Posts

WAASI CHA FDLR NDIYO KINACHODAIWA KUWA CHANZO CHA KUZOROTA KWA MAHUSIANO MAZURI BAINA YA RAIS JAKAYA KIKWETE NA RAIS POUL KAGAME

Image
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Rais Paul Kagame wa Rwanda wakati walipokutaba na kufanya mazungumzo ya faragha, katika Hoteli ya Munyonyo Commonwealth Resort, jijini Kampala, Uganda. UHUSIANO tete baina ya Tanzania na Rwanda bado unaendelea kupita chini kwa chini, licha ya viongozi wakuu wa nchi hizo kukutana juzi mjini Kampala, Uganda na kufanya mazungumzo ambayo hayakufika mwisho. Uhusiano huo ulizorota baada ya Rais Jakaya Kikwete kumshauri Rais Paul Kagame, kukutana na waasi wa kikundi cha FDLR kinachopigana mashariki mwa nchi ya Demokrasia ya Kongo (DRC).   Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe alisema marais hao walikutana juzi ambapo kila mmoja aliwasilisha dukuduku lake kwa mwenzake.     “Walikutana na walipotoka walionyesha nyuso za furaha, kwa kuwa kila mmoja aliwasilisha dukud uku lake. Kila mmoja alieleza j

MWANAMKE ALIEKAMATWA NA DAWA ZA KULEVYAHUU NDIO UTHIBITISHO WAKE WA URAI

Image
 Anthonia Ngaoja

Aibu: Mume amruhusu mkewe AJIUZE ili wapate pesa ya chakula

Image
KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida, hivi karibuni mwanamke mmoja aliyejitambulisha kwa jina moja la Aisha (26), mkazi wa Tabata, Dar es Salaam alinaswa akifanya ukahaba na kudai kwamba ana ruhusa kutoka kwa mumewe ambaye hakumtaja jina. Tukio hilo la aibu lilitokea Afrika Sana, Sinza jijini Dar ambako Aisha alisema ndiko anakofanyia biashara yake hiyo licha ya kuishi na mumewe mbali.   Mwanamke huyo ambaye hakuweka wazi kama ana watoto au la, alisema hayo kufuatia kuzuka kwa varangati la nguvu baada ya wanahabari  kumkuta yeye na mwanaume kwenye jumba moja bovu lililopo mbele kidogo ya Kituo cha Afya cha Kijitonyama, jijini Dar.   Baada ya kumulikwa na mwanga wa kamera na kubaini wameingiliwa , ndipo mwanamke huyo alikurupuka kwa hamaki na kusema:   “Pigeni hizo picha mnadhani nani ana wasiwasi. Kwa taarifa yenu mimi nina mume na mume wangu ndiye aliyeniruhusu nijiuze ili tupate pesa ya kula. “Sasa nyinyi kama mnadhani mume wangu akiona picha zangu atani

RAIS KIKWETE ZIARANI MISUNGWI MKOANI MWANZA

Image
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia ngoma za utamaduni wakati alipowasili katika Wilaya ya Misungwi Mkoani Mwanza kuanza ziara ya kikazi    Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akipanda mti wa kumbukumbu muda mfupi baada ya kuzindua rasmi Shule ya msingi Ntulya,iliyopo kata ya Mondo, Wilayani Misungwi,Mkoa wa Mwanza.   Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na bvaadhi ya watoto waliohudhuria sherehe za ufunguzi wa Shule ya Msingi Ntulya,katika kata ya Mondo,wilayani Misungwi   Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa amembeba motto Paulo Muhangwa muda mfupi baada ya kuzindua shule ya Msingi Ntulya wilayani Misungwi,Mkoani Mwanza   Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalmiana na baadhi ya wauguzi katika hospitali ya wilaya ya Misungwi wakati wa uzinduzi wa huduma ya X Ray katika hospitali hiyo, Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezoi katika hospitali ya wilaya ya Misungwi wakati wa uzinduzi wa huduma ya X Ray kat

Mbunge wa Mbeya maarufu kwa jina la SUGU ajisalimisha polisi baada ya kutafutwa kwa siku mbili

