Posts

RAIS KIKWETE AKUTANA NA WASAANI NYOTA WA FILAMU NA MUZIKI KUTOKA NCHINI MAREKANI JIJINI DAR LEO

Image
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na wasanii nyota wa filamu na muziki kutoka  Marekani walioko nchini kwa ziara ya kutoa mafunzo kwa wasanii wa Tanzania. Wasanii hao ni na  Terrence J. Jenkins, mwendeshaji wa kipindi cha muziki kwenye televisheni ya E! Entertainment (wa pili kulia) Chaka Zulu, Mtendaji wa Shughuli za Muziki kutoka Kampuni ya Disturbing The Peace Records (wa pili kushoto)  na Davis Banner, mwigizaji, mwanamuziki, mtunzi na msimamizi wa shughuli za muziki ambaye amepata kushinda tuzo maarufu ya Grammy.   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitumia simu yake ya mkononi kuwaonesha vivutio vya kitalii wasanii nyota wa muziki na filamu wa Kimarekani walioko nchini kwa ziara ya kutoa mafunzo kwa wasanii wa Tanzania. Wasanii hao ni   Terrence J. (Jenkins), mwendeshaji wa kipindi cha muziki kwenye televisheni ya E! Entertainment, mwigizaji wa filamu na mtunzi wa vitabu na Revi Shelton, Mtendaji wa Shugh...

SHUHUDIA MATESO HAYA: ATESEKA ICU KWA MIEZI 5

Image
Mwanafunzi Norat Rashid akipatiwa matibabu katika Taasisi ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu (MOI) iliyopo Hospitali ya Taifa Muhimbili. MATESO ya mwanafunzi Norat Rashid (16), anayesoma kidato cha pili katika Shule ya Sekondari Mtoni Relini, Wilaya ya Temeke, Dar es Salaam ni ya kuhuzunisha na kutia huruma kutokana na ajali ya pikipiki aliyoipata miezi nane iliyopita wakati akienda shuleni. Norat alimuambia mwandishi wetu hivi karibuni katika Taasisi ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu (MOI) katika Hospitali ya Muhimbili Jengo la Mwaisela chumba namba mbili kuwa ajali hiyo aliipata maeneo ya Mtoni kwa Azizi Ally saa za asubuhi wakati akivuka barabara akienda shule. Alisema mara baada ya ajali alipoteza fahamu na alipozinduka alijikuta amezungukwa na madaktari wa Muhimbili. Katika mahojiano hayo, Norat alikuwa na haya ya kusema: “Najua huu ndiyo mwisho wangu wa kusoma, ndoto ya kufika chuo kikuu imezimika ghafla kama taa, sikutegemea kama leo hii ningekuwa hivi, nili...

HAUSIGELI MIAKA 8 AJERUHIWA NA BOSI WAKE.

Image
 Mtoto Miseto (8) aliyejeruhiwa na anayedaiwa kuwa bosi wake. Mtoto Miseto (8), anayedaiwa alikuwa akifanya kazi za ndani kwa mama mmoja aliyejulikana kwa jina la  Mary Jerald mkazi wa Kijiji cha Busurwa, Wilaya ya Rorya, mkoani Mara ameokotwa ufukweni mwa Ziwa Victoria Juni 28, mwaka huu akiwa amejeruhiwa na anayedaiwa ni bosi wake. Taarifa kutoka kwa shuhuda wa tukio hilo, Akeyo Thomas ambaye ni mchuuzi wa samaki katika maeneo hayo alidai kwa wakati akiwa na wachuuzi wenzake walimuokota mtoto huyo akiwa amelala juu ya mchanga ufukweni mwa ziwa hilo huku akiwa na majeraha mbalimbali mwilini. Akizugumza na mwandishi wetu wiki iliyopita kwa njia ya simu na kuthibitishwa na mmoja wa askari wa Kituo cha Polisi cha Busurwa,  alisema siku hiyo saa 12 asubuhi walimuona mtoto akiwa amelala juu ya mchanga huku akiwa na rundo la nguo ambazo alidai aliambiwa na bosi wake azifue. “Tulimuuliza mtoto huyo sababu za kuwa na majeraha, akajibu kuwa ame...

