Posts

WAKIONGOZWA NA LIONEL MESSI, BARCELONA WACHAPWA

Image
Mabingwa wa Ulaya, FC Barcelona wamepoteza kwa kipigo kikali mechi ya kwanza ya Spanish Super Cup dhidi ya Athletico Bilbao. Wakiongozwa na mchawi wao, Lionel Messi, Barca wamedundwa 4-0. Aritz Aduriz ameingia kwenye vitabu vya kumbukumbu vya mashabiki wa Barcelona kufuatia kupiga mabao matatu peke yake 'Hat-trick' katika dakika za  53, 62, 68, huku Mikel San Jose naye akifunga goli moja dakika ya 13 kipindi cha kwanza. Nyota anayewaniwa na Manchester United, Pedro alianza kikosi cha kwanza, lakini alishindwa kabisa kupenya ngome ya Bilbao. Aduriz akicheka na nyavu Wakitokea kushinda 5-4 dhidi ya Sevilla katika mechi ya fainali ya Uefa Super Cup iliyochezwa kwa dakika 120, kocha wa Barca, Luis Enrique hakuwaanzisha  Gerard Pique, Sergi Busquets, Andres Iniesta na Ivan Rakitic. Wakati huo tayari alikuwa anawakosa wachezaji wanaosumbuliwa na Majeraha, Jordi Alba na Neymar. Ili kupindua kichapo hicho, Barcelona wanahitaji kushinda 5-0 nyumbani Ca

TAZAMA PICHA ZA MAPOKEZI YA LOWASA MBEYA

Image
Kutoka mbeya  hizi ni picha za awali kabisa za mapokezi ya mgombea wa UKAWA Edward lowasa wakati anaenda kutafuta wadhamini,Tizama hii.Picha nyingine zitakujia Mgombea Urais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa Ukawa kwa tiketi ya Chadema Mhe.Edward Lowassa akisalimiana na viongozi mbalimbali wa Ukawa baada ya kutua Jijini Mbeya leo kwa lengo la kujitambulisha .. Wapenzi wa Ukawa Jijini Mbeya wakati wa shamrashamra za kumpokea Mgombea Urais wa Ukawa kupitia Chadema Mhe. Edward Lowassa ambaye ametua Jijini humo leo.  Mgombea Urais wa UKAWA Kupitia CHADEMA Leo atakuwa Jijini Mbeya kwa ajili ya kutambulishwa na kusaka wadhamini. Hapa kuna picha kadhaa za shamrashamra za wananchi wakimsubiri kwa hamu kubwa uwanja wa ndege wa Songwe.

TCRA YATOA ADHABU KALI KWA TELEVISION YA ITV KWA HABARI ZA UONGO

Image
1.0 Utangulizi: Mnamo tarehe 10/08/2015, kituo cha ITV kilikiuka Kanuni za Huduma ya Utangazaji (Maudhui), 2005 kupitia kipindi cha Habari Zilizotufikia Hivi Punde kilichorushwa hewani kati ya saa 2.30 asubuhi hadi saa 5.30 asubuhi. Kipindi hiki kilikiuka Kanuni za Utangazaji kwa kutoa taarifa zisizo za kweli na za kichochezi zilizotangaza kwamba Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limepiga marufuku maandamano ya mgombea wa CHADEMA Mheshimiwa Edward Lowassa. Taarifa hiyo ilikuwa na maandishi yaliyosomeka kama ifuatavyo:- 1. “ Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam lapiga marufuku maandamano ya kumsindikiza kuchukua fomu mgombea Urais kupitia CHADEMA”. 2. “ Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam lakanusha kupiga marufuku maandamano kutokea ofisi za CUF kuchukua fomu Mgombea Urais kupitia CHADEMA. Katika kuhitimisha taarifa hiyo mtangazaji alisikika akisisitiza kwamba Kamishina Suleiman Kova alisema ni marufuku maan

RAIS KIKWETE AMZIKA KISUMO MWANGA

Image
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe mama Salma Kikwete wakitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza la Kada Mkongwe wa CCM  Marehemu Mzee Peter Kisumo wakati wa ibada ya mazishi iliyofanyika huko kijijini kwake Usangi- Mwanga Mkoani Kilimanjaro leo. Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimfariji Mama Hosiana Kisumo Mke wa Marehemu Peter Kisumo wakati wa mazishi yake huko Usangi Mwanga Mkoani Kilimanjaro. Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakiweka udongo katika kaburi la Kada Mkongwe wa CCM Marehemu Peter Kisumo wakati wa mazishi yaliyofanyika nyumbani kwake Usangi- Mwanga Mkoani Kilimanjaro. Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisaini kitabu cha maombolezo kilichowekwa kanisani wakati wa mazishi ya kada mkongwe wa CCM Mzee Peter Kisumo yaliyofanyika kijijini kwake Usangi-Mwanga Mkoani Kilimnjaro. (Picha na Freddy Maro)

