Posts

Ndege asafiri kutoka Finland hadi Uganda

Image
  Kampala, Uganda NDEGE mmoja ambaye inaaminika alitoka nchini Finland amepatikana katika uwanja wa ndege wa Entebbe nchini Uganda. Ndege huyo aina ya Osprey (mwewe) kwa sasa anatunzwa na maafisa wa kituo cha kuwahudumia wanyama cha Uganda Wildlife Education Centre (UWEC). Ndege huyo mkubwa, aligunduliwa na maafisa wa uwanja wa ndege katika njia inayotumiwa na ndege kupaa na kutua katika uwanja wa huo wa Entebbe. Isaac Mujaasi, afisa wa mauzo na mawasiliano katika UWEC, ameambia BBC kwamba ndege huyo alikuwa ameumia katika mabawa yake baada ya kugongwa na ndege iliyokuwa inapaa. Alikuwa na pete yenye maelezo kumhusu mguuni ambayo inaashiria kwamba alimilikiwa na makumbusho ya historia asilia nchini Finland.   Bw Mujaasi anasema waliwasiliana na maafisa wa makumbusho hao ambao wamethibitisha kwamba ndege huyo ni wao. “ Hili lilituthibitishia kwamba ndege huyu alisafiri kutoka Helsinki, Finland,” Bw Mujaasi amesema. “Tutamtibu ndege huyo na akipona

RAIS DKT. MAGUFULI AENDELEA NA ZIARA YAKE KATIKA WILAYA ZA IGUNGA NA NZEGA MKOANI TABORA

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na mamia ya wakazi wa Igunga mkoani Tabora katika ziara yake ya kikazi katika Mkoa huo wa Tabora. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wakazi wa Igunga mkoani Tabora mara baada ya kuwahutubia Wilayani hapo. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wakazi wa Igunga mkoani Tabora mara baada ya kuwahutubia Wilayani hapo. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wakazi wa Igunga mkoani Tabora mara baada ya kuwahutubia Wilayani hapo. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wakazi wa Igunga mkoani Tabora mara baada ya kuwahutubia Wilayani hapo. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mwenyekiti wa Kijiji cha Nanga Wilaya ya Igunga Ndugu Masesa Kishiwa Makala kutoka Chad

WASANII WAASWA KUZINGATIA MAADILI KATIKA UTENGENEZAJI WA KAZI ZAO.

Image
  Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura akisalimiana na Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi Joyce Fissoo wakati akiwasili katika hafla ya uzinduzi wa studio ya kisasa ya Wanene Entertainment Julai 29,2016 Jijini Dar es Salaam.   Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura akisalimiana na mmoja wa wakurugenzi wa Wanene Entertainment Bw. Darish Pandit wakati akiwasili katika hafla ya uzinduzi wa studio ya kisasa ya Wanene Entertainment Julai 29, 2016 Jijini Dar es Salaam. Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura (kushoto) akimsikiliza kwa makini mmoja wa wakurugenzi wa Wanene Entertainment Bw. Bhadresh Pandit (kulia) wakati wa hafla uzinduzi wa studio ya kisasa ya Wanene Entertainment Julai 29, 2016 Jijini Dar es Salaam katikati ni Katibu Mtendaji wa Bodi ya Fila

MWILI WA MAREHEMU JOSEPH SENGA WAWASILI DAR, KUAGWA JUMAPILI VIWANJA VYA SINZA-UZURI

Image
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, (watatu kushoto), mbunge wa Nsumve Richard Ndasa, (wanne kushoto) nabaadhi ya waaandishi na wapiga picha, wakilitama jeneza lenye mwikli wa hayati Joseph Senga, aliyekuwa Mpiga Picha Mkuu wa gazetila Tanzania Daima, wakati wafanyakazi wa Swissport wakilitoa jeenza hilo kwenye uwanjawa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, Julai 30, 2016 ulipowasili kutoka nchini India. MarehemuSenga alifariki katikati ya wiki hii nchini India, alikokwenda kwa matibabu. Taarifaza ndugu wa marehemu kuhusu taratibu za mazishi zinasema, Mwili wa marehemu umehifadhiwa kwenye hospitali ya Taifa Muhimbili, ambapo Jumapili asubuhi utapelekwa nyumbani kwake Sinza, kwa ajili ya ibada fupi na kisha utapelekwa viwanja vya Sinza-Uzuri kwa wananchi ndugu jamaa na marafiki kuuuaga. Taarifa hiyo pia inasema, Mwili wa Marehemu utasafirishwa baada ya zoezi la kuuaga Jumapili Julai 31, 2016. (PICHA NA K0-VIS MEDIA/Kh

‘Matiti ya Kajala, dawa za Kichina zinahusika’

Image
Stori: Imelda Mtema, Ijumaa Baada ya gumzo kubwa kuibuka juu ya muonekano mpya wa matiti ya msanii wa filamu Bongo, Kajala Masanja, shostito wake wa karibu amemwaga ubuyu kuwa, dawa za kuongeza matiti za Kichina zinahusika. Akipigia stori na Ijumaa hivi karibuni, mtoa ubuyu wetu ambaye aliomba hifadhi ya jina lake alisema kuwa, huko nyuma matiti ya Kajala yalikuwa ‘ndala’ akawa anatumia dawa f’lani za kupaka ili kuyafanya yatune. “Nyie muoneni vile tu lakini zile nido zake za sasa Mchina anahusika sana, hawezi kuanika ukweli lakini habari ndiyo hiyo,” alisema mtoa ubuyu huyo. Paparazi wetu alibahatika kuongea na Kajala juu ya madai hayo ambapo alisema: “Watu bwana wanaongea sana, je nikiamua sasa kutumia hizo dawa itakuwaje? Niseme tu kwamba matiti yangu ni orijino na siku zote yana mvuto ndiyo maana sionagi hatari kuyaanika.”

