Posts

KAULI YA MWIGULU KUHUSU BOMU LILILORUSHWA ARUSHA

Image
MWIGULU NAYE ADAI KUWA BOMU LILIRUSHWA NA CHADEMA...."KAMA SIO WAO, MCHUKUA VIDEO ALITAARIFIWA NA NANI KWAMBA BOMU LITARUSHWA???" Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Mwigulu Nchemba  amesema bungeni leo kwamba Chadema ilipanga kufanya shambulio la bomu kwenye mkutano wa Soweto jijini Arusha. Amesema hakuna jambo ambalo Chadema wamewahi kupanga wakashindwa. “Itakuaje mtu amechukua mkanda wa tukio la umwagaji wa damu bila kutikisika au mchukuaji kukimbia, haiwezekani- hiyo walipanga. “Inakuaje amechukua mkanda wa video kama mkanda wa harusi, yaani kama mkanda wa sendoff.? Amehoji Mwigulu huku wabunge wa CCM wakimuunga mkono kwa kupiga meza bungeni. Mapema wiki hii katika mkutano wa Chadema, mtu mmoja asiyefahamika alirusha bomu kwenye mkutano wa Chadema na kusababisha watu wanne  kufariki dunia na wengine 68 kujeruhiwa na kupelekwa katika Hospitali ya Mt Meru, Arusha.

"EDWARD LOWASSA ANAHUSIKA NA KUTEKWA KWANGU PAMOJA NI KIPIGO NILICHOPEWA"...NASSARI

Image
Mbunge wa Arumeru Mashariki (Chadema), Joshua Nassari amemtuhumu Mbunge wa Monduli Edward Lowassa kwamba anahusika na kipigo alichokipata kutokana na chuki aliyonayo kwake. Aidha amemtuhumu Spika wa Bunge, Anne Makinda kwamba naye ni miongoni mwa watu wanaomchukia pamoja na viongozi wengine wa Bunge, kwa kuwa hakuna kati yao aliyempigia simu au kumtumia ujumbe wa kumjulia hali kutokana na kipigo alichopata ambacho kimemsababishia maumivu makali. Akizungumza jana akiwa kwenye chumba alicholazwa katika Taasisi ya Tiba ya Magonjwa ya Mifupa na Ufahamu Muhimbili (Moi), Nassari alidai Lowassa ambaye amewahi kuwa waziri mkuu kabla ya kujiuzulu, amemchukia tangu alipomshinda mkwewe Sioi Sumari, kwenye uchaguzi mdogo wa ubunge uliofanyika Aprili mwaka jana. Nassari aliyekuwa amelazwa katika Hospitali ya Selian ya jijini Arusha kabla ya kuhamishiwa MOI, alidai kupigwa na kuchaniwa nguo na Green Guard wakati alipokuwa katika jitihada zake za kuhesabu kura kwenye ...

POMBE SI MAJI WAHENGA WALISEMA.....MWANAMKE AVUA NGUO NA KUCHEZA UCHI BAADA YA KUZIDISHA POMBE HUKO MBAGALA ZAKHEIM

Image
DADA mmoja ambaye jina lake halikuweza kujulukana mara moja aliuacha hoi umati wa watu waliokuwa kwenye baa moja hivi (jina kapuni) huko mbagala Zakheim mara baada ya kuvua nguo zote na kubaki uchi wa mnyama na hivyo kusababusha hali ya taharuki katika maeneo hayo.     Chanzo cha habari  kinadai kuwa dada huyo alifika maeneo hayo akiwa vizuri kabisa... Uchafu wake  ulianza baada ya yeye kunywa bia nyingi  mithiri ya mtu mwenye kiu ya maji .Pombe  ilipopanda kichwani, mrembo huyo alianza kukata mauno ovyo na  kusaula nguo mojamoja  mpaka  alipoyaanika na makalio yake..

PICHA ZA MAZISHI YA WAHANGA WA MLIPUKO WA BOMU HUKO ARUSHA

Image
  Picha za Mazishi ya mwenyekiti wa BAWACHA kata ya Sokoni I Judith William Moshi, aliye fariki kwa mlipuko wa bomu kwenye viwanja vya Soweto jijini Arusha siku ya kufunga kampeni za chaguzi ndogo tarehe 15.06.2013..

