Posts

ASKARI WA JWTZ AUAWA KINYAMA, VIUNGO VYA MWILI WAKE VYANYOFOLEWA IKIWEMO SEHEMU ZA SIRI

Image
Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Kikosi cha 27 Makoko kilichopo Musoma, Praiveti Wilfred Koko amekutwa ameuawa na kuondolewa sehemu ya viungo vya mwili katika eneo la kikosi hicho. Taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi mkoani Mara ilisema askari huyo MT-78227, aliokotwa katika eneo la jeshi Januari 30, mwaka huu saa sita mchana mwili wake ukiwa hauna baadhi ya viungo ukiwemo mguu wa kulia, viganja vya mikono yote na sehemu za siri. Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Ernest Kimola, alisema upande wa mguu wa kushoto wa marehemu ulikutwa na jeraha lililokatwa na kitu chenye ncha kali hali inayoonyesha huenda askari huyo aliuawa na kutupwa kwenye eneo hilo. Alisema huenda viungo vya askari huyo ambavyo havikukutwa vilikuwa vimeliwa na wanyama baada ya mwili huo kuonekana kukaa muda mrefu, kuanza kuharibika na kuingiliwa na wadudu.

HII NDIO JEURI YA PESA YA LADY JAY DEE!

Image
Msanii akishafanikiwa kuwashawishi mashabiki kulipa kiingilio na kuingia kwenye show yake, hana kazi ya ziada zaidi ya kufanya show nzuri ambayo huwafanya mashabiki wenyewe kuingia tena mifukoni na kuwatunza kwa misimbazi ya kutosha.Lady Jaydee kupitia Instagram ametuonesha noti za msimbazi ambazo alitunzwa jukwaani na mashabiki waliohudhuria show yake ya jana pale MOG. Kwenye picha hiyo ameandika:  “Asanteni wote mlionitunza jukwaani Nilitoka kwetu na alfu 6 Nikarudi mkoba umejaa  Kazi ya muziki nzuri jamani Ila Haka ka mkoba jana @niitesonga alikuwa anataka kuka kwapua Mi mwenyewe nna madeni kibao Nawaza nianze lipi kulilipa “

MWANAMKE ALIYECHINJWA NA MPENZI WAKE MPAKA KUFA -MANZESE FRIEND CORNER [SAMAHANI KWA PICHA HIZI]

Image
Mwili wa Msichana anaedaiwa kuchinjwa na mpenzi wake mtuhumiwa akiwa chini ya ulinzi Mwili wa Msichana anaedaiwa kuchinjwa na mpenzi wake juzi jioni maeneo ya Manzese Friends Corner ukitolewa katika eneo la tukio Kijana anaetuhumiwa kumchinja mpenzi wake sababu ya wivu wa mapenzi akiwa amepandishwa katika gari la Polisi akipelekwa kituoni huku akitokwa na damu shingoni baada ya kujaribu kujiua kwa kutumia kisu bila ya mafanikio. Email This BlogThis! Share to Twitter Share to Facebook

CHECK OUT THE BODY ON MISS CURVY 2014 NIGERIA, IFY ANADU

Image

LIPUMBA AKUTANA NA WAANDISHI WA HABARI LEO NA KUZUNGUMZA KWA UCHUNGU KWA KUPIGWA NA POLISI KWENYE MAANDAMANO...AMTAKA KIKWETE AFUTE KESI

Image
Mwenyekiti wa profesa  CUF IBRAHIM LIPUMBA akiwasili katika mkutano huo  Kwa mara ya Kwanza tangu kutokea kwa vurugu za kisiasa ambazo zilisababisha mwenyekiti wa chama cha wananchi CUF profesa IBRAHIM LIPUMBA kupigwa na kukamatwa na jeshi la polisi na hatimaye kupelekwa mahakamani mwenyekiti huyo amejitokeza leo jumapili mbele ya wanahabari na kueleza hali halisi ya tukio hilo huku akieleza adhma yake ya kutaka kumuona rais kikwete kumueleza matatizo ambayo polisi wa Tanzania wanayo ambayo yanapaswa kuzibitiwa mara moja. Akizungumza kwa uchungu mkubwa LIPUMBA amesema kuwa kilichotokea juzi huko mbagala ni ishara tosha kuwa Tanzania hakuna amani na democrasia ya kweli kwani kuzuia maandamanao ambayo kila mwaka huwa yanafanyika kwa amani na utulivu ni kuwanyima haki watanzania ya kuwakumbuka ndugu zao waliofariki katika vurugu za Zanzibar. Amesema kuwa kitendo walichokifanya polisi kimewasikitisha sana wao kama wapenda amani na haki kwani po...

