Posts

Showing posts from April, 2015

ISIS WAENDELEA KUFANYA MAUAJI YA KUTISHA HUKO SYRIA NA IRAQ

Image
Mmoja wa watuhumiwa wa uchawi akiwa tayari kuchinjwa na Kundi la ISIS huko Raqqa, Syria. Mtuhumiwa mwingine wa uchawi naye akiwa tayari kuchinjwa na ISIS. Mpiganaji wa ISIS akinyanyua tofali la zege kumpiga mmoja wa wanaume waliokamatwa kwa kuua wanawake. Adhabu ya kuwapiga mawe wanaume waliokamatwa kwa mauaji ya wanawake watatu ikiendelea huko Iraq Kabla ya kuuawa watuhumiwa hao walisomewa mashtaka yao na mmoja wa wapiganaji wa ISIS. Picha ya mashoga wawili waliowekwa mitandaoni na Kundi la ISIS kabla ya kuwapia mawe hadi kufa. Mashoga hao wakipigwa mawe hadi kufa na wapiganaji wa ISIS huko Syria.WAPIGANAJI wa ISIS wamefanya mauaji ya kutisha kwa mateka wawili wa kiume waliotuhumiwa kuwaua kwa kuwapiga virungu wanawake watatu huko nchini Iraq. ISIS waliwapiga watuhumiwa hao kwa matofali ya zege kichwani hadi kufa ikiwa ni adhabu kwa kitendo chao cha kuiba na kuwaua wanawake watatu. Tukio hilo limefanyika katika Mkoa wa Nineveh huko kaskazini mwa Iraq. Katika tukio lingin

UKAWA: UCHAGUZI MKUU OKTOBA 2015 LAZIMA, KIKWETE ASIONGEZEWE MUDA, KURA YA MAONI BAADAE

Image
Mwenyekiti wa CUF, Profesa Lipumba (kushoto)  akifafanua jambo kwa waandishi wa habari. Wa pili kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe (wa pili kulia) na Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Willbroad Slaa (kulia). VYAMA vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) leo vimetoa msimamo wao juu ya njama za kuahirisha Uchaguzi Mkuu unaotakiwa kufanyika Mwezi Oktoba mwaka huu. Ukawa imesisistiza kwamba kuahirisha kwa Uchaguzi Mkuu huo ni sawa na kumuongezea Rais Jakaya Kikwete na Chama chake cha CCM muda wa kuendelea kuitawala Tanzania. Ukawa imesema jaribio lolote la kuahirisha Uchaguzi Mkuu kwa kisingizio chochote kile litakuwa ni kinyume na katiba ya sasa ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Msimamo wa UKAWA unafuatia kumalizika kwa kikao cha Viongozi Wakuu wa Vyama vinavyounda umoja huo kilichofanyika katika Makao Makuu ya Chama cha Wananchi (CUF) jijini Dar kati ya tarehe 28 na 29 Aprili mwaka huu. Akieleza msima

CLOUDS FM YASHINDA TENA TUZO YA UBORA YA SUPERBRAND KWA MARA YA TATU AFRIKA MASHARIKI

Image
Picha ya pamoja ya baadhi ya makapuni binafsi waliopewa tuzo bora za viwango, kutoka shoto ni Bi. Dorothy Mashamsham kutoka kampuni ya Mafuta ya PetrolFuel, Mkurugenzi Mtendaji wa ITV/Radio One Bi Joyce Mhaville,Mkurugenzi wa Uzalishaji na Vipindi Clouds Media Group Bwa. Ruge Mutahaba, Meneja Masoko Bwa. Elisa Ernest kutoka kampuni ya bima ya Alliance Insurance. Mkuu wa Kitengo cha Idara ya Uchambuzi wa viwango Afrika Mashariki, Bwana Jawad Jaffer akiwa na baadhi ya viongozi wa juu wa kampuni ya Clouds Media Group, kutoka kulia ni Mkuu vipindi wa Clouds FM Sebastian Maganga,wa tatu ni Mkurugenzi wa vipindi na Uzalishaji Ruge Mutahaba na  Mkuu wa kitengo cha huduma,Promosheni na Tamasha Clouds Media Group. Bi Fauzia Kullane.  Mkuu wa Kitengo cha Idara ya Uchambuzi wa viwango Afrika Mashariki, Bwana Jawad Jaffer akimkabidhi tuzo bora ya viwango Mkurugenzi wa Uzalishaji na vipindi wa Clouds Media Group,Bwa. Ruge Mutahaba, kwenye hafla fupi ya utoaji

WAZIRI MKUU PINDA AKUTANA NA DANGOTE

Image
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Mwekezaji kutoka Nigeria anayejenga kiwanda cha saruji mkoani Mtwara, Bw.Aliko Dangote (kulia kwake) na ujumbe wake, ofisini kwake jijini Dar es salaam Aprili 30, 2015. Watatu kushoto ni Balozi wa Nigeria nchini, Dkt. Ishaya Samaila Majanbu.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwa katika picha ya pamoja na Mwekezaji kutoka Nigeria anayejenga kiwanda cha saruji mkoani Mtwara, Bw.Aliko Dangote (kulia kwake) na ujumbe wake baada ya mazungumzo yao,  ofisini kwake jijini Dar es salaam April 30, 2015. Kushoto kwake ni balozi wa Nigeria nchini, Dkt. Ishaya Samaila Majanbu. (picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiagana na Mwekezaji kutoka Nigeria anayejenga kiwanda cha saruji mkoani Mtwara, Bw.Aliko Dangote (kushoto) na  balozi wa Nigeria nchini, Dkt. Ishaya Samaila Majanbu (kulia) baada ya mazungumzo yao  ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Aprili 30, 2015. (picha na Ofisi ya

