Posts

Showing posts from April, 2017

Rais Magufuli Apokewa kwa Mapokezi Makubwa Mkoani Kilimanjaro Leo

Image
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akiongea na wananchi wa Bomang'ombe Wilaya ya Hai waliomsimamisha wakati akitokea uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro alipowsili tayari kwa kuanza ziara ya kikazi ya siku tatu mkoani humo Kilimanjaro Jumamosi Aprili 29, 2017.   Sehemu ya maelfu ya Wananchi wakimshangilia Rais Magufuli wakati akiongea nao   Mbunge Mstaafu na Mwalimu maarufu nchini Mwalimu Kham akimtyambulisha Rais Magufuli kwa mamia ya wanafunzi waliojitokeza kumlaki   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akiongea na wananchi Karanga Wilaya ya Moshi mjini waliofunga barabara kumsimamisha wakati akitokea uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro alipowsili tayari kwa kuanza ziara ya kikazi ya siku tatu mkoani humo Kilimanjaro  Wananchi Karanga Wilaya ya Moshi mjini waliofunga barabara kumsimamisha Rais Magufuli wakimshangilia  wakati akitokea uwanja wa ndege wa Kimataifa wa

MATUKIO KATIKA PICHA: YALIYOJIRI KATIKA KIKAO CHA KUMI NA TATU MKUTANO WA SABA BUNGE LA 11 MJINI DODOMA LEO APRIL 27, 2017.

Image
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Tulia Ackson akiongoza kikao cha kumi na tatu cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 27, 2017. Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge Ajira Kazi na watu wenye Ulemavu Mhe. Anthony Mavunde akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kikao cha kumi na tatu cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 27, 2017. Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Hamadi Masauni akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika katika kikao cha kumi na tatu cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 27, 2017. Naibu Waziri wa Ujenzi ,Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Edwin Nyonyani akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika katika kikao cha kumi na tatu cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 27, 2017. Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mhe. Rita Kabati akiuliza swali katika kikao cha kumi na tatu cha Mkutano wa saba

Mwenyekiti Mstaafu wa CCM Atiwa Mbaroni

Image
Jeshi la Polisi mkoani Iringa linamshikilia mwenyekiti wa zamani wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Iringa, Jesca Msambatavangu, kwa tuhuma za kumshambulia mwanamke mmoja na kumsababishia maumivu makali mwilini. Msambatavangu, ambaye alikuwa miongoni mwa wanaCCM waliofukuzwa uanachama katika Mkutano Mkuu Maalum wa chama hicho uliofanyika mwezi Machi, alikamatwa  jana mchana Kamanda wa Polisi mkoani Iringa, Julius Mjengi, alisema kuwa kiongozi mstaafu anatuhumiwa kutenda kosa hilo wiki iliyopita. Akifafanua, Kamanda Mjengi alibainisha kuwa kiongozi huyo alitenda kosa hilo akiwa na wenzake ambao asingeweza kuweka majina yao hadharani kwani wanaendelea kuwatafuta. “Ni kweli tunamshikilia Jesca Msambatavangu, tumemkamata leo(jana)  saa nane mchana na tunaendelea na uchunguzi dhidi yake,” alisema Mjengi na kuongeza:   “Jesca pamoja na wenzake wanatuhumiwa kumshambulia mwanamke mmoja mkazi wa Kibwabwa, walimshambulia na kisha kumchoma sindano ambayo mwa

Lowassa kumuunga mkono Uhuru Kenyatta.

Image
SIASA za Ukanda wa Afrika Mashariki zimechukua sura mpya baada ya Waziri Mkuu Mstaafu na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Edward Lowassa kutangaza rasmi kumuunga mkono Rais Uhuru Kenyatta. Kenyatta aliyeunga ushirika pamoja na William Rutto,  anaingia katika kinyang’anyiro cha kuwania awamu ya pili ya kuiongoza Kenya huku upande wa upinzani ukiwa umepitisha jina la Raila Odinga kupeperusha bendera ya upinzani. Wakati Lowassa akitangaza kumuunga mkono Kenyatta, kwa upande wake Odinga tayari ilishajulikana wazi urafiki wake na Rais Dk. John Magufuli ambao umeanza miaka mingi tangu akiwa Waziri wa Ujenzi. Hatua hiyo ya Lowassa ambaye anatajwa kuwa mwanasiasa mwenye ushawishi nchini na Afrika Mashariki imekuja baada ya kutembelewa jana nyumbani kwake Monduli na wabunge zaidi ya 20 na maofisa kutoka Kaunti ya Kajiado nchini Kenya. "Mimi naamini Uhuru Kenyatta anao uwezo mkubwa wa kuwaunganisha vema wananchi wa Kenya n

HUYU NDIO MPENZI MPYA WA FLORA MBASHA ANAETARAJIA KUFUNGANAE NDOA

Image
Kama Basi ulisikia kuwa Flora Mbasha anaolewa tena baada ya kuachana na Emmanuel Mbasha basi inasemekana huyo hapo ndio shemeji yetu mpya wakiwa katika picha ya Pamoja,...

