WOLPER AELEZEA ALIVYOFILISIWA
NYOTA wa filamu Bongo, Jacqueline Wolper amefunguka kuwa filamu yake aliyoitoa kumuenzi marehemu Steven Kanumba iitwayo After Death ilimlostisha kwa kuwa ilimpatia hasara kubwa. Jacqueline Wolper. “Nilitengeneza ile filamu kwa hela nyingi kidogo, kama milioni 35 au 40, nikafanya na uzinduzi pale Leaders Club uliogharimu kama milioni 13 hivi, lakini nilipokwenda kwa Wahindi wakanipa shilingi milioni 25, yaani inakatisha sana tamaa,” alisema muigizaji huyo wakati alipofanya mahojiano maalum na waandishi wetu. Alisema hasara aliyoipata na ambayo hata wasanii wenzake huipata inatokana na uwepo wa wasambazaji wachache wa kazi za wasanii, kitu kinachowafanya watu hao kujipangia bei bila kujali gharama ambazo wameingia katika utengenezaji wake.