Posts

Haya ndiyo madhara ya kuitana 'Sweet, Dear, Baby' kwenye mapenzi

Image
BABY ni neno la Kiingereza lenye maana ya mtoto, tena mara nyingi linatumika kwa mtoto mdogo. Pia lina maana nyingine ya mpenzi. Ni neno maarufu sana siku hizi; hata wazee kabisa, utasikia wanaitana baby! Mbali na hilo, yapo maneno mengine kama sweet, dear, honey na mengine mengi. Maneno yote hayo ya Kiingereza, yana maana zaidi ya moja, lakini kubwa zaidi ni kumaanisha mpenzi, mpendwa (hutumika katika kuonesha mapenzi ya dhati kwa mwingine). Leo nataka kukupa kitu kipya kabisa kichwani mwako. Unahitaji utulivu wa hali ya juu ili kujifunza hili. Ni maneno mazuri sana, ya kipekee lakini kwa upande mwingine ni hatari kwa sababu hukaribisha matatizo ambayo hayakutarajiwa na mtumiaji. HUTUMIKA WAPI HASA? “Dear, naomba uniamshe saa 12:00 asubuhi, kesho nina vikao vingi sana asubuhi,” inaweza kuwa kauli ya mume akimwambia mkewe, ambaye naye anamjibu: “Sawa sweet, usijali.” Kwa hakika ndipo sehemu sahihi zaidi kutumika. Ni maneno yenye mshawasha mkubwa na huonesha pe

BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI(NACTE)LINAKARIBISHA MAOMBI YA KUJIUNGA NA UALIMU 2015/2016

Image
Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) Dkt. Primus Nkwela (kushoto) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) kwenye Makao makuu ya ofisi hizo  Mikocheni B jijini Dar es Salaam, Wakati akiutangazia Umma juu ya kukaribisha maombi ya kujiunga na mafunzo ya Ualimu kwa mwaka wa masomo 2015/2016 kwa vijana waliomaliza kidato cha Nne  Oktoba 2014. na wengine wenye sifa mbalimbali  kama zinavyopatikana kwenye  tovuti ya baraza hilo: www.necte.go.tz.Waombaji  ; watakao omba kabla ya tarehe 10 Aprili 2015 wataruhusiwa kujiunga  na mafunzo mnamo Aprili 15 2015 kwenye vyuo mbali mbali kama vinavyopatikana kwenye tovuti yao.Kulia ni Katibu msaidizi wa Baraza hilo Ramadhani Samainda. Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) Dkt. Primus Nkwela (kulia) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari pichani katika Makao makuu ya ofisi hizo  zilizopo Mikocheni B jijini Dar es Salaam, waka

SYLVESTRE MARSH AAGWA JIJINI DAR

Image
Padre akiongoza ibada ya kuaga mwili wa aliyekuwa kocha msaidizi wa timu ya Taifa, Taifa Stars, Sylvestre Marsh. Waombolezaji wakifuatilia ibada ya kumuaga Marsh katika Hospitali ya Taifa Muhimbili. Mhariri Kiongozi wa Magazeti ya Michezo ya Championi, Saleh Ally akiaga mwili wa kocha Marsh. Wadau mbalimbali wakiuaga mwili wa Sylvestre Marsh. Mwili wa Marsh ukitolewa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili. Mapaparazi wakichukua matukio wakati wa zoezi hilo. Mwili wa Marsh ukiwa tayari kupelekwa kwenye gari. ALIYEKUWA kocha msaidizi wa timu ya Taifa, Taifa Stars, Sylvestre Marsh, ameagwa leo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam. Marsh aliyefariki dunia jana, alikuwa amelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili baada ya kuugua maradhi ya saratani ya koo kwa muda mrefu. Awali alilazwa hapo akapata nafuu na kupelekwa kwao Mwanza, lakini wiki iliyopita alirudishwa tena na ndipo umauti ulipomku

