Posts

Showing posts from May, 2017

DAKTARI AELEZA SUMU ILIYOMUUA MUME WA ZAMANI WA ZARI,AFICHUA SIRI NZITO

Image
Stori: Waandishi Wetu  KAMPALA: Imefichuka! Nyuma ya msiba ulioacha historia wa aliyekuwa mzazi mwenza wa staa wa Afrika Mashariki, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’, Ivan Ssemwanga ‘The Don’ aliyepatwa na umauti wiki iliyopita akiwa amelazwa kwenye Hospitali ya Steve Biko, Pretoria nchini Afrika Kusini, kuna mengi yanayosemwa, Wikienda liko bega kwa bega na kinachojiri. Miongoni mwa yanayosemwa ni madai ya jamaa huyo kupewa sumu iliyomdhuru moyo hivyo kusababisha kifo chake. MADAI YA SUMU Chanzo cha ndani ya familia ya Ivan kililieleza gazeti moja maarufu nchini Uganda kuwa, Ivan alilishwa sumu na watu ambao hawakuwataja na kwamba mara ya mwisho alikuwa akipata chakula na ndugu zake kabla ya hali yake kuanza kuwa mbaya kisha siku chache baadaye alikimbizwa katika Hospitali ya Steve Biko.Gazeti hilo lilimkariri mtu huyo akieleza kuwa, Ivan hakufa kwa shambulio la moyo wala moyo kushindwa kufanya kazi bali aliwekewa sumu kali kwenye chakula. MAUMIVU MAKALI

Maisha Ya Mke wa Deo Filikunjombe Baada ya Miaka Miwili ya Kifo Cha Mumewe

Image
Mkewe  wa Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Ludewa mkoani Njombe, marehemu Deo Haule Filikunjombe, Sarah Filikunjombe. STORI: BRIGHTON MASALU NA ANDREW CARLOS, IJUMAA, HABARI MAMA shujaa! Ikiwa imebaki miezi minne na siku kadhaa itimie miaka miwili kutokea kwa kifo cha aliyekuwa kada muaminifu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Mbunge wa Jimbo la Ludewa mkoani Njombe, marehemu Deo Haule Filikunjombe, mkewe Sarah Filikunjombe (Pichani) amethibitisha ushujaa kwa kuendelea kupambana na changamoto za kimaisha na kufikia vilele mbalimbali vya mafanikio, Ijumaa limemfungia kazi. Mwishoni mwa wiki iliyopita na mwanzoni mwa wiki hii, kwa siku tatu tofauti, waandishi wetu walijipa kazi ya ziada ya kumtafuta Sarah ili kujua nini kimeendelea katika maisha yake baada ya kuondoka kwa mumewe ambapo walibaini mambo mengi mazuri yenye kutia moyo, ambayo mama huyu licha ya kuonekana sistaduu, ameyafanya kwa ujasiri wa kipekee. IJUMAA NYUMBANI KWAKE Hatimaye Jumanne mchana, gazeti hili l

Undani wa Kifo Cha Mume wa Zari Nyuma ya Pazia

Image
Staa wa Uganda na Afrika Mashariki, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’, akiwa na aliyekuwa mume wake Tycoon Ivan Semwanga ‘The Don’ enzi za uhai wake.  STORI: SIFAEL PAUL, RISASI JUMAMOSI, MTANDAO KAMPALA: Kifo cha aliyekuwa mume wa staa wa Uganda na Afrika Mashariki, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’, Tycoon Ivan Semwanga ‘The Don’, raia wa Uganda, mwenye maskani yake Johannesburg na Pretoria, Afrika Kusini, kimeibua simulizi nzito nyuma ya pazia. Kwa mujibu wa chanzo cha ndani ya familia ya Ivan iliyopo Muyenga jijini Kampala, kilichokaririwa na mitandao ya kuaminika nchini Uganda, katika siku za mwisho za maisha yake kabla ya kuripotiwa kupatwa na ugonjwa wa shambulio la moyo ambao kitaalam huitwa Coronary Artery Disease (CAD). Ilifahamika kuwa, ugonjwa huo ndiyo uliomsababishia kifo usiku wa kuamkia juzi. Tycoon Ivan Semwanga ‘The Don’ alipokuwa hospitali. MARA YA MWISHO KUONEKANA Habari zilieleza kuwa, Ivan alionekana kwa mara ya mwisho kwenye Pat