Kama Unaumwa Tumbo Wakati Wa Hedhi soma hapa

Image
KARIBU sana katika makala yetu inayohusu afya. Kutokana na simu nyingi ninazozipata nikiulizwa maswali juu ya maumivu yanayowapata akina mama wengi wakati wa hedhi nimeona ni bora niandike makala hii ili iweze kuwasaidia na wengine kujua nini chanzo na mhusika afanye nini pale anapopatwa na tatizo hilo. Maumivu wakati wa hedhi (period pains) au kitaalamu dismenorrhea, ni maumivu yanayojitokeza sehemu ya chini ya tumbo au kiunoni wakati mwanamke anapoanza kupata siku zake au kabla ya hapo. Maumivu hayo huweza kuwa madogo au ya wastani huku baadhi ya wanawake wakipata maumivu makali sana. Maumivu hayo huanza pale yai linapotoka katika mrija (fallopian tube) na kuteremka chini ya mrija huo wakati wa Ovulation. AINA YA MAUMIVU Maumivu ya tumbo la hedhi yapo ya aina mbili.  Ya kwanza  ni maumivu yasiyokuwa na sababu zozote za kimsingi za kitiba. Katika aina hii maumivu ni ya kawaida na huhisiwa sehemu ya chini ya tumbo na kiunoni. Maumivu hayo huanza siku moja au mbi

Mali za Lugumi Mikononi mwa TRA

Image
Kampuni  ya udalali ya Yono, imefanikiwa kukamata mali za wafanyabiashara wanaodaiwa kodi ya serikali inayofikia zaidi ya Sh bilioni 68.1. Operesheni ya kukamata mali hizo kwenye maeneo mbalimbali ndani na nje ya Jiji la Dar es Salaam imefanywa ndani ya wiki moja. Katika operesheni hizo maofisa wa Yono wamekuwa wakishirikiana na maofisa wa Mamlaka ya Mapato(TRA), ambayo ndiyo imeipa kampuni hiyo kazi ya kukusanya kodi kwenye maeneo mbalimbali nchini. Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Yono, Scholastica Kevela, Yono imepewa kazi na TRA kukusanya madeni yake ya kodi kwenye mikoa ya Dar es Salaam, Pwani Njombe, Mbeya, Iringa na Zanzibar. Aliwataka watanzania kuunga mkono jitihada za Rais John Magufuli za kuleta maendeleo kwa kulipa kodi bila shuruti ili zipatikane fedha za kujenga miundombinu kama barabara, reli, shule, madaraja, hospitali na zahanati. Kuhusu taarifa zilizozagaa kwenye mitandao ya kijamii kwamba hata baadhi ya mali za Kampu

RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AONGOZA WANANCHI KATIKA SHEREHE ZA MIAKA 53 YA MUUNGANO WA TANGANIKA NA ZANZIBAR YENYE KAULI MBIU “MIAKA 53YA MUUNGANO; TUULINDE NA KUUIMARISHA,TUPIGE VITA DAWA ZA KULEVYA NA KUFANYA KAZI KWA BIDII” APRIL 26,2017

Image
 Amir jeshi mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wananchi katika sherehe za miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizofanyika kitaifa katika uwanja wa Jamhuri Mkoani Dodoma April 26,2017   Amiri jeshi mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati akipokea heshima na wimbo wa taifa ukipigwa  Amiri jeshi mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati akilekea kukagua gwaride liloandaliwa na vyombo vya ulizi na usalamaliloandaliwa na vyombo vya ulinzi na usalama kwa ajili ya kusherehekea miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizofanyika kitaifa katika uwanja wa Jamhuri Mkoani Dodoma April 26,2017 Amiri jeshi mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikagua gwaride liloandaliwa na vyombo vya ulinzi na usalama kwa ajili ya kusherehekea miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizofanyika k

Rais atoa msamaha kwa wafungwa katika kuadhimisha miaka 53 ya Muungano wa Tanzania

