Posts

Showing posts from August, 2013

MANSOUR AKATAA KWENDA MAHAKAMANI KUPINGA UAMUZI WA KUFUKUZWA CCM

Image
Aliyekuwa Mjumbe wa Baraza la Wawakilisihi Jimbo la Kiembe Samaki (CCM) Mansour Yussuf Himid amesema licha ya kufukuzwa Uanachama katika chama hicho hatoenda Mahakamani kutetea nafasi hiyo kwani kufanya hivyo ni kukaribisha Malumbano ambayo hayana tija. Amesema kwenda kupinga uamuzi huo Mahakamani ni kuhalalisha yeye kuwa Mwakilishi wa Mahakama badala ya Wananchi jambo ambalo hapendelei kutokea katika maisha yake. Mansour ameyasema hayo leo katika Kongamano la Kamati ya Maridhiano lililofanyika Ukumbi wa Hoteli ya Bwawani Mjini Zanzibar. Amesema amekuwa akiulizwa Maswali mengi na Watu tofauti kuhusu mustakabali wake kisiasa baada ya kufukuzwa uanachama na kuongeza kuwa hana Pesa za kuchezea kwenda kupinga uamuzi wa Chama cha Mapinduzi Mahakamani. "Wenzangu wamenipima na wameniona sifai ni haki yao, siendi Mahakamani, sina pesa za kuchezea wala sitaki kuwa Mwakilishi wa Mahakama" Alisema Mansour. Mansour aliyejiung

Maandalizi ya Kili Music Tour Kigoma yanavyoendelea

Image
 Kazi ya kufunga jukwaa na banner za kikwetu kwetu

SHULE YAWAZUIA ROBO TATU YA WANANFUNZI KUFANYA MITIHANI.

Image
Katika hali isiyokuwa ya kawaida robo tatu ya wanafunzi katika shule ya sekondari Uhuru, Manispaa ya Shinyanga wamezuiwa kufanya mitihani ya muhula wa pili kwa madai ya wazazi wao kushindwa kulipia michango Baadhi ya wanafunzi wanaosoma katika shule hiyo waliozungumza na waandishi wa habari jana mjini hapa walisema pamoja na kuzuiwa kufanya mitihani hiyo walimu wao waliwapa adhabu ya kukaa chini wakiwa juani na baadae walipewa kazi ya kumwagilia bustani wakati wenzao wachache wakiendelea na mitihani. Mmoja wa wanafunzi hao (jina tunalo) alisema walielezwa na walimu wao kwamba ye yote ambaye hatokuwa amelipa ada na michango mbalimbali shuleni hapo ikiwemo mchango wa mlinzi hatoruhusiwa kufanya mitihani hiyo mpaka pale wazazi wao watakapokuwa wamelipa michango wanayodaiwa. Mwanafunzi huyo alifafanua kuwa hata pale walipojaribu kuwaomba walimu wawaruhusu kufanya mitihani kwa vile suala la michango si jukumu lao bali la wazazi wal

WADAU WA UTOAJI HAKI WA CHAMA CHA MAJAJI WANAWAKE NCHINI WAKUTANA KUJADILI UTOKOMEZAJI WA MATUMIZI MABAYA YA MADARAKA YANAYOAMBATANA NA RUSHWA YA NGONO

Image
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo nchini (WAMA),mama Salma Kikwete (kulia) akizungumza na washiriki wa warsha ya utoaji Haki juu ya kutokomeza matumizi mabaya ya madaraka yanayoambatana na rushwa ya ngono mara baada ya kukabidhiwa kitabu cha mwongozo wa namna ya kushughulikia mashauri mbalimbali ya kisheria alichokabidhiwa na Rais wa Chama cha Majaji Wanawake Tanzania Mh. Jaji Engera Kileo  leo jijini Dar es salaam. Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo nchini (WAMA) mama Salma Kikwete akifungua warsha ya siku 1 ya utoaji Haki juu ya kutokomeza matumizi mabaya ya madaraka yanayoambatana na rushwa ya ngono iliyoandaliwa na Chama cha Majaji Wanawake Tanzania (TAWJA) leo jijini Dar es salaam. Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo nchini (WAMA) mama Salma Kikwete (kushoto) akizungumza jambo na Bi. Salome Anyoti Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia masuala ya

AJINYONGA NJE YA UKUMBI WA DISKO, MAMA AKATAA

Image
KULWA Shaban (18) mkazi wa Gongo la Mboto, jijini Dar amedaiwa kujinyonga na mwili wake kukutwa  ukinin’ginia kwenye mti pembezoni mwa ukumbi wa disko maarufu kwa jina la Majita. Akizungumza kwa machungu, mama wa kijana huyo, Rehema Omar alisema tukio hilo lilitokea hivi karibuni ambapo siku nne kabla ya kukutwa akiwa amejinyonga, Kulwa aligombana na baadhi ya marafiki zake ambao walichukua tofali na kumpiga nalo mdomoni na kusababisha meno mawili  kung’oka. “Tulimpa fedha kwa ajili ya kwenda kujitibia kisha alirejea nyumbani na kuendelea kujiuguza majeraha kwani yalikuwa ni makubwa,” alisema Rehema.NA GLOBAL PUBLISHER Mama huyo aliendelea kusema wakati mwanaye akiendelea kuuguza kidonda ndipo alipopatwa na maswahibu hayo baada ya kwenda disko na wenzake. “Siku hiyo niliingia kulala na ilipofika saa tisa usiku niligongewa mlango na watu wawili na kuambiwa hali ya mtoto wangu ni mbaya  pasipo kubainisha amefanya nini,” alisema mama h

