Posts

Hatimaye sababu za Wema Sepetu na Diamond kurudiana zajulikana, soma mchezo mzima ulivyokuwa!

Image
Baada ya kimya kirefu juu ya tetesi za kurudiana kwa mwanadada Wema Sepetu na Diamond kuzagaa kwenye mitandao hasa baada ya picha za wawili hao waliokuwa wamechana kuonekana wakila “bata” pamoja maeneo ya Hong Kong huko kwenye bara la Asia, sababu na ukweli wa namna wawili hao walivyorudiana umewekwa waza baada ya hivi karibuni msanii diamond platnumz kuzungumza na mtandao wa GPL na kuelezea jinsi tukio hilo zima lilivyokuwa. Katika mazungumzo hayo Diamond alitaja mambo haya makuu matano yaliyosababisha mpaka aamue kurudisha vikosi kwa mwanadada Sepetu. Sababu ya kwanza (1) – UKARIMU WA WEMA Diamond alisema kuwa alipotua Hong Kong alishangaa kukutana na mapokezi ya Wema kwenye uwanja wa ndege jambo ambalo hakulitegemea. “Alinionesha ukarimu wa hali ya juu mno. Wakati tulipokuwa hapa Bongo tulikuwa hatusalimiani. “Kuna vitu vingi vya ajabu vilitokea huko nyuma kati yangu na Wema. Sikufikiria wala kuwaza kama anaweza akawa mkarimu kwangu kiasi kile. A...

Diamond, Davido, Mohombi na Nay wa Mitego kufanya show ya bure Leaders Club leo saa tisa mchana

Image
Kutokana na kutokea hitilafu ya umeme Alfajiri ya leo kwenye show ya Serengeti Fiesta Dar, iliyopelekea baadhi ya wasanii waliokuwa wakitarajia kupanda jukwaani kutumbuiza akiwemo Davido, Mohombi, Diamond, Nay wa Mitego na wengine kushindwa kupanda, leo kuanzia saa tisa, wasanii hao watapanda tena jukwaani kuzikonga nyoyo za mashabiki wao bila kiingilio chochote. Ni katika uwanja ule ule, jukwaa lile lile la Serengeti Fiesta Dar es Salaam ambapo Diamond,Davido,Mohombi pamoja na Nay wa Mitego watapanda kuanzia saa 9 jioni mpaka saa 12. Show hiyo ya bure itapambwa pia na bendi ya Twanga Pepeta. -Habari kwa hisani ya bongo5

Tamasha la Serengeti Fiesta 2013 lilivyowasha moto usiku jana ndani ya viwanja vya Leaders Club

Image
KAMA ULIKUWEPO ULISHUHUDIA KAMA HUKUWEPO USIJALI PATA MATUKIO KWA PICHA HAPA , NA USISAHAU KULIKE UKURASA WETU WA FACEBOOK

"Sijawahi vua nguo na kufanya mapenzi na mwanaume yeyote tangu niachane na Diamond"...Jokate Mwegelo

Image
Mtangazaji wa Channel O mwenye mvuto wa aina yake, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ amefunguka kuwa tangu amwagane na mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond’ hajawahi kungonoka na mwanaume mwingine. Penzi la Jokate na Diamond lilichanua kwa takriban miezi miwili mwaka jana wakati Kidoti alipomwagana na aliyekuwa mpenzi wake, mcheza kikapu wa Ligi ya NBA ya Marekani, Hasheem Thabit. Alipoulizwa anamudu vipi hisia za matamanio ya kufanya mapenzi, Jokate alisisitiza kuwa kazi pekee ndiyo silaha kubwa ya kumuepusha na vishawishi ingawa anatambua upo umuhimu wa kuwa na mpenzi. “Akitokea mkweli, nipo tayari ingawa hadi sasa hata sijajua nani anaweza kuwa kama alivyokuwa Hasheem, nilimpenda sana,” alisema.

