Posts

Showing posts from October, 2017

KAULI YA LOWASSA BAADA YA LAZARO NYALANDU KUIHAMA CCM

Image
ALIYEKUWA Mgombea Urais wa Tanzania na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Edward Lowassa amemkaribisha aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu, ambaye amejivua uanachama na kuachia nyadhifa zote alizokuwa nazo ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM). Akionyesha kuwa na furaha alipozungumza na Mwananchi leo Jumatatu, Lowassa hakuwa na maneno mengi, akiyafupisha kwa kusema “tumelamba dume”. Nyalandu (47), ambaye pia alikuwa mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, alitumia nafasi hiyo kuomba kujiunga na Chadema, akisema anaiomba imfungulie mlango. Dakika chache tangu Nyalandu aombe kujiunga na Chadema, Lowassa alimkaribisha waziri huyo wa zamani wa Maliasili na Utalii huku akisema mwanasiasa huyo amechelewa kujiunga na upinzani. “Mbona amechelewa? Alitakiwa awe amejiunga muda mrefu, tena hasa wakati wa Uchaguzi Mkuu. Ninamkaribisha sana kwa sababu ni mwanasiasa mzuri na anayejua majukumu yake,” alisema Lowassa ambaye alikuwa waziri mkuu wa kwanza katika Se

Meya wa Jiji la Mwanza Akamatwa na Polisi

Image
James Bwire (kulia). TAARIFA zilizotufikia kwenye dawati letu la habari zinaeleza kuwa, Meya wa Jiji la Mwanza, James Bwire anashikiliwa na Polisi huku ikidaiwa kuwa amri ya kukamatwa kwake ni agizo la mkuu wa mkoa huo, John Mongella. Hayo yamesemwa na Mariam Lima ambaye ni katibu wa mitandao ya taasisi ya Alliance inayomilikiwa na Meya Bwire ambaye ameeleza kuwa kuwekwa kwake sentro ni kunatokana na agizo la mkuu wa mkoa. Hata hivyo, Mongella amekana kuamuru kukamatwa kwa kiongozi huyo anayeshikiliwa katika Kituo Kikuu cha Polisi cha Jiji la Mwanza. “Nimepata taarifa za meya kuwekwa mahabusu; mimi sihusiki na ninazifuatilia kujua kinachoendelea,” amesema Mongella leo Jumatatu Oktoba 30,2017. Taarifa zinasema meya Bwire amekamatwa katika Uwanja wa Ndege Mwanza wakati wa mapokezi ya Rais John Magufuli ambaye ziko ziarani mkoani humo. Lima amesema, “Tunafanya jitihada za kumwekea dhamana ingawa tunakabiliana na changamoto nyingi.” Tangu Aprili, Bwire na Mkur

ZITTO KABWE AMPA NENO NYALANDU BAADA YA KUIHAMA CCM

Image
MBUNGE wa Kigoma Mjini kwa tiketi ya ACT Wazalendo Zitto Kabwe amefunguka na kumpongeza aliyekuwa Mbunge wa Singida Kaskazini Nyalandu ambaye leo Oktoba 30, 2017 amefanya maamuzi ya kuachana na CCM na kusema kiongozi huyo amefanya maamuzi sahihi. Zitto Kabwe amesema kuwa kutokana na uchumi unavyoporomoka haki za watu zinavyovunjwa jambo alilofanya Nyalandu ni sawa na kuwa huko ndiyo kuonyesha uongozi. “Lazaro Nyalandu, umeonyesha Uongozi. Kwa namna haki za watu zinavyovunjwa na Uchumi wa nchi unavyoporomoka, unahitaji roho ngumu Sana kuwa CCM. Umefanya maamuzi sahihi, wakati sahihi na Kwa sababu sahihi. Kila la kheri|” aliandika Zitto Kabwe Lazaro Nyalandu leo ametangaza kujivua nafasi zake ndani ya Chama Cha Mapinduzi na kuandika barua yake ya kujiuzulu nafasi yake ya Ubunge kwa kile alichodai kuwa Chama Cha Mapinduzi na Bunge vimekuwa vikishindwa kuisimamia serikali na badala yake kutumiwa na serikali jambo ambalo yeye anaona halina afya katika maendeleo ya nch

