Posts

MOAT YAUPINGA MSWADA WA SHERIA YA VYOMBO VYA HABARI

Image
Mwenyekiti wa Umoja wa Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania (MOAT), Dk. Reginald Mengi (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu mswada wa sheria ya vyombo vya habari ambao ulitaka kuwasilishwa bungeni kwa dharula. Kulia ni Mwanasheria, Godfrey Mpandikizi. Mkurugenzi Mtendaji wa Sahara Comminication, Samuel Nyalla (katikati), akizungumza katika mkutano huo. Kulia ni Saed Kubenea kutoka Mwanahalisi Publishers na Mwanasheria, Godfrey Mpandikizi. Mwenyekiti wa Umoja wa Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania (MOAT), Dk. Reginald Mengi (kushoto), akisalimiana kwa kumbatiana na Mfanyabiashara maarufu nchini, Rostam Azizi ambaye pia ni mmoja wa wamiliki wa vyombo vya habari. Wadau na wamiliki wa vyombo vya habari wakiwa kwenye mkutano huo. Wanahabari na wadau wa vyombo vya habari wakiwa kwenye mkutano huo. wadau wa vyombo vya habari wakiwa kwenye mkutano huo. Na Dotto Mwaibale WAMILIKI wa Vyombo v

DIAMOND PLATINUMZ ATELEKEZA WATOTO SHULE!

Image
  Staa anayevuna fedha nyingi kupitia kipaji chake cha muziki, Bongo, Nasibu KABANG! Staa anayevuna fedha nyingi kupitia kipaji chake cha muziki, Bongo, Nasibu Abdul ‘Diamond’ amewatelekeza watoto katika Shule ya East Africa International jijini Dar ambao aliahidi kuwalipia ada, Risasi Mchanganyiko linakuwa la kwanza kukudondoshea.   Wanafunzi wanaodaiwa kutelekezwa na Staa anayevuna fedha nyingi kupitia kipaji chake cha muziki, Bongo, Nasibu Abdul ‘Diamond’. Chanzo makini kililiambia gazeti hili juzi kwamba, baada ya Diamond kuwashindanisha watoto hao, Hillary na Hamis (katika picha no. 1 na 2 zilizoko ukurasa wa mbele walipelekwa shule na Diamond) katika shindano la Ngololo lililonyika Januari, mwaka jana katika Viwanja vya Leaders Club, Dar na kushinda aliamua kuwapeleka katika shule hiyo na kuahidi kuwalipia ada kila mwaka lakini kuanzia hapo aliwatelekeza. “Jamani Diamond kila kukicha anafanya shoo za mamilioni lakini ameshindwa kuwalipia ada wale watoto amba

MAGAZETI YA LEO JUMATANO TAREHE 27.05.2015

Image
        MAGAZETI YA UDAKU LEO  

NEC YATOA RATIBA YA UCHAGUZI MKUU

Image
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi (Nec), Jaji mstaafu Damian Lubuva. TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetoa ratiba ya Uchaguzi Mkuu kwa mwaka huu 2015. Katika taarifa iliyotolewa na Mwenyekiti wa tume hiyo, Jaji Damian Lubuva ni kwamba; Agosti 21, 2015: Uteuzi wa wagombea Urais, Ubunge na Udiwani. Agosti 22 - Oktoba 24, 2015: Kampeni za uchaguzi. Oktoba 25, 2015: Siku ya kupiga kura.   NINI MAONI YAKO MDAU WETU

BOSS LADY ZARI ATUA MWANZA KWA SIRI SIKU YA JEMBEKA FESTIVAL.

Image
Mama kijacho wa msanii nyota Diamond Platinum atua jijini Mwanza kumsindikiza kipenzi chake kazini.Wengi hawakuweza kufahamu uwepo wake kutokana na usiri uliowekwa na star huyo wa bongo fleva kwa sasa. Tukio hilo linafananishwa na lile la ujio wa mwanamuziki wa hiphop Jay Z miaka ya nyuma na mkewe Beyonce bila mashabiki kutambua.Ingawa washabiki wa Diamond Platinum wana hamu ya kumuona boss lady huyo.

