Posts

WASTARA, CLOUD WAZURU MAKABURI YA WASANII WENZAO

Image
Cloud, Mtitu, Wastara, Steve Nyerere, Barafu na Chiki katika kaburi la Adam Kuambiana. Wastara akilia kwa uchungu.   Wastara na timu yake wakiweka mashada katika kaburi la Kuambiana.    Kaburi la marehemu Adam Kuambiana.   Wasanii katika kaburi la Steven Kanumba.   Wasanii pia walitembelea kaburi la msanii mwenzao John Maganga. Mwisho kabisa wasanii walitembelea kaburi la Zuhura Maftah Malisa. WASANII wa Bongo Movie Unity ambao hawakuwepo katika msiba wa Adam Kuambiana wakiwa nchini Uingereza, Issa Mussa ‘Cloud’ na Wastara Juma leo wamezuru kaburi Kuambiana pamoja na makaburi ya wasanii wengine ambao tayari walishatangulia mbele ya haki akiwemo John Maganga, Steven Kanumba na Zuhura Maftah Malisa. Wakizungumza na waandishi wetu, wasanii hao wamesema kuwa ni jambo la kumshukuru Mungu lakini watazidi kuwaombea wale wote waliotangulia kwa kuwa wote wako katika njia moja.

AJIFUNGUA WATOTO WANNE AOMBA MSAADA

Image
Mkaazi wa kunduchi Beachi  katika manispaa ya kinondoni  jijini Dar es salaa Riziki Daudi amejifungua watoto  alipojifungua kwa njia ya upasuaji wiki iliyopita katika hospitali ya Taifa muhimbili  kutopkana kuwa maisha magumu anaomba wasamaria wema kumsaidia kwa hali  na mali kutoka hali yake hususani nguo za watoto apamoja na misaada mingine  watoto hao wanatunzwa katika chumba maalum katika jengo la wazazi alikuwa anaomba kwa wale watakao gusa na tatizo hilo kuwasiliana na namba za simu 0783717648 ya Hadija Abeid na 0717 365040 ya Thuwaiba mohamed au 088711458 Daudi Haji  wadau naomba tumsaidie kwa kusambaza vyombo vyenu  

ANGALIA PICHA UKAWA WAKIWA BUKOBA

Image

ANGALIA PICHA YA WAZIRI AJIUA BAADA YA KUSHINDWA KATIKA UCHAGUZI MALAWI

Image
Naibu waziri wa serikali za mitaa wa Malawi amejipiga risasi na kujiua nyumbani kwake mjini Lilongwe. Godfrey Kamanya alikuwa anayegombea kutetea kiti chake cha ubunge katika jimbo la Nzonzi Kusini amejiua alfajiri ya leo katika mojawapo ya vyumba vya nyumba yake iliyopo Area Ten mjini Lilongwe. Mwili wa marehemu umehifadhiwa kwenye hospitali kuu ya Kamuzu mjini humo, na jeshi la polisi litatoa taarifa rasmi ya kifo hicho baada kukamilisha uchunguzi. Haijajulikana sababu za Kamanya kujiua japokuwa ameacha barua ya maelezo ambayo polisi wataitoa baadae. Matokeo ya kura bado hayajatangazwa rasmi katika kile kinachosemekana kuwa uchaguzi wenye ushindani mkali sana. Afisa mkuu wa uchaguzi, amesema kuwa mfumo wa elektroniki umeharibika na maafisa wanatumia matokeo kwa njia ya barua pepe.

