Posts

MAGAZETI YA UDAKU LEO,STORI KUBWA FAMILIA YA NDIKUMANA YAZUIA UWOYA ASIPIGWE, MOBETTO AMFANYIA UKATILI MWANAYE

Image
     

BREAKING NEWS: MUGABE ANG’OLEWA UENYEKITI WA ZANU-PF

Image
Chama tawala nchini Zimbabwe, ZANU-PF, kimemtimua Rais Robert Mugabe, kwenye uenyekiti wa chama na kumteua aliyekuwa Makamu wa Rais kabla ya kufutwa kazi na Mugabe, Emerson Mnangagwa kuongoza chama hicho.Anatakiwa ajiuzulu mwenyewe urais au kung’olewa madarakani kwa lazima kwa kupigiwa kura ya kutokuwa na imani naye na Bunge la nchi hiyo. Vilevile chama tawala ZANU-PF kimemfutia uanachama mke wa Rais Mugabe, Grace Mugabe. Hatua hiyo inamnyang’anya moja kwa moja cheo cha uenyekiti wa Baraza la Wanawake la chama hicho. Kikao cha Kamati Kuu ya chama tawala nchini Zimbabwe, ZANU-PF kinaendelea muda huu huku lengo ni kumng’oa madarakani Rais Robert Mugabe aliyedumu kwa miaka 37. Washiriki wa karibu wa Rais Robert Mugabe katika chama alichokianzisha wamemtaka kiongozi huyo kuondoka madarakani kufuatia shinikizo kubwa la maandamano linaloendelea nchini humo sanjari na jeshi kuingilia kati. Katika kikao hicho kinachoendelea leo, Novemba 19, viongozi wa juu wa chama hich

Haya Ndio Madhara 6 Ya Kutoa Mimba

Image
Kutoa mimba ni nini? Hii ni hali ya mwanamke kwa hiari yake mwenyewe kuharibu mimba iliyoingia ndani ya kizazi chake. Kutokana kuongezeka kwa idadi ya mahusiano duniani na kutotumia njia za uzazi wa mpango kwa watu wengi walioko kwenye mahusiano, wasichana wengi kwa sasa wanatoa mimba. Utafiti nilioufanya mwenyewe nimegundua kwamba zaidi ya asilimia tisini ya wasichana wanaokua kwenye mahusiano na wanaume zaidi ya mwaka mmoja kabla ya ndoa hutoa mimba na asilimia tano tu ya wote ndio wanaamua kuzaa. Sio ajabu kusikia mtu ameolewa akiwa ametoa mimba nne mpaka tano. Sasa unajiuliza bado kuna mtu humo au mfu? Hata hivyo hao wanaozaa pia hujikuta wamebeba mimba zingine wakati watoto wao wakiwa wadogo na kulazimika kuzitoa. Najua watu wengi wanatoa mimba kukwepa aibu, kutokua tayari kisaikolojia na kadhalika lakini ni bora kutumia njia za uzazi wa mpango kama condomu kuzuia mimba na kama kondomu huiwezi basi tumia njia zingine kama sindano na vijiti kwasababu wengi w

BONGO MOVIE NIAJE, WALIMSUSA LULU AU?

Image
KUNA mambo katika maisha siyo kanuni, lakini utamaduni umeyafanya kuwa kama ndiyo utaratibu. Na haya yako mengi kutegemea na mila za kila jamii. Huwezi kushtakiwa kwa kutokufanya, lakini wanaojumuika na wewe watakesha wakikushangaa. Jirani yako akipatwa na matatizo, siyo lazima ujitoe na kumsaidia kwa wakati huo, lakini utamaduni wetu unakuona mtu wa ajabu kama ikikutokea hivyo, halafu wewe badala ya kujumuika naye kwa kumfariji, unaalika watu wa ngoma na kufurahi pamoja nao. Hali iko hivyo kwa wafanyakazi wa ofisi moja, wa tasnia moja na hata watu wanaotoka jamii moja.Kwa mfano, watu wa makabila tofauti kutoka mikoa mbalimbali, wanapokutana katika mkoa au wilaya moja huwa kama ndugu na mmoja wao anapopatwa na matatizo au kuwa na shughuli, wengi hutazamiwa kuwepo. Katika eneo kama hilo, ingawa huwezi kumpeleka mtu kortini, lakini inapotokea mmoja anashindwa kuhudhuria shughuli hiyo, huonekana kama msaliti kwa wenzake, kitu ambacho kistaarabu kinatia doa. Na kushir

