Posts

Showing posts from November, 2015

TAMKO LA RAIS MAGUFULI KUFUTA SAFARI ZA NJE,VIKWAZO VITANO VYA TAJWA

Image
Agizo la Rais John Magufuli la kusitisha safari za nje linakabiliwa na ugumu katika utekelezaji wake kutokana na nchi kuwa na balozi 36 tu ambazo zitatakiwa kufanya kazi maeneo mbalimbali duniani. Muda mfupi baada ya kuapishwa na kuanza utekelezaji wa majukumu yake ya mkuu wa nchi, Rais alifuta safari zote za nje kwa watumishi wa Serikali na viongozi ili kuokoa fedha zinazotumika kwa ajili hiyo na kuagiza shughuli hizo zifanywe na mabalozi. Rais alisema safari hizo zitadhibitiwa na Ikulu ambayo itatoa kibali kwa safari maalumu, ikiwa ni pamoja na kuweka masharti ambayo mtumishi anayetakiwa kusafiri atatakiwa kuyatimiza kabla ya kupewa kibali. Lakini utekelezaji wa agizo hilo unakabiliwa na vikwazo vingi, hasa vikubwa vitano ambavyo ni uchache wa balozi za Tanzania nje ya nchi, ukomo wa madaraka ya mabalozi, wigo wa ufahamu wa mambo ya kitaalamu na ukosekana kwa mazungumzo endelevu iwapo suala moja litawakilishwa na watu wawili tofauti kwenye mikutano miwili tofauti. Takwimu za Umo

WAZIRI MKUU ATAKA KILA MKURUGENZI ASOME HOTUBA YA RAIS, AIFANYIE KAZI

Image
 Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa akisalimiana na katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa  (TAMISEMI) , Jumanne Sajini baada ya kuwasili kwenye Ofisi ndogo ya TAMISEMI jijini Dar es salaam kuzungumza na watumishi Novemba 24, 2015.  Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa akisalimiana na baadhi ya Wakurugenzi baada ya kuwasili kwenye Ofisi ndogo ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) jijini Dar es salaam kuzungumza na wafanyakazi Novemba 24, 2015.  Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa  akizungumza na baadhi ya watumishi wa Ofisi ndogo ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) jijini Dar es salaam Novemba 24, 2015.   Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majliwa akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Ofisi ndogo ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) jijini Dar es slaam baada ya kuzungumza nao Novemba 24, 2015.  (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) WAZIRI M

Yanayojiri Bungeni Dodoma Muda Huu..Wabunge wa Ukawa Walianzisha na Kutolewa Nje ya Bunge na Spika

Image
Wabunge  wanaounga  umoja  wa  Katiba  Ya  Wananchi, UKAWA  wametolewa  nje  ya  ukumbi  wa bunge  muda  huu  baada  ya  kugoma  kutambua  ujio  wa  Dr Shein bungeni  na  kuanza  kuzomea  huku  wakisema    Maalim Seif....Maalim Seif Spika  wa  bunge,Job Ndugai  aliwataka  wabunge  hao waache kuzomea  na  badala  yake  wakae chini  lakini  wakakaida, hali  iliyomfanya  awaamuru  watoke  nje kwa  hiari  yao  kabla  nguvu  ya  dola  haijatumika  kuwatoa.

Maandalizi ya tendo la ndoa (Foreplay).

Image
Kabla ya hili tunda kuliwa kuna umuhimu wa kuhakikisha linaandaliwa kwa uhakika na wewe unayetaka kulila ili uweze kulifaidi vizuri, si suala na kukurupuka na kulivamia bila maandalizi mazuri na ya kutosha. Kuna tofauti kubwa sana kati ya mwanaume na mwanamke linapokuja suala la tendo la ndoa au kufanya mapenzi au sex . Je, maandalizi ya tendo la ndoa (foreplay) ni nini? Ni kitu kinachofanyika kati ya wakati mmetoa nguo zote na kabla ya mwanaume kuingiza uume kwenye uke. Ni kubusiana, kugusana, na kuchezeana hadi mnakuwa mmesisimka vya kutosha kwa ajili ya tendo la ndoa. Ni kuuungana kihisia, kiroho na kimwili kwa muda wa kutosha kabla ya tendo la ndoa Ni msingi na kitu muhimu kwa ajili ya kuhakikisha unapata tendo la ndoa lenye kuridhisha. Ni sanaa ya kuelezea upendo na kukaribishana kwa ajili ya tendo la ndoa. Ni muhimu kwa ajili ya kumwandaa mwanamke kwa ajili ya tendo la ndoa. Ni kumhusisha partner wako vizuri zaidi kupata hisia za upendo na ukaribu kimahaba yeye ku