Breaking News: Nyalandu Ajiuzulu Ubunge, Ajivua Uanachama CCM, Kuhamia Chadema

Image
Lazaro Nyalandu, aliyekuwa Mbunge wa Singida Kaskazini kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) amejiuzulu uanachama na vyeo vyote alivyokuwa navyo ndani ya chama hicho, pamoja na kuachia nafasi ya ubunge, kwa kile alichoeleza kwamba ni kutoridhishwa na mwenendo wa kisiasa ndani ya chama hicho.Akizungumza na waandishi wa habari leo, Nyalandu amesema ameamua kuachia nyadhifa zote ndani ya chama hicho, kuanzia leo, Oktoba 30, 2017 na kama itawapendeza viongozi wa Chadema, anaomba kujiunga na chama hicho. Hiki ndicho alichokiandika Nyalandu: NIMEAMUA kujiuzulu NAFASI yangu ya Ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi CCM, pamoja na nafasi zote za Uongozi ndani ya Chama kuanzia leo, Oktoba 30, 2017. HALIKADHALIKA, asubuhi ya leo nimemwandikia Spika wa Bunge, Mh. Job Ndugai, Mb., barua ya kujiuzulu nafasi yangu ya UBUNGE wa Jimbo la Singida Kaskazini kupitia tiketi ya CCM, nafasi ambayo nimeitumikia kwa vipindi vinne mfululizo tangu nilipochaguliwa kwa mara

RAIS DKT. MAGUFULI AFUNGUA DARAJA LA WAENDA KWA MIGUU LA FURAHISHA JIJINI MWANZA

Image
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella pamoja na viongozi mbalimbali akikata utepe kuashiria ufunguzi wa Daraja la Waenda kwa miguu la Furahisha liliopo jijini Mwanza. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaMhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa pamoja na viongozi mbalimbali akivuta utepe kwenye jiwe la ufunguzi kuashiria ufunguzi wa wa Daraja la Waenda kwa miguu la Furahisha liliopo jijini Mwanza. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaMhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa mara baada ya kufungua daraja la Waenda kwa miguu la Furahisha jijini Mwanza. Sehemu ya wananchi waliohudhuria ufunguzi wa daraja la Waenda kwa miguu la Furahisha jijini Mwanza.     Rais wa Jamhuri ya Muungano wa

Hatimaye Mmoja wa Watoto Pacha Waliotenganishwa India Afungua Macho

Image
Mmoja wa watoto pacha ambao walizaliwa wakiwa wameshikana kwenye vichwa amefungua macho yake siku nne baada ya upasuaji wa kuwatenganisha nchini India. Jaga, mwenye umri wa miaka miwili aliweza kuitikia ishara ndogo kama kusongesha mikono yake. Watoto hao walizaliwa wakiwa wanatumia kwa pamoja mishiba na nyama za ubongo na upasuaji uliochukua saa 16 uliwatenganisha. Watoto hao wote wako hali nzuri na madaktari wameridhishwa na vile wanavyoendelea hadi sasa, Pacha hao wanaotokea kijiji kilicho mashariki mwa jimbo la Orissa nchin India, walishikana kwenye kichwa hali inayofahamika kama craniopagus. Craniopagus hukumba mtoto mmoja kati ya watoto milioni 3 wanaozaliwa na asilimia 50 ya wale wanaopatwa na hali hiyo hufariki saa 24 baada ya kuzaliwa.

