Posts

Rais Magufuli atoa samalu ya Eid kwa Waislam

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametoa salamu kwa waumini wa dini ya Kiislam na kuwatakia sikuu njema ya Eid. Katika ukurasa wake wa twitter Rais Magufuli ametoa ujumbe huo kuwatakia Eid njema, huku akihimiza kudumisha amani, upendo na mshikamano. "Nawatakia Waislamu na watanzania wote sikukuu njema ya Eid el-Hajj, tunaposherehekea sikukuu hii tuendelee kudumisha upendo,amani,umoja na mshikamano wetu. Eid Mubarak", aliandika Rais Magufuli. Waumini wa dini ya Kiislam nchini leo wanaungana na Waislam wenzao wote duniani, kusherehekea sikuku ya Eid ambayo huadhimishwa kila mwaka, mara baada ya ibada ya Hija kukamilika, na mara nyingi husherehekiwa kwa kuchinja wanyama waliohalalishwa kwa binadamu.

Mahakama imeelezwa Sethi wa IPTL Amewekwa Puto Tumboni

Image
Upande wa utetezi umeieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa Mmiliki wa Kampuni ya kufua umeme ya IPTL, Harbinder Singh Sethi amewekewa ‘Puto’ tumboni kutokana na ugonjwa unaomkabili hivyo asipohudumiwa inavyotakiwa anaweza kupoteza maisha. Mbali ya Seth, mwingine ni Mfanyabiashara James Rugemarila ambapo kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka 12, yakiwemo ya kutakatisha fedha na kuisababisha Serikali hasara ya TSh 309,461,300,158. Wakili wa utetezi, Joseph Mwakandege amemueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi kuwa mteja wake Seth anatakiwa apelekwe Hospital ya Taifa Muhimbili lakini hadi sasa hajapelekwa na ni dhahiri upande wa mashtaka umedharau amri mbili za Mahakama. ”Ugonjwa uliosababisha Seth atakiwe kwenda Muhimbili ni baada ya kufanyiwa upasuaji mkubwa ambapo tumboni kwake kumewekwa Balloon ‘Puto’ hivyo asipohudumiwa ipasavyo inaweza kusababisha kifo, naomba mshtakiwa apelekwe Muhimbili kwa sababu ni Hospitali ya juu na yenye vifaa na watalaamu wa kuto

Hakimu Akataa Msokoto wa Bangi Kesi ya Wema

Image
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu leo imekataa kupokea ushahidi wa msokoto wa bangi na vipisi viwili vya madawa hayo ya kulevya katika kesi inayomkabili mwigizaji Wema Sepetu . Uamuzi huo umetolewa na Hakimu, Thomas Simba , aliyesema mahakama haiwezi kupokea vielelezo hivyo kwa sababu msokoto wa bangi na vipisi vina kasoro kwa kuwa shahidi hakuvifafanua mahakamani. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Septemba 12 mwaka huu.

Serikali yataifisha magari yaliyoingizwa nchini kinyume na sheria

Image
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetaifisha jumla ya magari sita yakiwepo magari matatu aina ya Ranger Rover Sports yaliyoingizwa nchini kinyume na sheria baada ya watuhumiwa hao kukiri kuwa wamefanya kosa hilo. Rais Magufuli mwezi Machi mwaka huu alipokwenda bandarini alikuta kuna makontena yenye magari ndani yake huku wamiliki wa makontena hayo wakidai  makontena hayo yalikuwa na nguo na mabegi  lakini baada ya kufunguliwa zilionekana gari za kifahari zikiwa kwenye makontena hayo, jambo ambalo lilionekana wamiliki wa mahari hayo walikuwa wakiingiza magari hayo kinyume na utaratibu na sheria za nchi. Mkurugenzi wa Mashtaka nchini, DPP Biswalo Mganga amesema kuwa baada ya mahakama kuwakuta na hatia raia hao wakigeni ambao walidai kuwa kontena hizo zilikuwa na nguo na mabegi wakati ni magari hivyo serikali imetaifisha magari yao na sasa kuwa magari ya serikali. "Rais hao wamekiri makosa yao yote mawili na kutokana na kukiri kwao mahakama ime