MANCHESTER UNITED WAITANDIKA NEWCASTLE BAO 4,POGBA NA ZLATAN WAKIREJEA

Image
      MANCHESTER UNITED (4-1-4-1): De Gea 6; Valencia 6.5, Smalling 7, Lindelof 5.5, Young 7; Matic 6.5; Rashford 6, Mata 7.5 (Herrera 83), Pogba 8 (Fellaini 70 6), Martial 7 (Ibrahimovic 77 6); Lukaku 7 77) SUBS UNUSED: Romero, Rojo, Lingard, Herrera, Shaw GOALS: Martial, Smalling, Pogba, Lukaku BOOKED: Smalling NEWCASTLE (4-4-2): Elliot 6; Yedlin 6.5, Clark 6.5, Lejeune 6.5, Manquillo 6; Murphy 6, Shelvey 7, Hayden 6.5, Ritchie 6.5 (Aarons 66 6); Joselu 5.5 (Mitrovic 71 5.5), Gayle 6.5 (Diame 77 6) SUBS UNUSED: Diame, Perez, Mbemba, Darlow, Gamez GOAL: Gayle BOOKED: Hayden REFEREE: Craig Pawson

Amtosa Mumewe Ulaya, Achukuliwa na Kiserengeti cha Gambia

Image
Mama mwenye watoto tisa Heidi Hepworth (44) akiwa na mpenzi wake wa sasa Mamadou Jallow. MWANAUME mmoja mkazi wa Uingereza Andy Hepworth, amesimulia kwa huzuni jinsi mkewe Heidi Hepworth (44) alivyomtosa, akamwachia watoto tisa na hivi sasa anajirusha na kivulana cha kutoka Gambia, Afrika. Mwanamke huyo anaishi na kijana huyo anayejulikana kama Mamadou Jallow (30) baada ya kufahamiana kupitia Mtandao wa Facebook ambapo aliamua kumfuata hukohuko Gambia na mpaka sasa anaishi naye huko. Jinsi alivyokolewa na mapenzi hayo mapya, sasa Heidi anadai talaka na kusema kuwa amempata ampendaye zaidi. …Enzi ya ndoa yao na mume wake Andy. “Ni jambo la ajabu, alianza tabia ambazo sikuzifahamu. Alianza kwenda gym, akakodisha vitanda maalum vya kuotea jua kwenye fukwe, akaanza kujichora tattoo na kuvaa nguo za ajabu,” anasema Hepworth na kuongeza: “Amekuwa mtu wa ovyo. Mwanzoni alikuwa mama mwenye upendo na anayejua majukumu yake. Hivi sasa ni kama shetani ameukamata m

Alietajwa kufariki ajali ya ndege kumbe yupo hai

Image
Mfanyakazi wa hoteli za kitalii za andBeyond Serengeti, Moses Muhina aliyetajwa kuwa ni miongoni mwa abiria waliofariki dunia katika ajali ya ndege ya Shirika la Coastal Aviation, imebainika alibadili ndege muda mfupi kabla ya safari ili kuwahi kazini. Muhina ambaye ni mwongozaji watalii katika hoteli hiyo, alikuwa aondoke na ndege ya Coastal Aviation saa nne asubuhi lakini viongozi wa hoteli walimbadilishia ndege, hivyo aliondoka na Air Exel iliyofika salama Serengeti. Akizungumza na gazeti hili, meneja uendeshaji wa Hoteli ya andBeyond Serengeti Under Canvas, Mussa Matala alisema Muhina ambaye anasomeka kwenye orodha ya ndege kama Maina alikuwa apande ndege hiyo lakini walimbadilishia. Alisema waliomba aondolewe kwenye orodha ya wasafiri wa ndege hiyo lakini kwa bahati mbaya hadi ndege ilipoondoka jina lake lilikuwapo. Wakati huohuo, raia watano wa kigeni ambao walifariki dunia katika ajali hiyo, akiwamo rubani Dewald Raubenheimer raia wa Afrika Kusini, ambay

