Posts

TACAIDS YATOA TAKWIMU ZA UKIMWI...MKOA WA NJOMBE UNAONGOZA UKIFUATIWA NA IRINGA

Image
TUME ya Kudhibiti UKIMWI nchini (TACAIDS) imesema mkoa wa Njombe unaongoza kwa kuwa na maambukizi makubwa ya Virusi vya UKIMWI kwa asilimia 14.8 ikifuatiwa na Iringa kwa asilimia 9.1. Mkoa wa Mbeya unashika nafasi ya nne kwa asilimia tisa ukifuatiwa na Ruvuma (7.2), Shinyanga (7.4), Dar es Salaam (6.9) Rukwa (6.2), Katavi (5.9), Pwani (5.9),Tabora (5.1), Kagera (4.8) na Geita (4.7). Msemaji wa TACAIDS, Glory Mziray alisema hayo jana Dar es Salaam na wakati akizungumza na waandishi wa habari. Mikoa mingine na viwango vyake ni Mara (4.5), Mwanza (4.2),Mtwara (4.10), Kilimanjaro (3.8), Kigoma (3.4), Simiyu (3.6), Morogoro (3.8), Singida (3.3), Dodoma (2.9), Manyara (1.5), Lindi (2.9), Tanga (2.4), Unguja (1.9) na Pemba (0.3). Alisema takwimu hizo zinatokana na utafiti uliofanyika mwaka juzi hadi mwaka jana. Kutokana na matokeo hayo, alisema maambukizi ya UKIMWI yamepungua kwa kasi ndogo. Alisema watanzania walioonesha kuwa na ufahamu sahihi wa elimu kuhusu Virusi vya uki...

MAKAHABA WAENDELEA KUKICHAFUA CHUO KIKUU CHA DODOMA

Image
Ongezeko  la  makahaba  mjini  Dodoma  limeendelea  kuwa  kero  kwa  chuo  kikuu  cha Dodoma  na  wanafunzi  wake  kwa  ujumla.... Kero  hiyo  imekuwa  ikisababishwa  na  baadhi  ya  makahaba  hao  kujifanya  wanafunzi  wa  chuo  hicho  kwa  lengo la kujiimarisha  kibiashara...  Takribani miezi mitatu  iliyopita, kahaba mmoja alinasawa  na polisi   mjini Dodoma akijiuza kwa  kujinadi  kuwa  yeye  ni  mwanafunzi wa mwaka wa pili chuo kikuu cha Dodoma ..  Baada  ya  mahojiano  ya  kina  na Polisi Central,  ilibainika  kuwa  kahaba  huyo  hakuwa  Mtanzania  na  hakuwa  mwanafunzi  wa  chuo  chochote  hapa  nchini  na  badala  yake  alikuwa...

WANANCHI WAPEWA KICHAPO KIKALI NA MGAMBO BAADA YA KUMUUA PUNDA NA KUMTUPA MTONI HUKO MBEYA

Image
 Wakicharazwa viboko na mgambo baada ya kukamatwa.  Fimbo hizo ni silaha walizokuwa wakizitumia kukaidi sheria bila shuruti na kujeruhi kila aliyewakaribia huko Chilulumo wilaya ya Momba mkoani Mbeya. Watu wanaotuhumiwa kumwua punda na kisha kumtupa kwenye mto ambao wananchi wa kando kando wanayatumia maji yake kwa shughuli mbalimbali huko Momba, Mbeya, wamekamatwa na kuadhibiwa vibaya kwa kucharazwa viboko na  mgambo.

HAWA NDO MASTAA WA KIKE BONGO WANAOJIHESHIMU...

Image
BAADHI ya watu kwenye jamii wamezoea kusikia au kuona wasanii kibao wakifanya mambo ya ajabu na kuwa na skendo za hapa na pale kama kupigana, mapenzi na kuzungumza mambo yasiyofaa lakini leo tunakuletea listi ya mastaa wanaojiheshimu kwa hapa Bongo... SALOME NDUMBAGWE MISAYO ‘THEA’ Ni staa wa kitambo wa filamu za Kibongo. Ni mke wa ndoa wa mwigizaji Michael Sangu ‘Mike’. Thea amekuwa ni mfano wa kuigwa na kila msanii anayetaka au anayeingia kwenye tasnia ya filamu na jamii kwa jumla. Thea siyo mtu wa skendo kama walivyo wasanii wengine wa kike Bongo. Amedumu kwenye sanaa kwa muda mrefu akianzia Kundi la Sanaa la Kaole wakati wa michezo ya runingani leo, leo amefikia hatua ya kucheza filamu zake mwenyewe japokuwa kumekuwa na malalamiko haonekani sana kama zamani. SUZAN LEWIS ‘NATASHA’ Ni mkongwe wa maigizo ambaye ni mama wa mtoto mmoja. Natasha ni msanii mwenye heshima tele kwenye tasnia ya filamu Bongo ambapo hivi karibuni aliingia kwenye n...