ZITTO AKABIDHI AMBULANCEA JIMBONI KWAKE

Image
Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe jana March 14 ametoa gari mpya ya kubebea wagonjwa (Ambulance)kama moja ya ahadi zake alipokuwa kwenye kampeni ambapo aliahidi kabla ya kumaliza kipindi cha uongozi wake atatoa gari hiyo. Wakipokea msaada huo Michael Mwandezi ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Kigoma pamoja na Hamis Said Betese ambaye naye ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma ambapo kwa niaba ya wananchi wa kata ya Nyarubanda ambao ndio msaada huo wamemshukuru sana Mbunge Zitto Kabwe.  Hata hivyo kabla ya kuelekea kukabidhi Gari hiyo ya kubebea wagonjwa,Zitto Kabwe aliwatembelea Wanachama wa Chama cha Ushirika Rumaco ambao wanajishughulisha na kilimo cha Kahawa kutoka kijiji cha Matyazo Kigoma Kaskazini.  Hapa Zitto akiwa kwenye shamba lake la kahawa

KOCHA MARSH AFARIKI DUNIA

Image
Aliyekuwa kocha msaidizi wa timu ya Taifa, Taifa Stars, Sylvestre Marsh enzi za uhai wake. ALIYEKUWA kocha msaidizi wa timu ya Taifa, Taifa Stars, Sylvestre Marsh, amefariki dunia asubuhi ya leo. Marsh alikuwa amelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili baada ya kuungua maradhi ya saratani ya koo kwa muda mrefu, awali alilazwa hapo akapata nafuu na kupelekwa kwao Mwanza, lakini wiki iliyopita alirudishwa tena na ndipo umauti ulipomkuta. Sylvestre Marsh enzi za uhai wake akiwa na Kim Poulsen. Marsh ambaye aliwahi kuipa mafanikio makubwa klabu ya Kagera Sugar, amewahi kufundisha soka kwa mafanikio makubwa sana hapa nchini kuanzia mwaka 2003, alipokuwa kocha msaidizi wa timu ya vijana, chini ya Abdallah Kibadeni. Mwaka 2006, alipandishwa timu ya wakubwa na kuwa kocha msaidizi chini ya Mbrazil Marcio Maximo na baadaye akawa chini ya Wadenish, Kim Poulsen na Jan Poulsen. Hata hivyo, tangu mwaka jana kocha huyo

PAPA FRANCIS ATOA ISHARA ZA KUJIUZULU

Image
Papa Francis na alyiekuwa papa Benedict Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis amedokeza kwamba huenda akafuata nyayo za mtangulizi wake Papa Benedict kwa kujiuzulu.Akihojiwa na runinga moja ya nchini Mexico katika sherehe za maadhamisho yake ya pili tangu achaguliwe,Papa Francis amesema kuwa anahisi kwamba uongozi wake katika kanisa hilo hautaendelea kwa kipindi kirefu. Amesema kuwa hatua ya Benedict kujiuzulu mwaka 2013 ni ya ujasiri na haifai kuchukuliwa kama ya kipekee.Papa Benedict ndiye kiongozi wa kwanza wa kanisa hilo kujiuzulu tangu papa Gregory wa 12 mwaka 1415. Papa Francis anasema kuwa anatamani maisha yake ya kuwa muhubiri na angependelea kuzuru maeneo kadhaa bila kujulikana. CHANZO BBC

SIMBA SC WAICHAPA MTIBWA SUGAR BAO 1-0 TAIFA,OKWI AWAPA RAHA

Image
Wachezaji wa Simba SC wakimpongeza Okwi leo baada ya kufunga bao pekee la ushindi dakika za lala salama dhidi ya Mtibwa Sugar Na Mahmoud Zubeiry BAO la Emmanuel Anord Okwi dakika ya 90 ushei limeipa Simba SC ushindi wa 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam jioni hii katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara. Simba SC sasa inafikisha pointi 29 baada ya mechi 18 na kuendelea kukamata nafasi ya tatu, nyuma ya mabingwa watetezi, Azam FC pointi 30 za mechi 16 sawa na vinara Yanga SC, wenye pointi 31. Okwi alifunga bao hilo, wakati tayari baadhi ya wapenzi wa Simba SC wameanza kutoka uwanjani, wakiamni matokeo ni sare.  Mganda huyo, alifunga baada ya kupata pasi ya Abdi Banda na kumchambua vizuri kipa aliyefanya kazi nzuri leo, Said Mohamed Kasarama. Emmenuel Okwi akimtoka beki wa Mtibwa Sugar, Said Mkopi katika mchezo wa leo Beki wa Simba SC, Hassan Kessy akimtoka kiungo wa Mtibwa Sugar, Shaaban Nditi  Mch

HAPENDWI MTU INAPENDWA POCHI...JANGA LINALOVUNJA NDOA!