‘Masogange’ Ana Kesi ya Kujibu Dawa za Kulevya

Image
Video Queen, Agnes Gerald ‘Masogang aliyevaa gauni la kijani aikitoka mahakamani kusikiliza kesi inayomkabili. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imesema kuwa Video Queen , Agnes Gerald ‘Masogange’, anayo kesi ya kujibu kwa kudaiwa kutumia dawa za kulevya, hivyo anapaswa kujitetea. Kesi hiyo ambayo imeunguruma leo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri, amesema kuwa amekubaliana na hoja za ushahidi wa upande wa mashtaka ambapo mshtakiwa amekutwa na kesi ya kujibu na hivyo ana haki ya kujitetea. Baada ya kauli ya hakimu huyo, Masogange amesema atajitetea kwa njia ya kiapo na atakuwa na mashahidi watatu. Hakimu Mashauri ameiahirisha kesi hiyo hadi Oktoba 12, mwaka huu ambapo mtuhumiwa ataanza kujitetea. NA DENIS MTIMA/GPL

Ridhiwani Kikwete Amvaa Kigwangala

Image
 Mbunge wa jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete amemvaa Naibu waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.Khamis Kigwangala na kumwambia anaweza kuwa sehemu ya wachochezi kwa anachokifanya. Ridhiwani Kikwete amebainisha hayo kupitia ukurasa wake wa twitter baada ya  Mhe. Kigwangalla kuonyesha kusikitishwa na kitendo kilichofanywa na Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma katika kuwafanyia usaili baadhi ya wataalamu waliojitokeza kwenye usaili  wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ambao umefanyika mapema leo Agosti 30, 2017. "Unaweza dhani unauliza swali kumbe nawe unakuwa sehemu ya wachochezi! Mhe. Waziri unaweza kuwa hujui kusoma lakini picha inatoa jibu sahihi", aliandika Ridhiwani. Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma leo Agosti 30, 2017 ilifanya usaili kwa ajili ya nafasi za kazi katika Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) ambapo takribani watu 30,000 walijitokeza huku ikiwa watu 400 pekee ndiyo wanaotakiwa.

Zijue faida za uaminifu katika mahusiano ya Ndoa

Image
Suala la uaminifu katika mapenzi kwa karne hii limekuwa kikwazo kikubwa kwa watu wengi sana, wengi wemekuwa si waaminifu wakati mwingine kupelekea mahusiano hayo kufa. Hivyo uaminifu ni muhimu sana katika mapenzi kwa kuwa katika mahusiano ya kimapenzi kuna faida nyingi kwa mwili na akili. Watu walio katika mahusiano bora ya mapenzi huishi maisha marefu na kufurahia afya njema kuliko wale wasiokuwa katika mahusiano ya aina hiyo. Faida hii haina pingamizi kwa sababu ya ukweli kwamba watu wanaokuwa katika mahusiano ya karibu wanajijengea hisia na nguvu fulani ambayo huwasaidia kusaidiana na kujaliana wakati wa shida. Siyo tu kwamba watu walioko katika mahusiano ya aina hii wanaishi muda mrefu lakini pia ni kweli kwamba wanakuwa na furaha na wanaridhika na maisha kuliko wale wanaoshindwa kukaa katika mahusiano. Pili, kuwa katika mahusiano mazuri ya mapenzi kunasaidia katika mambo mbalimbali ya kimahitaji. Kusaidiana katika mahitaji mbalimbali baina ya wapenzi ni nji

