Posts

AMINI WA THT HATIMAYE AFUNGA NDOA NA BONGO MUVI STAR FARIDA

Image
Muimbaji na mtunzi wa nyimbo kutoka THT, Amini Mwinyimkuu jana June 22 ameukacha ukapela kwa kufunga ndoa na msanii Farida Bashir maarufu kama Namcy Vana aliyeimba ‘Kantangaze’. Tazama picha hapa... Amini akiwa na mkewe Ndoa hiyo imefanyika nyumbani kwa Namcy, Magomeni Dar es Salaam. Pongezi nyingi kwa Amin na mkewe

BREAKING NEWS: MWENDO KASI WASABABISHA GARI KUGONGA NA KUBOMOA NYUMBA MIDA HII MKOA WA MANYARA.

Image
 Picha zote na Manyara yetu Blog

BREAKING NEWS: KICHANGA KILICHO FARIKI CHAKUTWA KIMETUPWA KATIKA JALALA LA POSTA ENEO LA MAKAMA YA WILAYA IRINGA.

Image
   Kichanga kikiwa kimetupwa Jalalani na kuonekana asubuhi hii  Humo ndio Kichanga kilipo tupiwa  Eneo ambalo Kichanga kimetupiwa  Askari wakiwa wamefika eneo la tukio  Mashuhuda wakiwa wanashuhudia tukio hilo. Picha zote na Iringa yetu Blog

ANGALIA PICHA SISTA ALIYEUWAWA KWA KUPIGWA RISASI NA MAJAMBAZI

Image
Mwili wa Sista baada ya kupigwa risasi. Kidole cha dereva kilichokatwa kwa risasi. Ganda la risasi likiwa eneo hilo la tukio. Dereva akiwasiliana na jamaa zake baada ya kupigwa risasi na sista aliyekuwa naye kuuawa. Wananchi wakiwa eneo la tukio. SISTA wa Parokia ya Makoka iliyopo Kibangu, Dar ameuawa na majambazi yaliyokuwa kwenye bodoboda wakati akiingia kwenye gari akitokea dukani eneo la River Side, Ubungo jijini Dar es Salaam hivi punde. Kabla ya kuuawa sista huyo, dereva wake alipigwa risasi mkononi na majambazi hayo.Chanzo GPL

Waziri Membe azindua Filamu mpya ya 'I Love Mwanza' jijini Mwanza

Image
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe (wa pili kushoto), akisadiwa na Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF), Simon Mwakifwamba, kukata utepe kuzindua filamu mpya iitwayo ‘I Love Mwanza’ iliyoandaliwa na Lake Zone Youth Empowerment Foundation kwa kushirikiana na Tropical Media Tanzania Ltd, katika hafla iliyofanyika jijini Mwanza Jumamosi usiku. Wanaoshuhudia ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu (wa watatu kushoto), na Mwenyekiti wa Chama cha Sanaa za Maonyesho na Waigizaji Tanzania (TDFAA), Mkoani Mwanza, Anitha Kagemulo.  PICHA ZOTE/ JOHN BADI WA Daily Mitikasi Blog Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe (wa pili kushoto), akionyesha CD ya filamu mpya iitwayo ‘I Love Mwanza’, iliyoandaliwa na Lake Zone Youth Empowerment Foundation kwa kushirikiana na Tropical Media Tanzania Ltd, baada ya kuizindua katika hafla iliyofanyika jijini Mwanza Jumamosi usiku. Wanaoshuhudia ni Waziri wa Mali

SOMA ALICHOSEMA BUNGENI MBUNGE WA ARUSHA GODBLESS LEMA NA KUZUA KIZAAZAA

Image
Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema ni miongoni mwa waliowasha vipaza sauti kwenye bunge la bajeti linaloendelea Dodoma ambapo sehemu ya alichochangia ni hiki kinachofata hapa chini.  ‘Dola bilioni moja miaka kumi nyuma ilikua ni Trilioni 11 lakini sasa unaongelea Trilioni 17 kwa hiyo shilingi imeshuka thamani lakini unashangaa kwanini tunaendelea kuongeza ushuru kwenye pombe na sigara kama chanzo cha mapato ya taifa letu, nchi nyingi duniani zinazoongeza ushuru kwenye pombe na sigara lengo lake ni kuona idadi ya wanaokunywa na kuvuta inapungua tofauti na Tanzania ambako lengo limekua ni kukusanya mapato, hiki ni kitu cha kusikitisha sana’  ‘Nimekwenda Singida hivi karibuni kwenye ziara ya chama chetu na Mh. Tundu Lissu, ukiwa Singida na Dodoma unaona kuna jua kali… Singida Same serikali imeweka vikao barabarani >> NENDA POLEPOLE HAPA KUNA UPEPO MKALI UNAUA << ingekua ni taifa kama Israel, upepo mkali hauwekewi vibao vya kuua bali upepo mka