Rais Kikwete awatoa hofu watanzania kuhusu sakata la Mafuta....Amesema kwamba hiyo siyo mali ya wazungu, ni yetu watanzania

Image
RAIS Jakaya Kikwete amewatoa hofu Watanzania kwamba kuwaruhusu wawekezaji wa nje kufanya utafiti wa mafuta na gesi nchini, kuna hasara kubwa itakayolikumba taifa. Pia amewataka kupuuzia dhana kwamba kuwaruhusu wawekezaji hao kunaweza kusababisha wahamishe rasilimali za gesi na mafuta zitakazogunduliwa kunufaisha mataaifa ya nje. Rais Kikwete alitoa kauli hiyo, Dar es Salaam jana kabla ya kuzindua awamu ya nne ya ugawaji vitalu baharini katika kina kirefu Kaskazini mwa Ziwa Tanganyika. “Kumekuwa na maneno mengi kuwa mfumo huu wa sasa wakutoa leseni za utafutaji wa mafuta na gesi kwa wawekezaji wa nje, kuwa hakuwanufaishi Watanzania. Alisema sheria, mfumo na mikataba iliyowekwa haiwezi kuruhusu mianya hiyo ya kupata hasara na kwamba asilimia 75 ya faida itakayopatikana baada ya wawekezaji kurudisha gharama zao za utafiti, itakuwa ni ya taifa na asilimia 25 ndiyo itakayokuwa stahili yao. Kwa mujibu wa Rais Kikwete wapo baadhi ya watu wanaoeneza maneno potofu, kw...

Wema Sepetu atumia milioni 13 kuibadili ngozi yake akiwa China baada ya kuharibiwa sana na Mkorogo

Image
IMEVUJA! Kumbe ile safari ya nchini China ya Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu ‘Madam’ lengo lilikuwa kubadili ngozi ya mwili wake katika mwonekano mpya ambayo ilishaharibika kwa mkorogo. Wema Sepetu ‘Madam’. Kwa mujibu wa chanzo chetu makini, staa huyo aliingia nchini humo na mdogo wake aitwaye Bite ambaye kazi yake kubwa ilikuwa kufanya mawasiliano na nyumbani, Tanzania endapo lingetokea baya wakati wa zoezi hilo. KWA NINI ALIAMUA KUDILI NA NGOZI? Mpashaji wetu aliliambia Amani kwamba, Wema alichoshwa na ‘vijembe’ vya watu mbalimbali wakiwemo wabaya wake kuwa ngozi yake imebabuka kwa kutumia mkorogo kupitiliza. Miguu ya Wema Sepetu ‘Madam’ kabla ya kubadili ngozi. “Kuna wakati Wema alikuwa akikosa amani kutokana na maneno ya watu, wengine waliokuwa wakimrushia vijembe ni masupastaa wenzake, ndiyo maana akaamua kwenda China kubadili ngozi yake iwe na mwonekano mpya,” kilisema chanzo. Habari zaidi zilidai kwamba, supastaa huyo hakupenda kabisa Wabong...

CHADEMA wasalitiana na kufukuzana....Mbowe apigwa ngumi baada ya kudaiwa kuiba milioni 80 za chama , polisi waingilia kati huko Arusha

Image
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kanda ya Kaskazini, kimemsimamisha Uongozi Mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Arusha Samson Mwigamba kwa madai ya kukihujumu chama hicho. Taarifa ambazo tumezipata kutoka ndani ya kikao cha Baraza la uongozi kanda ya Kaskazini, kilichofanyika katika Hotel ya Corridor Spring leo usiku, zimedai uamuzi wa kusimamishwa Mwigamba umefikiwa na Kikao hicho baada ya kuwasilishwa kwa vielelezo kadhaa vya Mwigamba na yeye kukiri kuwa ni vyake huku vingine vikimuonyesha kuwa ndiye mmiliki wa Akaunti ya Jina la ‘Maskini Mkulima’ ambalo limekuwa likitumika kukichafua chama kwenye mitandao ya kijamii. Hakuna kiongozi ambaye amekuwa tayari kuzungumzia suala hili kiofisi, lakini taarifa za uhakika ambazo tumezipata kutokana na maamuzi ya kikao hicho zimebainisha kuwapo kwa maamuzi hayo pasipo shaka. “Kikao hicho kimemsimamisha Uongozi kupisha uchunguzi dhidi ya tuhuma zinazomkabili, hivyo kuanzia sasa mwigamba siyo kiongoz...