Mobeto Ampukutisha Zari

Image
Hamisa Mobeto. DAR ES SALAAM: Mwanamitindo Hamisa Mobeto amedaiwa kuwa sehemu ya kupungua mwili kwa mwanadada mjasiriamali maarufu, Zarina Hassan ‘Zari The Boss Lady’. Kwa mujibu wa chanzo makini, tangu Mobeto aanze kuibua mjadala mtandaoni kuhusiana na mtoto wake kudaiwa kuwa ni wa bwana wa Zari, mjasiriamali huyo amejikuta akipungua mwili kutokana na mawazo aliyonayo. “Zari kapungua mwili kweli jamani. Mobeto amemponza. Amemsababishia watu wamtukane sana Zari kiasi ambacho amekosa amani kabisa. Masikini mtoto wa watu kakonda kweli sasa hivi. Zari. “Ukitazama picha za Zari sasa hivi si Zari yule aliyetoka kujifungua. Tena kwa kawaida tunajua mtu ukitoka kujifungua unanenepa lakini kwa Zari mambo yamekuwa tofauti. Ngoja niwatumie picha yake ya sasa muone,” kilisema chanzo. Hata hivyo mwanahabari wetu aliingia kwenye ukurasa wa Instagram wa Zari na kujionea jinsi alivyopungua baada ya kuona picha zake mpya na kulinganisha na picha zake za zamani. Lic

Muigizaji wa Siri za Familia apata ajali

Image
Luwi Cappelo Muigizaji wa filamu Luwi Cappelo wa nchini Kenya ambaye ameigiza tamthilia ya Siri za Familia inayorushwa na East Africa Television, amepata ajali ya gari na kulazwa hospitali ya Pandya mjini Mombasa Kenya, katika chumba cha wa wagonjwa Mahututi. Mkurugenzi wa Jasson Production ambao ndio watengenezaji wa tamthilia ya Siri za Familia, Bw. Sanctus Mtsimbe, amesema kwamba mara ya mwisho aliwasiliana na Lui akiwa njiani kuelekea Mombasa kwenye harusi huku akiwa na wenzake, lakini baadaye alipata taarifa za ajali hiyo. Hata hivyo Siri za Familia zimetoa taarifa rasmi ya ajali hiyo kwenye ukurasa wake wa instagram, ukiandika...”Tumepata taarifa kupitia wenzetu wa Nairobi kuwa siku ya Jumapili saa 8 alfajiri, muigizaji wetu wa Siri za Familia msimu wa 4 kutoka Kenya Luwi na rafiki zake watatu, walipata ajali katika barabara ya Mombasa - Malindi wakiwa wanatoka kwenye sherehe ya harusi. Luwi alikuwa amekaa nyuma na aliumia, kwa sasa Luwi amelazwa Hospita

HESLB Yaongeza Muda wa Uombaji Mikopo Vyuo Vikuu

Image
Mkurugenzi Mkuu wa HESLB, Abdul-Razaq Badru. Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imeongeza muda wa wanafunzi kuwasilisha maombi ya mikopo. Hatua hiyo imeelezwa inalenga kutoa nafasi kwa wanafunzi walioshindwa kufuata masharti kuyakamilisha. Mkurugenzi Mkuu wa bodi hiyo, Abdul-Razaq Badru amesema muda huo umeongezwa hadi Septemba 11 badala ya Septemba 4. “Tumesogeza mbele kwa siku saba zaidi ili walioshindwa kufuata vigezo wakati wa kujaza fomu wafanye hivyo,” amesema. Amesema hadi kufikia jana Agosti 29 , wanafunzi waliojitokeza walikuwa 49,282 lakini ni 15,473 waliokamilisha maombi kwa njia ya mtandao.

VANESSA MDEE NA JUX ACHENI KUTUZUGA!