MWIMBAJI MWINGINE WA KWETU PAZURI APATA MWENZA

Image
Katika shangwe za GK siku ya leo, tunakupa picha chache kutoka Kigali nchini Rwanda, ambako mmoja kati ya waimbaji wa muda mrefu wa kundi la Ambassadors of Christ a.k.a Kwetu Pazuri aitwaye Furaha Sandrine , jumapili iliyopita aliutambulisha rasmi ubavu wake uitwao Ngabo Karangwa Tony katika sherehe ya kulipiwa mahari na kuvishwa pete ya uchumba rasmi iliyofanyika nyumbani kwao maeneo ya Gikondo  jijini Kigali, ambapo harusi inatarajiwa kufanyika tarehe 6/7/2014 katika kanisa la Wasabato la Gisenyi na kufuatiwa na shere ya kuwapongeza itakayofanyika katika pwani ya Lac Kivu beach. Furaha akivishwa pete ya uchumba. Baada ya pete ni  matabasamu tuuu. Pete ikionyeshwa na zawadi mkononi akikamata. Akipokea zawadi kutoka kwa mtarajiwa mumewe. Furaha mwenye Furaha. Furaha akiwa na marafiki zake akiwemo Kelly aliyesimama nyuma, mwimbaji wa Ambassadors.

KAZI IMEANZA, SIMBA SC YASAINI BEKI LA TAIFA STARS MIAKA MITATU...YANGA NA MAGAZETI YAO

Image
KAZI imeanza. Simba SC imesajili mchezaji wa kwanza kabisa kwa ajili ya msimu ujao, ambaye ni chipukizi wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars Joram Nason Mgeveke. Mchezaji huyo chipukizi pekee kutoka kikosi cha maboresho aliyebaki Taifa Stars chini ya kocha Mholanzi Mart Nooij, amesaini Mkataba wa miaka mitatu leo. Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe ameiambia BIN ZUBEIRY leo kwamba, Joram amesaini mjini Iringa na rasmi sasa ni mchezaji wa Simba SC. Kifaa cha kwanza 2014-2015; Joram Mgeveke akipeana mikono na Hans Poppe baada ya kusiani Mkataba wa miaka mitatu na Simba SC. Chini anasaini. “Tuna muda mfupi sana kwa ajili ya kufanya usajili, sasa tuna orodha ya wachezaji waliopendekezwa, kwa hiyo tunaanza kuwapandia ndege kuwafuata na kumalizana nao, ndani na nje ya nchi. Tumeanza na Joram, kwa sababu yuko Taifa Stars ambayo inakwenda kambini Botswana,”alisema Poppe.    Poppe amewahakikishia wana Simba SC

MGIMWA ATUMIA USAFIRI WA BAISKELI KUWATEMBELEA WANANCHI

Image
 Mbunge wa  jimbo la Kalenga mkoani Iringa Godfrey Mgimwa akitumia usafiri wa Baiskeli kuwafikia wapiga kura wake katika kijiji cha Kivalali kata ya Ifunda baada ya gari lake  kupata pacha  wakati wa zikara hiyo hivyo kulazimika kutafuta baiskeli ili kufika haraka mkutanoni kusikiliza kero za  wananchi wake ,amini ni mbunge wa kwanza mkoa wa Iringa kutumia usafiri kama huu kuwafikia wananchi wake,picha nyingine akisalimianana  wananchi wa kijiji Kivalali (picha na Francis Godwin Blog) Na Francis Godwin, Iringa MBUNGE  wa  jimbo la Kalenga  Godfrey Mgimwa amevunja rekodi ya  wabunge wa jimbo hilo na majimbo mengine ya mkoa wa Iringa na Tanzania kwa kuachana na matumizi ya magari ya kifahari na kuamua kutumia usafiri wa Baiskeli kuwatembelea  wapiga kura  wake. Huku wananchi wa kata ya Ifunda na Mgama wakisema kuwa ubunge wa Mgimwa si wa mwaka mmoja ama mitano bali  hadi mwaka 2025 hadi mwenyewe atakavyo sema yatosha .  Mbunge Mgimwa atumia usaf