PICHA YA MWANAUME ALIYEGEUZWA KUWA MWANAMKE BAADA YA KUZINI NA MKE WA MTU

Image
Mwanaume  mmoja  nchini  Kenya  amejikuta  akiambulia aibu  ya  mwaka  baada  ya  uume  wake  kubadilishwa  kuwa  uke.... Mwanaume  huyo  anadaiwa  kufanyiwa  mchezo  huo  baada  ya  kufumaniwa  akizini  na  mke  wa  mtu  katika  kitanda  cha  mumewe... Taarifa  zinadai  kwamba, mume  huyo  alipomfumania  mkewe  hakufanya  vurugu  yoyote  na  badala  yake  alitoweka  na  kwenda  kwa  mganga  wa  jadi  ambaye  aliuchukua  uke  wa  mkewe  na  kuupachika  katika  uume  wa  mzinzi  huyo. Picha  ni  ya  aibu  sana.BOFYA  HAPO  CHINI <<  BOFYA  HAPA  KUONA  PICHA>>

AIBU....AIBU.....AIBU........NANDO AKAMATWA BAADA YA KUIBA CAMERA MOJA YA BIG BROTHER....

Image
Nando  ameendelea  kuitia  aibu  Tanzania  baada  ya  kukumbwa  na  kashfa  mpya  ya  wizi  wa  kamera  ndani  ya  jumba  la  big  brother. Wizi  huo  unadaiwa  kutendeka  baada  ya  Nando  kualikwa  kushiriki  fainali  za  Big brother  ambapo Dillish aliibuka  mshindi  wa  shindano  hilo..... Baada  ya   wizi  huo, kamera  za  jumba  hilo  zilimuumbua.Nando  alikamatwa  na  kuamriwa  airejeshe  camera  hiyo. Source:  << BIG BROTHER>>

TAZAMA JINSI WEMA SEPETU ALIVYOMTOA MACHOZI MAMA KANUMBA...!!

Image
 Msanii wa filamu nchini Wema Sepetu akimtunza mama yake Kanumba Flora Mtegoa a.k.a. Mama mkwe wake mara baada ya mama huyu kumfwata msanii huyo wakati alipokuwa akicheza muziki uliokuwa ukitumbuizwa na Machozi Bendi katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa filamu ya Foolish Age iliyoandaliwa na msanii mwenzao Elizabety Michael 'Lulu'  Wema Sepetu akimfuta machozi mama yake Kanumba, Flora alijikuta akishindwa kuzuia hisia zake baada ya kutunza kiasi cha fedha cha kutosha kabisa kwa matumizi hata ya wiki nzima na mwanadada huyo Wema akionyesha heshima kwa kumpigia magoti mwanamama huyo ambaye alishawahi kuwa mkwe wake kipindi hicho

Wakali Wa Kili Music Tour Watembelea Makumbusho ya Doctor Livingstone Kigoma

Image
Kundi la kwanza la wasanii watakaotumbuiza katika tamasha la Kilimanjaro Music Tour 2013 limewasili mkoani Kigoma kwa ajili ya onyesho hilo. Wasanii hao  8 ni kati ya 12 watakaopanda katika jukwaa moja uwanja wa Lake Tanganyika siku ya Jumamosi. Kundi la pili la wasanii ambao ni Profesa Jay, Diamond, Lady Jaydee na Barnaba wanatarajiwa kuwasili siku ya Jumamosi asubuhi. Baada ya kupata mlo wa mchana ulioandaliwa na mwenyeji wao ambaye ni  Doctor Gerrard Mipango wasanii hao walipata nafasi ya kutembelea makumbusho ya Doctor Livingistone yaliyoko Ujiji na kujionea historia mbalimbali ya mzungu huyo anayetambuliwa kama mvumbuzi wa Ziwa Tanganyika na pia kuona maeneo biashara ya utumwa ilipokuwa ikifanyika na kujifunza kuhusu asili ya wenyeji wa Mkoa wa Kigoma.

