Posts

MAADHIMISHO YA SIKU YA MASHUJAA YAFANA MBEYA

Image
Mkuu wa wilaya ya Chunya Deodatus Kinawiro mwenye suti ya bluu ambaye pia ni mwenyekiti wa wakuu wa wilaya za mkoa Mbeya ndiye aliongoza maadhimisho hayo akimwakilisha mkuu wa mkoa Abbas Kandoro kulia kwake mkuu wa wilaya ya Mbeya Norman Sigalla  Mkuu wa wilaya ya Chunya Deodatus Kinawiro akiweka mkuki na ngao kuwakumbuka mashujaa waliokufa vitani Mwakilishi wa mstahiki meya wa jiji la mbeya akiweka shada lake Mzee Ernest Waya akiweka upinde na mshale kuwakumbuka wenzake aliokuanao vitani enzi hizo... Chifu Lyoto alikuwepo kuweka mshda kuwakumbuka mashujaa Viongozi mbali mbali wa dini waliwaombea duwa mashujaa wetu Mzee Ernest Paulo Waya aliyepigana vita kuu ya pili vya Dunia alikuwepo kuwakumbuka wenzake Picha na Mbeya yetu

RAIS KIKWETE AFUNGUA JENGO LA MAHAKAMA KUU KANDA YA BUKOBA

Image
Rais Jakaya Mrisho Kikwete  akikata utepe akisaidiwa na  Jaji Mkuu Mhe Mohamed Chande Othman wakifungua rasmi jengo la Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba leo Julai 25, 2013 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifungua pazia kuzindua rasmi jengo la Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba leo Julai 25, 2013 NA FULLSHANGWE Wananchi waliojitokeza kwa wingi katika ufunguzi huo wakiondoka baada ya uzinduzi huo Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitembezwa baada ya kufungua rasmi jengo la Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba leo Julai 25, 2013 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitembezwa baada ya kufungua rasmi jengo la Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba leo Julai 25, 2013 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na wakuu wa mahakama nchini mara  baada ya kufungua  rasmi jengo la Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba leo Julai 25, 2013 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiondioka baada ya kufungua  rasmi jengo la Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba leo Julai 25, 2013

MABINTI WAJIREKODI WAKIWA UCHI..... VIDEO YAVUJA

Image
Maadili ya kitanzania yamekuwa yakiporomoka  kila  kukicha  hasa kwa  watoto wa kike  ambao  wengi wao wamekuwa wakiendekeza  ufaska  wa   tamaduni  za  nchi  za  ng'ambo  wa  kujirekodi  wakiwa  uchi  na  kujipiga  wakiwa  uchi. Hii  ni  video  ya  mabinti  hao   walioamua  kujiumbua  wenyewe( Ni sharti uwe mtu mzima ) << BOFYA  HAPA  KUICHEIKI  ILIKO>>

PESA MWANAHARAMU:.. LADY GAGA AKUBALI KUPIGWA UCHI ILI KUUPAMBA UKURASA WA MBELE WA GAZETI

Image
  Lady  Gaga  ametoa  kali  ya  mwaka  baada  ya  kukubali  kufotolewa  akiwa  mtupu  ili  kuupamba  ukurasa  wa  mbele  wa  gazeti  la  V magazine... Baadhi  ya  fans  wake  wamefunguka  na  kudai  kuwa  uroho  wa  pesa  utamponza  huku wengine wakidai   kuwa  msanii  huyo  atakuwa  amekubali  kuanikwa  hivyo  ili  kuvuta  "attention"  ya  mashabiki  wake  kwa  ujio  wa  albam yake  mpya  itakayoitwa  Artpop Albamu hiyo inatarajiwa kuwa   sokoni mwezi wa 11 na nyimbo ya kwanza kutoka kwenye  album   hiyo  itatambulishwa mwezi wa nane tarehe 19.

