JAMAA WA ABIRIA WA MH370 WAKABILIANA NA POLISI
Familia za abiria wa ndege iliyotoweka ya Malaysia wakiandamana wakiwa wamebeba mabango. Polisi wakiwa tayari kuwatuliza wana familia waliopotelewa na ndugu zao. Mkusanyiko wana familia za abilia wa ndege iliyotoweka ya Malaysia wakiendelea na maandamano. Polisi wakiwatuliza wana familia wenye hasira kali. Familia za abiria wa ndege iliyotoweka ya Malaysia majuma mawili yaliyopita, wamekabiliana na polisi nje ya ubalozi wa Malaysia mjini Beijing. Wakiwa wamejawa na ghadhabu, wamelitaka shirika la ndege ya taifa hilo mjini Kuala Lumpur kueleza kilIchofanyika. Jamaa hao walibeba mabango yenye maandishi "Save MH370" jamaa hao wenye hasira walikabiliana na polisi na kuwalemea hadi kuingia katika ofisi ya ubalozi huo. Walifoka wakisema ..''Tunataka ukweli." hii ni ishara ya hasira na mafadhaiko wanayopitIa jamaa hao wa watu waliopotea. Kero la jamaa hao limekuja baada ya waziri mkuu wa Malaysia, Najib Razak kusema udadisi