HAWA NDO MASTAA WA KIKE BONGO WANAOJIHESHIMU...

Image
BAADHI ya watu kwenye jamii wamezoea kusikia au kuona wasanii kibao wakifanya mambo ya ajabu na kuwa na skendo za hapa na pale kama kupigana, mapenzi na kuzungumza mambo yasiyofaa lakini leo tunakuletea listi ya mastaa wanaojiheshimu kwa hapa Bongo... SALOME NDUMBAGWE MISAYO ‘THEA’ Ni staa wa kitambo wa filamu za Kibongo. Ni mke wa ndoa wa mwigizaji Michael Sangu ‘Mike’. Thea amekuwa ni mfano wa kuigwa na kila msanii anayetaka au anayeingia kwenye tasnia ya filamu na jamii kwa jumla. Thea siyo mtu wa skendo kama walivyo wasanii wengine wa kike Bongo. Amedumu kwenye sanaa kwa muda mrefu akianzia Kundi la Sanaa la Kaole wakati wa michezo ya runingani leo, leo amefikia hatua ya kucheza filamu zake mwenyewe japokuwa kumekuwa na malalamiko haonekani sana kama zamani. SUZAN LEWIS ‘NATASHA’ Ni mkongwe wa maigizo ambaye ni mama wa mtoto mmoja. Natasha ni msanii mwenye heshima tele kwenye tasnia ya filamu Bongo ambapo hivi karibuni aliingia kwenye n...

HAWA NDO MASTAA WA KIKE BONGO WANAOJIHESHIMU...

Image
BAADHI ya watu kwenye jamii wamezoea kusikia au kuona wasanii kibao wakifanya mambo ya ajabu na kuwa na skendo za hapa na pale kama kupigana, mapenzi na kuzungumza mambo yasiyofaa lakini leo tunakuletea listi ya mastaa wanaojiheshimu kwa hapa Bongo... SALOME NDUMBAGWE MISAYO ‘THEA’ Ni staa wa kitambo wa filamu za Kibongo. Ni mke wa ndoa wa mwigizaji Michael Sangu ‘Mike’. Thea amekuwa ni mfano wa kuigwa na kila msanii anayetaka au anayeingia kwenye tasnia ya filamu na jamii kwa jumla. Thea siyo mtu wa skendo kama walivyo wasanii wengine wa kike Bongo. Amedumu kwenye sanaa kwa muda mrefu akianzia Kundi la Sanaa la Kaole wakati wa michezo ya runingani leo, leo amefikia hatua ya kucheza filamu zake mwenyewe japokuwa kumekuwa na malalamiko haonekani sana kama zamani. SUZAN LEWIS ‘NATASHA’ Ni mkongwe wa maigizo ambaye ni mama wa mtoto mmoja. Natasha ni msanii mwenye heshima tele kwenye tasnia ya filamu Bongo ambapo hivi karibuni aliingia kwenye n...

WEMA SEPETU , IRENE UWOYA VITA RUNINGANI

Image
  VITA mpya imeibuka ikiwahusisha warembo wa Bongo Movies, Wema Isaac Sepetu na Irene Pancras Uwoya kufuatia kuanzisha vipindi vya runinga kwa mpigo. Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Utafiti na Masoko wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba, katika harakati za vipindi hivyo, alianza Wema kwa kuanzisha ‘aidia’ ya kipindi kipya kiitwacho In My Shoes ambacho kitaanza kuoneshwa kuanzia Alhamisi hii, saa tatu na nusu usiku kupitia Clouds TV. Alisema baada ya Wema kutengeneza kipindi hicho na kupata maoni mengi, Uwoya akajibu mapigo kwa kuanzisha cha kwake kinachoitwa Paradise ambacho kitakwenda hewani Jumanne hii (kesho). “Mashabiki wa Clouds TV watapata kuona vita ya kibiashara, Uwoya atakuwa akionekana katika kipindi hicho ambacho kitakuwa kinahusu upakaji rangi katika nyumba za watu mbalimbali huku Wema naye akikimbiza katika In My Shoes,” alisema Ruge. Source:Global Publisher

