Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba akifungua mkutano wa Baraza Kuu la Uongozi la CUF huko Buguruni, kulia ni Katibu Mkuu, Maalim Seif Sharif Hamad na Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Hamad Masoud Khamis Haji OMKR ā Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF, Profesa Ibrahim Lipumba amesema nchi inakumbwa na msukosuko mkubwa wa kiuongozi na Rais wa Jamhuri ya Muungano, Jakaya Kikwete anapaswa kuchukua maamuzi ya busara ya kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa hivi sasa, ili kulinusuru Taifa. Profesa Lipumba amesema hayo leo (21/12/2013) wakati alipokuwa akifungua mkutano wa Kawaida wa Baraza Kuu la Uongozi la CUF, unaofanyika Makao Makuu ya chama hicho Buguruni, Dar es Salaam.Amesema msukosuko huo unaonekana wazi kufuatia taarifa ya Ripoti ya Kamati ya Bunge ya Maliasili, Ardhi na Mazingira, Hali ya kukosekana kwa uwazi katika Mchakato wa katiba na Hatma ya Uchaguzi Mkuu 2015, pamoja na malalamiko ndani ya CCM kwamba kuna Mawaziri wengi ndani ya Serikali ni mizigo. ...