Image
Nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunizawadia pumzi yake ambayo imeniwezesha kuandika barua hii ya leo inayokufikia wewe msomaji ambaye pia umekuwa ukinisaidia kwa maoni na ushauri kuhusu safu yetu hii. Leo nina kazi ya kuzungumza na wanamuziki wawili ambao kwa muda mrefu, wametengeneza moja kati ya kapo bomba kabisa za wasanii wanaojihusisha kimapenzi. Unapozungumza kuhusu wasanii wanaofanya vizuri kwa sasa katika Bongo Fleva, huwezi kuwaacha kando Jux na Vanessa ambaye ni maarufu kama Vee Money, kwani hivi sasa ni miongoni mwa vijana wanaotupa uwakilishi mzuri kimataifa, kwa sababu kazi zake ni moto barani Afrika. Binafsi ninawakubali, maana mimi pia ni muumini mkubwa wa aina ya muziki wanaofanya. Maisha ya kimapenzi ya wasanii hawa siku za nyuma, leo yamenisukuma niseme nao kidogo, hasa kwa kuangalia matukio yanayoendelea hivi sasa kati yao. Uhusiano wao uliingia dosari kwa namna ambayo hakuna hata shabiki mmoja alitegemea, maana ni kama kitu cha g

Majambazi wateka basi, wapora madiwani

Image
MAJAMBAZI sita wameteka basi la Kampuni ya Safi na likitokea Kijiji cha Mamba wilayani Chunya kwenda jijini Mbeya na kisha kuwapora abiria jana. Miongoni mwa waliotekwa ni pamoja na baadhi ya madiwani waliokuwa wakielekea mjini Chunya kwa ajili ya kuhudhuria kikao cha Baraza la Madiwani Maalumu kwa ajili ya kupitia na kujadili Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kilichofanyika jana. Akizungumzia tukio hilo, Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya, Ramadhani Shumbi aliyekuwa mmoja wa waathirika wa uvamizi huo, alisema tukio hilo lilitokea saa moja kasorobo asubuhi katika eneo la Loge. Shumbi ambaye ni Diwani wa Kata ya Mamba, alisema walipofika eneo hilo lililo na msitu mkubwa, walikuta kuna gogo kubwa lililolazwa na kufunga barabara na kisha walijitokeza watu sita mmoja akiwa amebeba bunduki na wengine mapanga na fimbo. Alisema watu hao walipiga risasi tatu hewani na kuanza kupiga vioo vya basi wakiwaamuru abiria washuk

Mawakili wamgomea Tundu Lissu

Image
MAWAKILI WA KUJITEGEMEA WAKITOKA MAHAKAMNI BAADA YA KUMALIZA SHUGHULI ZAO KATIKA MAHAKAMA YA HAKIMU MKAZI KISUTU JIJINI DAR ES SALAAM JANA. MAWAKILI wa kujitegemea wamekaidi kutii wito wa Baraza la Uongozi wa Chama cha Mawakili (TLS) wa kutohudhuria mahakamani kwa siku mbili baada ya jana kujitokeza katika mahakama mbalimbali kutetea wateja wao. MAWAKILI wa kujitegemea wamekaidi kutii wito wa Baraza la Uongozi wa Chama cha Mawakili (TLS) wa kutohudhuria mahakamani kwa siku mbili baada ya jana kujitokeza katika mahakama mbalimbali kutetea wateja wao. Jumapili, baraza hilo kupitia Rais wa TLS, Tundu Lissu, lilitangaza maazimio matano likiwamo la kuwataka mawakili wote nchini kutohudhuria mahakamani na kwenye mabaraza kwa siku mbili, jana na leo, ikiwa ishara ya kupinga kuvamiwa na kulipuliwa kwa bomu kwa ofisi ya kampuni ya uwakili ya IMMMA jijini Dar es Salaam, usiku wa kuamkia Jumamosi iliyopita. Mawakili jana walionekana kukaidi wito huo baada ya kuhudhuria ma