SITA:WABUNGE WA VITI MAALUMU HAWANA UMUHIMU WOWOTE

Image
 Spika wa Bunge wa zamani, Samuel Sitta Wiki moja baada ya kukaririwa akisema baadhi ya wabunge wa CCM ni mizigo na kwamba hawana mchango wowote bungeni na wala hawatembelei majimbo yao wakisubiri kubebwa na chama, Spika wa Bunge wa zamani, Samuel Sitta amewageukia wabunge wa Viti Maalumu akisema hawana umuhimu wowote. Akizungumza kwa simu juzi, Sitta ambaye sasa ni Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki alisema: “Ninakerwa sana na mfumo wa Viti Maalumu, kwanza sioni umuhimu wa mfumo huu kuendelea kuwepo katika Katiba Mpya. Hawana umuhimu wowote.” Katika mkutano wake wa hadhara uliofanyika Uwanja wa Shule ya Msingi Nyamikoma, Kata ya Busega Mkoa wa Simiyu Julai 29, mwaka huu ikiwa ni sehemu ya kampeni za kuimarisha uhai wa chama, Sitta aliwajia juu bila ya kuwataja baadhi ya wabunge wa CCM. “Wanakwenda bungeni hawachangii, hawana hata hoja za k...

KESI YA MUME WA JOYCE KIRIA AITWAYE.. HENRI KILEWO NA WENZAKE YAFUTWA NA MAHAKAMA, SASA WAPO HURU

Image
Watuhumiwa wa Kesi  ya ugaidi  iliyokuwa inawakabili wanachama wa Chadema akiwemo Henry kilewo wameachiwa Huru Baada ya Kesi Yao kufutwa na jaji katika mahakama kuu Huko Tabora Habari zaidi zitakujia HAPAHAPA KAA nasi

RIPOTI YA MAUAJI YA ARUSHA YAVUJA....

Image
  HATIMAYE ripoti ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, kuhusu vitendo vya uvunjaji wa haki za binadamu na mauaji yaliyotokea Arusha Januari 5, 2011 kwenye maandamano ya CHADEMA imevuja. Licha ya ripoti hiyo kufichwa kwa kutosomwa hadharani kwenye vyombo vya habari kutokana na kulishutumu moja kwa moja Jeshi la Polisi, Tanzania Daima imefanikiwa kuinasa. Maandamano hayo ya CHADEMA ya kupinga ukiukwaji wa kanuni na sheria katika uchaguzi wa Meya ya Manispaa ya Arusha, Gaudence Lyimo, licha ya kuruhusiwa na polisi awali baadaye yalipigwa marufuku na Mkuu wa Jeshi hilo nchini, IGP Saidi Mwema. Hata hivyo, CHADEMA walikataa kutii agizo hilo kutokana na taarifa ya IGP kutowafikia kwa maandishi kama inavyoelekezwa kwa mujibu wa taratibu za utendaji wa jeshi hilo. Kufuatia vurugu hizo za polisi na wafuasi wa CHADEMA, watu watatu waliuawa kwa kupigwa risasi, wengine zaidi yya 30 kujeruhiwa na wafuasi zaidi ya 70 wakiwemo viongozi waandamizi wa chama ambao walifun...

" NILIKURUPUKA KUOLEWA MAPEMA" JACK PATRICK

Image
MWANAMITINDO marufu Bongo, Jacqueline Patrick ‘Jack’ amesema alikurupuka kuolewa na aliyekuwa mume wake, Abdulatif Fundikira ‘Tiff’ kwa kuwa hakufanya tathmini ya kina kabla ya kufanya maamuzi.  Akizungumza na mwandishi  wetu, Jack alisema laiti angekaa kwenye uchumba kwa angalau muda wa miaka miwili kuchunguzana kabla ya kuoana mwaka 2011, asingeweza kufikia hatua ya ndoa kwani wangeshindwana tabia mapema.   “Nilikosea, nikakurupuka kuolewa mapema bila kumchunguza tabia mpenzi wangu, uhusiano wetu ulidumu miezi mitano tu kisha tukafunga ndoa, lakini matokeo yake tabia hazikuendana na ndoa ikakosa uhai ndani ya muda mfupi,” alisema Jack.