MTOTO AFANYIWA UPASUAJI KUONDOA MIGUU MIWILI YA ZIADA

Image
Mtoto wa miezi miwili wa kiume nchini Namibia amefanyiwa upasuaji wa aina yake baada ya kuwa amezaliwa akiwa na miguu minne.   Andrew Palismwe, anayetokea Caprivi, anaendelea vizuri na matibabu baada ya kufanyiwa upasuaji uliochukua masaa tisa kuondoa miguu miwili kwenye Hospitali ya watoto ya Red Cross War Memorial  iliyoko mjini Cape Town, Afrika Kusini. Mtoto huyo sasa anaendelea kupata nafuu kwenye Hospitali ya Windhoek Central nchini Namibia, imeripotiwa. Alizaliwa akiwa na miguu miwili ya ziada chini ya tumbo lake Aprili 6. Hali hiyo inadhaniwa kuwa ni matokeo ya mapacha ambao hawakukamilika.   Daktari wa Hospitali ya Windhoek Central, Clarissa Pieper alisema: "Hii ni hali ambayo mapacha wameungana pamoja na kufuatia mimba ya mapacha ambayo hawakutengana kabisa, lakini kuunda watoto wawili wanaokua ndani ya kila mmoja. Katika suala hili, mtoto mwingine hauendelea kikamilifu."   Mama wa Andrew, Ruthy Mutanimiye alisema katika hospital...

KAULI YA DAKTARI KUHUSU KUMRUHUSU NASSARI JOSHUA"NI MUONGO NA NI MNAKI KWANI APEWA KIBALI KISHA ASEMA.......

Image
UONGOZI wa hospitali ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) ya Selian jijini Arusha umekanusha vikali taarifa zilizotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Chadema John Mnyika kuwa serikali ilipeleka maafisa wa usalama hospitalini hapo kwa lengo la kumdhuru mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki Joshua Nassari pamoja na majeruhi wa mabomu waliolazwa katika hospitali hiyo na kusema ni uzushi mtupu. Mnyika alisema kufuatia kitendo hicho mbunge Nassari alipiga kelele (yowe) akiwa katika korido ya wodi namba 14 aliyokua amelazwa ili kuomba msaada baada ya maafisa hao wa usalama waliokua wamevalia mavazi ya kitabibu na kubeba vifaa vya kitabibu kumtundikia drip aliyohisi ilikua na lengo la kumdhuru ambayo aliitoa na kuitupa. Mnyika alitoa kauli hiyo jana alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika viwanja vya mahakama kuu kanda ya Arusha wakati akisubiri wabunge wanne wa chama chake pamoja na wafuasi wao waliohusika na mkusanyiko usio halali katika viwan...

JOHN MNYINKA ADAI KUWA KESHO WATAWASHA MOTO TENA JIJINI ARUSHA

Image
WAKATI Jeshi la Polisi Mkoani Arusha ikiendelea kumsaka Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe na Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini Godbless Lema,Mbunge wa Ubungo John Mnyika kesho atawasha moto mwingine wa maombolezo uliotawanywa kwa mabomu jana. Mnyika atakuwa msatari wa mbele kuongoza wafuasi wa Chadema kuaga miili ya watu watatu waliouawa katika shambulio la kigaidi Jumamosi iliyopita kwenye Uwanja wa Soweto. Mbali na Mnyika zoezi hilo pia litasimamiwa na wabunge wanne wa Chadema walioachiwa huru kwa dhamana leo kwakua upelelezi wa kesi zao hazijakamilika. wabunge hao waliachiwa huru kwa dhamana katika Kituo Kikuu cha Polisi Mkoani hapo kabla ya kufikishwa Mahakamani na kutakiwa kurudi Polisi Julai 22 mwaka huu . Wabunge hao Said Arfi (Mpanda Mjini), Tundu Lissu (Singida Mashariki), Mustapha Akunaay (Mbulu) na Joyce Mukya (Viti Maalumu), walipewa dhama hiyo majira ya saa nane mchana. Kabla ya Wabunge hao kuachiwa huru kwa dhamana, maelfu ya wafuasi wa Chama hicho walijazana ...

IDD SIMBA NA WENZAKE WAACHIWA HURU KATIKA KESI YA KUHUJUMU UCHUMI

Image
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam leo hii imemwachiria huru Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA), Idd Simba pamoja na Mkurugenzi wa Bodi hiyo ambaye alikuwa Diwani wa Kata Sinza (CCM), Salum Mwaking’inda vile vile Meneja Mkuu wa shirika hilo Victor Milanzi na Mkurugenzi wa Kampuni ya Simon Group , Simon Kisena waliokuwa wakikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi wa shirika hilo. Mahakama imewaachia huru washitakiwa kwa sababu Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), Dk Eliezer Feleshi alliwasilisha hati ya kutokuwa na haja ya kuendelea kuwashitaki washitakiwa hao chini ya kifungu cha 91(1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya mwaka 2002. Simba anayetetewa na wakili maarufu nchini Alex Mgongolwa walifikishwa na mahakamani hapo kwa mara ya kwanza Mei 27 28 mwaka jana wakikabiliwa na makosa ya kula njama, matumizi mabaya ya madaraka na kughushi na hujumu uchumi. Hivyo kuanzia sasa, washitakiwa hao wapo huru.

