Posts

Showing posts from July, 2014
Image
RAIS BARACK OBAMA ASHIRIKI MKUTANO WA VIJANA WA AFRIKA Rais wa Marekani ,Barack Obama akizungumza na Viongozi vijana toka nchi mbalimbali za Afrika waliokuwa wakipata mafunzo katika vyuo vikuu vya Arkansas na Florida. Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani John Kerry akitoa hotuba yake kwa Viongozi vijana toka barani Afrika waliokuwa wakishiriki mafunzo katika vyuo vikuu vya Arkansas na Florida nchini Marekani. Rais Obama akiondoka Ukumbini mara baada ya kuzungumza na Viongozi vijana toka nchi mbalimbali za Afrika waliokuwa wakipata mafunzo katika vyuo vikuu vya Arkansas na Florida. Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki ,Joshua Nassari ni miongoni mwa Vongozi vijana toka barani Afrika waliohudhuria mkutano huo na Rais Barack Obama . Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki ,Joshua Nassari ni miongoni mwa Vongozi vijana toka barani Afrika waliohudhuria mkutano huo na Rais Barack Obama hapa akifuatilia kwa makini Hotuba ya Rais Obama. . Mbunge Jos

HAMISA MOBETO KUVISHWA PETE YA UCHUMBA TAREHE 2 YA MWEZI WA 8 NDANI ESCAPE 1.

Image
Wanasema kimya kingi kina mshondo baada ya kudaiwa, hapo mwanzo ilidaiwa kua     Hamisa Mobeto alikua akichepuka na Bwana Almas aka Dangote aka Diamond au Chibu kama mwenyewe anavyopenda kujiita. Lakini baada ikaja kujulikana kua yalikua ni maneno ya wabongo. Habari za kuaminika Bongoclan ilizozipata ni kua kwa sasa Mwanadada Hamisa kazama kabisa kwenye penzi zito la Seth De Jesus Giovan almaarufu kama Bikira wa kisukuma. Mmoja wa mashostito wa wapenzi hao ambaye hakupenda jina lake litajwe alisema kua Hamisa keshatambulishwa nyumbani kwao na Bikira na kilichobaki ni tukio la kuvishana pete ndo lililobakia. Team yetu iliamua kufatilia kama ni kuna ukweli     kuhusiana na ishu ya kuvishana pete kwa wapenzi hao na kugundua ni kweli kua watavishana pete tarehe 2 ya mwezi wa 8 ndani ya Escape 1 ambako pia ndani ya siku hiyo kutakua na Instagram Party. Kupitia akaunti yake bikira wa kisukuma alifunguka haya kuhusiana na tukio hilo " Mungu anipe nini mie...

MTOTO ALIYETESWA SIKU 730 ATOROSHWA

Image
  Mtoto Melina akiwa hospitali. YULE binti Melina (15) aliyeandikwa kwenye Gazeti la Uwazi toleo la Juni 17, mwaka huu kwa kichwa cha habari kisemacho; MTOTO ATESWA SIKU 730 amedaiwa kutoroshwa na kupelekwa kusikojulikana. Binti huyo aliyekuwa akifanya kazi za ndani ‘hausigeli,’ alidaiwa kuteswa na bosi wake aliyejulikana kwa jina la Yasinta Rwechungura, mkazi wa Boko Magengeni jijini Dar ambaye alifikishwa kwenye Makahama ya Wilaya Kinondoni, Dar kwa madai ya kumtesa mtoto huyo na kumsababishia majeraha. Kutoroshwa kwa binti huyo kunadaiwa kutokea wiki chache baada ya binti huyo kumaliza matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar alipokuwa akiuguza majeraha.  Chanzo cha ndani kinadai kuwa mara baada ya mtoto huyo kuruhusiwa kutoka hospitalini, alikutana na baba yake aliyefika jijini Dar kutokea Kagera kwa ajili ya kusikiliza kesi ya mwanaye na kuanzia hapo mtoto huyo hajaonekana tena hali iliyotafsiriwa kuwa ametoroshwa. ....akionyesha majeraha ali

Mganga Atoweka na seheme za siri za mtoto

Image
Mtoto Almasi mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi kumi akiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili Katika hali ya kushangaza madaktari na wauguzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), jijini Dar es Salaam walipigwa na butwaa baada ya mtoto Almasi mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi kumi kufikishwa hospitalini hapo akiwa amekatwa seheme zake za siri na mtu aliyedaiwa ni mganga wa kienyeji na kukimbilia kusikojulikana. Akizungumza kwa masikitiko makubwa wiki iliyopita, baba wa mtoto huyo, Ismail Kamaga alisema tukio hilo lilitokea hivi karibuni katika Kijiji cha Omukagando, Wilaya ya Karagwe mkoani Kagera. Alisema mganga huyo aliyemtaja kwa jina moja la Adinali alifanya kitendo hicho kwa watoto wawili akidai anawafanyia tohara.“Alidai anawafanyia tohara watoto wawili, baada ya muda mwenzake alipona wa kwangu hakuna kitu na nyeti aliondoka nayo, sina namna tena ya kumsaidia mwanangu. Nilimpeleka Hospitali ya Mugawa, Kagera ambako aliwekewa mpira wa kuto