Gharama za kumtunza Faru Fausta kupunguzwa

Image
Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), imeanza kulima majani aina ya lusini ambayo ni chakula cha Faru Fausta ili kupunguza gharama za kumtunza mnyama huyo. Faru Fausta mwenye miaka 54 anahifadhiwa kwenye banda ndani ya Hifadhi ya Ngorongoro ikiwa ni hatua ya kumlinda asiliwe na wanyama wengine kutokana na jicho lake kutoona. Amekuwa akitumia bandali 250 za majani kila baada ya miezi minne yanayoigharimu mamlaka hiyo Sh5 milioni. Majani hayo hununuliwa kutoka nchi jirani ya  Kenya. Akizungumza na waandishi wa habari, Meneja Idara ya Malisho na Usimamizi wa Wanyama NCAA, Hillary Mushi amesema mamlaka imeandaa shamba lenye ukubwa wa eka mbili na imepanda mbege za lusini. Amesema ndani ya miezi saba majani hayo yataanza kuvunwa. Mushi amesema NCAA imechukua hatua hiyo ili kupunguza gharama za kumtunza faru huyo, ambaye amekuwa moja ya kivutio cha watalii na watafiti kutokana na kuwa ndiye faru mwenye umri mkubwa kuliko wote duniani kati ya wanaoi

Tumia kitunguu swaumu ili kuzua kuwahi kufika kileleni mapema

Image
Hivi karibuni kumekuwapo na tatizo la wanaume wengi kuwahi kufika kileleni, huku kitendo hicho kikichangawa na sababu mbalimbali ikiwamo mawazo na sababu nyinginezo. Ikiwa wewe unatatizo la kuwahi kufika kileleni basi inasadikika ya kwamba kitunguu swaumu ni tiba tosha. Sifa kuu zinazokifanya kitunguu swaumu kuwa na uwezo na faida nyingi mwilini ni kule kuwa kwake na viasili kadhaa (ingredients) ambavyo vinafanya kazi tofauti tofauti. Uwezo wake wa kiutendaji unatokana na sifa zifuatazo: Vina uwezo wa kusababisha kutanuka kwa mishipa ya damu (vasodilation) kwa kubadilisha polysulfides zilizopo ndani yake kuwa hydrogen sulfides kwenye seli nyekundu za damu. Husaidia uthibiti wa kiwango cha sukari mwilini kwa kushusha kiwango cha kemikali ya homocystine na hivyo kupunguza madhara ya kisukari. Ukivikata vipande vidogo vidogo hivi (chop), vitunguu swaumu hutoa kemikali iitwayo kwa kitaalamu kama ‘Allicin’ ambayo ni dawa dhidi ya bakteria, na ‘Phytoncide’ ambayo

Heri ya Kuzaliwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Image
Rais John Pombe Magufuli. Siku kama ya leo, Oktoba 29, 1959, Rais John Pombe Magufuli alizaliwa. Kampuni ya Global Publishers, uongozi na wafanyakazi wote, wanakutakia heri ya siku ya kuzaliwa. Tunakuombea Mungu akulinde, akupe afya njema na kuendelea kuwatumikia Watanzania katika kipindi cha uongozi wako.

Dogo Janja Afunga Ndoa na Irene Uwoya?

Image
Msanii wa Filamu, Irene Uwoya. HABARI zilizoenea katika mitandao ya kijamii ni kwamba msanii wa muziki wa Hip Hop nchini, Dogo Janja, amefunga ndoa kimyakimya na mnyange wa filamu, Irene Uwoya. Baada kuenea kwa uvumi huo, mtandao wa Global Publishers ulifuatilia kujua ukweli juu ya ndoa hiyo iliyowashitua wengi. Hatua ya kwanza jana ni pale mwandishi wa mtandao alipowaendea wahariri wa Magazeti Pendwa ya Global Publishers yanayohusiana na habari za wasanii wa Bongo Muvi, Bongo Fleva na wengineo ambapo walijibu kwamba walikuwa wamemtafuta msanii Hamad Aly ‘Madee’ aliyewajibu kwamba alikuwa hajui chochote kuhusu suala hilo. Msanii wa muziki wa Hip Hop nchini, Dogo Janja. Mambo hayakuishia hapo kwani wahariri haohao walipowasiliana na Dogo Janja alijibu kwamba na yeye hakujua kinachoendelea. Mwishoni wahariri wakamalizia kwa kuongea kwenye simu na Irene Uwoya ambapo alipopokea aliulizwa kuhusu suala hilo la kufunga ndoa na Dogo Janja.  Jibu la kwanza la mrembo hu

