KUTANA NA MTOTO WA KWANZA KUZALIWA KWA NJIA YA UPANDIKIZAJI NCHINI
Unapoingia katika nyumba ya familia ya Salehe Saidi, macho na masikio yako hayawezi kukwepa ucheshi wa kijana wa miaka 13, Jumbe Salehe. Ni kijana anayeipa tabasamu familia hiyo. Jumbe ni mwenye nguvu, afya, akili darasani na uchangamfu ambao kila mzazi angependa kuuona kwa kijana wake. Lakini Jumbe Salehe, hakuzaliwa kama watoto wengine. Alipatikanaji katika mchakato mrefu, uliohusisha teknolojia ya hali ya juu na majaribio yaliyohitaji werevu. Jumbe alizaliwa kwa njia ya upandikizaji wa mbegu ambao kwa jina la kitaalamu unajulikana kama In-Vitro Fertilization (IVF). Mchakato huo ulisimamiwa na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Wanawake, Profesa Malise Kaisi. Kwa nini Jumbe alizaliwa kwa njia ya IVF? Mwanaidi Kombo, mama mzazi wa Jumbe, hakuwa na tatizo la uzazi hapo awali. Alifanikiwa kupata mtoto wake wa kwanza mwaka 1986. Mwaka 1988 alipata ujauzito mwingine lakini kwa bahati mbaya, uliharibika na kuanzia hapo ikawa ni vigumu kwake kushika mimba nyi