Ndoa ya pili ya Joyce Kiria na Henry Kilewo. Na Mwandishi Wetu MTANGAZAJI wa Runinga ya Channel 5, Joyce Kiria amefunguka na kufichua siri ya ndoa zake mbili alizofunga, Risasi Mchanganyiko lina habari kamili. Ndoa ya kwanza ya Joyce na DJ Nelly. Kwa mujibu wa mtandoa mmoja wa kijamii, Joyce alisema kwamba ndoa yake ya kwanza aliyofunga na Nelson Nkongo ‘DJ Nelly’ walichangisha watu ili kufanikisha ndoa hiyo. “Kama desturi na utamaduni wetu tulichangisha lakini pamoja na michango mingi, tuliingia gharama zetu na kama haitoshi tulikopa na baada ya shughuli tulianza kupiga miayo ya njaa, hatukuwa na fedha tena na madeni yakatuandama,” alisema Joyce. Joyce na Kilewo siku ya ndoa yao. Mtangazaji huyo wa Kipindi cha Wanawake Live alisema kwamba alijuta sana lakini ikafika hatua ndoa hiyo ikasambaratika. Akiizungumzia ndoa yake ya pili na Henry Kilewo, ambayo awali ilifungwa Bomani, Joyce alisema kwamba haikuwa na makeke na wala kuchangisha watu fedha.