MAAJABU YA CHADEMA: DR. SLAA AWAUNGA MKONO WAASI WA KONGO NA KUMKINGIA KIFUA KAGAME

Image
Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Wilbroad Slaa, amemkosoa Rais Jakaya Kikwete, kuhusu kauli  yake ya  kumshauri Rais wa Rwanda, Paul Kagame, kuzungumza na waasi wa serikali yake ... Dk. Slaa amesema haoni busara kwa Rais Kikwete kuwaambia viongozi wa Rwanda, akiwamo Rais Kagame, kuzungumza na wafuasi wa chama cha FDRL walioko Congo. Slaa  aliyasema hayo wakati akizungumza katika kongamano la vijana wa Chadema (BAVICHA) la uchumi na ajira lililofanyika jana jijini Dar es Salaam. “Rais Kikwete hapa nyumbani hawezi kuzungumza na wapinzani  na hajachukua hatua dhidi ya wauaji wa mwandishi Daudi Mwangosi... "Alishauriwa amuwajibishe Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa Michael Kamuhanda  na  badala  yake amempandisha cheo,” alisema Slaa. Kauli  Dk Slaa imekuja siku moja baada ya Rais Jakaya Kikwete kueleza kuwa Tanzania haina mgogoro na nchi ya Rwanda, kutokana na kauli za kejeli na ma...

"NINA JINSIA MBILI, NATAFUTA MPENZI WA JINSIA YOYOTE"...OMBI LA MDAU WETU

Image
Dunia  ina  mengi....Dawa  ya  tatizo  ni  kukubaliana  nalo. Huyu  ni  jamaa  mwenye  jinsia  mbili   na  kwa  mujibu  wa  maelezo  yake  anadai  kuwa  jinsia  zote  mbili  ziko  poa (Active)..  Kinachofurahisha  zaidi  ni  kwamba  jamaa kakubaliana  na  tatizo...Haoni  kama  ni  shida  na  anaisha  maisha  ya  kawaida  kabisa... Cha  kufurahisha  zaidi  ni  kwamba, jamaa  katangaza  kusaka  mchumba  wa  jinsia  yoyote.. Kama  upo  tayari, basi  funguka  kabla  hujawahiwa  na  wenzako. 

ROBERT MUGABE NDANI YA IKULU YA ZIMBABWE KWA MARA YA SABA....

Image
Baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa kinyan’ganyiro cha Urais wa Zimbabwe, Rais Robert Mugabe (89), amefikisha mihula saba ndani ya Ikulu ya nchi hiyo. Mugabe juzi alishinda tena kiti cha urais. Matokeo rasmi yalionyesha kuwa aliibuka na ushindi wa asilimia 61 wa kura dhidi ya mpinzani wake, aliyekuwa Waziri Mkuu, Morgan Tsvangirai ambaye alipata asilimia 34. Chama cha Zanu-PF kinachoongozwa na Mugabe na kile cha MDC cha Tsvangirai, viliunda Serikali ya Muungano mwaka 2008. Juzi, Tume ya Uchaguzi Zimbabwe (ZEC), ilimtangaza Mugabe kuwa mshindi katika uchaguzi wa Rais uliofanyika Jumatano iliyopita. Zanu-PF pia kilipata ushindi mkubwa katika uchaguzi wa wabunge baada ya kujinyakulia viti 137 kati ya 210. Hata hivyo, inaelezwa kuwa hali inaweza kuwa tete hasa baada ya matokeo hayo ambayo yalip...