ANGALIA PICHA MCHUNGAJI ALIYEHARIBIWA SURA KWA TINDIKALI, SASA AENDELEA VYEMA

Image
Mchungaji Umar Umulinde wa Uganda akiwa hospitalini. Hizi ni baadhi ya picha alizopiga hivi karibuni mchungaji Umar Umulinde wa Uganda ambaye alimwagiwa tindikali katika mkesha wa sikukuu ya christmas mwaka jana mara baada ya kumaliza ibada,ambapo mpaka sasa kikubwa ambacho mchungaji Umulinde ambaye alikuwa muumini wa dini ya kiislamu kabla ya kubadili na kuokoka anasema ni kwamba waliomwagia tindikali ni waumini wa dini yake ya zamani kwani kabla ya kumwagiwa huyo mtu alisema neno linalotumiwa na waumini wa dini hiyo,ingawa kumekuwa na kuhusishwa kwa watu wengine kuhusiana na tukio hilo ingawa mchungaji huyo hataki kuamini. sura yake ndivyo inavyoonekana kwasasa. Mchungaji Umulinde. Ambapo mpaka sasa amekuwa  akiuliza maswali mbalimbali kuhusiana na allah na Mungu wa biblia kama wana uhusiano wowote kwamaana Mungu wa biblia anayemuamini aruhusu mtu kuua ili akarithi mbingu kama allah anavyotaka,zaidi amewashukuru watu wanaoendelea kumuombea na kumtem...

WANAFUNZI WA CHUO CHA KUMBUKUMBU YA STEFANO MOSHI(SMMUCO) WAFUNGA BARABARA WAKITAKA KULIPWA PESA ZAO ZA MKOPO

Image
 Wanafunzi wakiwa katika Makundi mbalimbali katika mgomo huo  Mgomo ukiwa unaendelea huku wakidai pesa zao  Wanafunzi wakiwa wamefunga Njia muda huu Hapa wakiendelea na madai yao wakiwa ni wanafunzi wa Mwaka wa Kwanza wa Pili na Watatu

HAKIMU ASHINDWA KUENDESHA KESI BAADA YA WAFANYAKAZI KUFANYA MAPENZI CHUMBA CHA JIRANI NA MAHAKAMA HIYO

Image
Kituko kingine leo kinatoka Italia ambapo Jaji mmoja ameamua kusimamisha kesi baada ya kuona wafanyakazi wawili wa Mahakama hiyo wakifanya mapenzi kwenye chumba cha jirani wakati kesi ikiendelea. Jaji Anna Ivaldi alishtuka na kumuomba mwendesha mashtaka anyamaze baada ya kuona tukio hilo ndani ya ofisi pembeni ya mahakama ambapo wawili hao walidhani kioo kilichoua na tinted pembeni yao kisingeweza kumpa nafasi mtu wa upande wa pili kuona kinachoendelea ndani. Taarifa kutoka kwenye Mahakama hiyo zinaamplfy kwamba mmoja kati ya wawili hao anatambulika kuwa yuko kwenye ndoa  na hii ni kwamujibu wa mmoja wa wafanyakazi wa Mahakama.   Baada ya hii ishu ilibidi tu Jaji aamuru kuahirishwa kwa kesi hiyo mpaka wakati mwingine muda mfupi tu baada ya wakili Sabrina Monteverde kuanza kuzungumzia kesi ya hiyo ya Mmorocco Yasin Mahmoud ambae anashtakiwa kuua jambazi katika bandari nchini Italy mwaka jana. Mmoja kati ya waliokuwemo mahakamani amesema “wa...

MUME NA MKE MBARONI KWA KUMFICHA MTOTO NDANI YA BOX MIAKA 4, IMANI ZA KISHIRIKINA ZATAWALA MORO

Image
  Maria Said mama mkubwa wa Nasra, katikati ni  baba mzazi wa Nasra, Rashidi Mvungi, na kulia ni mume wa Mariam Said wakiwa katika ofisi za ustwawi wa jamii mjini Morogoro baada ya kukamatwa na kufikishwa polisi kwa tuhuma za kumficha mtoto huyo ndani ya box  kwa miaka  4 baada ya mama wa mtoto huyo kufariki dunia kwa ugonjwa wa malaria .   Muuguzi katika Wodi ya watoto hospitali ya rufaa ya Morogoro akimuhudumia mtoto Nasra Said mara baada ya kufikishwa hopsitalini hapo kupatiwa matibabu.  Mtoto Nasra akiwa katika wodi ya watoto hospitali ya mkoa wa Morogoro anakopatiwa matibabu kwa sasa.  Habari zaidi soma hapo chini.   MUME na mke  wanashikiliwa na polisi mkoani hapa kwa  tuhuma za kumficha mtoto kwa miaka 4 ndani ya Box . Kamanda  wa polisi mkoani Morogoro Leonard Paul alisema tukio hilo lilibainika Mei 20  mwaka huu majira ya saa 4.45  Asubuhi  katika ...

