Posts

Showing posts from February, 2017

Waziri Nape: Sikupinga vita dhidi ya biashara ya dawa za kulevya bali nilishauri busara itumike

Image
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye ametoa ufafanuzi juu ya kauli iliyonukuliwa ikionyesha kuwa alipinga vita dhidi ya dawa za kulevya iliyoanzishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda. Amedai kuwa hakupinga vita hiyo bali alitaka busara itumike kwa washukiwa. Waziri Nape alitoa ufafanuzi huo katika kipindi cha dakika 45 cha ITV, alipoulizwa swali na mtangazaji wa kipindi hicho kutaka kujua kuhusu kauli yake iliyoonesha kupinga utaratibu uliotumika wa kuwakamata au kuwapata watuhumiwa wa dawa za kulevya. “Niseme kwanza ilitokea nilikuwa na mkutano na waandishi wa habari, ukienda leo ukanitaja Nape ukaniambia baada ya siku mbili njoo kituoni, hata kama nilikuwa na madawa ya kulevya nyumbani kwangu hivi unayakutaje?  'Kwasababu kwa vyovyote vile nitayachukua, ntayaficha, ntakuja kituoni ntaripoti utanibana ntakwambia twende nyumbani kwangu ukakague mnaenda mnakagua mnakuta hamna, si basi!  &q

MKUU WA JESHI LA ULINZI TANZANIA NA MNADHIMU MKUU WALA KIAPO CHA UADILIFU KWA VIONGOZI WA UMMA

Image
 Mkuu wa Jeshi la Ulinzi Tanzania (CDF), Jenerali Venance Salvatory Mabeyo akila Kiapo cha Uadilifu kwa Viongozi wa Umma leo Jijini Dar es Salaam. Kulia anayeshuhudia ni Kamishna wa Maadili wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Mstaafu Harold Nsekela leo Jijini Dar es Salaam.  Mkuu wa Jeshi la Ulinzi Tanzania (CDF), Jenerali Venance Salvatory Mabeyo akitia saini katika Hati ya Kiapo cha Uadilifu kwa Viongozi wa Umma leo Jijini Dar es Salaam. Kulia anayeshuhudia ni Kamishna wa Maadili wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Mstaafu Harold Nsekela leo Jijini Dar es Salaam.  Mkuu wa Jeshi la Ulinzi Tanzania (CDF), Jenerali Venance Salvatory Mabeyo akipokea Hati ya Kiapo cha Uadilifu kwa Viongozi wa Umma kutoka kwa Kamishna wa Maadili wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Mstaafu Harold Nsekela leo Jijini Dar es Salaam.  Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi Tanzania, Luteni Jenerali James Alois Mw

WAZIRI NAPE ATUMA SALAMU ZA POLE KWA SHIRIKISHO LA RIADHA NCHINI

Image

MSANII YUSUPH MLELA ATOA MANENO HAYA KWA WASANI WENZAKE

Image
Msanii mkongwe wa filamu Yusuph Mlela amewataka wasanii wenzake wa filamu kuacha kulalamika na kufanya kazi kwa bidii kwani hiyo ndiyo njia pekee ya kuikomboa tasnia ya filamu. Akiongea na Bongo5 wiki hii, Mlela amedai kuwa wasanii wengi wanatakatamaa kwa kauli ya soko limeyumba wakati wao ndiyo watu pekee ambao wanaweza kuikomboa tasnia ya filamu. “Suala la soko wadau wanasema limeyumba, lakini naweza kusema huu ni wakati wa kuamka na kuanza kufanya kazi upya kulikomboa soko la filamu, kama wanasema kazi ni mbaya tufanye kazi nzuri, kila kitu tunaweza kufanya. Mimi nadhani huu ni wakati wa wasanii wa filamu kuamka na kufanya kazi kwa bidii ili kuirudisha ile hali ya zamani,” alisema Mlela. Muigizaji huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri ndani ya tamthilia ya Kashfa inayorushwa na Azam TV, anajipanga kuachia filamu yake mpya ‘Mr Bodaboda’ Machi mwaka huu.

MREMBO BATULI AMLIPUA LAIVE WEMA SEPETU

Image
Muigizaji wa filamu nchini, Yobnesh Yussuf maarufu kama Batuli amekanusha taarifa iliyotolewa na Wema Sepetu kuwa CCM haijawalipa pesa za kampeni ya Mama Ongea na Mwanao kwenye uchaguzi wa mwaka 2015. Akizungumza na wanahabari kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Protea, Yobnesh Yusuph ‘Batuli’ akiwa na Ndumbangwe Misayo ‘Thea’,amesema madai aliyoyatoa Wema Sepetu hayana ukweli wowote kwa sababu wasanii wote walilipwa. “Nikiwa kama makamu mwenyekiti wa group hili la Mama Ongea na Mwanao kwa muda ni kweli inasemekana kwenye mitandao kuwa tulifanya kampeni na hatukulipwa, mimi kama mwenyekiti msaidizi wa muda nakanusha taarifa hizo kuwa si za kweli. Ingawa kwenye msafara wa mamba kenge hawakosekani,wapo wanaoshawishiwa kulichafua kundi letu, kumchafua Makamu wa Rais Bi Samia Suluhu na kuichafua CCM, mimi nakataa, sote tumelipwa na mikataba ipo, haiwezekani we staa mkubwa unakaa kwenye media unaongea uongo kwamba wasanii hatujalipwa.” Ameongeza, “Zipo simu za kutus