Uwoya Roho Mkononi Rwanda! Anaswa na Mabaunsa

Image
Muigizaji Irene Uwoya Siku chache baada ya Hamad Ndikumana ‘Katauti’ kufariki dunia, imedaiwa kuwa, usalama wa mzazi mwenziye marehemu, muigizaji Irene Uwoya ambaye jana alikwea ‘pipa’ kwenda kuhani msiba nchini Rwanda ni mdogo. Uwoya ambaye alifunga ndoa na marehemu na kuishi naye kwa miaka kadhaa kabla ya kutengana, alianza kufanya mipango ya safari Jumatano iliyopita, saa chache mara baada ya kupokea taarifa za kifo hicho kilichotokea Jumanne usiku. CHANZO CHAFUNGUKA Kwa mujibu wa chanzo makini kutoka Rwanda, kuna kikundi cha watu ambacho kimekuwa na hasira na mrembo huyo kwa kile wanachofikiri kuwa kifo cha Ndikumana kimetokana na ‘stress’ zilizosababishwa na mrembo huyo. “Kwa kweli huku usalama wa Uwoya ni mdogo sana maana kama unavyojua kuna mashabiki ambao walikuwa wanamkubali Ndikumana ambaye alikuwa na mchango mkubwa sana katika soka la Rwanda,” kilidai chanzo hicho. WANAAMINI UWOYA NDIYO KIKWAZO Chanzo hicho kilizidi kumwaga data kuwa, wanac

DK Cheni Afunguka Lulu Kugomea Rufaa

Image
Muigizaji wa muda mrefu nchini, Mahsein Awadh maarufu kama Dk Cheni, akiwa na msanii Elizabeth Michael ‘Lulu’. DAR ES SALAAM: Muigizaji wa muda mrefu nchini, Mahsein Awadh maarufu kama Dk Cheni, amefunguka kuhusu tetesi zilizozagaa mitandaoni, zikimhusisha kuhusu kugomea rufaa kwa msanii Elizabeth Michael ‘Lulu’. Katika posti za watu mbalimbali mitandaoni, waliandika kuwa Dr Cheki alisema Lulu ambaye ameanza maisha ya gerezani, alikataa ndugu zake wasikate rufaa kwa kile alichosema, anataka kumaliza kifungo chake mapema ili awe huru kisaikolojia. Lakini juzi, Dk Cheni ambaye alikuwa staa pekee aliyekuwa akihudhuria mahakamani wakati kesi hiyo ikifanyika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, alikanusha kuzungumza na Lulu, kwani hata siku ya hukumu hakuwepo kortini. “Siyo kweli, mimi sijazungumza na Lulu tangu siku ile ya hukumu, kwanza sikuwepo mahakamani na hadi leo ninapoongea na wewe sijaenda kumtembelea gerezani, kwa hiyo hayo maneno siyo yangu,” alisema mui

IRENE UWOYA ROHO MKONONI RWANDA! ANASWA NA MABAUNSA

Image
Muigizaji Irene Uwoya Siku chache baada ya Hamad Ndikumana ‘Katauti’ kufariki dunia, imedaiwa kuwa, usalama wa mzazi mwenziye marehemu, muigizaji Irene Uwoya ambaye jana alikwea ‘pipa’ kwenda kuhani msiba nchini Rwanda ni mdogo. Uwoya ambaye alifunga ndoa na marehemu na kuishi naye kwa miaka kadhaa kabla ya kutengana, alianza kufanya mipango ya safari Jumatano iliyopita, saa chache mara baada ya kupokea taarifa za kifo hicho kilichotokea Jumanne usiku. CHANZO CHAFUNGUKA Kwa mujibu wa chanzo makini kutoka Rwanda, kuna kikundi cha watu ambacho kimekuwa na hasira na mrembo huyo kwa kile wanachofikiri kuwa kifo cha Ndikumana kimetokana na ‘stress’ zilizosababishwa na mrembo huyo. “Kwa kweli huku usalama wa Uwoya ni mdogo sana maana kama unavyojua kuna mashabiki ambao walikuwa wanamkubali Ndikumana ambaye alikuwa na mchango mkubwa sana katika soka la Rwanda,” kilidai chanzo hicho. WANAAMINI UWOYA NDIYO KIKWAZO Chanzo hicho kilizidi kumwaga data kuwa, wan