RAIS KIKWETE AONGOZA SHEREHE ZA MIAKA 38 YA KUZALIWA CCM MJINI SONGEA

Image
Mwenyekiti wa Chama Tawala cha CCM,Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na maelfu ya wananchi wakati akiingia katika uwanja wa MajiMaji mjini Songea leo kuongoza kilele cha sherehe za kuadhimisha miaka 38 ya kuzaliwa kwa CCM.

DIAMOND PLUTNAMZ ATUA NA MPENZI WAKE ZARI MJINI SONGEA

Image
Mwanamuziki Diamond Platnumz na mpenzi wake Zari wakiwasili kwenye uwanja wa ndege wa Songea tayari kwa kufanya onesho kubwa kwenye sherehe za miaka 38 ya kuzaliwa kwa CCM zinazofanyika kwenye uwanja wa Majimaji mjini Songea leo ambapo viongozi mbalimbali wakiongozwa na Mwenyekiti wa chama hicho Dr. Jakaya Kikwete.PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-SONGEA. Diamonda Plutnamz akiongozana na mpenzi wake Zari wakiondoka kwenye uwanja wa ndege wa Songea kuelekea hotelini.   Mkuu wa wilaya ya Songea Bw.Joseph Mkirikiti akisalimiana na Zari Mpenzi wa Diamond Plutnamz. Diamond Plutnamz akifanya vitu vyake kwenye uwanja wa Majimaji mjini Songea wakati wa sherehe za miaka 38 ya CCM. Diamond Plutnamz akiimba pamoja na mwanamuziki Abdul Misambano wa kundi la TOT katika sherehe za miaka 38 ya CCM mjini Songea mchana huu.   Umati wa wananchi waliohudhuria katika uwanja huo 

Baby Madaha: Naota nafanya mapenzi kila siku

Image
Msanii wa muziki na filamu Bongo, Baby Joseph Madaha ametoa kali ya mwaka baada ya kueleza sababu za kutodumu na wanaume kimapenzi kwamba ni kutokana na kuota anafanya mapenzi kila siku.    Awali rafiki wa Madaha aliyeomba hifadhi ya jina lake alisema kuwa, mara kwa mara msanii huyo amekuwa akilalamika kuwa kila siku anaota akifanya mapenzi hali inayomfanya asiwe na hamu ya kuwa na mpenzi.   “Mwenyewe anasema ni hali inayomtesa sana, asubuhi akiamka anakuwa amechoka na muda mwingi anakuwa hana hamu ya kuwa na mpenzi,” kilidai chanzo hicho.   Baada ya kupata ‘tipu’ hiyo, mwandishi wetu alimtafuta Baby Madaha, alipopatikana alisema: “Ni kweli ndoto za kimapenzi zinanitesa sana na huwezi amini nimekuwa nikiota nafanya mapenzi na mwanaume mwenye sura ya Ronaldo (Mwanasoka wa kimataifa anayechezea Timu ya Real Madrid).

Mh.Mbatia: Jeshi la polisi lifanyiwe marekebisho ya kimfumo ili kuboresha utendaji wake

Image
Serikali imeshauriwa jeshi la polisi lifanyiwe marekebisho ya kimfumo ili kuboresha utendaji wake ambao kwa sasa unalalamikiwa kwa sehemu kubwa na wananchi kwa kukiuka haki za binadamu.   Akizungumza jana mjini Dodoma katika kuhitimisha hoja kuhusu kukamatwa kwa kiongozi wa wa chama cha CUF, Prof Ibrahim Lipumba na wanachama wake,Mbatia alisema kuwa kitendo hicho kilikiuka haki za binadamu ikiwemo wanawake kudhalilishwa kijinsia.   Mh. Mbatia emeongeza kuwa ili chaguzi zijazo ziwe za amani na utulivu ameishauri serikali kubadilisha sera za vyama vya siasa na utawala pamoja na mfumo wa jeshi la polisi kuendeleza amani na utulivu ambavyo kwa sasa vinaonekana kuanza kutoweka.

