mmoja kati ya waimbaji wachache wabongo waliowahi kupata nafasi ya kuimba kwenye stage moja na mkali kutoka Congo DRC Fally Ipupa, BARNABA BOI amezungumzia stori za kumpa binti mmoja mrembo, ujauzito. akiongea EXCLUSIVE na millardayo.com, amesema “ni kweli na wala sio siri, hii sio bahati mba ya , girlfriend wangu ana ujauzito na Mungu akijalia ndani ya miezi miwili ijayo au mwezi mmoja na nusu atajifungua, ya ni naona kama nimetoa wimbo mp ya tu” – Barnaba B amesema kiumri hawajapishana sana, “mimi Barnaba nina miaka 22, yeye 21 na tumeanza kuishi pamoja huu ni mwezi wa nane, na uhusiano wetu wa kimapenzi una miaka miwili na nusu sasa hivi na wazazi wanafaham”