RAIS MAGUFULI AMEANZA RASMI ZIARA YA SIKU NNE... KUTIMUA VUMBI MIKOA YA SINGIDA, TABORA, SHINYANGA NA GEITA

Image

BREAKING NEWSS: ACT WAZALENDO WAPINGANA NA OPERESHENI YA CHADEMA ,WATOA TAMKO HILI ZITO.

Image
KATIKA kile kinachoweza kusemwa kuwa ni sawa na CHADEMA,Chama cha ACT Wazalendo mapema leo hii wametoa tamko lao kuhusu oparesheni ya UKUTA. Jana CHADEMA wakiongozwa na Mwenyekiti wao Mbowe,walitangaza kuianza operesheni hiyo ifikapo mwezi wa tisa mwaka huu kwa madai ya kupinga kile wanachokiita udikteta. ACT Wazalendo leo hii kupitia ukurasa wao wa Twitter wamesema kuwa hawakubaliani na jambo hilo kufanywa na CHADEMA.

Waziri Mkuu: Nitahamia Dodoma Septemba Mwaka Huu

Image
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa  alipokuwa akiwasalimia na kuwashukuru mamia ya wakazi wa mji wa Dodoma mapema leo asubuhi  waliojitokeza kushuhudia  maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa yaliyofanyika kwenye uwanja wa Mashujaa, mjini Dodoma. *Asema akishahamia, Mawaziri na Naibu Mawaziri wote wafuatie mara moja WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema atahamia Dodoma ifikapo Septemba, mwaka huu kuonyesha kuwa Serikali imedhamiria kutekeleza ahadi ilizotoa kwa wananchi. Ametoa kauli hiyo leo asubuhi (Jumatatu, Julai 25, 2016) wakati akizungumza na mamia ya wakazi wa mkoa wa Dodoma na kuwashukuru kwa ushiriki wao kwenye maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa zilizofanyika kwenye uwanja wa Mashujaa, mjini Dodoma. “Jana nilimwita Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu na kumwambia akamilishe matengenezo kwenye nyumba yangu kwa sababu ninataka kuhamia Dodoma ifikapo Septemba,” amesema na kushangiliwa na mamia ya wakazi wa mji wa Dodoma waliohudhuria maadhimisho hayo.

Mtuhumiwa Mauaji ya Mwangosi Akutwa na Hatia.

Image
Daud Mwangosi. Mahakama Kuu Kanda ya Iringa leo imemtia hatiani, Pacificius Cleophace Simon ambaye ni mtuhumiwa wa mauaji ya aliyekuwa  mwandishi wa habari wa Channel Ten na Mwenyekiti  wa Chama cha Waandishi wa  Habari Mkoa  wa  Iringa, Daud Mwangosi kwa kuua bila kukusudia. Mahakama imesema itatoa hukumu ya kesi hiyo keshokutwa Julai 27, mwaka huu. Pacificius anatuhumiwa kumuua Mwangosi katika tukio lilitokea katika Kijiji cha Nyololo, wilayani Mufindi Mkoani Iringa Septemba 2, 2012.

Babu Seya taabani

Image
yaStori: Elvan Stambuli, Wikienda DAR ES SALAAM: Mwanamuziki nguli nchini anayetumikia kifungo cha maisha jela, Nguza Viking ‘Babu Seya’ anadaiwa yu taaban ambapo amekimbizwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) kwa matibabu. Mwandishi wetu alimshuhudia Babu Seya akiwa Muhimbili chini ya ulinzi wa askari magereza watatu na wafungwa wengine watano katika Jengo la Taasisi ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu (MOI) huku akiwa amedhoofu. Haikuweza kujulikana mara moja ugonjwa uliosababisha Babu Seya ahamishiwe Muhimbili kwa matibabu kwa sababu Jeshi la Magereza lina hospitali yake na mwandishi alipoomba kwa mmoja wa askari magereza ili aweze kumsalimia mwanamuziki huyo, hakupewa ruhusa. Baadhi ya wananchi waliomshuhudia mwanamuziki huyo akiwa Muhimbili na kuingizwa katika chumba cha daktari namba 112 walisema, anavyoonekana ni dhahiri ni mgonjwa kwa sababu hakuwa mchangamfu kama ilivyo kawaida yake. “Nguza (Babu Seya) mara nyingi huwa mchangamfu lakini leo ameku

MAGAZETI YA LEO JUMATATU TAREHE 25.07.2016

Image