TRENI YA MWAKYEMBE ILIPATA AJALI JANA ASUBUHI ....HIVYO HUDUMA ZA TRENI ZIKAHAIRISHWA
Leo mnamo saa 11:30 asubuhi vichwa viwili vya treni ya huduma la jiji la Dar es Salaam vilipata ajali ya kugongwa na roli la mizigo aina ya Fusso katika makutano ya reli na barabara ya Kawawa jijini Dar es salaam , katika jali hiyo dereva wa Fusso alifariki duniani papohapo hata hivyo Utingo wake alinusurika. Hata hivyo vichwa hivyo vya treni vilipata mkosi tena wa ajali ambapo viligongwa na basi dogo la Daladala aina ya Isuzu katika makutano ya reli eneo la Kamata. Tukio hilo lilisababisha majeruhi kadhaa katika basi hilo la daladala ambapo majeruhi wamelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbil wakiwemo askari wawili Polisi kutoka Kikosi cha Reli mmojawapo akiwa mahututi. Vichwa hivyo viifanikiwa kufika stehesheni kwa wakati na kuanza kutoa huduma ya usafiri wa treni jijini kutoka Dar Stesheni kwenda Ubungo Maziwa hadi saa 5 asubuhi hata hivyo huduma ya leo jioni Julai 01, 2013, imesogezwa mbele na itaanza saa 12 jioni badala ya saa 10:30 alasi