WEMA, AUNT KIMENUKA KISA ZARI
KIMENUKA! Mashosti wa kufa na kuzikana, Wema Isaac Sepetu na Aunt Ezekiel Grayson wanadaiwa kugombana baada ya Aunt ‘kuposti’ kwenye ukurasa wake wa Instagram tangazo lililohusiana na pati ya mwandani wa mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ iliyofanyika Mlimani City jijini Dar wikiendi iliyopita. Mashosti wa kufa na kuzikana, Wema Isaac Sepetu na Aunt Ezekiel Grayson. Kwa mujibu wa mtu wa karibu wa mastaa hao wa sinema za Kibongo, baada ya Aunt kuposti tangazo hilo akiwalaumu watu wa mtandao wa huduma za simu waliomtumia ndipo Wema akaona na kuja juu. Ilielezwa kwamba baada ya Aunt kutupia picha ya tangazo hilo, Wema alichukizwa na kitendo hicho huku akimuona Aunt kuwa amemsaliti. Aunt Ezekiel Grayson. Ilisemekana kwamba katika utetezi wake, Aunt hakupendezwa na tangazo hilo alilotumiwa na mtandao huo wa simu. “Wema alivyoona alichukia na kusema Aunt alikuwa akimsaliti na...