ANGALIA PICHA MATESO ANAYOPATA YATIMA ,AOTA NYAMA YA AJABU

Image
STORI: MAKONGORO  Kwa kweli duniani kuna mateso, lakini ya mtoto huyu yatima ni makali na maisha yake yapo hatarini kama hatawahi kupata matibabu. Fuatilia mkasa wake hapa chini ambao naamini utakuhuzunisha. Kijana Twaha Sultan (16) ambaye ni yatima mkazi wa Kipawa Karakata, Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam akisimulia mkasa wake alikuwa na haya ya kusema: Akionyesha nyama ya ajabu iliyomuota kijana. “Ndugu zangu, kufuatia maradhi ya ajabu yanayonisumbua sina raha ya maisha, niheri ningewafuata wazazi wangu waliotangulia mbele ya haki nikapumzike.“Nimekuwa mtu wa maumivu wakati wote, kulala na kula kwangu ni shida tupu mbaya zaidi ndugu ninaoishi nao hawana uwezo. “Naamini kama wangekuwa na uwezo huenda ningekuwa nimepona maradhi haya yaliyoanza kama utani baada ya kunipeleka katika hospitali kubwa na kupatiwa tiba ya uhakika, kwa kweli nateseka jamani! “Naumia zaidi ninapowaona vijana wa umri wangu wakiwa wanasoma na wenye furaha, wakati mimi nateswa na h

RAIS KIKWETE ASALI SWALA YA IDDI DAR ES SALAAAM

Image
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na baadhi ya waumini wa dini ya kiislamu muda mfupi baada ya kuswali sala ya Iddi El Fitr katika mshikiti wa Maamur Upanga jijini Dar es Salaam leo asubuhi. Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na baadhi ya waumini wa dini ya kiislamu muda mfupi baada ya kuswali sala ya Iddi El Fitr katika mshikiti wa Maamur Upanga jijini Dar es Salaam leo asubuhi. Baadhi ya waumini wa dini ya kiislamu wakiswali sala ya Iddi El Fitr katika masjid Maamur Upanga jijini Dar es Salaam leo asubuhi(picha na Freddy Maro)

UGONJWA WA AJABU WAMTESA KIJANA HUYU.

Image
 Kijana Lawrent Lawrian, akiwa na uvimbe wa ajabu kichwani mwake. Lawrent Lawrian, 42 (pichani), ni mkazi wa Kijiji cha Nyakisogo, Wilaya ya Biharamlo, mkoani Kagera, amekuwa mwenye huzuni na kukosa raha kwa muda wa miaka 35 kutokana na gonjwa la ajabu linalomtesa ambalo limemsababishia mambo mengi ikiwa ni pamoja na kutoendelea na masomo.  Gonjwa hilo la ajabu ni uvimbe kama nundu kichwani wenye uzito wa kilo 3, ulimuanza akiwa darasa la kwanza.Akielezea zaidi kwa njia ya simu hivi karibuni Lawrent alisema:  “Gonjwa hili lilianza kama kauvimbe nikiwa na umri wa miaka saba, wakati huo nilikuwa na wazazi wote na ilipofika mwaka 1992 baba akafariki dunia.  “Nikabakia na mama tukawa tunaishi kwa kutegemea kilimo cha kawaida, nilikuwa nikienda shule lakini ilifikia hatua nilishindwa kutokana na maumivu na manyanyaso.  “Darasa la saba nilimaliza kwa tabu sana, kwani wanafunzi wenzangu walikuwa wakinicheka na kunitenga, licha ya kuadhibiwa na walimu lakini hawakuacha t