ALICHOKISEMA PROF LIPUMBA BAADA YA KUREJEA NCHINI

Image
Dar es Salaam. Aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahimu Lipumba alirejea nchini jana jioni akitokea Kigali, Rwanda alikokwenda mara tu baada ya kujiuzulu wadhifa huo siku nane zilizopita. Profesa Lipumba aliwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIA) saa 10.10 jioni kwa ndege ya Rwanda Air. Akihojiwa na Azam Tv kwa simu akiwa Kigali, siku tatu baada ya kuondoka nchini, Profesa Lipumba alisema alikuwa nchini humo akifanya utafiti kuona namna gani Tanzania inaweza kujifunza mambo ya kiuchumi kutokana na nchi hiyo kupiga hatua kubwa katika sekta hiyo. Alipoulizwa jana, Profesa Lipumba alisema akiwa huko alikuwa na mazungumzo na Bodi ya Maendeleo ya Rwanda (RDB), wadau wa masuala ya rushwa, waziri wa fedha wa nchi hiyo na makamu mwenyekiti wa Bodi ya Utawala. “Wenzetu wamepiga hatua kubwa katika kukuza uchumi ndani ya kipindi kifupi, hivyo safari yangu ilikuwa ya kujifunza mbinu walizotumia kufikia malengo yao,” alisema.

ANGALIA PICHA LOWASSA ALIVYOWASILI MBEYA MUDA HUU

Image
Mgombea Urais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa Ukawa kwa tiketi ya Chadema Mhe.Edward Lowassa akisalimiana na viongozi mbalimbali wa Ukawa baada ya kutua Jijini Mbeya leo kwa lengo la kujitambulisha .. Wapenzi wa Ukawa Jijini Mbeya wakati wa shamrashamra za kumpokea Mgombea Urais wa Ukawa kupitia Chadema Mhe. Edward Lowassa ambaye ametua Jijini humo leo.    CHANZO:  http://www.ajiratz.info/2015/08/angalia-picha-lowassa-alivyowasili.html

MAJINA YA WALIOTEULIWA UBUNGE, UWAKILISHI NA VITI MAALUM CCM YATANGAZWA RASMI

Image
 Mwenyekiti wa CCM Taifa ,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete akionyesha kitabu cha Ilani ya Uchaguzi ya 2015-2020 ya CCM wakati wa kufunga kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa mara baada ya kumaliza zoezi la kupitisha majina ya wagombea Ubunge na Uwakilishi mjini Dodoma.Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar) Dk. Ali Mohamed Shein na kulia ni Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.  Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk.John Pombe Magufuli akipitia orodha ya majina ya waliopendekezwa kwenye nafasi za Ubunge na Uwakilishi,kulia ni Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe.Mizengo Pinda. MNEC wa Wilaya ya Lindi mjini Mama Salma Kikwete akipitia kitabu cha ilani ya Uchaguzi ya CCM kitakachotumika kwa mwaka 2015-2020.  Dk. Salim Ahmed Salim akipitia majina ya walioteuliwa wakatia wa kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM mjini Dodoma.  Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma ambapo alit

FAHAMU HUU UMUHIMU WA MASSAGE KWA MWILI WAKO

Image
Je, kuna siku umewahi kuamka asubuhi na kujikuta ukiwa mchovu sana kupita kiasi? hivi ulihisi nini baada ya kuamka hivyo? Je, ulihisi una kahoma kidogo? au uliwaza huenda ni uchovu wa kazi za jana yake? naamini kuna mengi ulijiuliza na huenda hukupata jibu la uhakika. Kwa kawaida huwa kuna sababu nyingi za mtu kuamka akiwa mchovu wa mwili, miongoni mwa sababu hizo ni pamoja na uchovu wa kazi, michezo n.k. Lakini unaweza kuepukana na hili suala la kuamka na uchovu endapo tu utajenga utaratibu wa kupata huduma ya kukandwa ( massage ) mwili kila baada ya muda fulani. Huduma hii ni vyema ukafanyiwa na mwezi (mke au mume) wako nyumbani ikiwa unahitaji kufanya kwa lengo la kuweka mwili wako sawa  sawa tu. Mtaalam wa masuala ya 'massage' kutoka Mandai Herbalist Clinic Mathayo Masinema Bahebe anasema kuwa massage husaidia kupunguza na kuondoa maumivu yote ya mwili pamoja na kurekebisha mzunguko wa damu mwilini na kuweka sawa sehemu zote za maungio ya mifupa 