DIAMOND PLATINUM ALIVYOPOKELEWA AIRPORT AKITOKEA CHINA

Image
Nasibu Abdul 'Diamond Platnumz' (katikati) akilakiwa na m ama yake mzazi, Sanura Kassim 'Sandra' alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere akitokea nchini China leo. Mama Diamond akisalimiana na rafiki wa Diamond aliyetua naye leo.… Nasibu Abdul 'Diamond Platnumz' (katikati) akilakiwa na m ama yake mzazi, Sanura Kassim 'Sandra' alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere akitokea nchini China leo. Mama Diamond akisalimiana na rafiki wa Diamond aliyetua naye leo. Diamond akipozi na mama yake mzazi alipowasili uwanjani hapo majira ya saa nane mchana leo. Bi. Sandra akimlaki Rommy Jones uwanjani hapo. MSANII mahiri wa Muziki wa Kizazi Kipya, Nasibu Abdul 'Diamond Platnumz' leo ametua nchini akiambatana na ndugu yake pamoja na rafiki yake wakitokea nchini China. Msanii huyo pamoja na alioambatana nao, wamewasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere majira y...

DANCER WA ''BOB JUNIOUR'' MWENYE UMRI MDOGO KULIKO WOTE AKUTWA KWENYE KONA "AKIBAMBIA"

Image
 DANCER wa Bob Juniour anaetambulika kwa jina maarufu Nurdin A.k.a dogo T, Akutwa live akijiandaa kufanya mambo ya wakubwa na dada huyo pichani jina lake limehifadhiwa...!!! Dogo alishangaa ghafla mwanga wa Camera kitu ambacho hakukitegemea na hapo ndipo zoezi lao lilipoishia, Tukio hili lilitokea hivi karibuni katika Gloserry flani jijini Dar Es Salaam. Kitendo hicho kimemsababishia adhabu kali ya kutoshiriki baadhi ya Show zitakazofanywa na kundi hilo lililochukua ushindi katika mpambano wa Dance mia mia mwaka huu na kusani mkataba kwa Mr Chocolate ( Bob Juniour ) Rais wa Masharobaro

Wastara Juma afichua siri.....Adai kioo kilimfanya amvulie nguo Sajuki

Image
Wastara amefichua siri kwamba kioo ndicho kilisababisha aanzishe uhusiano wa mapenzi na marehemu Juma Issa Kilowoko ‘Sajuki’ aliyefariki Januari 2, mwaka huu.. Wastara aliweka bayana kuwa marehemu Sajuki ambaye alikuwa mumewe, hakuwahi kumtongoza lakini kioo ndiyo kilikuwa chanzo kilichosababisha wajikute wameingia dhambini kwa mara ya kwanza. Akizungumza na gpl, Wastara alisema kuwa siku hiyo walikuwa wakifanya mazoezi ya filamu moja (hakutaja jina) nyumbani kwake na Sajuki alikuwa muongozaji wa sinema hiyo. “Ilikuwa ni usiku wa manane tukiwa nyumbani kwangu tukifanya mazoezi ya filamu moja, sasa ilikuwa ni scene ya mapenzi tukawa mbele ya kioo huku tumekumbatiana. “Tukaendelea hivyoo, mmh! Sasa tulivyokitazama, tukahisi tunaendana. Tukaendelea kujifanyia tathmini na ghafla tukajikuta tunafanya kweli, kioo kilisababisha tukajikuta tunafanya mapenzi,” alisema Wastara kwa uso wa aibu..

