Posts

bayern ni mabingwa wa UEFA Super Cup

Image
Bayern Munich imeshinda taji la EUFA Super Cup kwa kuichapa Chelsea mabao 5-4 kupitia mikwaju ya penalti katika mechi iliyochezwa jana usiku kwenye uwanja wa Eden Arena mjini Prague, Jamhuri ya Cheki. (P.T) Bayern Munich, ikiongozwa na kocha wao mpya, Pep Guardiola, imelipiza kisasi kwa kushindwa na Chelsea katika fainali ya Champions League mwaka 2012 baada ya kuifunga klabu hiyo mabao 5-4 kupitia mikwaju ya penalti kufuatia mtanange wa kuwania kombe la UEFA Super Cup kuishia sare ya mabao 2-2 baada ya muda wa ziada kumalizika. Bao la Bayern sekunde chache kabla mchezo kumalizika, liliufungua mlango wa kuelekea ushindi kupitia penalti dhidi ya Chelsea chini ya kocha wao mpya, Jose Mourinho. Penalti zote tisa ziliutikisa wavu kabla mkwaju wa penalti wa mchezaji wa Chelsea, Romeu Lukaku, kuokolewa na kipa wa Bayern Munich, Manuel Neuer, na hivyo kuwapa ushindi mabingwa wa Ulaya, Bayern Munich, dhidi ya mabingwa wa ligi ya Ulaya, Chels

FRANCIS CHEKA NI MOTO WA KUOTEA MBALI.....AMGALAGAZA MMAREKANI VIBAYA MNO NA KUCHUKUA UBINGWA WA DUNIA

Image
 Mgeni Rasmi katika Mpambano wa Kimataifa wa kuwani Mkanda wa Ubingwa wa Dunia wa WBU,kati ya Mabondia Francis Cheka wa Tanzania na Phil Williams wa Marekani,Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo,Mh. Dkt. Fenella Mukangala (mwenye koti jeupe) akimvisha Mkanda wa Ubingwa huo,Bondia Francis Cheka baada ya kumshinda kwa Point Mpinzani wake,katika Mchezo uliomalizika usiku huu kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee,Jijini Dar es Salaam.Kulia ni Bingwa wa Zamani wa Masumbwi,Fransous Bhotha.  Bondia Francis Cheka wa Tanzania (kushoto) akimrushia makonde makali mpinzani wake,Phil Williams kutoka nchini Marekani wakati wa mpambano wao wa Kimataifa kuwania Mkanda wa Ubingwa wa Dunia wa WBU,uliofanyika usiku huu kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee,Jijini Dar es Salaam.Bondia Francis Cheka ameibuka kidedea baada ya kumchapa mpinzani wake huyo kwa Point. Bondia Phil Williams kutoka nchini Marekani (kulia) nae alikuwa akijibu mashambulizi kwa mpinz

LULU AJAZWA MAHELA MA MAPEDESHEE BAADA YA KUIMBA WIMBO YAHAYA WA LADY JAY DEE

Image
UIMBAJI stadi wa Wibo wa YAHAYA wa Nguli wa muziki wa Kizaki kipya Lady Jay Dee umemjaza mahela Msanii wa Filamu aliyejizolea umaarufu kwa miaka ya hivi karibuni, Elizabeth Michael ‘Lulu’ wakati akiimba wimbo huo na Jide wakati wa uzinduzi wa Video yake mpya na yakwanza kusimama peke yake ya FOOLISH AGE. Baada ya move hiyo kali ya dakika 120 iliyooesha ukali wa staa huyo kuoneshwa kwa dakika 20 tu na kubakisha zingine 100 kusubiri wateja kuziona majumbani kwao alipanda jukwaani kujitambulisha na kutoa shukrani kwa wamepenzi wa tasnia ya filamu nchini Tanzania kwa muitikio wao alipanda na kuimba wimbo huo wa Yahaya. Akianzia kuimba kiitikio cha wimbo huo akiwa Back Stage, Lulu aliwashangaza watu pale alipomudu vyema wimbo huo kiasi cha mashabiki ‘Mapedeshee’ wakiongozwa na Pedeshee Rich Rich, kupanda jukwaani na kumtunza fedha kibao ambazo hakika zilimpagawisha msanii huyo na mwisho wa wimbo huo alisema mziki unalipa. “Jamanieee kumbe mziki unalipa ile

WABUNGE WATAKA MBIO ZA MWENGE WA UHURU ZIFUTWE

Image
MBIO za Mwenge wa Uhuru nusura ziahirishe shughuli za Bunge baada ya baadhi ya wabunge kutaka zifutwe na hoja hiyo ijadiliwe bungeni.   Hata hivyo, suala hilo liligeuka shubiri kwa Waziri wa Nchi, Ofisa ya Rais (Utawala Bora), George Mkuchika, kuzomewa na kurushiwa maneno ya kejeli alipojaribu kuzitetea mbio hizo.   Chanzo cha mzozo huo kilitokana na maswali ya mbunge wa Musoma Mjini, Vicent Nyerere (CHADEMA), aliyeihoji serikali kama kuna uwezekano wa kutoukimbiza Mwenge katika maeneo ya watu wasiouhitaji.   Nyerere alisema watu wa wilaya ya Musoma, mkoani Mara, hawautaki Mwenge huo kwa sababu unachochea uhasama, chuki na upotevu wa rasilimali.   “Wakati wa mbio za Mwenge Musoma Mjini walilazimisha kuchukua magari ya halmashauri likiwemo la wagonjwa... huduma za afya zilisimama na hivyo kuleta chuki badala ya mwanga,” alidai.   Nyerere pia alitaka kujua nini faida za mbio hizo, bajeti yake ni kiasi gani kwa mwaka na matumizi yake kama yana