KWA WADADA AMBAO HAWAJA OLEWA NA WANAPENDA MAISHA YA NDOA

Image

UJUMBE MZITO KUTOKA KWA IRENE UWOYA KWENDA KWA JOHARI

Image
Katika pita pita zetu leo hii tuliweza kupata ujumbe mmoja mzito na wa kutia moyo toka kwa mwanadada Irene Uwoya aliomwandikia mkongwe wa bongo movies nchini kwa upande wa kinadada Blandina Chagula maarufu kama Johari wiki chache zilizopita. Ujumbe huu wa Irene ni ujumbe wa kutia moyo na unaweza kuwa kama “Motivation message” kwa wadada wengi hapa mjini ili badala ya kukaa na kuwaza kupata mali au mafanikio kwa njia za mkato au zisizo halali basi wafanye kazi kwa bidii ili kujikwamua kiuchumi. Tukinukuu ujumbe huo Irene kwa Johari aliandika…. “Wewe nimwanamke wapekee...mchapakaz sana...atawaongeee vp kaza moyo...one thng u hav to know if God say yes no body I mean no body can say no...so don gv r f*ck Hii inawahusu wadada wote jamani. Nyie ni wanawake wapekee, wachapakazi, kazeni moyo. If God say yes, nobody can say no (Mungu akisema ndio hakuna awezaye kusema hapana)

Huyu ndo Mtu Ambaye Hajaoga Wala Kukata Nywele kwa Zaidi ya Miaka 37

Image
Mr Singh na Mkewe Hakika haya tunaweza kuyaita mafanikio ya ajabu kwa mzee huyu kutokana maamuzi yake. Labda tumite Mr Adui wa Maji ila jina lake kamili ni Mr Kailash Singh akiwa na ndiye anayeshikilia rekodi ya mtu anayenuka zaidi kutokana na kutokuoga kwa zaidi ya miaka 37 sasa. Mr Singh, 65, hajaoga na hata kukata nywele zake zenye urefu wa futi 6 toka mwaka 1974, mda mfupi mara baada ya kutoka kuoa. Akielezea juu ya uamuzi wake wakushangaza, Mr Singh anasema mchungaji alimuahidi zawadi ya mtoto wa kiume kama atafata ushauri.  Licha ya majirani kuwa wanamtania na kumdhihaki jamaa huyo walishindwa kubadili maamuzi yake na namna ya kipekee alifanikiwa kumshawishi mke wake, ila cha ajabu zaidi ni pale ambapo imani yake imeonekana kumdanganya kwani ameishia kupata watoto saba ambao wote ni wa kike.

DIWANI CHAMBO WA CCM AMTWANGA MKEWE............................

Image
Mke wa Diwani, Imelda Chambo akiwa kulazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Morogoro. Kwa mujibu wa mashuhuda, ugomvi huo ulichukua nafasi Alhamisi iliyopita saa 6 usiku nyumbani kwa wanandoa hao, Kihonda. Mke naye ni Diwani wa Kata ya Mkundi kwa ‘leseni’ ya CCM. Inadaiwa kuwa, baada ya mheshimiwa diwani kumtwanga mkewe na kummwagisha damu, mke naye alichukua chupa ya bia na ‘kujirudishia’’, wote wakawa chapachapa kwa damu. Siku ya tukio, paparazi wetu alipofika nyumbani kwa wanandoa hao alikuta tayari wameshakimbizwa hospitalini ndipo alielezwa kuwa chanzo cha ugomvi wao ni wivu wa mapenzi.  Paparazi wetu alitinga hospitali ya mkoa na kumkuta mke wa diwani huyo akiwa hoi kwenye wadi namba tatu. na GPL Akizungumza kwa tabu na gazeti hili, Diwani Imelda alisema ndoa yao imedumu kwa miaka 30 na kubahatika kuzaa watoto watatu. “Naweza kusema nusu ya maisha yetu ya ndoa ni migogoro na mapigano. “Ugomvi wa leo hauna kichwa

WEMA SEPETU HATIMAYE AVUTAMKOKOMPYA.

