Posts

WEMA SEPETU NA MTANGAZAJI TV MAIMARTHA JESSE BIFU MWANZO MWISHO, WAFIKISHANA POLISI KISA HIKI HAPA

Image
Staa wa filamu, Wema Sepetu Mwandishi Wetu KUMEKUCHA! Hivyo ndivyo unavyoweza kusema kufuatia mtifuano kati ya mtangazaji maarufu wa televisheni, Maimartha Jesse na staa wa filamu, Wema Sepetu baada ya bifu la wawili hao kufika jeshi la polisi. Akipiga stori na gazeti hili, Maimartha alisema Wema alikuwa na nia ya kumdhalilisha kwani baada ya kumtafuta na polisi na kumkosa, waliamua kumpigia simu na kumuita kituoni Kijitonyama (Mabatini) ambako alisomewa mashtaka ya kumtukana Wema katika mtandao wa kijamii wa Instagram. Mtangazaji maarufu wa televisheni, Maimartha Jesse “Yaani Wema alitaka kunidhalilisha ndiyo maana polisi walikuja kibao kwenye gari lao hapa dukani kwangu na waliponikosa ndiyo wakanipigia simu kwamba niende mwenyewe kituoni, nikaenda nikatoa maelezo yangu ila sasa nitakula naye sahani moja kwani watu wake wanaendelea kunitukana sana mtandaoni nami siwezi kukubali,” alisema Maimartha.

FILIKUNJOMBE APITA BILA KUPINGWA WAPINZANI WAKE WAINGIA MITINI NA FOMU ,MGOMBEA WA CHADEMA ASHINDWA KUJAZA TAREHE NA KUTORUDISHA FOMU MMOJA‏

Image
fomu ya mgombea wa Chadema ubunge Ludewa zikiwa hazijatimia baada ya tomu ya tamko kukosekana Fomu ya mgombea wa Chadema ikiwa haijazwa senemu ya tarehe ,mwezi na mwaka Mzee Kada wa Chadema akimpongeza mbunge wa Ludewa Deo Filikunjombe baada ya kupewa barua ya kupita bila kupingwa Mbunge wa Ludewa Deo Filikunjombe akizungumza na wanachama wa CCM na wananchi wa Ludewa baada ya kupita bila kupingwa Filikunjombe akionyesha barua ya kupita bila kupingwa Msimamizi wa uchaguzi jimbo la Ludewa Bw Wiliam Waziri akimpongeza mbunge Filikunjombe baada ya kumkabidhi barua ya kupita bila kuingwa ubunge jana  Na Matukiodaima Blog ALIYEKUWA mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe (CCM) amepita bila kupingwa baada ya mgombea wa chama cha Demokrasia na maendeleo (chadema) Barthomew Mkinga kushindwa kutimiza Masharti na Taratibu za Ujazaji wa Fomu. Msimamizi wa Uchaguzi Wilaya ya Ludewa Bw Wi...

BONGO LA AIBU: STAA WA BONGO MOVIE RAY AANGUA KILIO MKUMBINI

Image
Msanii wa filamu Vicent Kigosi ‘Ray’ akibembelezwa. BONGE la soo! Katika hali ya kushangaza, msanii wa filamu Vicent Kigosi ‘Ray’ hivi karibuni alijikuta akiangua kilio ukumbini baada ya mshindi wa shindano la kusaka vipaji vya kuigiza kufananishwa na marehemu Steven Kanumba. Tukio hilo lilitokea mwishoni mwa wiki iliyopita katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa, Posta, jijini Dar kulipokuwa na fainali za Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) ambapo washiriki 10 ndiyo walikuwa wakiwania kitita cha shilingi milioni 50. Mara baada ya mshindi wa shindano hilo kutangazwa, ukumbi mzima ulizizima kwa kelele za furaha na kwenda kumpongeza Dennis Laswai aliyeibuka kidedea na wengi walikubaliana kuwa ni haki yake kutokana na kufanya vizuri. Wakati mshindi na mashabiki wake wakiendelea kufurahia ushindi, kundi la vijana lilipanda jukwaani wakiwa wameshika fulana yenye picha ya marehemu Kanumba huku wakisema mrithi wake amepatikana. Ndipo ghafla, Ray ambaye alikuwa na upin...

TUKIO RASMI KATIKA PICHA: LOWASSA NDANI YA DALADALA JIJINI DAR LEO‏

Image
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akisalimiana na Bi. Kulwa Juma ambaye ni mfanyabiashara ndogo ndogo ya kuuza Mihogo ya Kukaanga katika Kituo cha Mabasi cha Gongo la Mboto mwisho, Jijini Dar es salaam leo, wakati alipofanya ziara ya kushtukiza eneo hilo ili kujionea hali halishi ya biashara ndogo ndogo. Mh. Lowassa aliianza ziara yake eneo hilo la Gongo la Mboto na baadae alipanda daladala mpaka Pugu Kajiungeni, jijini Dar.PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akimsikiliza Bi. Kulwa Juma ambaye ni mfanyabiashara ndogo ndogo ya kuuza Mihogo ya Kukaanga katika Kituo cha Mabasi cha Gongo la Mboto mwisho, Jijini Dar es salaam leo. Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akizungumza na vijana wanaoendesha Bodaboda waliokuwep...