TASWIRA VURUGU ZINAZOENDELEA NCHINI BURUNDI

Image
    Images credit: Reuters / AFP

RAIS KIKWETE AIFARIJI FAMILIA YA MAREHEMU BRIGEDIA JENERALI MSTAAFU HASHIM MBITA LEO

Image
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini katika kitabu cha maombolezo alipokwenda kuifariji  familia ya Marehemu Brigedia Jeneral Mstaafu Hashim Mbita TemekeChang'ombe jijini Dar es salaam jioni ya leo April 27, 2015. Marehemu anatarajiwa kuzikwa siku ya Jumatano katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam baada ya Swala ya Alasiri katika msikito wa Mtoro, baada ya kupata heshima zote za kijeshi asubuhi yake katika makao makuu ya Jeshi Upanga, Dar es salaam. Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia wakati Mama Salma Kikwete akiweka saini katika kitabu cha  maombolezo alipokwenda kuifariji familia ya Marehemu Brigedia Jeneral Mstaafu Hashim Mbita Temeke Chang'ombe jijini Dar es salaam jioni ya leo April 27, 2015. Marehemu anatarajiwa kuzikwa siku ya Jumatano katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam baada ya Swala ya Alasiri katika msikito wa Mtoro, baada ya kupata heshima zote za kijeshi asubuhi yake katika makao makuu ya Jeshi Upanga, Dar es

MANNY PACQUIAO ATUA LAS VEGAS TAYARI KWA PAMBANO LAKE LA KIHISTORIA DHIDI YA FLOYD MAYWEATHER

Image
Manny Pacquiao akiwasalimia mashabiki wake waliofika kumpokea alipowasili katika Hoteli ya Mandalay Bay jijini Las Vegas jana usiku. Basi lililobeba wageni na timu ya walimu wa mafunzo wa Pacquiao likielekea Las Vegas jana mchana. Pacquiao akiwa amembeba mwanaye aitwaye Israel baada ya kushuka kwenye basi lake.… Manny Pacquiao (36) na Floyd Mayweather (38) watazichapa usiku wa Jumamosi, Mei 2, mwaka huu kwenye Ukumbi wa MGM Grand uliopo Las Vegas, Marekani. Manny alitupia picha hii katika akaunti yake ya on Instagram akiwa kwenye basi lake la kifahari wakati akielekea Las Vegas akitokea Los Angeles alipokuwa ameweka kambi. Pacquiao akijifua kwa mara ya mwisho jijini Los Angeles kabla ya kuelekea Las Vegas. Gari lililokuwa limembeba Manny likiwa limezingirwa na mashabiki wake nje ya ukumbi wa mazoezi huko Los Angeles wakitaka kumuaga kabla ya kuelekea Las Vegas. Waendesha pikipiki wenye bendera za

UCHAMBUZI WA SHERIA YA MAKOSA YA MTANDAO, 2015

Image
UTANGULIZI Sheria hii ya Makosa ya Jinai kupitia Mtandao, 2015 ina mapungufu mengi. Mapungufu hayo yamebainika kuwa, kama sheria ikipita yanaweza kuifanya nchi ikawa ni kati nchi adui za matumizi ya mtandao wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano duniani. Watanzania wote wanatakiwa kufahamu kuwa muswada ukipita utatumika nchini kote yani Tanzania Bara na Visiwani. Watanzania walio wengi hawafahamu Sheria hii inawahusu kwa namna gani; lakini kwa lugha rahisi ni kuwa itamuathiri mtu yeyote anayeweza tumia Mtandao wa Intaneti kwa kutimia kifaa chochote iwe kompyuta kubwa au vifaa vyenye uwezo wa kufanya kazi kama kompyuta kama Simu za mikononi, saa, televisheni na vifaa vingine vinavyoendana na hivyo. Malengo ya Sheria hii ni kuainisha makosa yanayohusiana na matumizi ya mfumo wa kompyuta na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, kuweka utaratibu wa upelelezi, ukusanyaji na matumizi ya ushahidi wa kielektroniki na

SERIKALI YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YATANGAZA AJIRA ZA WALIMU 30,000

Image
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Jumanne Sagini (kulia) akizungumza jambo. Dar es Salaam. Serikali imetangaza ajira mpya za walimu 31,056 wanaotakiwa kuanza kazi kuanzia Mei Mosi, mwaka huu. Mbali na walimu, pia imetangaza ajira kwa mafundi sanifu wa maabara 10,625 ambao pia wataanza kazi sambamba na walimu hao.Akizungumza jana, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Jumanne Sagini alisema Serikali imetenga Sh9 bilioni kwa ajili ya posho za kujikimu na nauli kwa walimu na mafundi sanifu maabara. Alisema kiasi cha fedha kilichotengwa ni posho ya siku saba na fedha za nauli ambazo zinatakiwa kulipwa na halmashauri ambazo ndiyo mwajiri. Alisema posho hizo zinatakiwa kulipwa ndani ya siku saba na kwamba isizidi siku 14 tangu kuripoti kwa mwalimu katika kituo cha kazi. “Hatutapenda kusikia malalamiko kutoka kwa walimu hao, halmashauri zijipange kuwapokea waajiriwa wao wapya,”

MAGAZETI LEO JUMANNE TAREHE 28.4.2O15

Image
  MAGAZETI YA UDAKU LEO   MAGAZETI YA MICHEZO NA BURUDANI