MUME AUWAWA NA WANANCHI WENYE HASIRA KALI BAADA YA KUMNYONGA MKEWE

Image
MWANAMUME mmoja amemnyonga hadi kufa mke wake na yeye akauawa na wananchi wenye hasira, katika Wilaya ya Bunda mkoani Mara. Tukio hilo lililothibitishwa na polisi wilayani hapa, lilitokea usiku wa kuamkia juzi katika Kijiji cha Kisangwa Kata ya Mcharo, kwenye sherehe ya ufunguzi wa nyumba ya ndugu yao. Ofisa Mtendaji wa Kata ya Mcharo, Waziri Kingi, alimtaja mwanamke aliyeuawa kwa kunyongwa na mume wake kuwa ni Paulina Samson Misinzo. Kingi alimtaja mwanamume huyo ambaye pia aliuawa na wananchi wenye hasira, baada ya kukimbilia mlimani kuwa ni Batule Masanja, mkazi wa kijiji hicho. Imeelezwa kuwa siku ya tukio mwanamume huyo aliyekuwa amekwishatengana na mke wake kwa zaidi ya miezi miwili baada ya kutokea ugomvi wa kifamilia, alimfuata mke wake kwenye sherehe hiyo usiku. Imedaiwa kuwa baada ya kufika nyumbani hapo huku akiwa na watoto wao wawili, alimuita mke wake aliyekuwa anacheza muziki na kumpeleka nyuma ya nyumba, ambapo alimnyonga kwa kutumia mikono ya...

JAJI FRANCIS MUTUNGI ATEULIWA KUWA MSAJILI MPYA WA VYAMA VYA SIASA...

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Mheshimiwa Jaji Francis S.K. Mutungi kuwa Msajili wa Vyama vya Siasa. Taarifa iliyotolewa Dar Es Salaam leo, Jumatatu, Agosti 5, 2013, na kutiwa saini na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue imesema kuwa uteuzi huo ulianza Ijumaa iliyopita Agosti 2, 2013. Jaji Mutungi anachukua nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Msajili wa Vyama vya Siasa, Mhe. John Tendwa ambaye amestaafu Utumishi wa Umma kwa mujibu wa sheria. Kabla ya uteuzi huo, Jaji Mutungi alikuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dodoma. Imetolewa na: Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, DAR ES SALAAM.

MKE WA MTU ANUSURIKA KUUAWA BAADA YA KUNASWA AKIIBA NGUO KARIAKOO

Image
Jimama mwenye hadhi yake ambaye ni mke wa mtu aliyetajwa kwa jina moja la Mary au Mama Gilo, mkazi wa Sinza jijini Dar amekula kichapo cha kutisha almanusra apoteze uhai baada ya kunaswa akiiba nguo kwa ajili ya Sikukuu ya Eid El Fitr. Tukio hilo la aibu lililoshuhudiwa na  mwandishi wetu lilijiri katika moja ya maduka makubwa ya nguo Kariakoo, Dar mwishoni mwa wiki iliyopita. Mama Gilo ambaye anafahamika Kariakoo na Sinza, alinaswa akiiba nguo za sikukuu ikiwa ni pamoja na ‘madira’ ya kumalizia mfungo. Katika tukio hilo lililokusanya kadamnasi, mwanamke huyo alipigwa chabo kwenye duka la mfanyabiashara Rehema Kessy ambapo alidai kuwa alifika Kariakoo kwa lengo la kununua madira lakini alijikuta akiingiwa na tamaa ya kuiba ndipo akanaswa. Awali, kabla ya kuwekwa chini ya ulinzi na raia waliokuwa na hasira kali, mwanamke huyo alidaiwa kukwapua mkoba wa mwanamke mwenzake na kujichomeka kwenye maduka kumkwepa aliyemuibia ‘pimajoto’ lake l...

ANGALIA PICHA ZA WASANII WALIVYO FUTURU NA RAIS KIKWETE IKULU JANA

Image
Wasanii mbali mbali na watangazaji walipata kualikwa ikulu jijini Dar, kwa ajili ya kuftari na Mh Raisi pamoja na familia yake.mara baada ya kuftari Mh Kikwete aliongea mawili matatu ikiwa ni pamoja na kuwapa moyo wasanii kwa kuendeleza sanaa maana hata yeye anapenda kusikiliza miziki yao B12 Fetty Dj Mully B Jafarai na inspector Haroon Qchief na Babu Tale  Mwasiti, Fetty na Shilole Chege, Nyandu Tozi na Madee Kassim Mganga Adama Mchomvu Ben Pol (wa pili kutoka kulia) Linex (wa kwanza kulia) Looking good MashAllah, TID, Jafarai na Z Anto Mzee mkorofi, Suma Lee hahahaa Mbwiga nae hakukosa Shekh AY na Ali Kiba Marlow na Sam Misago Feruz na Fela Lamar na P Funk Quick kama sio yeye loooool  Hemedi Phd Adama Juma Dogo Asley King Crazy GK Shilole its more about music industry a...