Posts

WAGHANA WAMLAANI NANDO WA TANZANIA KWA KUZINI NA DEMU WAO ( SELLY) NDANI YA BBA......MAMA MZAZI WA BINTI AMTETEA

Image
  Wiki iliyopita wapenzi Nando wa Tanzania na Selly wa Ghana  waliucheza ule mchezo wa kikubwa   katika Big Brother ‘The Chase’ inayoendelea, na inasemekana baada ya Ghana na Afrika kwa ujumla kushuhudia mechi hiyo ya kirafiki watu wa karibu na mpenzi wa Selly wamemshauri ampige kibuti. Wote tunafahamu kwamba washiriki wote wa BBA wana maisha yao nje ya Big Brother na inawezekana kila mmoja anamahusiano huko alikotoka, lakini mission iliyowapeleka BBA ‘The Chase’ ni kushinda $300,000 inayomsubiri kinara mmoja, na ili kupenya njia nyembamba za kuufikia ushindi kila mmoja anajitahidi kufumba macho na kujisahaulisha kama camera ziko on ili aweze ku accomplish mission hiyo bila kujali njia anazotumia. Baada ya video clip ya wapenzi wa BBA The chase Nando na Selly wakifanya mapenzi kusambaa ,baadhi ya watu wa karibu na boyfriend wa Selly wa Ghana wametoa maoni yao juu ya kitendo hicho cha ‘aibu’. Steven Fiawoo maarufu nchini Ghana kama Praye Ti

GEORGE BUSH NA MKEWE KUTUA NCHINI KESHO

Image
RAIS mstaafu wa Marekani, George W. Bush na mkewe, Laura wanatarajiwa kesho kuwa nchini kuhutubia kongamano linalojadili wajibu wa wake wa marais katika kuinua wanawake duniani. Kuwasili kwa Bush, ni mwendelezo wa wiki hii Jiji la Dar es Salaam kuwa katika pilikapilika za kupokea ugeni wa watu maarufu. Kongamano hilo limeandaliwa na Taasisi ya George Bush na litafanyika kesho na keshokutwa. Taarifa iliyotolewa na taasisi hiyo kwa vyombo vya habari , inasema kongamano hilo litahudhuriwa na wake mbalimbali wa marais akiwemo mke wa Rais wa Marekani, Michelle Obama. Pia Mwanzilishi wa Taasisi ya Wanawake ya Cherie, Cherie Blair atahudhuria. Wake wa marais wa Afrika watakaohudhuria ni Mama Salma Kikwete, Chantal Campaore wa Burkina Faso, Roman Tesfaye wa Ethiopia, Maria da Luz Dai Guebuza (Msumbiji), Penehupifo Pohamba (Namibia), Sia Nyama Koroma (Sierra Leone), Janet Museveni (Uganda) na Christine Kaseba wa Zambia. Kongamano hilo litajikita zaidi kati

MAANDALIZI YA KUMPOKEA OBAMA YAKAMILIKA...HIZI NI TASWIRA ZA IKULU LEO ASUBUHI

Image
Taswira mbalimbali zinazoonesha maandalizi ya mapokezi makubwa ya Rais wa Marekani Barack Obama atapowasili Ikulu jijini Dar es salaam mchana huu.  Rais Jakaya Mrisho Kikwete kama ilivyo kawaida yake amepita kila mahali kuangalia kwamba mambo yanaenda vizuri, ikiwa ni pamoja na kusaliamiana na makundi ya wananchi wa Dar es salaam walioko katika lango kuu la Mashariki.  Bendera zikiwa zimepangwa na kupangika katika upande wa lango kuu la Mashariki,Ikulu. Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisaliamiana na makundi ya wananchi wa Dar es salaam walioko katika lango kuu la Mashariki. Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia Kibao cha Barabara wa Barack Obama. Jengo la Ikulu. Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,Mh. Bernard Membe akisoma ratiba. makundi ya wananchi wa Dar es salaam walikishangilia wakati Rais Jakaya Mrisho Kikwete alipopita kuwasalimia.

HELCOPTA ATAKAYOITUMIA OBAMA ATAKAPOKUJA LEO TANZANIA

Image
Hii ni helcopter ya Obama,inafahamika kama MARINE ONE Hii ni moja ya helcopter za kijeshi zinazokuwa nyuma  ya MARINE ONE alimo Obama MARINE ONE(iliyojitenga karibu na miti)ikiwa imezungukwa  na baadhi ya helcopter za kijeshi,hapo zikiwa zimetuwa mjini Pretoria Africa kusini MARINE ONE ikiwa angani nchini Africa kusin

