DINI YA AJABU YAIBUKA KIGOMA,YAKAZA WATU KWENDA SHULE NA HOSPITALI
Dini mpya iitwayo Matengenezo inayozuia waumini wake kwenda sekondari na hospitali, imeingia wilayani Kakonko mkoani Kigoma. Inakataza waumini wasiende sekondari na hospitali, kwa madai kuwa Biblia inawakataza kufanya hivyo. Mkuu wa Wilaya hiyo, Peter Toima alibaini hayo juzi katika Kijiji cha Rumashi Kata ya Nyabibuye wilayani humo. Alikuwa kwenye ziara katika shule za sekondari za wilaya hiyo mpya, ambapo kwanza aligundua wanafunzi wengi hawajaripoti shuleni kuanza Kidato cha Kwanza. Toima alipohoji kulikoni hawajaripoti katika shule walizopangiwa huku wale walioandikishwa darasa la kwanza, pia nao hawaripoti, alielezwa kuwa sababu za kiimani zinazokataza wengine kusoma. Mkuu huyo wa Wilaya alikatiza ziara yake na kuanza msako wa kuwasaka wanafunzi hao ambao hawajaripoti shuleni pamoja na waumini wa dini hiyo ya Matengenezo. Alisema aliamua kufanya hivyo, kwa sababu dini hiyo inawakosesha watoto haki yao ya msingi na kukiuka sheria