MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AZINDUA WIKI YA MAZINGIRA DUNIANI KWA KUPANDA MITI KATIKA KAMBI YA KIKOSI CHA JESHI LA KUJENGA TAIFA RUVU
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohameed Gharib Bilal, akihutubia wakati wa hafla ya uzinduzi wa Wiki ya Mazingira Duniani, wakati alipofika kwenye Kambi ya JKT Ruvu kwa ajili ya kupanda miti ikiwa ni sehemu ya uzinduzi huo, ambapo jumla ya miti 8,000, imeandaliwa kupandwa katika eneo hilo. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipanda mti katika eneo la Kambi ya Jeshi la Kujenga Taifa, JKT Ruvu, ikiwa ni sehemu ya uzinduzi wa Wiki ya mazingira Duniani. jumla ya miti 8,000 inatarajia kupandwa katika eneo hilo.