HUYU NDO GAIDI ALIYE FANYA MASHABULIZI YA NCHINI UFARANSA

Image
Mtuhumiwa namba aliyepanga mashambulizi ya Paris, Abdelhamid Abaaoud ‘Mastermind’ enzi za uhai wake. Abdelhamid Abaaoud akifanya mazoezi ya kulenga shabaha. …Akiwafunga na kuwaburuza kwenye gari mateka aliowaua tayari. Jinsi oparesheni ya kuwasaka watuhumiwa kwenye Kitongoji cha Saint-Denis, Paris yalivyofanyika jana. Mmoja wa watuhumiwa akiwa amepigwa risasi na kuuawa. Polisi na kikosi cha uokoaji wakiwa kazini kwenye oparesheni ya jana. Mtuhumiwa namba mbili wa mashambulizi ya Paris, Hasna Ait Boulahacen “The Cow Girl’. Hasna Ait Boulahacen alivyopishana na askari kwenye lango la nyumba waliyokuwa wakiishambulia askari kuwasaka watuhumiwa. Uvamizi wa askari katika Kitongoji cha Saint Denis, jana. Polisi walivyojipanga kukivamia Kitongoji cha Saint Denis, Paris jana. Watu walivyouawa kwenye shambulio la Ijumaa, Paris, Ufaransa. Paris, Ufaransa MWENDESHA  mashtaka nchini Ufaransa amethibitisha kwamba, mtuhumiwa namba aliyepanga mashambulizi ya Paris, Abdelhamid Abaaoud

BREAKING NEWS..!! MTANGAZAJI MAARUFU NCHINI TANZANIA AFARIKI DUNIA.

Image
Mtangazaji maarufu nchini Tanzania Prince Baina Kamukulu amefariki dunia leo alfajiri. Kamukulu amefariki dunia katika hospitali ya Kigamboni jijini Dar es salaam ambapo taarifa za awali zinadai kuwa alianguka akiwa mazoezini kisha kukimbizwa katika hospitali hiyo jana usiku. Kamukulu aliwahi kuwa Mtangazaji wa Kipindi cha Afrika Bambataa cha Clouds Fm,pia amewahi kufanya kazi Star Tv na Radio Free Africa. R.I.P Kamukulu. Chanzo- BEN MWANTALA

BREAKING NEWS : SPIKA WA BUNGE MH JOB NDUGAI AWATOA WABUNGE WA UPINZANIA BUNGENI

Image
  Spika wa Bunge la Tanzania Mh Job Ndugai aweamuru Wabunge ukawa Kutoka Nje ya Bunge,Hali hiyo Imetokana na Wabunge hao Kupiga kelele Kipindi Viongozi wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Pamoja Viongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Wakiingia Bungeni

SHEREHE ZA KUAPISHWA WAZIRI MKUU WA AWAMU YA TANO VIWANJA VYA IKULU NDOGO CHAMWINO MJINI DODOMA

Image
Rais Dkt. John Pombe Magufuli, akimwapisha Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa, kuwa Waziri Mkuu wa awamu ya tano, wakati wa sherehe hizo zilizofanyika leo Nov 20, 2015 kwenye Viwanja vya Ikulu ndogo Chamwino mjini Dodoma. Rais Dkt. John Pombe Magufuli, akimkabidhi nyaraka za Serikali baada ya kumwapisha Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa, kuwa Waziri Mkuu wa awamu ya tano, wakati wa sherehe hizo zilizofanyika leo Nov 20, 2015 kwenye Viwanja vya Ikulu ndogo Chamwino mjini Dodoma. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimpongeza Waziri Mkuu mpya wa awamu ya Tano, Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa baada ya kuapishwa rasmi leo kwenye Viwanja vya Ikulu ndogo Chamwino mjini Dodoma, leo Nov 20, 2015. Rais Dkt. John Magufuli (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Makamu wake, Mhe. Samia Suluhu Hassan (kushoto) na Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa, baada ya kuapishwa Waziri huyo Mkuu kwenye Viwanja vya Ikulu Ndogo Chamwino mjin

