ANGALIA PICHA MTOTO WA MAAJABU ALIYEZALIWA KATIKA HOSPITALI YA MKOA WA SINGIDA.
WADAU KUMRADHI KWA PICHA IFUATAYO HAPO CHINI KAMA ITAWAKWAZA. Mtoto mchanga aliyezaliwa akiwa hana mikono, kifua, shingo na kichwa, ila ana anasehemu ya miguu , makalio na tumbo akiwa katika hospitali ya mkoa wa Singida muda mfupi baada ya kuzaliwa na Bi. Amina Bilau mkazi wa kijiji cha Mtamaa tarafa ya Mwakonko manispaa ya Singida . (Picha na Nathaniel Limu). Na Nathaniel Limu. Mtoto mchanga amezaliwa katika hospitali ya mkoa wa Singida akiwa hana baadhi ya sehemu za mwili kuanzia kifuani hadi kichwani. Kaimu mganga mfawidhi wa hospitali ya mkoa wa Singida Dkt. Joseph Malunda, amesema hospitali ya mkoa wa Singida ni mara ya kwanza kuzaliwa kiumbe kama hicho tangu kuwa hospital ya mkoa. Dkt. Malunda amesema watoto hao ambao wamezaliwa mapacha wote wa kike wakiwa na miezi saba, mmoja ambaye ana viungo vyote alikuwa na kilo 1.3 lakini alifariki baada ya saa sita kupita. Dkt. Malunda amesema baada ya mama mzazi wa watoto hao Amina Bilau kujifungua