JOYCE KIRIA AELEZA BANGI ZILIVYOMKOMESHA

Image
  Joyce Kiria. MTANGAZAJI maarufu Bongo, Joyce Kiria amefunguka jinsi alivyokomolewa na kitendo chake cha kuvuta bangi, akidhani kingempa ujasiri, lakini badala yake akajikuta akishindwa kabisa kufanya kitu alichokusudia. Akizungumza na Za Motomoto News, Joyce alisema kwa mara ya kwanza alivuta bangi alipoanza utangazaji katika kituo kimoja cha redio kipindi hicho na alifanya hivyo ili apate ujasiri wa kutangaza kwani alikuwa hajui, lakini aliambulia kuona vitu viwiliviwili na kushindwa kabisa kutangaza. “Nimewahi kuvuta bangi mara moja ili niweze kutangaza maana nilikuwa naogopa, lakini nilipofika studio nikawa naona mic mbilimbili, watu wawiliwawili mwisho nikarudi nyumbani ambako nilikaa siku mbili nzima ndiyo nikawa sawa, sijawahi kurudia tena na sina mpango maana nilikoma siku hiyo,” alisema Joyce. STORI: GLADNESS MALLYA| RISASI

BREAKING NEWS: Lissu Awaongoza Mawakili Kugoma Kuingia Mahakamani

Image
Tundu Lissu akiakiwa na mawakili wengine wakati wakizungumza na wanahabari katika Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu, Dar. RAIS wa Chama cha Mawakili Tanzania (TLS), Tundu Lissu amewaongoza mawakili nchini kugoma kuingia mahakamani kwa muda wa siku mbili Agosti 29 na 30, 2017 wakilaani tukio la kushambuliwa kwa ofisi za Kampuni ya Mawakili ya IMMMA Advocates iliyolipuliwa kwa bomu usiku wa kumakia Jumamosi iliyopita. “Mengi wamefanyiwa mawakili lakini hili la juzi tumesema hatukubali kukaa kimya wakati mawakili wetu wanashambuliwa. Kwa busara za TLS tuliona tufanye maamuzi ya kusimamisha kazi kwa siku mbili ili kupeleka ujumbe kuwa jambo hilo si jema,” alisema Lissu. Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu LHRC Dr. Hellen Kijo Bisimba akizungumza na wanahabari . Kuhusu endapo mawakili wote wamegoma Lissu alisema hawezi kulizungumzia kwa sasa, hadi jioni ambapo ripoti kamili itakuwa imepatikana kwa kuwa kuna mawakili wengine walikuwa na kesi as

Mbunge wa Tunduma atakiwa kukamatwa

Image
Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Momba mkoani Songwe imeagiza kukamatwa mara moja kwa Mbunge wa Jimbo la Tunduma kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mh.Frank Mwakajoka kwa tuhuma za kuwadhihaki wateule wa Rais. Kamati ya Ulinzi na usalama wilayani ya Momba imeagiza kiongozi huyo kukamatwa baada ya kumdhihaki Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Mkuu wa Mkoa wa Songwe Mhe. Chiku Galawa pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Momba Mhe. Juma Said Irando.

Manara alalamikia Bodi ya ligi

Image
Afisa habari wa klabu ya Simba, Haji Manara Afisa habari wa klabu ya Simba, Haji Manara amefunguka kwa kuwatupia lawama Bodi ya Ligi (TPLB) ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kuwa wanachokifanya siyo sawa wanabidi wabadilike. Manara ameeleza hayo baada ya Bodi hiyo kufanya mabadiliko ya ratiba za mechi zinazoshiriki katika Ligi Kuu ili kupisha mechi ya kirafiki baina ya Tanzania na Botswana iweze kuchezwa mnamo Septemba 2 mwishoni mwa juma hili. "Nimesikitika sana kuona kwamba ratiba ya Ligi Kuu imebadilishwa, mechi hizi zipo kwenye kalenda ya FIFA. Mnapanga ratiba mechi ya pili tu mnaanza kubadilisha ratiba kwa hiyo sisi mechi yetu na Azam FC haitakuwepo ?", alisema Manara Pamoja na hayo, Manara ameendelea kwa kusema "mnatupunguza ile nguvu tuliyoanza nayo, hili jambo nilishalisema sana kwa nini mnavyopanga ratiba zenu bodi ya Ligi msiwe mnaangalia kalenda ya FIFA. Hivi mshawahi kusikia wapi duniani mtu anabadilisha ratiba la