DIAMOND ATOA ZAWADI YA GARI KWA MZEE GURUMO

Image
Msanii mkongwe wa muziki wa dansi, Muhidin Gurumo akijaribu gari dogo alilokabidhiwa na mwanamuziki wa bongo fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond ‘ kutokana na kutambua mchango wake baada ya kustaafu kazi ya muziki. Muhidin Gurumo akipokea funguo ya gari kutoka kwa Diamond Gari alilozawadiwa mzee Gurumo.

DIAMOND NA LINAH WANASWA TENA WAKITOMASANA HADHARANI

Image
Staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ amenaswa na msanii mwenzake, Esterlina Sanga ‘Linah’ wakiwa kwenye mapozi ya kimahaba ambayo yametafsiriwa vibaya.   Katika tukio hilo lililojiri juzikati kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora ndani ya Tamasha la Serengeti Fiesta, Diamond alishuhudiwa akiwa amempakata Linah ndani ya basi huku mikono ya jamaa huyo ikishika maeneo nyeti.   Mara baada ya kutimba uwanjani hapo wakitokea hotelini tayari kwa kufanya shoo, Diamond na Linah walibaki kwenye basi wakiwa wamepakatana na hata msichana huyo alipomaliza shoo yake kali mishale ya saa 3: 00 usiku, alirejea mikononi mwa Diamond ambaye alimpachika mapajani. Kwa mujibu wa mashuhuda, kama kweli mchumba wa Diamond, Penniel Mungwilwa ‘Penny’ anakubali mambo kama hayo, basi atakuwa na roho ngumu au moyo wa chuma.   Siyo mara ya kwanza Diamond na Linah kuripotiwa wakiwa wamepozi kimahaba kwani mwaka jana walifanya hivyo wakiwa jijini Mbeya hivyo kutafsir

HAYA NDIO MATUKIO YA UZINDUZI WA "FOOLISH AGE" YA LULU MICHAEL

Image
            MSANII wa Filamu Bongo, Elizabeth Michael 'Lulu', usiku wa kuamkia leo amefanikisha zoezi la uzinduzi wa filamu yake mpya inayokwenda kwa jina la Foolish Age .   Baada ya move hiyo kali ya dakika 120 iliyooesha ukali wa staa huyo kuoneshwa kwa dakika 20 tu na kubakisha zingine 100 kusubiri wateja kuziona majumbani kwao alipanda jukwaani kujitambulisha na kutoa shukrani kwa wamepenzi wa tasnia ya filamu nchini Tanzania kwa muitikio wao alipanda na kuimba wimbo huo wa Yahaya. Akianzia kuimba kiitikio cha wimbo huo akiwa Back Stage, Lulu aliwashangaza watu pale alipomudu vyema wimbo huo kiasi cha mashabiki ‘Mapedeshee’ wakiongozwa na Pedeshee Rich Rich, kupanda jukwaani na kumtunza fedha kibao ambazo hakika zilimpagawisha msanii huyo na mwisho wa wimbo huo alisema mziki unalipa. Tukio la uzinduzi huo lilifanyika katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar, na kuhudhuriwa na mastaa kibao wa tasnia mbalimbali hapa Bongo, wakiwemo;

AIBU KWA TANZANIA.....MKUU WA JESHI LA POLISI TANZANIAI INSPEKTA JENERALI SAIDI MWEMA AIBIWA UPANGA WENYE THAMANI YA SH600 MILIONI JIJINI DAR ES SALAAM.

Image
  JESHI la Polisi limeingia katika kashfa nzito baada ya mkuu wake, Inspekta Jenerali Said Mwema, kuibiwa upanga wa dhahabu ambao ni mali ya Shirikisho la Wakuu wa Majeshi ya Polisi wa nchi za Kusini mwa Afrika (SARPCCO). Upanga huo wenye uzito wa takriban kilo tatu na wenye thamani ya zaidi ya fedha za Tanzania Sh600 milioni, ni kielelezo kwa nchi inayokabidhiwa uongozi wa SARPCCO. Mwaka jana Tanzania ilikuwa mwenyekiti wa SARPCCO, ambapo upanga huo ulikabidhiwa kw a IGP Mwema na Jenerali Magwashi Victoria ‘Riah’ Phiyega, ambaye ni Kamishna wa Taifa wa Polisi wa Afrika Kusini aliyekuwa amemaliza muda wake kwa wakati huo. Hilo ni tukio la pili la wizi la mali zinazohusu ofisi ya IGP, ambapo mwaka jana ndani ya ofisi hiyo kuliibwa kompyuta ndogo (laptop), ikiwa na taarifa muhimu za kipolisi. Hadi sasa hakuna taarifa za kupatikana kwa kompyuta hiyo. IGP Mwema alikabidhiwa upanga huo Septemba 5, 2012, katika mkutano saba wa SARPCCO uliofanyika