BREAKING NEWS : UKAWA WACHAFUA HALI YA HEWA BUNGENI KISA RAIS WA ZANZIBAR

Image
Wabunge wa Upinzani katika Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Watanzania Wanazomea Bungeni mara baada ya Kutangazwa Kuingia kwa Rais wa Zanzibar Mh Dk Ali Mohamed Shein.Wanachopinga wabunge hao wanadai hawamtambui Dk Shein Kama Rais Halali wa Za nzibar.Hali hiyo ilianza pale Naibu spika alipom ui ta Mwanasheria Mkuu wa Seri kali  Kutengua Kanuni ili Viongozi wa Serikali ya Mapin duzi ya Zanzibar wameze Kuongozana  na R ais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Magufuli wakati atakapokuja Kulihutubia Bunge na Kulizindua Rasmi ,

RAIS MAGUFULI ASAINI KITABU CHA MAOMBOLEZO KATIKA UBALOZI WA UFARANSA NCHINI

Image
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisaini kitabu cha Maombolezo katika Ubalozi wa Ufaransa nchini kufuatia vifo vya Watu zaidi 130 vilivyotokana na mashambulizi ya kigaidi.(Picha na Ikulu)   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpa pole Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Malika Berak kufuatia vifo vya Watu zaidi 130 vilivyotokana na mashambulizi ya kigaidi.   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Balozi wa Ufaransa nchini Malika Berak Tanzania mara baada ya kusaini Kitabu cha Maombolezo na kutoa salamu za pole kwa Rais wa Ufaransa Mheshimiwa Francois Hollande kufuatia vifo vifo vya Watu zaidi 130 vilivyotokana na mashambulizi ya kigaidi.   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wa pili akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Ufaransa (kushoto) pamoja na Maofisa mbalimbali wa Ubalozi huo mara baada ya kutia saini kita

Chanzo Lulu Kutodumu na Wanaume Chatajwa

Image
 Ubuyu! Licha kujaliwa umbo matata na mvuto wa aina yake, staa wa Bongo Movies Elizabeth Michael ‘Lulu’, anadaiwa kutodumu na mwanaume, Ijumaa Wikienda limetajiwa chanzo cha hali hiyo. Kwa mujibu wa sosi wa ndani wa familia ya staa huyo, chanzo kikubwa cha Lulu kutodumu na mwanaume anayempata kama mwandani wake ni mama yake, Lucresia Karugila. Ilidaiwa kwamba, kama ilivyokuwa kwa Wema Sepetu zamani, mama yake, Miriam Sepetu alidaiwa kumwekea ‘patroo’ mrembo huyo kwa kumchagulia mwanaume wa kuwa naye, jambo lililomfanya Wema ashindwe kudumu na mwanaume mmoja. “Hiyo ndiyo hali halisi inayomkuta Lulu. Yaani ni kama Wema zamani,” kilisema chanzo hicho. “Unajua mama Lulu anataka mwanaye awe na mwanaume mwenye fedha ili amsaidie kuhudumia familia. “Inapotokea mwanaume anashindwa kuhimili matumizi, basi mama huyo humtaka mwanaye kusitisha uhusiano huo mara moja kwani unakuwa si wa masilahi,” kilidai chanzo hicho. Baada ya kunyetishiwa ishu hiyo, gazeti hili lilitinga nyumb

BREAKING NEWZZ...ALIYEKUWA MGOMBEA WA UBUNGE JIMBO LA KIGOMA KUSINI DAVID KAFULILA AIBUKIA MAHAKAMANI

Image
Hatimaye David Kafulila afungua Shauri Mahakama kuu kanda ya Tabora Lakupinga matokeo ya Ubunge Jimbo la Kigoma Kusini,Ameitaka Mahakama hiyo Kumtangaza Mshindi