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Anusurika Kufa

Image
Msafara wa mkuu wa mkoa wa Morogoro Dr. Rajab Rudenge umepata ajali katka eneo la Msavu barabara ya Morogoro Iringa majira ya saa tisa alasiri. Katika ajali hiyo Meya wa Manispaa ya Morogoro Amily Nondo na mwaandishi wa habari wa ITV wamejeruhiwa vibaya na wanaendelea na matibabu katika hosptali ya Rufaa ya mkoa wa Morogoro. Wengine walio jeruhiwa katika ajali hii ni pamoja na Dereva wa Meya na mwandishi wa habari wa Tbc. Tupe Maoni Yako

Shilole aomba radhi kwa kumdunda Nuh Mziwanda .......Nuh naye kasema yupo tayari kupigwa mpaka AKOME!!!

Image
Baada ya Shilole  kumchapa vibao mchumba wake Nuh Mziwanda, Shilole amelazimika kuomba radhi. Shilole amewaomba radhi mashabiki wake kwenye mtandao wa Instagram kwa kupost picha akiwa na mpenzi wake huyo na kuandika:   “ Huyu hapa mjanja wangu mimi, daah nimekamatika hapa, na naamini ni mwanaume sahihi kwangu maana hawezagi kurusha hata ngumi japo namchokozaga mie mjeuri tu, mnao muhandama mme wangu mmeshindwa, kugombana ni kawaida sana kwenye mapenzi na kama nliwaudhi mashabiki wangu mnisamehe mie nampenda mme wangu.”   Naye Nuh Mziwanda aliandika: Mwanaume lijali aliekamilika ampigi mpenzi wake wala kurudishia kibao au kofi alilopigwa na mpenzi wake.naamini kwenye mapenzi ya kweli wivu lazima na kugombana kwenye mapenzi ni kama kwenda chooni ni swala la kawaida sana.aaaaaaaya mke wangu nimekup rukhsa nipige mpaka nikome.ila all i know its love dats it.Nawapenda Mashabiki wangu pamoja sana .#zimaTaa sie tayar

Baba AJIUA Baada ya kuona picha za Uchi za Binti yake

Image
Wazazi wamekua na nafasi kubwa sana katika malezi ya watoto wao hata wakati  wanapokuwa watu wazima lakini baba huyu kutokana na upendo kwa mwanaye aliamua kujiua baada ya kuona picha za mtoto wake alizopiga akiwa mtupu katika jarida la Playboy nchini Romania.     Loredana Chivu aliamua kuweka picha hizo akiwa amepiga katika staili tofauti katika mitandao mbalimbali ya kijamii ambapo baba yake baada ya kuziona alimkana mwanaye huyo. Kwa mujibu wa mtandao wa The Mirror , msichana huyo akisimulia kwa machungu baada ya kifo cha baba yake alisema hakutegemea kama ipo siku baba yake angekasirika kiasi cha kujitoa uhai. Tupe Maoni Yako

NAPE AANZA AMSHA-AMSHA YA MIAKA 38 YA CCM MJINI SONGEA

Image
 Wananchi wakiwa katika shamrashamra za kumpokea Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye leo kwenye Ofisi ya CCM mkoa wa Ruvuma mjini Songea leo, alipowasli kwa ajili ya kuanzisha amsha amsha ya Maadhimisho ya miaka 38 ya CCM ambayo inafanyika Jumapili hii, Kitaifa mjini Songea kwa kuongozwa na Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete.  Mratibu wa Maadhimisho ya Miaka 38 ya CCM, Emaanuel John Nchimbi akiwasili kwenye Ofisi hiyo ya CCM mkoa wa Ruvuma leo kumpokea Nape  Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye (kushoto) akiongoza wananchi kwenda katika maeneo mbalimbali kuzindua mashina ya Wajasiriamali wa CCM na kuhutubia mkutano wa hadhara, baada ya kuwasili leo mjini Songea   Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye (kushoto) akiongoza wananchi kwenda katika maeneo mbalimbali kuzindua mashina ya Wajasiriamali wa CCM na kuhutubia mkutano wa hadhara, baada ya kuwasili leo mjini Songea   Katibu wa NEC, Itikadi na U...