KIONGOZI wa vijana waliopata mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), waliokuwa wakiishinikiza Serikali kuwapatia ajira, George Mgoba, amelazwa katika Hospitali ya Amana, jijini Dar es Salaam, baada ya kutekwa nyara na kisha kuteswa na watu wasiojulikana. Mgoba ni miongoni mwa vijana waliowawakilisha wenzao zaidi ya 300 kukutana na viongozi wa juu wa Serikali hivi karibuni, akiwemo Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, kuzungumzia kilio chao na kupinga upendeleo wa ajira ndani ya Jeshi. Tukio hilo ambalo kwa kiasi kikubwa linafanana na kile alichofanyiwa Mwenyekiti wa Chama cha Madaktari nchini, Dk. Steven Ulimboka au Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya New Habari (2006) Ltd, Absalom Kibanda, lilimfika Mgoba Jumatatu wiki hii saa 11:00 jioni. Mgoba, ambaye analindwa na vijana wenzake waliomaliza mafunzo ya JKT katika wodi namba saba aliyolazwa, anadai kufanyiwa vitendo vya kinyama ikiwa pamoja na kuchomwa sindano ambayo haijul...