BRAZIL MABINGWA KOMBE LA MABARA, WAITANDIKA SPAIN 3-0

Image
Hawa ndo wachawi wa soka wakifanya yao pale walipouthirishia ulimwengu kuwa wa ndo mabingwa mara tatu mfululizo Ndiyo maana soka ni mchezo unaopendwa na watu wengi zaidi duniani kwa kuwa hauna matokeo yanayotabirika na Hispania wanaweza kuwa shahidi wa hilo katika mechi ya fainali ya Kombe la Mabara iliyomalizika punde. hapa ni gori la kwanza la ufundi likipachikwa na fred Wenyeji Brazil wametawazwa kuwa mabingwa baada ya kuwafunga mabingwa wa dunia, Hispania kwa mabao 3-0. Mechi hiyo kwenye Uwanja wa Maraccana ilikuwa burudani tupu na Brazil walipata bao lao la kwanza katika dakika ya 2 mfungaji akiwa Fred na dakika 44, Neymar akafunga bao la pili kwa shuti kali. Kipindi cha pili, dakika ya tatu, Fred tena akafunga bao la tatu ambalo lilionyesha kumaliza matumaini ya Hispania ambayo baadaye Sergio Ramos alikosa mkwaju wa penalti. Baada ya hapo, wenyeji ambao walianza soka kwa kasi tokea kipindi cha kwanza, walionekana kuendelea kuwabana mabingw

ANGALIA BARABARA ZIKIPIGWA DEKI LEO HII KUTOKANA NA UJIO WA OBAMA

Image
Serikali imesema kupigwa deki kwa barabara ya Morogoro hadi Ubungo Tanesco kutokea mjini hakuna uhusiano na Ujio wa Barack Obama!!   Je, wewe unalichukuliaje hili, tupe maoni yako

WATANZANIA 60 WAKAMATWA AFRIKA KUSINI WAKATI WA ZIARA YA OBAMA

Image
Watanzania 60 wamekamatwa Afrika Kusini kutokana na maandalizi yaliofanyika nchini humo ya kumpokea Rais Barack Obama wa Marekani.    Rais Obama aliwasili Afrika Kuisini  wiki iliyopita  kwa ziara ya siku tatu akitokea Senegal. Watu hao wamekamatwa baada ya kudaiwa kuishi kinyume cha sheria Afrika Kusini.  Baada ya Watanzania hao kutiwa mbaroni na vyombo vya usalama wamehifadhiwa hapa nchini kusubiri  hatua za kisheria zaidi.   Ofisa mmoja wa Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere, Sadiki Msele amesema Watanzania hao walirejeshwa nchini juzi  na kwamba hivi sasa wanasubiri sheria kuchukua mkondo wake. “Safisha safisha kama iliofanyika jijini Dar es Salaam, pia imefanyika Afrika Kusini na kuwaathiri wafanyabiashara na watu wengine,” amesema ofisa huyo. Leo mchana  Rais Obama na ujumbe wake anatarajiwa kutua Tanzania kwa ziara ya siku mbili na Jumanne ataondoka kurejea Marekani.

Hawa ndo WAPENZI WALIODONDOKA NA KUFA WAKATI WAKIFANYA MAPENZI DIRISHANI

Image
Wapelelezi wakifunika miili ya wapenzi hao eneo la tukio. Wapenzi wameanguka na kufa baada ya dirisha walipokuwa wakifanyia mapenzi kufunguka ghafla nchini China. Wawili hao wanasemekana kudondoka kutoka kwenye dirisha la jengo moja la makazi kwenye jiji la Wuhan nchini humo pale dirisha hilo walilokuwa wameegemea kufunguka. Mashuhuda walivieleza vyombo vya habari vya China kwamba wapenzi hao walikumbatiana wakati wakianguka kwenye njia ya waenda kwa miguu nje. Kwa mujibu wa The Sun, chanzo kimoja cha habari kilisema: "Huku wawili hao wakiwa wameshikamana vilivyo, walianguka nje ya jengo hilo." Picha za kuogofya zimefichuliwa kwenye tovuti za nchini humo zikionesha wapenzi hao wakiwa wamefunikwa kwa mashuka na polisi. Damu ilitapakaa kwenye njia ya waenda kwa miguu karibu na wapelelezi wanaonekana wakichunguza eneo la tukio. Miili ya wapenzi hao ilipigwa picha karibu na baiskeli ambayo ilikuwa imelazwa chini, lakini hakukuwa na ripoti zozote kwa

OBAMA na MKEWE WAKIWA WAMEVAA VAZI LA KIASILI LA KIZULU

Image

HATIMAYE LULU AFANYA INTERVIEW YA KWANZA TANGU ATOKE JELA, UTAIPATA HAPA

Image
Hatimaye mwanadada Elizabeth Michael a.k.a Lulu amefanya interview yake ya kwanza rasmi baada ya kipindi cha takribani mwaka mmoja na nusu toka atoke jela. Katika kipindi hicho kitakachorushwa hivi karibuni lulu ameongelea mambo mengi sana hasahasa experience yake ya maisha ya jela na mambo mengine mengi. Naye Lulu kupitia mtandao mmoja wa kijamii aliandika. “Kwa zaidi ya mwaka na nusu sasa!!!hii ni interview yangu ya kwanza baada ya kipindi chote hicho....thanks zamaradi….” Unahisi ameongelea mambo gani mengine? Tupe maoni yako