Image
Hiindiogari mpya wema kama inavyoonekana katika picha   Haya ndio Maneno ya Martin Kadinda aliyoandika facebook na kuweka picha ya Wema akiwa na gari hilo "samahani kwa ubora wa picha kuwa hafifu....... Ila huyu dada anapenda pink kupitiliza..... haya she gat new pink Car.... mkutane barabarani..." aliandika Martin.

BAADA YA KUPIGWA CHINI BIG BROTHER, HUDDAH AAMUA KUMALIZA HASIRA ZAKE KWA KUJIPIGA UCHI

Image
Wengi waliamini  kwamba    Big Brother  imempa  fundisho  mrembo  huyu  na  kutegemea  mabadiliko   makubwa  ikiwa  ni  pamoja  na  kuuuheshimu  mwili  wake  baada  ya  Video  zake  za  uchi  kuvuja  akioga  bafuni... Hali  imekuwa  ni  tofauti  kwa  mrembo  huyu  asiyeijua  thamani  ya  mwili  wake.Tabia  ni  ngozi.Skendo,picha  za  uchi  huenda  ziko  katika  mishipa  ya  damu  yake.... Hizi  ni  picha  zake  za  nusu  uchi  alizotupia  mtandaoni.  

Msafara wa Baba Mtakatifu Francis 1 wapotea njia nchini Brazil ukitokea uwanja wa ndege.

Image
  Maelfu ya wananchi wa Brazil katika mitaa ya Rio de Janeiro wameivamia na kulizunguka gari lilokuwa limembeba  Baba Mtakatifu Francis 1 wakati msafara wake ulipopotea njia ulipokuwa ukitokea uwanja wa ndege alipowasili nchini humo kwa ziara. Katibu wa Usafiri wa Rio Carlos Osorio amesema gari aina ya Fiat alilokuwemo Baba Mtakatifu lilikuwa likitokea uwanja wa ndege kuelekea katikati ya mji, lilipita njia tofauti lilipofika katika mgawanyiko wa barabara 12 unaofahamika kama Avenida Presidente Vargas. Badala ya kupita njia za upande wa kushoto za mgawanyiko huo ambako hakukuwa na msongamano wa magari, gari hilo lilipita njia za upande wa kulia ambako kuna magari mengi yakiwemo mabasi na teksi nyingi, hatua iliyosababisha gari hilo kusimama. Maelfu ya watu waliokuwa wamejipanga mitaani walilikimbilia gari hilo na kufika katika dirisha la upande alipokaa , huku wengi wao wakimpiga picha. Msemaji wa Vatican Padri Federico Lombardi amet

Bomu lanaswa ziara ya Papa Francis nchini Brazil

Image
  Mbali ya kufurahia mapokezi makubwa nchini Brazil, ziara ya Papa Francis imeingia doa baada ya bomu kugunduliwa chooni katika mji ambao atauzuru leo. Bomu hilo la kutengenezwa kienyeji liligunduliwa na maofisa usalama likiwa katika choo katika Kanisa la Bikira Maria wa Aparecida katika mji huo mdogo ambao kiongozi huyo atautembelea kama sehemu ya ziara yake kwa kwanza nje ya Vatican. “Lilikuwa bomu la kutengenezwa kienyeji lenye uwezekano mdogo wa kusababisha maafa,” imeeleza taarifa ya Jeshi la Anga la Brazil. “Ni tukio linaloshtua, limefanyiwa kazi na wana usalama ambao wamejiandaa vyema kwa ziara hii. Kwa hakika haliwezi kuzua hofu, vikosi vya usalama vimejiandaa kikamilifu kwa matukio kama haya.” Kulingana na vyombo hivyo, bomu hilo liliteguliwa na kisha kuharibiwa baada ya kugundulika kwake katika mji huo mdogo kwenye viunga vya Rio de Janeiro baada ya mazoezi ya vikosi vya usalama, limeeleza gazeti la Grupo Estado. Bikira Maria wa Aparecid