LUNDENGA AMTIMUA MREMBO JUKWAANI BAADA YA KUTINGA NA KIVAZI CHA NUSU UCHI....

Image
MWENYEKITI wa Kamati ya Mashindano ya Miss Tanzania, Hashimu Lundenga Jumamosi iliyopita alimtimua mshiriki wa shindano la Redd’s Miss Morogoro 2013, Saphina Chumba (20) jukwaani wakati shindano hilo lilipokuwa likiendelea. Tukio hilo lilitokea Jumamosi iliyopita katika Ukumbi wa Hoteli ya Kitalii ya Nashera mjini hapa wakati mrembo huyo alipokuwa akiwania kuvaa taji la mkoa huo.  Kisa cha mrembo huyo aliyevalia namba 5 kutimuliwa ni kukiuka maadili na kanuni za mashindano hayo kwa kuvaa nusu utupu mbele ya mgeni rasmi ambaye alikuwa Mbunge wa Kilosa, Mustapha Mkulo na mbele ya Kamati nzima ya Miss Tanzania. Baada ya kuona jinsi alivyovaa, Lundenga na kamati yake walikubaliana kumtimua mshiriki huyo kwa kumwita Jaji Mkuu wa shindano, Alex Niktasi na kumtaka amuondoe haraka. Mbali na Chumba, pia jaji alimtimu mrembo mwingine aliyevalia namba 8, Neema Joel (20) kutokana na kushiriki shindano  hilo mara mbili mwaka huu, inadaiwa mara ya kwanza a...

KISWAHILI KITUMIKA HADI VYUO VIKUU MBUGE AJENGA HOJA

Image
MBUNGE wa Karagwe, Gosbert Blandes (CCM), amehoji lini serikali itapitisha Kiswahili kitumike kuanzia Shule za Msingi hadi Vyuo Vikuu. Aidha, alisema mwaka 2004, Umoja wa Afrika ulipitisha Kiswahili kiwe ni lugha ambayo itatumika katika mikutano na shughuli mbalimbali. “Je, serikali imejiandaa vipi kupeleka wakalimani wa kutosha kutoka Tanzania ili waweze kujipatia ajira?” alihoji. Akijibu maswali hayo, Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Amos Makala alisema jitihada zinafanywa na taasisi hizo za kukuza Kiswahili mojawapo kuandika vitabu vingi vya kufundishia na kuongeza wataalamu. “Nasema wazo hilo tumelipokea na sisi ndani ya serikali tunaendelea kulifanyia kazi na hata wakati tunawasilisha bajeti yetu zilitoka hoja hizo za kuwa Kiswahili kifundishwe madarasani,” alisema. Aidha, Makala alikiri kupitishwa kwa azimio hilo na kuongeza kuwa: “Kama Tanzania tumeona kuwa hii ni fursa muhimu na tayari moja ya kazi zinazofanywa na Taasisi za k...

ARUSHA KWACHAFUKA TENA.....MABOMU YA MACHOZI YATUMIKA KUWATAWANYA WANANCHI

Image
  Hali kutoka mkoani si nzuri...mabomu ya machozi yanapigwa  kuwatawanya  wananchi  waliojitokeza  kuiaga  miili ya  wananchi  waliofariki katika mlipuko wa bomu... Hivi sasa polisi wanapiga mabomu ya machozi kuwatawanya wafuasi wa CHADEMA waliofurika katika uwanja wa Soweto Mjini Arusha ulipotokea mlipuko wa bomu Jumamosi kuomboleza ambapo polisi inasema mkusanyiko huo si halali Taarifa toka mkoani humo zinadai kuwa gari la mh. Lissu liteketezwa vibaya kwa bomu.

