FILAMU MPYA YA AUNT EZEKIEL YAZUILIWA BAADA YA KUWA NA VIPANDE VYENYE KUCHOCHEA NGONO
SERIKALI kupitia bodi ya filamu nchini imemkalia kooni mwigizaji, Aunt Ezekiel na kumtaka aondoe baadhi ya vipande vya sinema yake mpya iitwayo Scola vinginevyo haitaruhusiwa kuingia mtaani. Taarifa kutoka ndani ya bodi hiyo inayosimamia maadili ya sinema za Kitanzania, imeeleza kuwa Aunt aliipeleka filamu hiyo ili ikakaguliwe kama zilivyo taratibu lakini bahati mbaya ikagundulika kuna ‘sini’ tatu ambazo zilitoka nje ya maadili ya mtanzania. “Kuna vipande vitatu ambavyo kimsingi vimevuka matakwa ya maadili ya Kitanzania hivyo hakuna jinsi, lazima avitoe kama anataka kuiingiza sokoni sinema hiyo,” kilieleza chanzo makini ndani ya bodi hiyo kilichoomba hifadhi ya jina. Kabla ya mwandishi wetu hajazungumza na Aunt, alimpata rafiki wa karibu na staa huyo ambaye alifafanua kuwa rafiki yake (Aunt) amekaliwa kooni na bodi hiyo lakini bado yupo katika mazungumzo kuona kama anaweza kuruhusiwa aendelee. “Amejaribu kuwasihi ili kama kuna uwezekano iingie m