MSANII DIAMOND AWAKEBEI UKAWA

Image

Wanachama zaidi ya 500 wa CHADEMA wahamia ACT...Kadi Zachomwa Moto Laivu

Image
Zaidi ya wanachama 500 wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wakiwemo viongozi wa kata mbalimbali katika wilaya ya Ludewa mkoani Njombe, wamekihama chama hicho na kujiunga na chama cha ACT-Wazalendo. Zaidi ya wanachama 500 wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wakiwemo viongozi wa kata mbalimbali katika wilaya ya Ludewa mkoani Njombe, wamekihama chama hicho na kujiunga na chama cha ACT-Wazalendo. Wanachama hao wamefikia maamuzi ya kukihama chama hicho huku wakiwalalamikia viongozi wao wa CHADEMA wilaya na taifa kumkata mgombea wao wa ubunge jimbo la Ludewa waliyemuhitaji Bwana Okol Haule na kumuweka mgombea wanayemuhitaji wao bwana Bathoromeo Mkinga. Mamia ya wanachama hawa kutoka wilaya ya Ludewa, wamefanya maandamano ya amani kutoka mtaa wa Kilimahewa hadi katika ofisi za chama hicho zilizopo mjini Ludewa wakiwa na mabango ya aina mbalimbali yakilaani viongozi wa CHADEMA wilaya na taifa kumkata Okol Haule aliyeshinda katika kura za maoni kug...

ASKOFU ABAKA MWANAFUNZI HUKO SHINYANGA...HIKI NDICHO KILICHOMKUTA!

Image
Askofu wa Kanisa la Tanzania Field Evangelism (TFE) la mkoani Shinyanga, Edson Simon. Mashaka Baltazar, MwanzaDunia imekwisha na kama mti mbichi unatenda haya itakuwaje kwa mti mkavu? Askofu wa Kanisa la Tanzania Field Evangelism (TFE) la mkoani Shinyanga, Edson Simon, amehukumiwa kwenda jela miaka 30 baada ya kupatikana na hatia ya ubakaji wa mwanafunzi katika kesi iliyokuwa ikimkabili.  Askofu Simon alihukumiwa kifungo hicho Agosti 14, mwaka huu na Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Nyamagana mkoani hapa, Martha Mpanze baada ya kujiridhisha na ushahidi wa upande wa mashitaka.  Habari zilizopatikana mahakamani hapo zilieleza kuwa, hukumu hiyo ilisomwa na Abesizya Kalegeya kwa niaba ya Hakimu Mpaze aliyeisikiliza kesi hiyo na kuandaa hukumu hiyo.  Akisoma hukumu hiyo, Kalegeya aliiambia mahakama hiyo kuwa, kulingana na ushahidi uliotolewa na upande wa mashitaka, ulithibitisha mshitakiwa alitenda kosa hilo, kinyume na kifungu cha 130, kifungu...

ASSISTANT MANAGER FINANCIAL PLANNING & ANALYTICS JOB AT TIGO TANZANIA

Image
Providing reporting support to the Business units/Departmental team as well as managing the Financial Planning & Analytics (FP & A) reporting requirements. Key Responsibilities • Drive the budgeting and planning process as well as financial analysis of the commercial team, with key emphasis on subscriber and revenue generating products. • Develop the short and long term forecast (Quarterly) including the preparation and accumulation of appropriate documentation supporting key assumptions and financial information • Analyze key business drivers and revenues, used to develop the detailed budget and short/long term forecast with emphasis on zonal and corporate structure. • Partner with senior management to establish business units and zonal-level budgets. • Preparation of internal reporting of monthly financial data and key business metrics by zones • Preparation of internal reporting of monthly financial data and key business metrics by busin...