Nafasi za Kazi Kutoka Wizara Ya Fedha

Image
VACANCIES ANNOUNCEMENT President’s Office, Public Service Recruitment Secretariat on behalf of the Ministry of Finance and Planning, invites qualified Tanzanians to fill twelve (12) vacant posts as mentioned below; 1.0 BACKGROUND 1.1 MINISTRY OF FINANCE AND PLANNING The Ministry of Finance and Economic Affairs manages the overall revenue, expenditure and financing of the Government of the United Republic of Tanzania and provides the Government with advice on the broad financial and economic affairs of Tanzania in support of the Government’s economic and social objectives. GENERAL CONDITIONS i.        All applicants must be Citizens of Tanzania of not more than 45 years of age; ii.        Applicants must attach an up-to-date Curriculum Vitae (CV) having reliable contacts; postal address/post code, e-mail and telephone numbers; iii.        Applicants should apply on the strength of the information given in this advertisement; iv.        Applicants must

MATUKIO YA SHEREHE HARUSI YA JOTI YAZIDI KUFANA USIKU HUU UKUMBI WAMLIMANI CITY,THE COMEDY WOTE NDAN.

Image

Mbunge:Bobi Wine Amekataa Fedha Milioni 29 Alizohongwa

Image
Mwanamuziki Uganda, ambaye ni Mbunge Kyadondo East , Bobi Wine amekataa fedha milioni 29 za Uganda alizohongwa na serikali ili aweze kukubaliana na mapendekezo ya kufanyia marekebisho kipengele cha katiba na kuondoa ukomo wa miaka 75 kuongoza nchi. Bobi Wine ameiamuru benki ambayo amewekewa fedha hizo kuzirudisha kwa watu ambao wameziweka na kusema kutokana na taarifa ya mawasiliano wabunge wote wa Uganda 449 wamepewa fedha hizo ili waweze kukubaliana na hoja hiyo na kuoandoa ukomo wa miaka 75 ili kuweza kumpa nafasi tena Yoweri Kaguta Museveni (73) kugombea nafasi ya Urais tena kwa awamu ya sita 2021. “Oktoba 24, 2017 Milioni 29 wa Uganda ziliwekwa kwenye Account yangu ya benki, pesa hizo walipewa wabunge wote wa Uganda kwa mujibu wa taarifa rasmi pesa hizo walizopewa wabunge ni ili kukubaliana na pendekezo la kufanyia marekebisho kipengele cha 102 (b) cha Katiba ya Uganda na kuondoa ukomo wa miaka 75 kama sifa ya kusimama kama Rais wa Uganda” alisema Bobi W

ZARI THE BOSS LADY NA HAMISA MOBETTO MAPYA TENA,WAONYWA VIKALI,WAWEKWA KITI MOTO

Image
Warembo waliokuwa kwenye vita ya maneno, Hamisa Mobeto na Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ wamedaiwa kuwekwa kitimoto ili waache kurushiana maneno kwenye mitandao ya kijamii. Risasi Jumamosi limeelezwa kuwa, kwa nyakati tofauti wawili hao waliwekwa kitimoto na ndugu wa msanii wa Mzazi Mwenzao na kutakiwa waache malumbano hayo mitandaoni kwani hayaleti picha nzuri kwao na ukizingatia kosa limeshafanyika na msanii kukiri hadharani. “Walichoelezwa tu ni kwamba, waache kutupiana vijembe mitandaoni maana wao sasa hata kama hawatakuwa wake wenza lakini tayari msanii ana damu yake kwa Mobeto. Amekiri kwamba aliteleza na kujikuta ameingia kwenye uhusiano naye hadi kufikia hatua ya kupata mtoto. Zarinah Hassan. “Mtoto ameshazaliwa na ni damu ya msanii na mwisho wa siku msanii atalazimika kumpa mahitaji yake kama mwanaye hata kama yeye hataendeleza uhusiano na mama wa mtoto. Zari ni mama wa watoto wake wawili, wamedumu muda mrefu hivyo yeye ataendelea tu kushikilia usuk