Posts

ANGALIA PICHA KIJANA AUAWA KWA KUPIGWA MAWE NA KUCHOMWA MOTO,MWINGINE ANUSURIKA KUFA,

Image
Kulia ni mwili wa marehemu baada ya kuchomwa moto-kushoto ni Machela  ikiandaliwa  kuupakia  mwili wa kijana aliyeuawa kwa kuchomwa moto   Kijana  aliyejulikana kwa jina la Mangi  akiwa  ndani  ya  gari, pembeni  yake  ni  maiti  ya  mwenzake Polisi  wakikagua  makoti  ambayo  kijana  aliyenusurika  alikuwa  ameyavaa Mtu mmoja anaesadikiwa kuwa ni jambazi ambaye hakufahamika jina anayekadiliwa kuwa na umri wa miaka 25 ameuwawa kwa kupigwa mawe kisha kuchomwa moto na mwingine kunusurika kuuwawa. Tukio hilo limetokea jana  alfajiri  katika kijiji cha Shibula kata ya Bugongwa wilayani Ilemela Mkoani Mwanza kufuatia tukio la wizi lilotokea usiku wa kuamkia jana katika mtaa  wa  Nyamwilolelwa ambapo pikipiki moja na paneli ya solar ziliibiwa.    Katibu wa Sungusungu katika kijiji cha Shibula John Mashalia amesema kuwa kufuatia tukio hilo waliamua kuweka ulinzi shirikishi kuzunguka vijiji vyote na ndipo walipokutana na kijana huyo aliyeuwaw

ANGALIA NAFASI MPYA ZA KAZI 482 KUTOKA SERIKALINI

Image
1 JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA Kumb. Na EA.7/96/01/G/09 01 Aprili, 2014 TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI Sekretariati ya Ajira katika Utumishi wa Umma ni chombo ambacho kimeundwa kwa mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma Na. 8  ya mwaka 2002 kama ilivyorekebishwa na Sheria Na. 18 ya mwaka 2007 kifungu 29(1). Kwa mujibu wa Sheria hiyo, chombo hiki, pamoja na kazi zingine kimepewa jukumu la kutangaza nafasi wazi za kazi zinazotokea katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Waajiri (Taasisi za Umma). Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma anakaribisha maombi kwa Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi 482 za kazi kwa waajiri mbalimbali kama ifuatavyo: MASHARTI YA JUMLA KWA KAZI ZOTE. i. Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania. ii. Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa. iii. Waombaji ambao tayari ni Watumishi wa Umma na wa

ANGALIA PICHA ZA WEMA ALIVYOFANYA VURUGU OFISI ZA GLOBAL PUBLISHER

Image
HOVYOOO! Wema Isaac Sepetu aliye pia Miss Tanzania 2006, amejitoa fahamu kwa kupandisha mzuka na kutinga makao makuu ya Kampuni ya Global Publishers, Bamaga-Mwenge, Dar na kuzua timbwili la aina yake kisa kikiwa ni kuandikwa kwa habari zake na mpenziwe, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’. Tukio hilo la kumchoresha staa huyo mwenye vituko kila kukicha, lilijiri Jumatatu iliyopita kwenye ofisi za Global ambao ni wachapishaji wa gazeti hili (Amani), Uwazi, Ijumaa, Ijumaa Wikienda, Championi na Risasi majira ya mchana kweupe hivyo kufunga mtaa huku wapita njia wakimzodoa kwa maneno ya kejeli. Wema akiwa ndani ya ofisi za Global na sura ya 'kuua mtu', mkononi akiwa na gazeti la Ijumaa Wikienda lenye stori: DIAMOND ATAMANI USHOGA. Kushoto ni mpambe na mfanyakazi wake Petit Man Wakuache. ATINGA NA WAPAMBE DHAIFU Akiwa na kundi la wapambe dhaifu na goigoi wakiongozwa na meneja wake, Martin Kadinda waliosimama nje ya ofisi hizo, Wema alifika kwa upole