Image
Katika kuadhimisha Miaka 53 ya Muungano wa Tanzania tarehe 26 Aprili, 2017 Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutumia madaraka aliyopewa chini ya Ibara ya 45(1)(d) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ametoa msamaha kwa wafungwa wafuatao:- Wafungwa wote ambao baada ya punguzo la kawaida la moja ya tatu (1/3) linalotolewa chini ya Kifungu 49(1) cha Sheria ya Magereza Sura ya 58, wawe wametumikia nusu (½) ya vifungo vyao vilivyobaki, isipokuwa wafungwa walioorodheshwa katika Ibara ya 2(i – xxi). Wafungwa wagonjwa wenye magonjwa kama UKIMWI, Kifua kikuu (TB) na Saratani (Cancer) ambao wako kwenye “terminal stage”. Wafungwa hawa wathibitishwe na Jopo la Waganga chini ya Uenyekiti wa Mganga Mkuu wa Mkoa/Mganga Mkuu wa Wilaya. Wafungwa wazee wenye umri wa miaka sabini (70) au zaidi. Umri huo uthibitishwe na Jopo la Waganga chini ya Uenyekiti wa Mganga Mkuu wa Mkoa/Mganga Mkuu wa Wilaya. Wafungwa wa kike walioingia na mi

Warembo Washikiana Visu Kisa Penzi la Chuz

Image
WAREMBO wawili wanaofanya tamthiliya ya Closet Chapter, waliofahamika kwa majina moja moja ya Shugga na Kanjo, hivi karibuni walishikiana visu katika ugomvi unaotajwa kuwa ni wa kumgombea bosi wao, Jumanne Kihangala ‘Mr Chuz’. Kwa mujibu wa chanzo chetu kilicho karibu na wasanii hao, sekeseke hilo lilitokea mwishoni mwa wiki, baada ya Shugga ambaye ni mchumba wa Chuz kumuonya Kanjo apunguze mazoea na mpenzi wake huyo. “Ishu hiyo ilitokea wakati wapo kambini Lushoto wakiwa wanashuti, ndipo Shugga akampiga mkwara Kanjo aache kumshobokea, mwenzake naye akaja juu wakaanza kudundana hadi kushikiana visu, wakidai bora wauane wakose wote, ” kilisema chanzo. Baada ya kupata habari hizo, Za Motomoto News ilimtafuta Mr Chuz  mbaye alikiri kutokea kwa ishu hiyo na kusema kinachomponza mchumba wake ni wivu wa kupindukia alionao.

Shuhudia LIVE Makomando Wakionesha matukio ya ujasiri Kwenye Sherehe za Miaka 53 ya Muungano

Image
Sherehe za maadhimisho ya miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zinafanyika leo April 26, 2017 mjini Dodoma ambapo mgeni rasmi ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli.Tanganyika na Zanzibar ziliungana April 26, 1964 chini ya hayati Baba wa Taifa, Mwalim Julius Nyerere na hayati Sheikh Abeid Karume. Kikosi cha makamandoo wakitoa saluti mbele ya Amri Jeshi mkuu katika sherehe za miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizofanyika kitaifa katika uwanja wa Jamhuri Mkoani Dodoma April 26,2017 Kikosi cha makomandoo wakionyesha umahili wa mazoezi  mbele ya Amri Jeshi mkuu katika sherehe za miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizofanyika kitaifa katika uwanja wa Jamhuri Mkoani Dodoma April 26,2017 Hapa ni kikundi cha Makomando wakionyesha uwezo, Bonyeza play hapa chini kutazama

Sakata la Bosi wa UN kufukuzwa latua bungeni

Image
Dodoma. Sakata la kufukuzwa nchini la bosi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Tanzania, Awa Dabo, limetua bungeni. Mbunge wa Mbozi, Pascal Haonga(Chadema) akizungumza bungeni leo,  aliitaka serikali kufafanua sababu za kumfukuza nchini Mkurugenzi Mkazi huyo wa UNDP Tanzania kwa kumpa saa 24. Hata hivyo, Mwenyekiti wa Bunge, Andrew Chenge aliliambia bunge kuwa serikali ina mamlaka yote katika masuala ya kidiplomasia na hivyo bunge haliwezi kuhoji  sababu za mkurugenzi huyo kufukuzwa.

MREMBO DAYNA NYANGE NA GONJWA LA KUWEWESEKA

Image
Staa wa Bongo Fleva, Mwanaisha Saidi ‘Dayna Nyange’. STAA wa Bongo Fleva, Mwanaisha Saidi ‘ Dayna Nyange ’ amefunguka kuwa siku za hivi karibuni amekumbwa na gonjwa la kuweweseka linalomkosesha raha. Akipiga stori na  Uwazi Showbiz , Dayna alieleza kuwa kuweweseka huko kunatokana na msongo wa mawazo alionao kwani anawaza kazi mpya atakayoitoa baada ya Wimbo wa Komelo kuendelea kufanya vizuri kwani muziki kwa sasa una ushindani mkubwa mno. “Kiukweli ninavyowaza kuhusu ujio mpya mpaka najikuta naweweseka usiku wakati nikiwa nimelala, nikishtuka natuliza mawazo na kujipa moyo kuwa Mungu atanisaidia nitaandaa kazi nzuri ambayo itafika mbali zaidi ya hii niliyotoa sasa,” alisema Dayna.