Sababu za Mbowe kutomuheshimu Lipumba hizi hapa

Image
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Freeman Mbowe amedai kwamba Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF anayetambuliwa na msajili wa vyama Prof. Ibrahim Lipumba kuwa ni Profesa wa ajabu ambaye anaweza kubomoa chama alichokijenga. Akiwa kwenye kampeni za uchaguzi mdogo Mtwara, Mh. Mbowe amesema kwamba hana ugomvi wowote na Prof Lipumba ingawa amekiri atakuwa muongo akisema kwamba anamuheshimu kwani anatumika katika kukivuruga chama alichokuwa akikiongoza kwa muda mrefu. Mh. Mbowe amesema kwamba wakati CUF ikishirikiana na UKAWA kwa ujumla kutafuta kura na kuongeza wabunge wa chama hicho bungeni, yeye Prof Lipumba alikuwa mafichoni na anamshanga sasa hivi anavyorudi ndani ya chama hicho na kutaka kukisambaratisha. "Sina ugomvi na Prof Lipumba lakini nikisema namuheshimu nitakuwa muongo sana. Prof Lipumba ni msomi sana tena msimchezee kwenye elimu lakini usomi ni jinsi unavyotumia elimu yako lakini siyo wingi wa vyeti. Ni Profesa wa aja

Baada ya hukumu Lulu, Mama Kanumba afunguka

Image
Mama wa Muigizaji Marehemu Steven Kanumba, Flora Mtegoa amefunguka na kusema kwamba leo atakwenda makaburi ya kinondonni alipoziikwa mwanaye ili kwenda kumzika upya. Mama Kanumba ametoa kauli hiyo muda mfupi baada ya Mahakama Kuu kumhukumu kifungo cha miaka miwili Muigizaji Elizabeth Michael ambaye alikuwa mtuhumiwa katika kesi ya mauaji bila kukusudia yaliyopelekea kifo cha muigizaji huyo. "Kwa sasa sina la kusema ila  naishukuru sana Mahakama kwa kutenda haki, pia niishukuru sana Serikali yangu lakini pia nikitoka hapa nitakwenda makaburini kwa ajili ya kumzika upya mwanangu Kanumba". Mama Kanumba. Kwa upande wa Wakili wa Muigizaji Lulu Peter Kibatala ameweka wazi kwamba watakata rufaa kufuatia hukumu ya Mahakama iliyotolewa leo kwa mteja wake. Muigizaji Lulu leo amehukumiwa kifungo cha miaka miwili jela baada ya kukutwa na hatia ya kumuua muigizaji mwenzake ambaye pia alikuwa mpenzi wake Steven Kanumba usiku wa Aprili 7 2012.

Zitto aizungumzia Bombadier Bungeni

Image
Serikali imekiri kujitoa kwenye Mpango wa Kimataifa wa uendeshaji wa shughuli za serikali kwa uwazi (OGP), ambao serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilijiunga Septemba 21 mwaka 2011. Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Mh. George Mkuchika wakati akijibu swali la Mbunge wa Kigoma Mjini Mh. Zitto Kabwe lililohoji kwanini serikali imejitoa kwenye Mpango wa Kimataifa wa uendeshaji serikali kwa uwazi (OGP). Mh. Mkuchika amesema baada ya serikali kushiriki kwenye utekelezaji wa mpango huo kwa muda wa miaka minne imeamua kujitoa, ambapo ameongeza kuwa sio nchi ya kwanza kujitoa kwenye mpango huo. “Baada ya serikali kushiriki utekelezaji wa mpango huo kwa muda wa miaka minne imeamua kujitoa, na Tanzania sio nchi pekee iliyojitoa, zipo nchi kama Hungury na Urusi zilijiunga na baadae kujitoa”, amesema Waziri Mkuchika. Kwa upande mwingine Mh. Zitto ameshauri kuwa serikali ingeendelea kuwa mwanachama wa (OGP) ingefaidi