SABABU ZA JESHI LA POLISI KUTUMIA NGUVU YA MABOMU JIJINI ARUSHA

Image
Jeshi la polisi limekipiga marufuku chama cha demokrasia na maendelo(CHADEMA)kufanya shughuli zozote za kuaga miili ya marehemu kwenye viwanja vya Soweto kwani zoezi la uchunguzi bado linaendelea kwenye viwanja hivyo . Akizungumza ofisini kwake kamanda wa polisi mkoani Arusha, Liberatus Sabas amesema kutokana na uchunguzi unaoendelea wa tukio la bomu kwenye viwanja hivyo imeonelea kuwa si busara kuweka mkusanyiko wa watu kwani kutaharibu upelelezi. Kamanda Sabas amedai  kuwa  jeshi la polisi  liliwataka viongozi wa chama hicho kuwaeleza wafuasi wao mahali sahihi watakapoweza kufanyia shughuli hiyo lakini si kwenye viwanja hivyo. Hali kwenye viwanja hivyo imekuwa ya pilika pilika tangu juzi kwa wafuasi wa chama hicho kujikusanya tokea asubuhi hadi jioni kwa madai ya kuomboleza .. Hata hivyo viongozi wa chama cha demokrasia na maendeleo walikaidi agizo hilo na  kuanza  kujikusanya uwanjani hapo pamoja na wafuasi wa CHADEMA , hali iliyo...

NAPE , GODBLESS LEMA NA MBOWE WATAKIWA KUPELEKA ASHAHIDI WAO POLISI, VINGINEVYO SHERIA ITACHUKUA MKONDO WAKE

Image
Jeshi la Polisi limetishia kuwakamata Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema na limesema litamhoji Katibu Mwenezi wa CCM, Nape Nnauye baada ya wanasiasa hao kudai kufahamu watu waliohusika na tukio la kurushwa bomu mwishoni mwa wiki iliyopita. Akizungumza na waandishi wa habari mjini Arusha jana, Mkuu wa Operesheni wa Polisi, Kamishna Paul Chagonja aliwataka wanasiasa hao kuwasilisha ushahidi wa kile wanachofahamu kuhusu kulipuliwa kwa bomu hilo. Juzi, Mbowe akiwa na Lema, alisema wana ushahidi wa picha za video zikiwahusisha polisi na kulipuliwa kwa bomu hilo katika Uwanja wa Soweto wakati wa mkutano wa kuhitimisha kampeni za udiwani kwa Chadema, Jumamosi iliyopita. Mkwara wa Chagonja Kamishna Chagonja aliwataka Mbowe na Lema kupeleka ushahidi ili kusaidia uchunguzi wa tukio hilo. “Tunamtaka Mbowe na Lema kutoa ushahidi wa askari wetu kuhusika na tukio la bomu pale Soweto. Wasipofanya hivyo tutatumia sheria kuwalazimisha kufa...

CCM YAPINGA UWEPO WA SERIKALI TATU....

Image
Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimepinga muundo wa Muungano wa Serikali tatu unaopendekezwa katika rasimu ya Katiba Mpya iliyotolewa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba mwanzoni mwa wiki iliyopita. Chama hicho tawala kimesema bado kinaamini katika muundo wa Serikali mbili.   Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye aliwaambia waandishi wa habari mjini Dodoma jana kwamba mapendekezo yaliyowasilishwa mbele ya Tume hiyo yanabaki kama yalivyo, hivyo msimamo wao ni kuwapo kwa muungano wenye muundo wa Serikali mbili. “Mapendekezo ambayo ndiyo msimamo wa chama tulishayawasilisha kwenye Tume kuwa sisi tunapendekeza mfumo wa Serikali mbili na siyo tatu wala moja,” alisema Nape alipokuwa akitoa taarifa ya uamuzi wa Kamati Kuu (CC) ya CCM iliyokutana usiku wa kuamkia jana kujadili suala hilo.   Kauli ya Nape inafanana na matamshi ambayo yamewahi kutolewa na baadhi ya wanasiasa wakongwe ambao ni makada wa CCM wakiwamo, mawaziri wakuu wastaafu, Frederick ...

HATIMAYE THE PLATINUM AULA TENA

Image
Wanasema hela huenda kwa wenye hela na mwenye nacho huongezewa zaidi. Sina uhakika, lakini kwa mujibu wa picha nilizoziona kwenye akaunti ya Instagram ya Diamond Platnumz, inaonekana kama the lad is about get some serious money from wazee wa machapati ‘Azam’. Katika akaunti hiyo, Diamond ameweka picha kadhaa ambazo zote zinamuonesha akiwa amebeba magunia ya unga wa ngano wa Azam na katika picha moja ameandika, “Guess what???. Tutegemee surprise siku si nyingi!!