WEMA SEPETU ALIZWA VIBAYA

Image
  Staa wa sinema za  Bongo na Miss Tanzania 2006, Wema Isaac Sepetu. KUNA STAA wa sinema za  Bongo na Miss Tanzania 2006, Wema Isaac Sepetu ‘ameingizwa mjini’ na mhariri wa filamu Bongo mwenye asili ya Kiarabu aliyejulikana kwa jina moja la Chidy kwa kuingia mitini na shilingi 5,000,000 alizompa ili azihariri filamu zake mbili lakini kazi haikufanyika.  Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya Jeshi la Polisi Tanzania Kituo Kikuu jijini Dar es Salaam, kilisema ilikuwa mwaka jana (2013) ambapo Wema alimkabidhi mhariri huyo filamu mbili, Super Star na Vian Unaspect. MALIPO YAFANYWA, KAZI HAKUNA Ikazidi kudaiwa kwamba mbali na filamu hizo, Wema alimlipa jamaa shilingi 2,500,000 ili kuzihariri (editing) filamu hizo ikiwa ni hatua ya mwisho kabla ya kuingia sokoni. JAMAA AINGIA MITINI, AMKWEPA WEMA Habari zikazidi kudai kwamba, baada ya kuudaka ‘mpunga’ huo jamaa huyo amekuwa akimzungusha Wema kufanya kazi zake na kumkabidhi ili azipeleke sokoni ...

JE, WAJUA SIFA NA MATUKIO YA MWEZI ULIOZALIWA? SOMA HAPA MATUKIO NA SIFA ZA KUZALIWA KWA WATU MBALIMBALI UFURAHIE.

Image
This is funny and interesting kama ulizaliwa July na Dec its just crazy Jan ---------------JANUARY BABY-------------------- Pretty/handsome. Loves to dress up. Easily bored. Fussy. Seldom shows emotions. Takes time to recover when hurt. Sensitive. Down-to-Earth. Stubborn. Re-post this in 5 min and you will meet someone new in 8 days that will perfectly balance your personality. Feb ----------FEBRUARY BABY -------------------- Abstract thoughts. Loves reality and abstract. Intelligent and clever. Changing personality. Attractive. sexiest out of everyone. Temperamental. Quiet, shy and humble. Honest and loyal. Determined to reach goals. Loves freedom. Rebellious when restricted. Loves aggressiveness. Too sensitive and easily hurt. Gets angry really easily but does not show it. Dislikes unnecessary things. Loves making friends but rarely shows it. Horny. Daring and stubborn. Ambitious. Realizing dreams and hopes. Sharp. Loves ente...

RAIS KIKWETE AFUTARISHA WANANCHI WA MBEYA

Image
Mbunge wa Mbeya Mhe Joseph Mbilinyi “Sugu” akipata futari na wananchi wenzie wa Mbeya katika futari iliyoandaliwa na Rais Jakaya mrisho Kikwete katika ukumbi wa Shule ya Sekondari ya Mbeya Day jijini Mbeya Jumapili Julai 13, 2014. PICHA NA IKULU Meza Kuu k atika futari iliyoandaliwa na Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika ukumbi wa Shule ya Sekondari ya Mbeya Day jijini Mbeya Jumapili Julai 13, 2014. Wananchi wa Mbeya waliohudhuria futari iliyoandaliwa na Rais Jakaya mrisho Kikwete katika ukumbi wa Shule ya Sekondari ya Mbeya Day jijini MbeyaJumapili Julai 13, 2014. Wananchi wa Mbeya waliohudhuria futari iliyoandaliwa na Rais Jakaya mrisho Kikwete katika ukumbi wa Shule ya Sekondari ya Mbeya Day jijini MbeyaJumapili Julai 13, 2014.   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akishukuru wananchi wa Mbeya kwa kujitokeza kwa wingi katika futari aliyoiandaa katika katika ukumbi wa Shule ya Sekondari ya Mbeya Day jijini Mbeya Jumapili Julai 13, 2014...