MBUNGE PAULINA GEKUL APATAA AJALI MBAYA ALAZWA ICU

Image
Mbunge wa jimbo la Babati mjini Paulina Gekul amenusurika kifo baada ya gari lake lenye namba za usajili T 189 BHQ kuacha njia na kupinduka vibaya ambapo mbunge huyo alikuwa katika msafara wa naibu waziri wa Mazingira Luhaga Mpina wilayani Babati mkoa wa Manyara. Baada ya ajali hii kutokea mmbunge Paulina Gekul ambaye ni mmbunge wa babati mjini akakimbizwa hospitali ya mkoa wa manyara na kulazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi I.C.U huku wanahabari wakikatazwa kuingia katika chumba hiki na madakatari ambao wanamuhudumia mbunge huyo Hata hivyo baada ya ajali kutokea naibu waziri wa mazingira amelazimika kuahirisha ziara yake ya kutembelea maeneo mbalimbali ndani ya mji wa babati huku mpina akiipongeza halmasahauri ya mji wa babati kwa kutambua umuhimu wa kutunza mazingira katika hali ya usafi baada ya kununua gari kwaajili ya kubebea taka lenye thamani ya zaidi ya milioni 200.

RAIS YOWERI MUSEVENI AMALIZA ZIARA YAKE YA SIKU MBILI NA KUREJEA NCHINI KWAKE

Image
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpokea Mgeni wake Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Terminal 1 kwa ajili ya kurejea nchini kwake Uganda mara baada ya kumaliza ziara yake ya siku mbili hapa nchini.   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na mgeni wake Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Terminal 1 kabla ya kuondoka    ma kurejea nchini kwake.   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsindikiza kuelekea kwenye ndege mgeni wake Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni mara baada ya kumaliza ziara yake ya siku mbili hapa nchini     Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni wakati nyimbo za Mataifa mawili zilipokuwa zikipigwa katika uwanja w

VIGOGO 4 WA SHIRIKA LA POSTA WATUMBULIWA

Image
BODI ya Wakurugenzi wa Shirika la Posta Tanzania, imetengua nafasi tatu za mameneja na ofisa mwandamizi kutokana na vitendo vya umangimeza, urasimu, kufanya kazi kwa mazoea, ubadhirifu na wizi. Mameneja waliotenguliwa ni James Sando ambaye alikuwa Meneja Mkuu, Menejimenti ya Rasilimali. Macrice Mbodo ameteuliwa kushika nafasi hiyo. Mwingine aliyetenguliwa ni Meneja Mkuu Uendeshaji wa Biashara Janeth Msofe. Aliyekuwa Meneja wa Mkoa Shinyanga, Hassan Mwang'ombe kateuliwa kushika nafasi hiyo. Bodi pia imewasimamisha kazi Meneja Msaidizi wa Barua na Logistic, Jasson Kalile na Ofisa Mwandamizi wa Usafirishaji, Ambrose John. Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya shirika hilo, Dk. Haruni Kondo, ameyasema hayo wakatia akizungumza na waandishi wa habari kuwajulisha uamuzi uliofanywa na bodi. Dk. Kondo amesema, imebainika na imewaridhisha kuwa baadhi ya watendaji wakuu wa makao makuu ya Posta wamekuwa kikwazo katika dhana ya uwajibikaji, weledi na kujituma katika

VIGOGO 4 WA SHIRIKA LA POSTA WATUMBULIWA

Image
BODI ya Wakurugenzi wa Shirika la Posta Tanzania, imetengua nafasi tatu za mameneja na ofisa mwandamizi kutokana na vitendo vya umangimeza, urasimu, kufanya kazi kwa mazoea, ubadhirifu na wizi. Mameneja waliotenguliwa ni James Sando ambaye alikuwa Meneja Mkuu, Menejimenti ya Rasilimali. Macrice Mbodo ameteuliwa kushika nafasi hiyo. Mwingine aliyetenguliwa ni Meneja Mkuu Uendeshaji wa Biashara Janeth Msofe. Aliyekuwa Meneja wa Mkoa Shinyanga, Hassan Mwang'ombe kateuliwa kushika nafasi hiyo. Bodi pia imewasimamisha kazi Meneja Msaidizi wa Barua na Logistic, Jasson Kalile na Ofisa Mwandamizi wa Usafirishaji, Ambrose John. Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya shirika hilo, Dk. Haruni Kondo, ameyasema hayo wakatia akizungumza na waandishi wa habari kuwajulisha uamuzi uliofanywa na bodi. Dk. Kondo amesema, imebainika na imewaridhisha kuwa baadhi ya watendaji wakuu wa makao makuu ya Posta wamekuwa kikwazo katika dhana ya uwajibikaji, weledi na kujituma katika

RAIS MUSEVENI ATEMBELEA VIWANDA VYA BAKHRESA LEO JIJINI DAR

Image
  Rais wa Uganda Mhe.Yoweri Museveni(wapili kushoto) akiulizia jambo wakati wa ziara yake katika viwanda vya Kuzalisha Juisi cha Azam kilichopo Vingunguti jijini Dar es Salaam leo. Kutoka kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Kundi la Makampuni ya Bakhresa Bw. Salim Aziz, Mkurugenzi wa Mahusiano wa Kundi la Makampuni ya Bakhresa Hussein Sufiani na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Dkt. Adelhelm Meru.   Afisa Mtendaji Mkuu wa Kundi la Makampuni ya Bakhresa    Bw. Salim Aziz akimkabidhi zawadi Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni baada ya kumaliza ziara katika viwanda vya Kuzalisha Unga wa Ngano Cha Bakhresa Food Products kilichopo Buguruni    na    Kiwanda cha Juisi cha Azam kilichopo Vingunguti Jijini Dar es Salaam leo.  Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni akifurahia zawadi aliyopewa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kundi la Makampuni ya Bakhresa Bw. Salim Aziz (wapili kulia) mara baada ya kumaliza ziara katika viwanda vya K