Kikwete: "Nisingekuwa Rais Ningekuwa Msanii Mkali wa Bongo Fleva.".........HOTUBA ya Rais Kikwete Aliyoitoa Jana Mei Mosi
RAIS Dkt. Jakaya Kikwete, ametamba kuwa angakuwa msanii wa muziki wa kizazi kipya basi angelikuwa wa “BongoFleva” kutokana na kuwa na sauti nzuri yenye kumudu kuimba nyimbo kwa ufasaha zaidi.
Kauli
hiyo aliitoa jana jijini Mwanza kwenye uwanja wa michezo wa CCM
Kirumba wakati wa maadhimisho ya kilele cha sherehe za Mei mosi
zilizofanyika Kitaifa jijini Mwanza kwa mwaka huu wa mwisho wa utawala
wake.
Dkt. Kikwete aliimba wimbo wa Bendi ya OSS (Ochestra Safari Sound) wenye mashairi yasemayo "Mimi msafiri bado niko njiani sijui lini nitafika... naulizia watu kule ninakokwenda....” na kukonga nyoyo za mashabiki wa muziki wa dansi waliomshangilia ambapo alijiamba kuwa na sauti ya mauzo.
“Mmesikia
sauti yangu si mbaya sana, hakika nisingekuwa Rais wa Nchi hii basi
nigekuwa msanii wa bongo fleva kama akina Ali Kiba, Diamond na wasanii
wengine wakali nikiuza album zangu kwani ningekuwa tishio kwa
kuimba...” alisema.
Rais
pia alimpongeza msanii maarufu nchini wa kizazi kipya mwenye mashairi
na misamiati ya maneno magumu, Mrisho Mpoto, kwa kumtaka kujibu bango la
walimu lililokuwa na ujumbe uliosomeka “Shemeji Unatuachaje??” ambapo alijibu kwa kusema kuwa "kuoa mwalimu nitabu kweli kweli haya nimesikia."
Comments
Post a Comment