MSAFARA WA MAGUFULI WANUSURIKA TENA KUPATA AJALI

MSAFARA wa mgombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli, umenusurika kupata ajali, baada ya lori la mizigo kuuvamia na kugonga magari matatu likiwamo lililokuwa limembeba mpiga debe wa chama hicho, Amon Mpanju. Ajali hiyo ilitokea jana asubuhi katika eneo la Njia Panda jirani kilomita chache kabla ya kuingia Maswa mjini.Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu, Gemin Mushi jana alikiri kutokea kwa tukio hilo. Alisema wakati msafara huo ukitoka wilayani Meatu, askari polisi waliokuwa wakiuongoza msafara huo walimuaru dereva wa lori hilo lenye namba za usajili T 217 DDY kuegesha pembeni gari lake, lakini alikaidi.āMsafara wa mgombea urais ulikuwa jirani kuingia Maswa, dereva wa lori aliamuriwa kuliweka pembeni akakaidi, tena kibaya akaongeza mwendo hali iliyosababisha ajali. āLori hili ni mali ya Kampuni ya Dilchadri Mill Ltd ya jijini Mwanza, liligonga magari matatu likiwamo gari lenye namba za usajili T 217 CYM aina ya Toyota Land Cruser a...