Breaking News: Lulu ahukumiwa kwenda jela

Image
Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imemhukumu kwenda jela miaka miwili muigizaji wa filamu bongo Elizabeth Michael (Lulu) ambaye alikuwa anakabiliwa na kesi ya kuua bila kukusudia. Hukumu hiyo imetolewa leo na Jaji Sam Rumanyika aliyekuwa anaendesha kesi hiyo, na kusema kwamba mshtakiwa amekutwa na hatia ya kuua bila kukusudia kutokana na ushahidi wa mazingira, hivyo atatumikia kifungo cha miaka miwili jela. "Ushahidi wa mazingira unaweza kutumika kama msingi pekee wa kumtia hatiani mshtakiwa tena mshtakiwa pekee, sasa ninapokwenda kuangalia maelezo ya mshtakiwa kama yanakidhi vigezo nilivyosema awali, kwa mujibu wa mshtakiwa alisema alianza kupigwa na marehemu, marehemu alilewa lakini mshtakiwa alitakiwa kutoa maelezo yanayo jitosheleza, kwa hili mshtakiwa alijikanganya", amesema Jaji Rumanyika. Jaji Rumanyika ameendelea kwa kusema kwamba.."mshtakiwa katika maelezo yake hakueleza kuwa marehemu alianguka au laah wakati anamkimbiza, mae

Orodha kamili ya washindi wa tuzo za AFRIMA 2017

Image
Zoezi la ugawaji wa tuzo za muziki za AFRIMA (All Africa Music Awards) kwa mwaka 2017 limehitimishwa jana nchini Nigeria katika Hoteli ya Eko.Mastaa kadhaa wameweza kujishindia tuzo hiyo kubwa ya muziki kama vile Wizkid, Simi, M.I, Tiwa Savage, Ycee, Orezi, 2Baba, Alikiba na wengineo. Kwa upande wa Wizkid aliondoka tatu ambazo ni Song of the Year, Artist of the Year & Best West African Act (Male), na kwa msanii Alikiba aliondoka na tuzo mbili Best Africa Collaboration na Best Artist or Group in Africa RnB and Soul. Orodha kamili ya washindi; Best Central African Act (Male) – Locko Best Central African Act (Female) – Montess Best East African Act (Male) – Eddy Kenzo Best East African Act (Female) – Nandy Best Southern Africa Act (Male) – Emtee Best West African Act (Male) – Wizkid Best West African Act (Female) – Tiwa Savage Best African Collaboration – Alikiba feat M.I – “AJE“ Best Artist in African Rock – Gilad Millo (Kenya) Best Artist or Grou

Zitto Kabwe aomba msaada serikalini

Image
Mbunge wa Kigoma Mjini kupitia ACT Wazalendo, Zitto Zuberi Kabwe, ameonyeshwa kushangazwa na kitendo cha serikali kutangaza mradi mkubwa wa ujenzi wa reli ya Standard Gauge huku vifaa vingi vikiagizwa kutoka nje ya nchi na kuomba msaada wa ufafanuzi. Kwenye ukurasa wake wa facebook Zitto Kabwe ameandika waraka akitaka maelezo kutoka serikalini, ni kwa namna gani serikali inaendesha mradi mkubwa kama huo bila kuweka vifungu vya kufungamanisha na sekta nyengine nchini, na kudhamiria kuagiza chuma nje wakati nchi ina chuma ambacho bado hakijaanzwa kuchimbwa. Usome ujumbe wote hapa chini.

BASATA yaongea kuhusu Msondo Ngoma kumdai Diamond Milioni 300

Image
Baada ya Band ya Msondo Ngoma kutaka ilipwe shilingi milioni 300 na kundi la WCB kwa kutumia bila ruhusa vionjo vya wimbo wake kwenye wimbo wa “Zilipendwa”  Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) Godfrey Mngereza ameongea yafuatayo. “Unaweza kuitazama katika mitizamo mbalimbali lakini unapoangalia kwamba wanaanza kushtakiana kimsingi ni taratibu ambayo inagusa sana mambo ya haki miliki, kabla ya kuitumia kazi ya mtu ni vizuri ukamuona mwenye kazi mkubaliane” “Ukitumia kazi ya mtu bila utaratibu hiyo moja kwa moja ni kosa, cha msingi hata kabla ya kumuweka Mwanasheria ili kudai haki yako ni vizuri ukawafata au ukawasiliana na alietumia kazi yako bila ruhusa…. katika hili linalojitokeza sasa hivi ni swala la kuamshana kwamba kazi ya sanaa ya mtu flani haina tofauti na mali ya mtu ya aina nyingine, huwezi kutumia gari la mtu bila ridhaa yake” – Mngereza