HUU NDO MJENGO UNAOSEMEKANA KUWA NI WA MCHUNGAJI MTARAJIWA a.k.a MASANJA

Image
MJENGO WA MSANII MASANJA ULIOPO JIJINI DSM

FAMILIA YA NGWEA YAMKATAA MTOTO WAKE ALIYELETWA NA MAMA YAKE MAKABURINI

Image
Siku chache baada ya aliyekuwa mkali wa Hip Hop Bongo, Albert Kenneth Mangweha ‘Ngwea’ kupumzishwa kaburini kufuatia kifo cha usingizini nchini Afrika Kusini kilichotokea Mei 28, mwaka huu, mambo kibao yanazidi kuibuka.  Mtoto wa Ngwea akiwa na baadhi ya wanafamilia wakati wa mazishi ya baba yake. Habari zinadai kuwa familia ya marehemu Ngwea imemkataa mtoto aliyeletwa na mama yake makaburini akidaiwa kuwa ni mtoto wa Ngwea. Juni 6, mwaka huu wakati wa mazishi, mwanamke aliyejitambulisha kwa jina la Paulina Jeremiah, mkazi wa Kigamboni, Dodoma alitimba akiwa na mtoto huyo wa kike aitwaye Neema Albert na kudai kuwa alimzaa na Ngwea mwaka 2001, wakati msanii huyo akisoma Sekondari ya Mazengo. Wakati akijieleza, ndugu wa Ngwea, Anthony Mangweha alikuwa akimsikiliza ambapo aliwataja wanandugu wa marehemu waliokuwa wakijua suala hilo. Waliotajwa kujua kuwa mtoto huyo alikuwa wa Ngwea ni Frank, Jotam na Amani ambao waliwahi kutumwa na marehemu kwenda ...

YULE MUUAJI WA DADA ALIYECHINJWA KAMA KUKU UKO MIKOCHENI "B" HATIMAYE APATIKANA

Image
MFANYAKAZI wa Jaji Kileo, Philemon Laiza (27) anadaiwa kumchinja mtumishi wa ndani wa jaji huyo, ambaye ni raia wa Kenya, Perpetua Mainab (30).  Mtuhumiwa huyo, ambaye alikuwa ni mtunza bustani katika nyumba ya Jaji Kileo, alifanya unyama huo wiki iliyopita.  Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Kamishna wa Polisi Kanda Maalum, Suleiman Kova, alisema mwili wa mtumishi huyo wa ndani ulikutwa kwenye dampo la kutupia takataka maeneo ya Mikocheni B. “Tukio hilo lilitokea karibu na dampo la kutupia taka Mikocheni ‘B’, katika eneo linalomilikiwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA). “Mfanyakazi huyo wa ndani alikutwa ameshakufa baada ya mwili wake kuchinjwa sehemu ya shingo, jeraha sehemu ya mkono wa kushoto karibu na kiganja, jeraha kwenye paji la uso na mwili wake ukiwa umetapakaa damu sehemu za kichwani,” alisema Kova. Alieleza kuwa mtuhumiwa huyo ambaye alikuwa akifanya kazi pamoja na marehemu, alikiri kuwa na marehemu siku hiyo...

WAKENYA WALIVYOANDAMANA JUNE 11 NA KINYAGO CHA NGURUWE NA DAMU WAKIPINGA MISHAHARA YA WABUNGE

Image
Miungano ya kijamii ikiongozwa na Bunge la mwananchi,Muhuri na pawa 254 miongoni mwa mengine yameandaa maandamano ya pili kupinga juhudi za wabunge kuhujumu tume ya kuratibu mishahara nchini kenya SRC ili kujiongezea mishahara ya hadi laki nane kinyume na ilivyopendekezwa na SRC. Tofauti na wiki kadhaa zilizo pita ambapo waandamanaji waliwaelekeza nguruwe walioandikwa majina ya wabunge walio unga mkono mswada huo, hii leo waandamanaji walibeba kinyago wa nguruwe na damu walio ashiria mwisho wawabunge kukandamiza wakenya. huku wakijimwagilia damu kama ishara ya kuumizwa na kodi ya kuwalipa wabunge.  Waandamanaji pia walibeba mfano wa noti za shillingi alfu moja pesa za kenya zilizo chorwa Nguruwe mkubwa kwa upande mmoja na wanawe kwa upande wa pili, huku wakiwarushia wabunge noti hizo kuashiria kujitakia makuu kwa wabunge hao. Viongozi wa waandamanaji wameahidi kuendeleza maandamano hadi pale wabunge watakapo sitisha hujuma dhidi ya tume ya bi...

MAZISHI YA MSANII WA BONGO MOVIE ( KASHI ) ALIYEFARIKI JANA

Image
              Pichani juu ni mazishi ya msanii ya mwigizaji  Jaji Khamis 'Kashi' aliyefariki jana mchana katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar yaliyofanyika leo mchana majira ya saa nane kwenye makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam. Marehemu Kashi alikumbwa na umauti baada ya kuugua ghafla malaria na kifua. Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu Kashi mahali pema peponi. AMEN!