HATIMAYE UKWELI KUHUSU CHUKI YA ZITTO KWA MSICHANA MSOMI DR. TULIA YATAJWA KUMBE KUNA MENGI NYUMA YA PAZIA

Image
Jamii ya wanazuoni imekuwa ikijiuliza ni kwanini mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe anampiga vita mgombea unaibu spika Dk.Tulia Ackson. Wanahoji ni kwanini Zitto Kabwe anamhofia huyu mwanamama wakati ana vigezo vyote vinavyompa "credibility" ya kugombea.Imefikia hatua Zitto anamnadi Mussa Azzan ambaye ni mbunge wa Ccm na kusahau kuwa yeye ni mpinzani ndani na nje ya bunge. Hapa ndipo dhana ya usaliti kwa Zitto Kabwe inapozidi kumea kwenye masikio ya watanzania.Zitto Kabwe hataki kukubali kuwa siasa ya bunge sio yake peke yake. Mnakumbuka sakata la aliyekuwa mkurugenzi mkuu wa TPDC ambaye PAC ikiongozwa na Zitto Kabwe iliamuru akamatwe na kuwasilishwa polisi!?Tena kwa makosa ambayo PAC ilikuja kuangukia pua!! Namzungumzia Andilile Mwainyekule.Huyu ni mume wa ndoa wa Dk.Tulia Ackson.Zitto Kabwe anauona ugumu wa yeye kuiyumbisha serikali kwa skendo za kupika kama kiti kitasimamiwa na Dk.Tulia Ackson. Zitto Kabwe anahofia Dk.Tulia Ackson kutumia mwanya wa

MAMA: Miezi 11 Mwanangu Anaishi Kwa Mateso Bila Upasuaji!

Image
Mtoto Asmina Abdallah. Makongoro Oging’ na Haruni Sanchawa Mtoto Asmina Abdallah mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi minne, mkazi wa Kijiji cha Mgambo, Unguja, Zanzibar anaishi kwa mateso bila kufanyiwa upasuaji kwa madai ya kutokamilika kwa vipimo kufuatia upungufu wa mashine katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Mtoto Asmina Abdallah akiwa na mama yake, Amina Maburuki Amani.Maisha ya mtoto huyo kwa sasa yapo hatarini kutokana na uvimbe uliopo machoni kuongezeka na haujapatiwa ufumbuzi wa matibabu kwa miezi 11 huku ukienda sambamba na maumivu makali.  Akizungumza na waandishi wa habari hii wiki iliyopita katika wodi ya watoto ya Makuti A Muhimbili, mama mzazi wa mtoto huyo, Amina Maburuki Amani alisema kwamba hali ya mtoto wake inazidi kuwa mbaya na anaelekea kukata tamaa.  Akifafanua zaidi mama huyo alikuwa na haya ya kusema:  “Hali ya mtoto wangu imekuwa ikibadilika kila kukicha huku akilia kutokana na maumivu makali, nimechoka safari ya kila mara

KOBE 201 WALIOKUWA WAKISAFIRSHWA NJE YA NCHI WAKAMATWA UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA J.K NYERERE

Image
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Adelhelm Meru akikagua mabegi matano yenye Kobe 201 yaliyokamatwa usiku wa kuamkia leo na askari wanyamapori kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama katika uwanja wa Kimataifa wa J.K. Nyerere jijini Dar es Salaam.   Watuhumiwa hao wa usafirishaji wa wanyamapori wametajwa kuwa ni David Mungi mkazi wa Muheza Mkoani Tanga na Mohammed Suleiman (43) mkazi wa Zanzibar ambao katika tukio hilo walishafanikiwa kupita kwenye mitambo ya ukaguzi lakini mbwa maalum (sniffer dogs) wakasaidia kugundua uhalifu huo. Kwa pamoja watuhumiwa hao walikamatwa na tiketi za kusafiria kuelekea nchini Malaysia.  Kobe wapatao 201 waliokamatwa na askari wanyamapori kwa ushirikiano na vyombo vya ulinzi na usalama kwa kutumia mbwa maalum (sniffer dogs).      Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Maliasili na Utalii Bi. Dorina Makaya kulia na Mmoja wa Askari wanyamapori wakiangalia kobe 103 waliotelekezw