Image
NImatumaini yangu wapenzi wasomaji wa safu hii mko poa na mnaendelea na majukumu yenu ya kila siku. Tumshukuru Mungu kwa kutuwezesha kufika siku ya leo na kuweza kuperuzi ukurasa huu muhimu wa kuzungumzia masuala ya uhusiano. Leo napenda nizungumze nanyi kuhusu mada iliyopo hapo juu. Kwa uchunguzi mdogo nilioufanya, inaonekana ndoa zilizofungwa miaka ya 80 kurudi nyuma zilikuwa na uhai mrefu kuliko miaka ya juu ya hapo. Ndoa miaka ya hivi karibuni zimekuwa zikisuasua, hazina umri mrefu. Watu wanaingia kwenye ndoa kwa kufuata kitu flani mbele ya safari kikitoweka, hayupo tayari kuvumilia, unakuwa ugomvi na ndoa kuvunjika. Wazee wetu walifunga ndoa kwa kufuata misingi ya ndoa. Kigezo cha fedha hakikupewa nafasi kubwa katika mapenzi, walitazama zaidi suala la maisha ya kusaidiana na matakwa ya Mungu katika sheria za ndoa. Mume alijua wajibu wake kama baba wa familia lakini mke pia alijua wajibu wake ndani ya familia. Kila mmoja alifuata kiapo alichokula siku ya ndo

THIS IS WHAT THE MOST CONTROVERSIAL COUPLE IN EAST AFRICA,ZARI AND DIAMOND WILL BE DOING IN KENYA

Image
After making their relationship public and official, Zari and Diamond have been the trending topic on most social media platforms. Their 15 year age difference and the fact that Zari is currently heavy with diamond’s child has made their story even more intriguing. Amazingly, they have managed to silence their critics, their relationship has continued to flourish though many had predicted it was a passing fling. The couple is expected to jet into the country soon to attend the Art of Luxury event that will be hosted by Zari and Huddah Monroe on the 21st of March 2015. Diamond will be performing at the event and a number of DJ’s including DJ Namonsky, DJ Crème de la Crème, DJ Pierra and DJ Incredible will be show casting at the event which will be held at the Skyluxx lounge. Can’t wait to see how everything will goes down.

ANGALIA JINSI ZITTO ALIVYOITEKA KIGOMA,MAPOKEZI YAKE YASHTUA WENGI

Image
Mh zitto kabwe baada ya chama chake cha CHADEMA kutangaza kumfukuza uanachama ndani ya chama hicho ameamua kufanya ziara ya siku tatu ndani ya kigoma kuzumgumza na wananchi wake juu ya hali ya kisiasa inayomkabili kwa sasa,hizi hapa ni baadhi picha za mapokezi yake kigoma  Ikiwa bado sakata la kufukuzwa uanachama kwa mbunge wa kigoma kaskazini (CHADEMA) mh ZITTO KABWE linaendelea kuchukua nafasi katika vichwa vya watanzania na wapenda siasa,mbunge huyo ameanza kufanya ziara ya siku tatu jimboni kwake kuzungumza na watanzania mbalimbali. Akiwa katika ziara yake MBUNGE wa Kigoma Kaskazini,Zitto Kabwe(Chadema),amewataka wakazi wa mkoa wa kigoma wasisikitishwe na mambo yanayomkabili kwa sasa kwa kile alichoeleza kuwa asilimia kubwa ya wanasiasa makini walishapitia misuko suko kama yake. Amewaeleza kuwa jambo la msingi ni kumuunga mkono katika hatua yoyote atakayochukua kwa ajili ya wanakigoma na Taifa kwa ujumla katika kumaliza mgogoro uliopo bai