Image
BAADA ya Jeshi la Polisi mkoani Dodoma kumsaka kwa siku mbili bila mafanikio mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi, maarufu kama Sugu (CHADEMA), akidaiwa kumpiga na kumjeruhi mmoja wa askari wa Bunge, hatimaye alijisalimisha mwenyewe jana jioni. Taarifa zilizotufikia wakati tunakwenda mitamboni, Sugu alikwenda polisi akiongozana na Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, na wabunge Tundu Lissu (Singida Mashariki), John Mnyika (Ubungo) na Joshua Nassari (Arumeru Mashariki). Akizungumza na  mwandishi wetu, Mnyika alisema kuwa Sugu hakukamatwa bali alijipeleka mwenyewe polisi kwa hiari yake na kwamba jioni hiyo majira ya saa 1:10 alikuwa akiandikisha maelezo yake. Wakati Sugu akijisalimisha, wanasheria wa Bunge nao walikuwa wamejifungia kuangalia namna ya kumkabidhi mbunge huyo mikononi mwa sheria. Juzi na jana viwanja vya Bunge vilitawaliwa na idadi kubwa ya polisi waliotumwa kumkamata Sugu lakini mpaka Bunge linaahirishwa jioni haikujulikana ni wapi alikokuw

Serikali yasalimu amri na kukubali kulipa mishahara ya wafanyakazi wa TAZARA waliokuwa wamegoma

Image
HATIMAYE serikali imesalimu amri na kuamua kuwalipa mishahara ya miezi minne wafanyakazi wa Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) waliogoma wakishinikiza kulipwa stahiki zao. Uamuzi wa kuwalipa wafanyakazi hao ulitangazwa jana bungeni na Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe, alipokuwa akitoa kauli ya serikali kuhusu mgomo wa wafanyakazi hao ulioanza Agosti 23 mwaka huu. Dk. Mwakyembe alisema serikali ilifanya mazungumzo na serikali ya Zambia ambayo imeshatuma dola milioni tano ambazo ni zaidi ya sh bilioni nane huku Tanzania ikitoa sh bilioni mbili kwa TAZARA. Alisema fedha hizo zilizopatikana pamoja na dola milioni 3.17 ambazo TAZARA inazidai kutoka kwa wateja wake mbalimbali zinatosha kurejesha hali ya kawaida katika mamlaka hiyo. “Tayari wafanyakazi wameshalipwa mshahara wa Mei mwaka huu, ifikapo Septemba 9, watakuwa wameshalipwa mishaahara yao ya Juni, Julai na Agosti,” alisema. Mwakyembe alisema serikali inatarajia wafan

Msikiti wa Answar Sunna ulipo mjini DODOMA wateketea kwa moto mchana huu.

Image
Msikiti mkubwa wa  Answar Sunna  uliopo  barabara ya saba mjini Dodoma  umewaka  moto  mchana  huu  ikiwa  ni  muda  mfupi  baada  ya  swala  ya  mchana  kumalizika.... Akiongea  kwa  njia  ya  simu  na  Mpekuzi wetu, mmoja  wa  mashuhuda  walioshuhudia  tukio  hilo  amedai  kuwa  chanzo  cha  moto  huo  ni  moto wa  JIKO  la  wakazi  wa    ghorofa ya  juu  ya  jengo  la  msikiti  huo... Hata  hivyo, shuhuda  mwingine  aliyeongea  na  mtandao  huu  amedai    kuwa  chanzo  cha  moto  huo  ni  hitilafu  ya  umeme  iliyoanzia  ghorofa  ya  juu  ya  jengo  hilo.   Kwa  mujibu  wa  mashuhuda  hao, moto  huo  umefanikiwa  kudhibitiwa  na  jeshi  la  zima  moto  na  kwamba  hakuna  mtu  aliyepoteza  maisha  kutokana  na  moto  huo. Tunaendelea  kufuatilia  undani  wa  tukio  hili.

Picha tano za yule daktari FEKI aliyenaswa katika hospitali ya KCMC

Image
      Daktari feki aliyenaswa katika hosptali ya KCMC aliyetambulika kwa jina la Alex Massawe akiwa amefungwa pingu mikononi mwake katika eneo la hosptali hiyo. Daktari Feki akisindikizwa na baadhi ya wafanyakazi wa hosptali ya KCMC kutoka katika moja ya wodi ambayo alikuwa 'akihudumia'. Ofisa Uhusiano wa KCMC, Gabriel Chisseo (kushoto) akimwonesha Daktari Feki, Alex Massawe. Daktari Feki akiwa katika gari la polisi tayari kupelekwa kituoni. Uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya KCMC ya mjini Moshi, jana ulimnasa 'Daktari Feki' aitwaye Alex Sumni Massawe (33). Massawe alikamatwa saa 5:00 asubuhi ndani ya hospitali hiyo na kuwekwa chini ya ulinzi mkali wa makachero wa Jeshi la Polisi waliokuwa wamevalia nguo za kiraia. Inadaiwa kuwa mtuhumiwa huyo alikuwa amepanga kumfanyia upasuaji wa ngozi, Makasi Tipesa ambaye anasumbuliwa na ugonjwa huo baada ya kukutana na mama yake na kumuahidi kumpatia huduma kwa malipo ya Sh. 200,000. Habari zinase