FLAVIANA AADHIMISHA KUMBUKUMBU YA AJALI YA MV BUKOBA

Image
Flaviana na Balozi Mwanaidi Maajar walishiriki kuweka mashada katika mababuri Msanii wa muziki wa kizazi kipya Ambwene Yesaya almaarufu kama AY alikuwepo kuungana na Flaviana Matata Baba Mzazi wa Mwanamitindo huyo nae alikuwepo kwenye misa ya kuwaombea

JOTI AJA NA "SANDUKU LA BABU"

Image
MSANII wa Komedi Bongo Lucas Mhuvile ‘Joti’ akiandaa promo ya "Sanduku la Babu" MSANII wa Komedi Bongo Lucas Mhuvile ‘Joti’ akiwa kama Amijee MSANII wa Komedi Bongo Lucas Mhuvile ‘Joti’ akiwa kama Bi Kiboga. MSANII wa Komedi Bongo Lucas Mhuvile ‘Joti’ ametengeneza filamu inayokwenda kwa jina la Sanduku la Babu. Msanii huyo anajivunia aina ya mfumo aliotumia katika kuandaa sinema hiyo kwa kuirekodi na kushiriki katika nafasi zote pekee yake na kuifanya kuwa filamu sawa na iliyoshirikisha wasanii wengi.  Filamu hiyo ambayo inaonekana ni ya maajabu ni kutokana na Teknolojia iliyotumika kwa nafasi zote kuchezwa na mhusika mmoja, ambapo Joti amecheza katika sinema ya Sanduku la Babu kucheza nafasi ya Babu wa Sumbawanga, Bi. Kiboga, Amijee, na kuwashirikisha kidogo wasanii chipukizi.  “Nilikuwa nikifikiria sana kuhusu kuingia katika tasnia ya filamu kwani nilitaka kujua baada ya kutengeneza kazi yangu nitaipeleka wapi? Lakini baada ya kukutana na...

ANGALIA PICHA FISI WAKUTWA NA SHANGA NA ROZALI KIUNONI.

Image
MSAKO wa Fisi waliovamia makazi ya Vitongoji vitatu vya Kijiji cha Hungumalwa Kata ya Hungumarwa wilayani Kwimba mkoani Mwanza, umezua maajabu. Maajabu hayo yamehusishwa na imani za kishirikina, baada ya fisi wawili kati ya 12 waliouawa, kukutwa wamevalishwa shanga na Rozali, kiunoni.  Msako huo wasiku tatu ulioanza juzi(Jumapili) unahusisha mamia ya wananchi wa Kijiji hicho na vitongoji vyake vya Mwanzabalemi, Mwanega na Mwang’ombe, wanaotumia siraha za jadi na mbwa wapatao 50. Habari za ndani kutoka Kijijini humo zimesema kwamba, kabla ya wananchi hao kuingia ‘vitani’ kusaka wanyama hao ambao baadhi wanadaiwa kumilikiwa na watu wachache wanaojihusisha na vitendo vya ushirikina, wazee wa Kijiji na Vitongoji hivyo, walifanya mazindiko (kinga) ya kujikinga na nguvu za washirikina ambazo zinge kwamisha zoezi hilo. Kwa mujibu wa baadhi ya wazee wa kijiji hicho ambao hawakutaka majina yao yaandikwe, walisema kuwa makamanda wa jadi wanaoongoza msa...