ANGALIA PICHA KIJANA AJICHINJA KWA SIME AKIWA NDANI YA BASI
Akiandika barua AMA kweli duniani kuna mambo kwani dereva na abiria wa basi la Manchester ambalo namba yake haikujulikana mara moja, lililokua likitoka Lindi kwenda jijini Dar es Salaam walijikuta wakiangua vilio baada ya kumuona mwenzao akijichinja hadi kufa kwa kisu ndani ya gari hilo. Kwa mujibu wa chanzo, tukio hilo la kusikitisha lilitokea saa tisa alasiri, Jumatano wiki iliyopita mara basi hilo lilipofika katika hoteli moja ya Nangulukulu kwa ajili ya kupatia chakula. Wakizungumza kwa nyakati tofauti na waandishi wa habari hii jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita, baadhi ya abiria walioshuhudia tukio hilo walisema kuwa mara walipofika katika hoteli hiyo, kila mmoja alitawanyika kwa lengo la kujipatia chakula na baadhi yao walienda maliwatoni akiwemo marehemu huyo. Polisi katika jitihada za kumtoa katika basi Walisema kwamba marehemu huyo ambaye jina lake halikupatikana mara moja, wakati wa kushuka hakuonekana na kisu aina ya sim