Daz Baba achanganyikiwa na kuwa KICHAA... wadau wasema ni Bangi na Madawa ya kulevya

Image
Habari kutoka kwa chanzo cha uhakika zinadai kuwa msanii wa zamani wa kundi Daz Nundaz na hitmaker wa ‘Figure Namba 8′ Daz Baba amechanganyikiwa kutokana na hivi karibuni kuonekana akifanya vitendo ambavyo havilingani na mtu mwenye akili timamu. Chanzo hicho kimesema Daz alionekana maeneo ya Morogoro akiwa katika hali iliyowatia mashaka ndugu, mashabiki wa muziki pamoja na wasanii wenzake. Rafiki wa karibu na Daz Baba amemwambia  mwandishi wetu  jana akiwa mkoani Morogoro kuwa hali ya msanii huyo ni mbaya na ana dalili zote za mtu ambaye  ni  Kichaa na amekuwa mtu wakuzunguka barabarani huku akifanya matukio ya ajabu. “Hivi juzi juzi Daz alienda nyumbani kwa Afande usiku, akapiga kelele sana, Afande akaamka na kumkuta Daz akiwa mchafu na akiongea maneno ambayo hayaeleweki, baadaye alitaka kumfanyia tendo baya kwa mfanyakazi wa kike wa Afande lakini hakufanikiwa, ila watu wakajua kweli Daz hayuko sawa,” alisema. Baada ya taarifa hiyo mwandishi wetu  a

Ripoti maalumu ya gazeti la MWANANCHI kuhusu vurugu zilizotokea jana bungeni

Image
  Jana, Bingwa wa Dunia wa uzani wa kati (super middle), unaotambuliwa na Shirikisho la Ngumi Duniani (WBF), Francis Cheka alitembelea Bunge baada ya kutwaa taji hilo karibuni na jana hiyohiyo, Bunge hilo lilishuhudia ngumi kavukavu katika vurugu kubwa pengine kuliko zote zilizowahi kutokea katika ukumbi wake. Katika masumbwi hayo yasiyo rasmi, Mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ anadaiwa kumpiga kichwa Askari wa Bunge na kumchania sare na kung’oa kipaza sauti. Mbilinyi jana alisema alikuwa anatafutwa na polisi huku akisema hilo limemshangaza akidai kwamba yeye ndiye aliyeshambuliwa na askari huyo. Vurugu hizo zilitokea baada ya Naibu Spika, Job Ndugai kuamuru kutolewa nje kwa Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe. Katika vurugu hizo Mbilinyi alibebwa juujuu na polisi hadi nje ya ukumbi huk

Polisi na Mawaziri wadaiwa kujihusisha na biashara haramu ya NGONO

Image
BAADHI ya mawaziri na polisi wametajwa kuwa ni wateja wakubwa wa wanawake wanaouza miili yao, maarufu kwa jina la Changudoa. Hayo yameelezwa jana na Jukwaa la Wanaharakati Wanawake Vijana (YFF), walipokuwa wakiwasilisha ujumbe wao kwa njia ya sanaa ya ngonjera, katika tamasha la 11 la Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) linaloendelea eneo la Mabibo jijini Dar es Salam. Wanaharakati hao wanawake vijana, walisema tatizo liko kwenye jamii ambayo inawahukumu changudoa bila kujiuliza kuwa wateja wao ni kina nani. ‘’… jamani hebu tuulizane, kwani changudoa mteja wake nani? Kwa taarifa yako, mawaziri, wabunge na mapolisi wamo; na hii ni changamoto kwa jamii,’’ walisema wanaharakati hao.   Akizungumza na Tanzania Daima baada ya kutoka jukwaani, kiongozi wa wanaharakati hao, Aisha Kijavala, alisema wameamua kutoa ujumbe huo kwa washiriki wa tamasha hilo ili jamii ijue wateja wa changudoa hao. Alisema wateja hao wakiacha kununua ngono, pia wanawake wanaouza miili