POLISI 117 WATIMULIWA KAMBINI KWA UTOVU WA NIDHAMU

Image
Wanafunzi 117 wa Polisi, wamefukuzwa katika Chuo cha Taaluma na Mafunzo ya Polisi (MPA), kilichopo Manispaa ya Moshi, mkoani Kilimanjaro.  Waliotupiwa virago na kufutwa kwenye kozi hiyo ni wale waliopoteza sifa za kuendelea na mafunzo ya kijeshi baada ya kukutwa na makosa ya utovu wa nidhamu, utoro na matatizo ya kiafya. Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Matanga Mbushi, ambaye ni mkuu wa chuo hicho alisema katika mahojiano maalumu kwamba, waliotimuliwa chuoni ni kati ya askari wanafunzi 3,189 waliokuwa wamesajiliwa kuanza mafunzo ya kijeshi katika chuo hicho, Oktoba 25 mwaka jana.   Kati yao askari 115 ni wale wa Polisi na askari wawili wanatoka katika Idara ya Uhamiaji iliyopo chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani. Kufukuzwa kwa wanafunzi hao , kuna akisi moja kwa moja jinsi menejimenti ya chuo hicho ilivyojipanga upya kupunguza wimbi la baadhi ya askari walioko kazini na ambao wanalipaka matope jeshi hilo kutokana na kupotoka kimaadili kwa kutaka kujinufaisha k

HUYU NDIE MTANZANIA MWENYE WATOTO KUMI SOMA NA SHUHUDIA MWENYEWE

Image
Bi. Rejina Moshwa (37) mkazi wa Kijiji cha Isoso akizungumza na mwandishi wa habari kutoka Clouds FM Aziz Kindamba Paschal Kulwa Manyinzi (42) mkazi wa Kijiji cha Isoso akiwa katika picha na baadhi ya watoto wake baada ya mazungumzo na Thehabari.com ……………….. Na Thehabari.com, Kishapu WASUKUMA ni moja ya makabila nchini Tanzania ambayo awali yalishikilia desturi ya familia kuwa na idadi kubwa ya watoto. Familia moja yaani baba na mama waliendelea kuzaa kadri walivyo jaaliwa kupata watoto bila kujali ukubwa wa familia. Mume pia hakuwa na kizuizi katika familia cha kuongeza mke mwingine endapo atakuwa na ardhi (mashamba) na mifugo (hasa ng’ombe) ya kutosha kuweza kuihudumia familia aliyonayo. Wapo walioamini kwamba kuwa na ukubwa wa familia ni kuongeza nguvu kazi katika uzalishaji kwa kutumia ukubwa wa familia. Hata hivyo pia wapo walioamini uzazi ni mpangilio wa Mungu hivyo haupaswi kupangiliwa na wazazi bali mola mwenyewe.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA MKUTANO WA KIMATAIFA WA MABADILIKO YA TABIANCHI, CHANGAMOTO ZA MAENDELEO NA UKUAJI WA MIJI BARANI AFRIKA, JIJINI ARUSHA LEO

Image
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake ya ufunguzi  wa Mkutano wa Kimataifa kuhusu mabadiliko ya Tabianchi, Chanagamoto za Maendeleo na ukuaji wa Miji Barani Afrika.  Mkutano huo umefunguliwa leo Julai 24, 2013 Jijini Arusha. Picha na OMR Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea zawadi ya Jarida la Sayansi , kutoka kwa Mkurugenzi wa Sayansi ‘Physical Sciences’ (COSTECH) Prof. Clavery Tungaraza,  baada ya Makamu kufungua rasmi mkutano huo uliofanyika kwenye Hoteli ya Mount Meru, Jijini Arusha leo Julai 24, 2013.  Picha na OMR Makamu mkuu wa chuo kikuu cha Dar es salaam, Profesa Rwekaza Mukangara, akizungumza kabla ya kumkaribisha Makamu wa Rais kufungua mkutano huo Baadhi ya washiriki wa mkutano huo wakimsikiliza Makamu wa Rais wakati akisoma hotuba yake ya  ufunguzi. Picha na OMR Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mo