Ajali yaua na kujeruhi Moshi

Image
Watu kadhaa wanasadikika kufariki na wengine kujeruhiwa kwenye ajali ya gari iliyotokea mchana huu mkoani Kilimanjaro ikihusisha roli na gari ndogo aina ya Noah ya abiria ya Sanya Juu - Moshi Ajali hiyo mbaya imetokea mchana  huu maeneo ya Kikavu  karibu na Kwasadala Mkoani Kilimanjaro ambapo Roli kubwa lilikuwa linajaribu kulipita gari lingine  ndipo likakutana uso kwa uso  na Gari ndogo aina ya Noah iliyokuwa imebeba abiria likitokea Moshi mjini kwenda  Sanya Juu. Taarifa kamili za ajali hiyo bado hazijatolewa lakini mashuhuda wa tukio wanasema huenda baadhi ya abiria waliokuwa kwenye Noah wamejeruhiwa. Aidha mashuhuda hao wameeleza kuwa watu wanne ndio wanaonekana kuwa bado ni majeruhi lakini hali zao ni mbaya na taratibu za kuwafikisha hospitali kwaajili ya matibabu zinaendelea. Hata hivyo bado majina ya abiria waliokuwemo kwenye Noah hayajapatikana mara moja tunaendelea kufuatilia taarifa kamili kutoka kwa kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro na tut

AJALI; Wawili wafariki katika ajali wilayani Ikungi

Image
Watu wawili wamekufa papo hapo na wengine wawili wamelazwa katika hospitali ya wilaya ya Ikungi,kufuatia gari aina ya Toyota Landcruiser kugongana uso kwa uso na basi la Taqwa.                                                                                            Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo Kaimu Kamanda wa polisi mkoa wa Sigida SSP Isaya Mbughi amesema,ajali imetokea katika kijiji cha Kideka wilayani Ikungi  majira ya saa tano asubuhi na imehusisha basi la Taqwa lenye usajili wa nambat 159 CWH lilokuwa likitokea Kampala  nchini Uganda na kuelekea jiji Dar-es-Salaam ,kugongana uso kwa uso na gari ndogo aina ya Toyota Landcruiser yenye usajili wa namba T 862 DJN ilyokuwa ikitokea Dodoma,na kusema chanzo cha ajali ni uzembe wa gari dogo kuliafuta basi. Mganga wa zamu wa hospitali ya mkoa wa Singida daktari Ramadhani Irunde amethibitisha kupokea maiti mbili zilizotambulika kwa majina ya Inocent Ngonyani na Gabriel William  ambao wamepata majeraha k

Wema Sepetu apata pigo hili

Image
  Serikali kupitia mamlaka zake imezifungia rangi za midomo zinazozalishwa na Mwanadada aliyewahi kuwa Miss Tanzania na Muigizaji wa Filamu, Wema Sepetu. Rangi hizo zinajulikana kwa jina la "Kiss". Kwa mujibu wa taarifa ya Mamlaka ya Chakula na Dawa(TFDA) pamoja na Shirika la Viwango Nchini(TBS) wamebaini kuwa rangi hizo hazina ubora kwa matumizi ya binadamu. Kwa upande wa Meneja wa Wema Sepetu, Happy Shame alipotakiwa kuzungumzia suala hilo amefunguka na kusema kwamba taarifa za kufungiwa kwa bidhaa hizo yeye kama Meneja hajazipata bali anachofahamu mzigo ulikuwa haujaingia sokoni na kwamba muigizajin huyo alikuwa bado akifuatilia vibali kutoka mamlaka husika. Rangi hizo za mdomo za muigizaji Wema Sepetu zilizinduliwa kwa mara ya kwanza mwaka 2015 usiku wa birthday yake.