Tshirt na Jinsi ya Manji yazua gumzo

Image
Huku akitia huruma, baadhi ya wananchi jijini hapa wameibua gumzo kuhusiana na nguo anazovaa mfanyabiashara maarufu, Yusufu Manji ambaye ana kesi mbili zinazomkabili. Manji ambaye alifikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza Februari 17, mwaka huu amekuwa akikabiliwa na kesi mbili, moja ikihusu uhujumu uchumi na ya pili ni madai ya matumizi ya dawa za kulevya. Baadhi ya wananchi wamekuwa wakidai kwamba wamekuwa wakimshuhudia Manji akija mahakamani akiwa amevaa tisheti ya rangi nyeusi kwa zaidi ya mara kumi, jambo ambalo limeleta gumzo kwa kuwa wanaamini ana nguo nyingi. “Hatujui sababu, huyu bwana ni tajiri sana lakini kila akifika mahakamani anavaa tisheti nyeusi ileile, kwa nini?” alihoji mwananchi mmoja. Wapo waliomuonea huruma na kudai kwamba inawezekana anafanyiwa figisufigisu kwa kutoruhusiwa kupelekewa nguo na wengine wanadai kwamba inawezekana ameamua mwenyewe awe hivyo kama alivyoamua kutonyoa ndevu. UWAZI liliamua kumtafuta mtaalamu wa utabiri (Astrologer

FAIDA ZA UGALI WA DONA

Image
MARA nyingi baadhi ya watu huwahimiza watu wengine kutumia unga wa mahindi au nafaka zingine usiokobolewa bila ya kubainisha hasara ya unga wa aina hiyo. Watu wengi (bila shaka hata wewe msomaji wa makala haya), hawako tayari kutumia unga usiokobolewa maarufu kama dona. Kuwalazimisha watu wa aina hiyo kutumia unga usikobolewa (unga wa dona) ni sawa na kuwaweka watu hao katika hatari ya kuwa na lishe duni. UNGA WA MAHINDI Unga wa mahindi, ulezi, uwele, mtama na kadhalika ni chanzo kikubwa kwa watu wengi barani Afrika cha virutubisho kama vile wanga, protini, madini na vitamini. Hata hivyo, namna ya usagaji na matumizi ya unga wa mahindi na nafaka hizo inaweza kuukosesha mwili faida ya virutubisho vilivyomo katika nafaka hiyo. UNGA ULIOKOBOLEWA Mahindi yaliyokobolewa yaani sembe au nafaka zingine zikikobolewa kama mtama, ulezi n.k hupoteza sehemu fulani ya nafaka hizo. Kama mahindi au mtama na ulezi utasagwa bila kukobolewa unga wake huitwa unga wa dona (whole-g

Zitto Kabwe: Rais Magufuli Akiniteua Nitakataa!

Image
Rais Magufuli (kulia) akisalimiana na Zitto Kabwe, kushoto ni Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete. KIONGOZI wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe amesema kuwa hatokubali endapo Rais Dkt Magufuli atamteua kushika nafasi yoyote ya uongozi kwani hatakuwa na fursa ya kukijenga chama chake ili kiwe tayari kushinda uchaguzi na kushika dola. Zitto ambaye chama anachotoka tayari kimetoa viongozi wawili ambao ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Prof. Kitila Mkumbo na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Elisha Mghwira alisema endapo atateuliwa, atamshukuru Rais na kukataa uteuzi huo. Zitto Kabwe ambaye ni Mbunge wa Kigoma Mjini aliyasema hayo alipokuwa akifanya mahojiano na gazeti la Mwananchi wakati akijibu swali kuhusu uteuzi wa viongozi wa chama chao ambao mmoja alikuwa mshauri wa chama na mwingine alikuwa mwenyekiti wa chama hicho kichanga Tanzania. “Sitakubali uteuzi kwa sababu jukumu langu na viongozi wengine wa ACT- Wazalendo ni kujenga chama ili kupata ushawis