MJOMBA AIBA MKE WA MPWA WAKE ,WAPIGANA,MCHEPUKO SIO DILI BAKI NJIA KUU,

Image
Mjomba akiomba msamaha kwa mpwa wake. TIMBWILI la aina yake lilifumuka ndani ya gesti moja iliyopo Mbezi Afrikana jijini Dar es Salaam (jina kapuni), kufuatia kijana aliyefahamika kwa jina moja la Kelvin kumkuta chumbani mtu aliyedai ni mjomba wake, Joseph akiwa na mkewe wa ndoa, Emiliani. Mjomba wa Kelvin(Joseph) akimsihi Mpwa wake amsamehe mara baada ya kukutwa gesti na mke wa Kelvin.  Mkasa huo wa ajabu ulijiri usiku wa Jumamosi iliyopita kwenye gesti hiyo iliyopo Mbezi ya Afrikana jijini Dar es Salaam.  MPISHI WA FUTARI AUZA ISHU OFM Mama mmoja aliyedai ni mpishi wa futari maeneo hayo, alipiga simu kwa makamanda wa Oparesheni Fichua Maovu (OFM) na kusema: Kelvin (kulia)'akidili'  kisawasawa  na mjomba wake.  “Mimi ni mpishi wa futari hapa Mbezi Afrikana kuna baba mmoja na ndugu zake wanachakazana, kisa wamefumaniana kwenye gesti ya (akaitaja jina). Ipo hapahapa jirani njooni muwahi.” Mlinzi wa gesti akijaribu kumzuia Kelvin

ANGALIA PICHA DIAMOND, LADY JAY DEE WANGARA TUZO ZA AFRIMMA

Image
Diamond akiwa na tuzo ya Msanii bora wa kiume Afrika Mashariki. Diamond akiwa na Davido. STAA wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul 'Diamond Platnumz' ameendelea kufanya vizuri katika tasnia ya muziki ndani na nje ya nchi baada ya kutwaa tuzo ya AFRIMMA 2014 ya Msanii bora wa kiume Afrika Mashariki. Diamond wakati akielekea kwenye ukumbi  linapofanyika zoezi la utoaji tuzo za Afrimma. Tuzo hizo za Africa Music Magazine (AFRIMMA) zimetolewa leo alfajiri jijini Texas nchini Marekani. Staa huyo alikuwa anawania tuzo katika vipengele vitano ambavyo ni: Msanii bora wa mwaka Afrika, Wimbo wa mwaka, Collabo bora, Video bora ya mwaka na Msanii bora wa kiume wa Afrika Mashariki. WASHINDI WA TUZO HIZO ZA AFRIMMA 2014 NI KAMA IFUATAVYO: Best DJ Africa 2014- Dj Black (Ghana) Best African DJ USA 2014 – Dj Josh (Kenya) Best Video of the Year 2014- Flavour (Nigeria) Best Male East Africa 2014- Diamond (Tanzania) Best Male W

CHANZO DIDA KUACHANA NA MUMEWE SASA SIO SIRI TENA

Image
Dida na Ezden wakifunga ndoa July,2013 Dida Shaibu, mtangazaji wa kipindi cha Mitikisiko ya Pwani amefunguka Exclusively kupitia Sunrise ya 100.5 Times Fm  inayoongozwa na Fadhili Haule na kueleza chanzo cha ndoa yake  na Ezden ‘The Rocker’ Jumanne kuvunjika. Ndoa iliyodumu kwa muda wa mwaka mmoja tu. Dida ameeleza kuwa mzizi wa tatizo lililopelekea ugomvi mkubwa kati yao ni simu ya mkononi ya mumewe huyo wa wazamani baada ya kutaka kuitumia kucheza game na kugundua kuwa imewekewa password kwa mara ya kwanza katika uhusiano wao.  “Tatizo kubwa la ugomvi wangu na X-Husband, tatizo kubwa lilikuwa ni simu. Nakumbuka ilikuwa siku ya Jumatano tumetoka kazini. Tukawa tuko kawaida, unajua sisi huwa tunataniana sana. Kwa hiyo aliacha simu yake kitandani, unajua mimi huwa nacheza game kupitia simu yake. Kwa hiyo mimi nikachukua simu yake nikakuta ameweka password kitu ambacho sio cha kawaida. Kwa hiyo mimi ikabidi nimuulize. nikamuita, tulikuwa tunaitana ‘ mshik

Bilal awaongoza maelfu ya Waumini wa Kiislam katika Swala ya Eid El Fitr katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar leo

Image
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Mohamed Gharib Bilal (katikati),Sheikh Mkuu,Issa Shaaban Simba,Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Mh. Said Meck Sadick na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Sheikh Mussa Salum wakijumuika na Waumini wengine wa Dini ya Kiislam kwenye Swala ya Eid El Fitr iliyofanyika Kitaifa kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja,Jijini Dar es Salaam leo.CHANZO MTAA KWA MTAA BLOG Sehemu ya Waumini wa Dini ya Kiislam wakiwa kwenye Ibada ya Eid el Fitr katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo.  Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam,Sheikh Mussa Salum akitoa Khotuba katika Idada ya Swala ya Eid El Fitr iliyofanyika Kitaifa kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja,Jijini Dar es Salaam leo.  Mawaidha yakiendelea mara baada ya Swala ya Eid el Fitr. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Mohamed Gharib Bilal akitoa salamu za Eid el Fitr leo mara baada ya Swala iliyofanyika Kitaifa kwenye Viwanja vya Mn