BREAKING NEWS: WAZIRI MKUU MSTAAFU FREDRECK SUMAYE AONDOKA CCM NA KUJIUNGA NA CHADEMA

Image
  Waziri Mkuu mstaafu, Fredreck Sumaye (kushoto), akizungumza na wanahabari wakati akitangaza kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), leo mchana.  Waziri Mkuu mstaafu, Fredreck Sumaye (kulia), akipeana mkono na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe Dar es Salaam leo mchana, baada ya kujiunga na chama hicho. Anayeshuhudia katikati ni Mgombea urais wa Tanzania kupitia chama hicho, Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa.  Sumaye akisisitiza jambo Sumaye (wa tatu kulia), akiwa na viongozi wanaunda Umoja wa Katiba (UKAWA) baada ya kuondoka CCM na kujiunga na Chadema. (Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba-0712-727062)

Hali tete Bunda, viongozi Chadema wajiuzulu

Image
Esther Bulaya akiwa na wanachama wa Chadema. SIKU chache baada ya mgombea ubunge wa Jimbo la Bunda Mjini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Esther Bulaya kuteuliwa na chama hicho na kuchukua fomu ya kuwania nafasi hiyo, hali ndani ya chama hicho wilayani  Bunda imekuwa tete. Hatua hiyo inatokana na uamuzi wa aliyekuwa mpinzani wa Bulaya katika kura za maoni ndani ya chama hicho, Pius Masururi, kujitoa katika chama hicho na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM). Tayari Masururi ametangaza kumuunga mkono Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Stephen Wasira katika mbio za ubunge huku viongozi 11 wa Chadema katika jimbo hilo wakisimamishwa uongozi. Inaelezwa kuwa sababu ya kusimamishwa kwa viongozi hao kunatokana na kile kilichodaiwa kuwa kusimamisha wagombea mamluki katika nafasi ya ubunge na udiwani. Akizungumza jana mjini hapa kupitia Redio ya Kijamii ya Mazingira FM,  Masururi alitangaza kujiunga na CCM jana muda mfupi kabla ya kuondoka ...

DIAMOND PLATNUMZ NOMA SANA...AMDAKA NEYO NAIROBI NA KUFANYA NAYE COLLABO MOJA MATATA SANA

Image
Huwa nawashangaa sana wanao semega eti Diamond ni freemanson wakati juhudi zake za kupita kiasi zinaonekana ..Unaambiwa Neyo amekuja kufanya Coke Studio na Kiba ila Diamond hapo hapo akachukua fursa bila kupoteza muda na kumburuza NEYO studio kutoa kitu kipya..ANGALIA PICHA HIZO USHAHIDI WAKIWA STUDIO NA SHEDDY CLEVER YULE PRODUCER WA NGOLOLO.. Hahah Natumaini kiba na yeye atakamata fursa...ole wako urudi bongo bila collabo

Wema avunja ndoa

Image
Wema Isaac Sepetu. Waandishi wetu H ALI si shwari kwenye familia ya Kampuni ya Endless Fame Productions kufuatia madai mazito yanayomgusa mkurugenzi wake, Wema Isaac Sepetu akihusishwa na kuvunjika kwa ndoa ya mdogo wa mkali wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ almaarufu kwa jina la Esma Platnumz aliyeolewa na Hamad Manungwa ‘Petit Man’. Mdogo wa mkali wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ almaarufu kwa jina la Esma Platnumz akiwa na mume wake  Hamad Manungwa ‘Petit Man’ siku walipofunga ndoa. MAI NDANI Katika sakata hilo, mtangazaji maarufu Bongo, Maimartha Jesse ‘Mai’, Esma na Mtangazaji Nasra Rajesh ‘Lady Naa’ wanadaiwa kuunda kundi lenye lengo la kuwasuta wezi wa waume za watu (Wema aliwekwa kwenye tageti) lililopewa jina la Al-Shabaab. Esma Platnumz akiwa na mume wake  Hamad Manungwa ‘Petit Man’. Wakati mpango huo ukiendelea, Mai anadaiwa alielezea mkasa wa kuvunjika kwa ndoa ya Esma na Petit Man kwenye Ins...

SHUHUDIA DK. MAGUFULI ALIVYORUDISHA FOMU ZA URAIS NEC LEO

Image
  Mgombea urais kupitia CCM Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Damiani Lubuva, wakati alipowasili ofisi hizo. …Akiwa na mgombea mwenza, Samiah Hassan Suluhu. Viongozi wa CCM waliomsindikiza mgombea wao wa urais. Lubuva (kulia) akizungumza jambo wakati wa kurudisha fomu hizo. Magufuli akionyesha fomu wakati wa kurudisha. Mgombea urais kupitia CCM Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na wanahabari baada ya kurudisha fomu. Wanahabari wakiwa kazini katika hafla hiyo. Magufuli akitoka ofisi za NEC baada ya kukamilisha zoezi hilo. MGOMBEA urais kwa tiketi ya CCM, John Pombe Magufuli, leo amerudisha fomu ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC). NEC iliwataka wagombea wote wa urais kupitia vyama vyote vya siasa kurudisha fomu leo Agosti 21 baada ya kuzunguka mikoa ya Tanzania kutafuta wadhamini, ambapo vyama vyote hivyo viwili vimeonekana kukidhi vigezo na kurudisha fomu hizo. (PICHA: DENIS MTIM...