TONTO DIKEH AOLEWA, ABADILI JINA INSTAGRAM

Image
Muigizaji kiwango kutoka Nigeria, Tonto Dikeh. Lagos ,NIgeria MUIGIZAJI kiwango kutoka Nigeria, Tonto Dikeh ameolewa rasmi na aliyekuwa mpenzi wake, Churchill Olakunle Oladunni wiki iliyopita.Tarifa za kuolewa zilianza kuzagaa mapema wiki iliyopita baada ya staa huyo kubadili jina lake kwenye Mtandao wa Kijamii wa Instagram na kujiita, Mrs Tonto Wigo Dikeh-Churchill. Lakini wikiendi iliyopita zilizagaa picha mitandaoni zikimuonyesha staa huyo akiwa na mumewe huyo mpya lakini kubwa zaidi ni ile ambayo amepiga na bibi yake wakiwa wanapongezwa kwenye sherehe hiyo. Tayari inadaiwa kuwa Tonto ni mjamzito na bibi yake huyo ameonekana kuumia zaidi baada ya kudai kuwa anamuacha peke yake kwani alizoea kuishi naye lakini amemtakia maisha mema na mumewe huyo.

BREAKING NEWZZ..BAADA YA KAMATI KUU CCM KUFUTA MATOKEO MAJIMBO MATANO,HII NDIYO KAULI NZITO YA MEYA JERRY SILAA WA UKONGA

Image
Mungu hamtupi mtu mwenye dhamira ya kweli, hawezi shindwa hawezi kata tamaa... Wana CCM jimbo la Ukonga tukutane kwenye matawi ya CCM kesho kutwa tarehe 13 tuchague Mbunge wa CCM tunayemtaka NINI MAONI YAKO NDUGU

KAMATI KUU YA CCM LEO MJINI DODOMA

Image
  Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akifungua kikao cha Kamati Kuu ya CCM, leo Agosti, 11, 2015 katika ukumbi wa Jengo la White House Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM, Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein na kulia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Philip Mangula na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.     Kikao cha Kamati Kuu ya CCM, leo Agosti, 11, 2015 katika ukumbi wa Jengo la White House Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma.    Wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Steven Wasira na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye na Adam Kimbisa wakibadilishana mawazo kabla ya kuanza kikao cha Kamati Kuu ya CCM leo mjini Dodoma.   Wajumbe wa Kamati Kuu, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye na Adam Kimbisa na Dk. Emmanuel Nchimbi, wakibadilishana mawazo kabla ya kuanza kikao cha Kamati Kuu ya CCM leo mjini Dodoma.   Wajumbe wa Kamati Kuu, Dk. Maua Daftari na Samia Suluhu Hassan, wakibadilishana mawazo ukumbini,

Wema Aibu mpya! Anaswa na mwanaume hotelini

Image
Wem Sepetu ‘Madam’ akidendeka na mwanaume  mwenye asili ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), wakiwa kwenye Mgahawa wa hoteli  iliyopo Msasani jijini Dar. Mwandishi wetu Licha ya kudai kwamba skendo za ngono sasa basi, staa wa sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ amekwaa aibu mpya baada ya picha zake kunaswa akiwa na mwanaume mwingine kwa mara nyingine, mwenye asili ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), wakiwa kwenye Mgahawa wa hoteli iliyotajwa kwa jina la Cape-town Fish Market iliyopo Msasani jijini Dar. Wakiendelea kufanya yao. MADAI MAZITO Chanzo chetu ambacho ni makini kilipenyeza kuwa, katika tukio hilo la hivi karibuni, staa huyo alikuwa hafahamiani na mwanaume huyo, lakini kuna kijana mmoja ambaye mara nyingi anawakuwadia mastaa wa Bongo kwa matajiri, alidaiwa kumtonya Wema kuwa kuna ‘mchati’ anataka kutoka naye. Kilifunguka kwamba, baada ya Wema kung’atwa sikio juu ya Mkongomani ambaye ana ‘hela chafu’, alidaiwa kuonekana kuchach