LIPUMBA AKUTANA NA WAANDISHI WA HABARI LEO NA KUZUNGUMZA KWA UCHUNGU KWA KUPIGWA NA POLISI KWENYE MAANDAMANO...AMTAKA KIKWETE AFUTE KESI
Mwenyekiti wa profesa CUF IBRAHIM LIPUMBA akiwasili katika mkutano huo Kwa mara ya Kwanza tangu kutokea kwa vurugu za kisiasa ambazo zilisababisha mwenyekiti wa chama cha wananchi CUF profesa IBRAHIM LIPUMBA kupigwa na kukamatwa na jeshi la polisi na hatimaye kupelekwa mahakamani mwenyekiti huyo amejitokeza leo jumapili mbele ya wanahabari na kueleza hali halisi ya tukio hilo huku akieleza adhma yake ya kutaka kumuona rais kikwete kumueleza matatizo ambayo polisi wa Tanzania wanayo ambayo yanapaswa kuzibitiwa mara moja. Akizungumza kwa uchungu mkubwa LIPUMBA amesema kuwa kilichotokea juzi huko mbagala ni ishara tosha kuwa Tanzania hakuna amani na democrasia ya kweli kwani kuzuia maandamanao ambayo kila mwaka huwa yanafanyika kwa amani na utulivu ni kuwanyima haki watanzania ya kuwakumbuka ndugu zao waliofariki katika vurugu za Zanzibar. Amesema kuwa kitendo walichokifanya polisi kimewasikitisha sana wao kama wapenda amani na haki kwani polisi hao