Taarifa kwa mujibu wa ITV — Wanafunzi wawili wa kidato cha kwanza katika shule ya sekondari Matombo katika wilaya ya Morogoro wamejeruhiwa, baada ya kulipukiwa na kitu kinachosadikiwa kuwa ni bomu, wakati wakitoka shuleni. Wanafunzi hao waliojeruhiwa katika sehemu mbalimbali za miili yao ni Luciani Juma (14) na Anthonia Charles (15), wakazi wa kijiji cha Konde, Tarafa ya Matombo wilayani Morogoro, ambapo Luciani aliyelazwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro kwa matibabu, ameiambia ITV kuwa walikumbwa na tukio hilo wakati wakitokea shuleni, ambapo njiani walikutana na kitu mfano wa balbu ya tochi ambacho hata asubuhi wakati wa kwenda shule walikiona na kukipuuza, ndipo mmoja wawanafunzi alikirushia ganda la muwa aliokuwa akila, na kililipuka na kutoa mshindo mkubwa. Daktari anayemtibu Lucien katika wadi namba moja ya hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro, aliyejulikana kwa jina moja Dk. Francis amesema majeruhi huyo anaendelea vizuri, na amepata majeraha...