BINTI AOZA MKONO BAADA YA KUANGUKA KATIKA BAISKELI....MADAKTARI WAMESHINDWA KUUPONYA, MAOMBEZI YAHITAJIKA

Image
Janeth Nicholaus (25)mkazi wa Rwanzari Manispaa ya Tabora akionesha mkono wake wa kulia ukiwa tayari umeanza kuoza baada ya kupata ajali ya baiskeli maarufu daladala wakati akitokea nyumbani kwenda Soko kuu la Tabora mjini ajali ambayo ilitokea kwenye makutano ya barabara ya NBC.  Huu ndio mkono wenyewe unavyoendelea kuharibika baada ya kupita hospitali kadhaa hapa Tabora mjini na kushindikana kupona lakini sasa aliamua kufika kwenye huduma ya Maombezi  Kanisa la AGAPE MIRACLE CENTER Mwanza road Tabora manispaa kwa Mchungaji Mbagata.

LOWASSA AMTAKA OBAMA ASIZUNGUMIE MAMBO YA USHOGA NA NDOA ZA JINSIA MOJA AKIWA TANZANIA

Image
Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo yaNje na Ushirikiano wa Kimataifa, Edward Lowassa, amemtahadhalisha kujiepusha na kauli za kuunga mkono ushoga.   Lowassa ambaye pia ni Mbunge wa Monduli, ameliambia NIPASHE Jumapili ofisini kwake jijini hapa jana kuwa ushoga na hai za ndoa kwa watu wa jinsia moja vinaweza `kuiharibu’ ziara yake hapa nchini. Mapema wiki hii, Rais Obama alikaririwa akizungumzia masuala hayo yanayotajwa kuwa ni moja ya haki za msingi za binadamu, alipokuwa Senegal, lakini akapingwa.   “Watanzania hawatalikubali na wataendelea kushikilia uhuru na heshima walizojengewa tangu awali, kwamba ushoga na ndoa za jinsia moja havikubaliki,” alisema. Akiwa Senegal, Rais Obama alitaka serikali za Afrika kutoa haki kwa mashoga kama inavyotoa kwa raia wengine.   "Ninachotegemea, I pray and hope (ninasali na kutegemea) kwamba kuhusu mashoga na ndoa za jinsia moja, Rais Obama hatarudia kauli aliyoitoa kule Senegal,” alisema. Aliongeza, "ninasema hivi k

AFYA YA NELSON MANDELA BADO TETE

Image
Taarifa kutoka Ikulu ya Afrika Kusini zinasema kuwa hali ya kiafya ya rais mstaafu Nelson Mandela sio nzuri na kuwa imezorota katika saa 48 zilizopita. Baada ya kumtembelea hospitalini, mwanawe mkubwa wa kike Makaziwa, alisema hali inaonekana kuwa mbaya lakini akaongeza kuwa Mandela anaweza kuwasikia jamaa zake wanapomuita huku akijaribu kufungua macho yake. Makaziwe amesema “Nimekasirishwa sana. Kwa sababu Mandela ni kiongozi mashuhuri duniani, haimaanishi utu wake udhalilishwe pamoja na kuvuka mipaka kuingilia mambo yake binafsi. Hapa naona kuna ubaguzi wa rangi, huku vyombo vingi vya kimataifa vikivuka mipaka, ni kama ndege aina ya Tai au Vulture wanaosubiri Simba kumla mnyama aliomuwinda kisha wakimbilie mzoga. Wamevuka mipaka ya maadili. Wakati hayati Margaret Thatcher alipokuwa mgonjwa mbona sikuona, ukaribu wa vyombo vya habari kiasi ninachokiona kwa banangu? Ni kwa sababu hii ni nchi ya kiafrika. Wanahisi kuwa hapa wanaweza kuvuka mipaka w

CHUO KIKUU HURIA TANZANIA KITAMTUNUKU PhD RAIS OBAMA

Image
Chuo Kikuu Huria Tanzania (OUT),kimepanga kumtunuku Rais wa Marekani, Barack Obama Shahada ya Heshima ya Uzamivu kwa kutambua mchango wake kwa jamii husasani kwenye maendeleo ya kukuza uchumi. Akizungumza na waandishi wa habari jana,Makamu Mkuu wa chuo hicho,Profesa Tolly Mbwete alisema tuzo hiyo imethibitishwa na Baraza Kuu la Chuo hicho baadaye kupitishwa na Mkuu wa OUT, Dk Asha Rose Migiro. “Tumeangalia vigezo vyote muhimu ambavyo mtu anastahili kupewa tuzo kama hii na tukaridhika kuwa Rais huyo anastahili kutunukiwa,” alisema Profesa Mbwete. Kwa mujibu wa Profesa Mbwete, Rais Obama anakuwa mtu wa tano kutunukiwa tuzo hiyo baada ya kutanguliwa na Mwalimu Julias Nyerere, Rais wa kwanza mweusi wa Afrika ya Kusini, Nelson Mandela, Rais wa awamu ya tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Benjamin Mkapa. Alisema hadi sasa OUT imetoa shahada saba za heshima, ambapo kati ya hizo mbili walitunukiwa mwanataaluma kutoka Mareka