EDWARD LOWASSA AFUNGUKA MAZITO DODOMA LEO

Image
Waziri Mkuu aliejiuzulu Edward Lowassa amesafirisha wahariri wakuu wa vyombo vyote vya habari toka Dar es salaam na kufanya nao mkutano maalum leo nyumbani kwake mjini Dodoma. Katika mkutano huo kwa ufupi Lowassa amesema yafuatayo; 1. Amesema Hahusiki lolote na sakata la Richmond na ndio sababu hata kamati ya Mwakyembe haikuona sababu ya kumhoji. Amesisitiza kuwa cheo cha uwaziri mkuu ndio ilikuwa lengo la kamati ya mwakyembe na spika wa bunge kipindi hicho Samwel Sitta. Amesisitiza hicho sio kikwazo kwake katika kuingia Ikulu kwani sakata la Richmond lilipikwa kumchafua. Amechukua muda mrefu kuzungumzia hili la Richmond na amesema atalisema zaidi Arusha wikendi hii. 2. Anaamini kila mtangaza nia ana makundi ya kumuunga mkono. Yeye katika mkutano huu na wahariri leo ameambatana na Nazir Karamagi, Peter serukamba, Diana chilolo, Hussein Bashe na wengineo huku wengi wakiwa ni waliojeruhiwa katika serikali ya awamu ya nne akiwemo Aliekuwa DC Igunga Elibariki K

HISTORIA MPYA ALIYOANDIKA DIAMOND PLUTNUMZ MWANZA

Image
Diamond Plutnumz alikwenda mwanza kufanya show ya jembeka festival ila mapokezi yake yali dhihirisha kuwa msanii huyu ni mtu wawatu kama unamchukulia poa tazama picha zote hapa!! MAPOKEZI YA DIAMOND YALIKUWA HIVI UNAAMBIWA AKIENDA KUFANYA SOUND CHEK TAYARI WALIKU WAWANAMNGOJEA  BODA BODA WALIAMUA KUMSINDIKIZA MTU WA WATU  SOUND CHECK SHOW BADO DONE AKISEMA NA WATU WAKE  Posted by Boss Ngasa

RAIS JAKAYA KIKWETE APANGUA TENA WAKUU WA WILAYA

Image
THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS Telephone: 255-22-2114512, 2116898 E-mail: ikulucommpress@googlemail.com Website : www.ikulu.go.tz  Fax: 255-22-2113425 PRESIDENT’S OFFICE, STATE HOUSE, 1 BARACK OBAMA ROAD,  11400 DAR ES SALAAM. Tanzania. TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bwana Anthony Peter Mavunde kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa, Mkoa wa Dodoma, kuanzia leo, Jumatatu, Mei 25, 2015. Aidha, Rais Kikwete amefanya uhamisho wa wakuu 10 wa Wilaya kwa nia ya kuongeza ufanisi katika uongozi wa Wilaya mbali mbali nchini. Katika mabadiliko hayo, Rais Kikwete amemhamisha Luteni Edward Ole Lenga kutoka Wilaya ya Mkalama, Mkoa wa Singida kwenda kuwa mkuu wa wilaya mpya ya Kyerwa, Mkoa wa Kagera. Luteni Lenga anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Luteni Kanali Benedict Kulikela Kitenga ambaye alifariki dunia Aprili 20, mwaka

KIONGOZI WA CHAMA CHA UPINZANI BURUNDI AUAWA

Image
Baadhi wananchi wakiwa eneo alipouawa Zedi Feruzi. KIONGOZI wa chama kidogo cha upinzani nchini Burundi ameuawa kwa kupigwa risasi katika Mji mkuu wa nchi hiyo Bujumbura. Mwili wa Zedi Feruzi amabye alikuwa kiongozi wa Chama cha Union for Peace and Development ulipatikana nje ya nyumba yake kwenye mji wa Bujumbura. Juzi Ijumaa watu wawili waliuawa katika maandamano hayo yaliyochukua wiki kadhaa huku watu zaidi ya 100,000 wakiwa wameihama nchi hiyo kutokana na vurugu hizo za kupinga uamuzi wa Rais Pierre Nkurunziza kuwania urais kwa muhula wa tatu.

TUZO ZA FILAMU 2015 ZAFANA, SERIKALI YAHAIDI NEEMA

Image
Mama yake na Steven Kanumba akipokea tuzo ya mchango mkubwa kwenye filamu aliyotwaa mwanaye (marehemu Kanumba) kwenye tuzo za Filamu 2015. Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenela Mukangala akitoa shukrani baada ya kupokea tuzo aliyopewa Rais Jakaya Kikwete na Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFA) kwenye hafla ya Tuzo za Filamu 2015. Mama yake na Steven Kanumba akipeana mkono na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenela Mukangala mara baada ya kupokea tuzo ya mwanaye kwenye hafla ya Tuzo za Filamu 2015 jana. Mama yake na Steven Kanumba akilia baada ya kuitwa ampokelee tuzo mwanaye. Irene Paul (Best Actress) akipokea tuzo yake kwenye hafla ya Tuzo za Filamu 2015 jana. Irene Paul (Best Actress) akipongezwa na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenela Mukangala kwenye hafla ya Tuzo za Filamu 2015 jana. John Kalage (Best Director) akipokea tuzo yake kwenye hafla ya Tuzo za Filamu