Video ya ngono ya wabongo yavuja.....Ni siku chache baada ya ile ya Mrisho Ngasa kunaswa

Image
Baada  ya  video  ya  ngono  ya  Mrisho  Ngasa  kuvuja  na  kusambaa  kwa  kasi, video  nyingine  ya  wabongo  imevuja  wakifanya  uchafu  wao  huku  wakijirekodi..... <<VIDEO  IKO  HAPA,  BOFYA  HAPA>>

Hali ya msanii Banza Stone ni mbaya

Image
NGULI wa muziki wa Dansi Bongo, Ramadhan Masanja ‘Banza Stone’ ameanza kuugua tena ambapo tangu Sikukuu ya Iddi hadi sasa yupo hoi kitandani. Akizungumza kwa huzuni na mwandishi wetu, Banza alisema alipomaliza shoo ya Sikukuu ya Iddi na Bendi ya Extra Bongo, alianza kuugua, akaenda Hospitali ya Yemen iliyopo Sinza, Dar ikagundulika ana malaria kali ambapo alipewa dozi ya siku saba. “Nilipewa dawa za malaria nikameza nikaambiwa baada ya siku saba nitajisikia vizuri lakini mpaka sasa sioni mabadiliko yoyote, bado mwili unaniuma sana, nashinda kitandani kila siku hivyo muziki basi kwa sasa,” alisema Banza na kuongeza:   “Najua mashabiki wangu watanimisi lakini kwa sasa muziki nimepumzika, naomba mashabiki waniombee.”

Hatimaye mshindi wa Big Brother afanikiwa kumpata baba yake ( Ni yuleyule aliyemkana )

Image
Hatimaye teknolojia imefanikisha kuwakutanisha wazazi wa mshindi wa Big Brother Afrika ‘The Chase’ Dillish Mathews baada ya mwanaume mmoja aitwaye Abdi Galgayo Guyo kuja hadharani na kudai kuwa ni baba mzazi wa mshindi huyo wa The Chase. Siku moja tu iliyopita, Pulse iliandika habari kuhusu mwanaume wa Kenya aitwaye Abdi Galgayo Guyo aliyetembelea ofisi za Standard Media ya Kenya na kudai kuwa yeye ndiye baba mzazi wa mshindi wa BBA Th Chase.  Abdi ambaye kwa mujibu wa Standard ana asili ya Somalia alielezea jinsi alivyokutana na mama yake Dillish aitwaye Selma kati ya (April 1989) na (March 1990) alipoenda Namibia akiwa mmoja wa maaskari wa Kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa kilichopelekwa nchini humo kusimamia amani.   Habari hizo zilipokelewa kwa hisia tofauti na watu mbalimbali ambao wengi wao walionekana kuamini kuwa Abdi anazusha ili apate pesa, na Dillish alivunja ukimya kwa kutweet akimshangaa mwanaume huyo na kusema baba yake ana asili

MAANDAMANO YA KUMKUMBUKA MAREHEMU MWANGOSI MKOANI IRINGA

Image
Katibu wa IPC Francis Godwin akiongoza maandamano ya wanahabari na wadau huku akiwa juu ya gari na picha ya marehemu Daud Mwangosi. Maandamano ya wanahabari na wadau wa habari mkoa wa Iringa ya kumuenzi marehemu Daudi Mwangosi yakipita eneo ya Uhindini. Wanahabari Iringa katika maandamano ya kumuenzi marehemu Mwangosi jana. Wanahabari wa vyombo mbalimbali na wadau wa habari mkoa wa Iringa wakiwa katika maandamano ya amani ya kumuenzi aliyekuwa mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Iringa (IPC). Maandamano ya wanahabari na wadau wa habari yakipita eneo la soko kuu la manispaa ya Iringa.   Wananchi wakishuhudia maandamano hayo. Katibu Mtendaji wa IPC, Francis Godwin akitoa taarifa ya kuanza kwa maandamano ya kumuenzi marehemu Daud Mwangosi jana. Katibu wa IPC Francis Godwin (kushoto) akikabidhi picha ya marehemu Daud Mwangosi kwa Mwenyekiti wa IPC Frank Leonard (kulia), wanaoshuhudia ni Mzee Fulgence Malangalila na