Mnazi Mmoja mkoani Lindi  Wasanii wa Bongo Movie kina Wema Sepetu wakiwa kwenye mkutano wa kampeni uliofanywa na Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan katika eneo la Mnazi Mmoja mkoani Lindi leo  Aliyekuwa Katibu wa wilaya ya Lindi mjini wa Chadema, Abdalla Madebe ambaye alikuwa ndiye mpigadebe mkubwa wa Mbunge anayemaliza mda wake wa Lindi mjini, maarufu kwa jina la Bwege, akibebwa na wananchi baada ya kutangaza kuhamia CCM, katika mkutano wa kampeni uliofanywa na Mgo