bayern ni mabingwa wa UEFA Super Cup

Image
Bayern Munich imeshinda taji la EUFA Super Cup kwa kuichapa Chelsea mabao 5-4 kupitia mikwaju ya penalti katika mechi iliyochezwa jana usiku kwenye uwanja wa Eden Arena mjini Prague, Jamhuri ya Cheki. (P.T) Bayern Munich, ikiongozwa na kocha wao mpya, Pep Guardiola, imelipiza kisasi kwa kushindwa na Chelsea katika fainali ya Champions League mwaka 2012 baada ya kuifunga klabu hiyo mabao 5-4 kupitia mikwaju ya penalti kufuatia mtanange wa kuwania kombe la UEFA Super Cup kuishia sare ya mabao 2-2 baada ya muda wa ziada kumalizika. Bao la Bayern sekunde chache kabla mchezo kumalizika, liliufungua mlango wa kuelekea ushindi kupitia penalti dhidi ya Chelsea chini ya kocha wao mpya, Jose Mourinho. Penalti zote tisa ziliutikisa wavu kabla mkwaju wa penalti wa mchezaji wa Chelsea, Romeu Lukaku, kuokolewa na kipa wa Bayern Munich, Manuel Neuer, na hivyo kuwapa ushindi mabingwa wa Ulaya, Bayern Munich, dhidi ya mabingwa wa ligi ya Ulaya, Chels

FRANCIS CHEKA NI MOTO WA KUOTEA MBALI.....AMGALAGAZA MMAREKANI VIBAYA MNO NA KUCHUKUA UBINGWA WA DUNIA

Image
 Mgeni Rasmi katika Mpambano wa Kimataifa wa kuwani Mkanda wa Ubingwa wa Dunia wa WBU,kati ya Mabondia Francis Cheka wa Tanzania na Phil Williams wa Marekani,Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo,Mh. Dkt. Fenella Mukangala (mwenye koti jeupe) akimvisha Mkanda wa Ubingwa huo,Bondia Francis Cheka baada ya kumshinda kwa Point Mpinzani wake,katika Mchezo uliomalizika usiku huu kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee,Jijini Dar es Salaam.Kulia ni Bingwa wa Zamani wa Masumbwi,Fransous Bhotha.  Bondia Francis Cheka wa Tanzania (kushoto) akimrushia makonde makali mpinzani wake,Phil Williams kutoka nchini Marekani wakati wa mpambano wao wa Kimataifa kuwania Mkanda wa Ubingwa wa Dunia wa WBU,uliofanyika usiku huu kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee,Jijini Dar es Salaam.Bondia Francis Cheka ameibuka kidedea baada ya kumchapa mpinzani wake huyo kwa Point. Bondia Phil Williams kutoka nchini Marekani (kulia) nae alikuwa akijibu mashambulizi kwa mpinz

LULU AJAZWA MAHELA MA MAPEDESHEE BAADA YA KUIMBA WIMBO YAHAYA WA LADY JAY DEE

Image
UIMBAJI stadi wa Wibo wa YAHAYA wa Nguli wa muziki wa Kizaki kipya Lady Jay Dee umemjaza mahela Msanii wa Filamu aliyejizolea umaarufu kwa miaka ya hivi karibuni, Elizabeth Michael ‘Lulu’ wakati akiimba wimbo huo na Jide wakati wa uzinduzi wa Video yake mpya na yakwanza kusimama peke yake ya FOOLISH AGE. Baada ya move hiyo kali ya dakika 120 iliyooesha ukali wa staa huyo kuoneshwa kwa dakika 20 tu na kubakisha zingine 100 kusubiri wateja kuziona majumbani kwao alipanda jukwaani kujitambulisha na kutoa shukrani kwa wamepenzi wa tasnia ya filamu nchini Tanzania kwa muitikio wao alipanda na kuimba wimbo huo wa Yahaya. Akianzia kuimba kiitikio cha wimbo huo akiwa Back Stage, Lulu aliwashangaza watu pale alipomudu vyema wimbo huo kiasi cha mashabiki ‘Mapedeshee’ wakiongozwa na Pedeshee Rich Rich, kupanda jukwaani na kumtunza fedha kibao ambazo hakika zilimpagawisha msanii huyo na mwisho wa wimbo huo alisema mziki unalipa. “Jamanieee kumbe mziki unalipa ile

WABUNGE WATAKA MBIO ZA MWENGE WA UHURU ZIFUTWE

Image
MBIO za Mwenge wa Uhuru nusura ziahirishe shughuli za Bunge baada ya baadhi ya wabunge kutaka zifutwe na hoja hiyo ijadiliwe bungeni.   Hata hivyo, suala hilo liligeuka shubiri kwa Waziri wa Nchi, Ofisa ya Rais (Utawala Bora), George Mkuchika, kuzomewa na kurushiwa maneno ya kejeli alipojaribu kuzitetea mbio hizo.   Chanzo cha mzozo huo kilitokana na maswali ya mbunge wa Musoma Mjini, Vicent Nyerere (CHADEMA), aliyeihoji serikali kama kuna uwezekano wa kutoukimbiza Mwenge katika maeneo ya watu wasiouhitaji.   Nyerere alisema watu wa wilaya ya Musoma, mkoani Mara, hawautaki Mwenge huo kwa sababu unachochea uhasama, chuki na upotevu wa rasilimali.   “Wakati wa mbio za Mwenge Musoma Mjini walilazimisha kuchukua magari ya halmashauri likiwemo la wagonjwa... huduma za afya zilisimama na hivyo kuleta chuki badala ya mwanga,” alidai.   Nyerere pia alitaka kujua nini faida za mbio hizo, bajeti yake ni kiasi gani kwa mwaka na matumizi yake kama yana