DENTI WA KIDATO CHA NNE AKIMBIZWA HOSPITALINI MARA BAADA YA KUCHAPWA VIBOKO 100 NA MWALIMU WAKE

Image
Mwanafunzi wa shule ya sekondari Idodi wilayani Iringa amelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Iringa kwa madai ya kupigwa viboko zaidi ya 100 na mtu anayedaiwa kuwa ni mwalimu wa shule hiyo na kufungiwa katika bweni kwa siku 3 ili kuificha siri hiyo. Tukio hilo linakuja wakati harakati mbalimbali za kijamii na asasi za kiraia zikipiga kelele kupinga vitendo vya ukatili wakati jeshi la Polisi likianzisha dawati la jinsia kwa ajili ya kutokomeza masuala hayo. Ni mwanafunzi Lusinde Nyaulingo, wa kidato cha tatu katika shule ya sekondari Idodi, ambaye anaugulia maumivu makali katika Hospitali hii ya rufaa ya mkoa wa Iringa, word namba tano ya majeruhi, kutokana na ukatili uliosababisha majeraha sehemu mbalimbali za mwili wake, hasa maeneo ya mapaja, makalio na mgongo, baada ya kupigwa kwa tuhuma za kuchukua simu ya mwanafunzo mwenzie, jambo linalomfanya mwanafunzi huyu apoteze muda mwingi wa masomo wakati akipatiwa matibabu ili kurudisha afya yake. Lusinde ...

MUUZA CHIPS AMTEKA MTOTO TANDALE DAR NA KUTOKOMEA NAE KUSIKOJULIKANA

Image
MTOTO wa kike mwenye umri wa miaka mitatu, Maryment Ibrahim ambaye anaishi Tandale jijini Dar es Salaam, hivi karibuni alipatwa na masahibu makubwa baada ya kutekwa nyara na kutoroshwa hadi Gairo mkoani Morogoro huku mtekaji akidaiwa kutaka apewe shilingi milioni 6 ili amuachie. Mama mzazi wa mtoto aliyetekwa akiwa na mwanaye. Tukio hilo la kusikitisha lilitokea Oktoba 16 mwaka huu baada ya kijana mmoja, anayefanya biashara ya kuuza chipsi anayejulikana kwa jina la Issa Ramadhani, kudaiwa kumchukua mtoto huyo aliyekuwa akicheza nyumbani kwao na kutoweka naye kabla ya wazazi wake kubaini na kwenda kutoa taarifa kituo cha Polisi Kijitonyama ‘Mabatini’. Awali, ilidaiwa Ramadhan alikuwa na tabia ya kuwachukua watoto wadogo wa mtaani hapo na kuondoka nao na kuwarudisha baadaye, kitu kilichowafanya wazazi wa mtoto huyo kutokuwa na wasiwasi. Mtuhumiwa wa utekaji. Wakizungumza na mwandishi wetu, wazazi wa mtoto huyo walisema waliamua kutoa taarifa polisi na ...

Msanii wa bongo movie anusurika kuliwa KIBOGA.....Alizidisha pombe na kujikuta chooni akiwa mtupu.

Image
Muigizaji wa filamu za kibongo anayejulikana kwa jina la Danny Cloud maarufu kama Danny mtoto wa mama ambaye alipata umaarufu wa jina hilo kupitia filamu ya mtoto wa mama amenusurika kubakwa ( kuliwa kiboga ) Akizungumza na mpekuzi wetu, rafiki wa karibu wa msanii huyo alidai kwamba Danny alikuwa maeneo ya Bilcanas ambapo alipewa ofa ya pombe na jamaa zake... Rafiki huyo alidai kuwa, baada ya kupewa ofa hiyo adimu, msanii huyo alianza kuiparamia pombe mfano wa mtu mwenye kiu kali ya maji, hali iliyomfanya asijitambue na kuanza kuvua nguo... "Kuna wakati Danny alinyanyuka na kuelea chooni huku akipepesuka...Alipofika huko alidondoka na kulala huko huko chooni, hali iliyowafanya vibaka watake kumla kiboga"...Alisema huyo rafiki yake na kuongeza: "Baada ya kimya kirefu, ilibidi tukamwangalie ambapo tuliwakurupusha vijana watatu wakiwa wameshamvua nguo"