WEMA: MUME WA ZARI ANATAKA KUNIOA

Image
MAMBO hadharani! Supastaa wa Bongo, Wema Sepetu ‘madam’ ameanika siri zilizojificha nyuma ya pazia kati yake na aliyekuwa mume wa mwanamuziki nyota wa Uganda, Zarina Hassan ‘Zari’, Ivan Semwanga, kuwa anataka kumuoa, Risasi Jumamosi lina full stori. Supastaa wa Bongo Movie, Wema Sepetu ‘madam’. WALIANZIA KUKUTANA SAUZ Katika mazungumzo yake exclusive na mwanahabari wetu juzi jijini Dar, Wema alianza kwa kuweka bayana kwamba, mawasiliano yake na Ivan yalianzia nchini Afrika Kusini wakati alipokwenda kikazi, Februari, mwaka huu. “Nilikwenda na Ommy Dimpoz (Faraj Nyembo). Tulikuwa na project yake lakini tulipokuwa kule, Ivan na marafiki zake walisikia kuwa mimi nipo, wakatuomba sana kupitia kwa wenyeji wetu kuwa wanataka kutuona na kutoka nao out pamoja.” ALIBANA, AKALEGEZA “Mimi nilikuwa bize sana na kazi zangu, awali niliwaambia kuwa hatutaweza lakini baadaye walitubahatisha klabu, wakaomba kukaa na sisi, mwish

KISA BWANA, PENNY ADAIWA KUNYWA SUMU

Image
Stori: MWANDISHI WETU/Risasi MTANGAZAJI maarufu Bongo na aliyekuwa mpenzi wa Nasibu Abdul ‘Diamond’, Penniel Mungilwa ‘Penny’ amedaiwa kunywa sumu kufuatia kunyang’anywa bwana na shosti yake aliyefahamika kwa jina la Diana. Mtangazaji maarufu Bongo na aliyekuwa mpenzi wa Nasibu Abdul ‘Diamond’, Penniel Mungilwa ‘Penny’. Kwa mujibu wa chanzo, Penny na Diana walikuwa marafiki lakini wakatofautiana baada ya Diana kumteka akili mwanaume wa rafiki yake huyo na kumkoleza mapenzi hadi kufikia hatua ya kumtangazia ndoa. “Diana kampagawisha mwanaume wa watu, jamaa akatangaza ndoa na hivi ninavyokwambia siku siyo nyingi Diana anaolewa hicho ndicho kikasababisha Penny apandwe na presha hadi kufikia hatua ya kunywa sumu, alikimbizwa hospitali, akalazwa lakini sasa ametoka anaendelea vizuri,” kilisema chanzo hicho. Baada ya kuzinyaka habari hizo, mwanahabari wetu alimtafuta Penny ili kujua anazungumziaje habari hizo za kunywa sumu hadi kulazwa hospitali ambapo alikanusha mad

ZITTO KABWE ALIVYOVULIWA UBUNGE WA KIGOMA KASKAZINI

Image
Mnadhimu Mkuu Kambi ya Upinzani Bungeni, Tundu Lissu, akitoa tamko la kumvua uanachama Zitto Zuberi Kabwe leo. Waandishi wa habari wakifuatilia tukio hilo. Lissu akitoa ufafanuzi baada ya kuulizwa maswali na wanahabari. Katibu Mkuu wa Chadema Willbroad Slaa (kulia) akifuatilia mkutano huo wa kumvua uanachama Zitto Kabwe.MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zuberi Zitto Kabwe, amevuliwa uanachama wake mchana huu katika ofisi za Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) jijini Dar es Salaam katika hatua iliyotangazwa na mnadhimu mkuu wa chama hicho, Tundu Lissu, baada ya mbunge huyo kushindwa kesi iliyokuwa amefungua katika Mahakama Kuu ya Tanzania. Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi hizo, Lissu alisema Zitto amefutwa uanachama kwa mujibu wa taratibu na sheria ya chama isemayo kwamba endapo mwanachama atapata tatizo lolote binafsi ama la kichama, malalamiko yote yatasuluhishwa ndani ya chama na si mahakamani. “Hivyo, kwa mujibu